Sakata la tuhuma za Rushwa kwenye Kamati ya Huduma za Jamii: Zitto na Bashe waitwa TAKUKURU

Navyomjua wanasiasa sitashangaa atakavyosema amejiuzuru kutokana Na tuuma za gazeti kwa hayo ndio maelezo
 
Na mbunge yeyote ikidhibitika kaomba rushwa afukuzwe na ubunge italeta heshima
Mkuu,mbunge anachaguliwa na wananchi si takukuru isipokuwa takukuru watampa adhabu akibainika na pia spika na kamati yake atakachofanya ni kutoa adhabu ikiwa ni pamoja na kuvuliwa nyazifa zao. Wenye hali mbaya ni wale waliotoa rushwa kwani kama ni watumishi wa serikali watatakiwa kuachishwa kazi na kupelekwa mahakamani. Hii itasaidia pia kuleta ajira kwa nafasi zinazobaki wazi.
 
Hayo mbona yalitegemewa..kipindi cha mchakato wa ubunge kupitia chama changu Rushwa iliripotiwa waziwazi..Mkurugenzi wa Takukuru akasema eti mbaka uchahguzi uishe ndio atafungulia watu mashitaka kweliii?? Sasa mnalalamika nini akina Lizaboni kuhusu RUSHWA..walichofanya ni sawa tu na sio rushwa ni ahsante hiyo wameomba. Tukisema tumekiharibu CHAMA kwa kuwaaminisha wanachama wetu kuwa bila kupewa kitu hachagui yasingefika hapa tulipo..wabunge wanafanya kama kitu cha kawaida tu...hasa kama wanatoka kwenye CHAMA CHANGU haina shida maana asilimia kubwa mbaka wale maalum walikuwa wanahonga kupata nafasi..nani kakemea kwa dhati au kuchukua hatua madhubutu ndani ya chama. . Nachukia Rushwa Sana Mimi...
 
Utasikia uchunguzi bado unaendelea wabunge wachumia tumbo wataumbuka sana hasa yale CCM
 
Utasikia uchunguzi bado unaendelea wabunge wachumia tumbo wataumbuka sana hasa yale CCM
Lakini hii imekaa vibaya wadau kumbukeni kuwa yuko mr. yuda (zito) ambaye pamoja na kasoro zake huwa hakurupuki saaaana. Hii maana yake ni kuwa kuna kaukweli flani. Pili huyu bwana zito kamati aliyopangiwa ndo hivo haina kick kiviile kwa hiyo kwenye kick ni hapa pa kuchungulia wajingawajinga na kuwachoma baaasi.
 
Na mbunge yeyote ikidhibitika kaomba rushwa afukuzwe na ubunge italeta heshima
Wazo lako zuri isipokuwa watatumia kifungu kipi cha sheri cha kumvua ubunge? Njia pekee ni chama chake kumfuta au kumvua uanachama hivyo AUTOMATICALLY atapoteza ubunge. Lakini asije akakimbilia mahakamani na kubaki na ubunge kupitia mahakamani kama walivyofanya wengine katika bunge lililopita.
 
Mbona Magufuli ni mwanasiasa lakini hafanyi siasa?
politics is about power and authority-hasa kwenye nchi za kiafrika ambazo rais ndio above kila kitu.mfano Takukuru wakimchunguza magufuli kwa tuhuma za ufisadi na ikathibitika ni nani ambaye atamfunga magufuli
 
Ni kweli kabisa. Kama wanavyotumbuliwa watendaji wa serikali, basi na hawa waheshimiwa watumbuliwe ama wajitumbue wenyewe
Mhalifu wa CCM hatumbuliwi labda huyo Zitto ambaye hata hivyo CCM wanamkubali kwa vile ndege wa manyoya yaliyofanana huruka pamoja
 
takokuru ni wasanii,kwa nini wasimuite Ndungai?maana yeye ndie aliewaondoa wabunge kwa hizo tuhuma, inakuwaje waitwe waliojiuzulu? eti na kuna watu wanaona huo ndio utendaji kazi
 
Kitendo cha waheshimiwa wabunge kutuhumiana kwenye rushwa ni kitendo cha aibu sana! Watumbuliwe tu.
 
Mkuu, TAKUKURU haitoi adhabu. Wao wanafanya uchunguzi na wakidhani una kesi kesi ya kujibu basi wanakuburuza mahakamani. Mahakama ndio itaamua kama una hatia ama la na itatoa adhabu kwa mujibu wa sheria.
 
Safi sana Zitto.
 
Ngoja mimi niangalie eneo tofauti kidogo,
Kwenye hii tweet, Mh Zitto anamtaja Mh Bashe kwa title ya Ndg. Kwa tamaduni na staha za kibunge, ile heshima ya title ya Mh isipokuwepo inaweza kutafsiriwa kuwa huthamini hadhi ya mwenzio.
Pili, baada ya kusikia tu kuwa Mh Bashe naye ameitwa, nawe ukuanza kutoa kauli za ujumla za kumuunganisha Mh Bashe, kana kwamba wewe ni msemaji wake kwa kutoa ahadi ya ushirikiano mtakaoutoa kwa TAKUKURU pia ni kutokuthamini hadhi ya mwenzio.
USHAURI: Punguza mihemko!
 
Kuna yule mbunge aliyeshikishwa fedha za moto na mkurugenzi wa Mkuranga halafu eti akashinda kesi....sasa kwa kuwa mahakama ilionesha ulegevu kwenye hili ndio maana wanaendeleza tabia hii.

Waomba rushwa wengine ni wakaguzi TAKUKURU iwafuatilie pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…