Sakata la madawa ya kulevya: Hizi ndizo faida za RC makonda kutaja majina maarufu hadharani

Dankbar

Member
Jul 11, 2015
98
113
Baada ya RC Makonda kutaja majina ya watu maarufu hadharani kwa kuwahusisha na madawa ya kulevya, faida zifuatazo zimepatikana na zitapatikana:
1. Ubaya wa kumtaja mtu kwa tuhuma hadharani pasipo uthibitisho

2. Wanyonge waliotajwa hadharani kujua haki zao kikatiba
baada ya kuwataja watu maarufu akiwemo mwenyekiti wa Chadema

3. Wakuu wa Mikoa kujua mipaka yao na namna ya kushughilika na Mambo mbalimbali katika Mikoa yao

4. Nguvu ya Bunge katika kuwadhibiti viongozi wateuliwa na kuilazimisha mamlaka ya uteuzi kutengua uteuzi

5. Ongeza faida zingine kwa mwendelezo huo kabla hatujaangalia upande wa hasara zake
 
Kama kijana,namwonea huruma Makonda ila ataponzwa na tamaa na ujinga wake.
 
Jambo hili kila mtu hulitazama kwa eneo alilosimama.

Nape amesema ni kuua brand ya wasanii waliyojenga kwa muda mrefu. Nape ni waziri wa utamaduni.

Gwajima amesema ni shambulizi dhidi ya ukristo na maaskofu. Gwajima ni Askofu.

Manji amesema ni kuua reputation ya wafanyabiashara wakubwa waonekane utajiri wao ni wa madawa. Manji ni Billionaire na diwani wa ccm mbagala. Hajazungumzia siasa sababu its nothing kwake. Kwake biashara ni kitu. Amesimamia eneo la biashara

Mbowe amesema ni shambulio dhidi ya upinzania Tanzania ili kuua upinzani.

unatazama jambo pale uliposimamia

*Mimi naona Makonda anapiga deal na wafanyabiashara wakubwa kwa kuwataja wasiohusika na kuwaacha wanaohusika, kwa namna hiyo anamdanganya Rais

*Deal hilo linaweza likaanzia kwa utajiri wa ghafla wa Makonda kadri ya maneno ya Msukuma aliyeomba Makonda kuchunguzwa*

Mimi naamini Rais akijua kuwa hizi ni drama, kwa sababu naye anapenda drama za sifa, akafikiri Makonda anapiga kazi anajidanganya.

Nina mashaka sana na unprofessional approach ya watuhumiwa kuanzia na karatasi yenye majina utadhani majina ya wapiga kelele yaliyoandikwa Monitress mnoko mwenye sura mbaya wa darasa la Nne B.
 
Tujiandae kulipa Lawsuit yake. Manji najua si chini ya B1, Gwajima mpenda sifa B50, Mbowe B100 hapo anaunganisha na ishu ya National Housing kabisa.

Wanyonge tunaenda kulipa hizo pesa.
wanaotaka kusafishwa hudai sh.moja tu.
Hayo mabilioni hudaiwa makampuni tu.Mbowe adai B100,yeye ana biashara na hadhi ya bilioni ngapi?
acha ushabiki maandazi
 
Sure! Mchezo mchafu inaitaji umakini kuchunguza ukweli wa hili jambo natamani iundwe tume kuchunguza sakata hili kwa undani wale wanaotuhumiwa makonda mwenyewe pamoja na hao watu wanaotajwa ni marafiki zake ukweli uwekwe mchana kweupe
 
Ccm walichoweza ni kumfunga mbunge wa cdm Lijuakali na kuhangaisha familia ya Lema mahakamani kwa kesi za kijinga zisizo na athari za kitaifa,kesi za majungu eti ccm sasa imekomaa nalo wewe,na mahakama yetu ya Arusha iko mfukoni mwa mkuu wa mkoa kila jambo la Lema analoomba wanakrash,igeni mahakama ya Marekani ilivyosimama kidete kumpinga Trump wanasomamia katiba ,nyie mmebaki kuendesha kesi za majungu hizo za ccm,mmekomaa nzo hamna ata aibu,mbunge mzima mwenye kutambulika mmemgeuza Kama mke wenza wenu,alaaniwe yeyeote anayetesa familia ya Lema kwa majungu na siyo sirias ishu kwa kumnyima dhamana
 
Mizizi ya dawa ya kulevya imejichimba chini ya nyumba yenyewe na mpangaji hawezi kubomoa labda ahamie nyumba nyingine tu na pia mengine ni makaburi ya zamani.
 
wanaotaka kusafishwa hudai sh.moja tu.
Hayo mabilioni hudaiwa makampuni tu.Mbowe adai B100,yeye ana biashara na hadhi ya bilioni ngapi?
acha ushabiki maandazi

Kwani Mbowe sio Brand?? Kwa hiyo mnachafua watu kusudi mnafikiri mtadaiwa sh1. Safari hii mtajuta.
 
Kila lenye uzito lina wepesi na kheri zake, bora na mimi ningetajwa ili nipate fidia ya bwerereeeeeeeee, hivyo wale wadogowadogo waliosingiziwa wasihofu neema inakuja hata km wamelala selo siku kadhaa
 
Tujiandae kulipa Lawsuit yake. Manji najua si chini ya B1, Gwajima mpenda sifa B50, Mbowe B100 hapo anaunganisha na ishu ya National Housing kabisa.

Wanyonge tunaenda kulipa hizo pesa.
Mbowe amesema hanashida na Jamuhuri anamshataki Makonda.So wala hatulipi hizo pesa ajiandae tu.

Hata Gwajima atamshtaki Makonda waanze kuuza hizo assets
 
Back
Top Bottom