Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 14,536
- 22,954
Ni kweli mafao ya wastaafu hayatoshi (si wao tu asilimia kubwa ya wabangaizaji Tanzania either hakuna wanachopata na wakipata hakitoshi)...; Lakini wakati tunachemsha Bongo jinsi ya kuwarekebishia hawa kidogo kiwe kikubwa kidogo, ni vema tukaangalia ni vipi hatari inayokuja kesho ya wazee wa kesho ambao watakuwa hata hicho kidogo hawana....
Mafao / Pensheni moja ya sababu yake kubwa ni pale huyu mchumia juani nguvu zake zitakapomtupa aweze kupata hata mahitaji yake muhimu na asiwe omba omba wala kusumbua jamii inayomzunguka..., lakini kinachotokea sasa, sababu wengi wa vijana hawana sehemu ya kuchumia uzee wao watakuwa sio tu kwamba hawana nguvu hata kile kidogo cha kuwawezesha kitakuwa hakipo....
Na hapo ndio tutakuwa na Taifa la Wazee wengi omba omba na hii itakuwa sio Haki kwa vijana wa wakati huo au Taifa kuzungukwa na omba omba (Taifa linaloshindwa kuangalia wazee wao)