Sakata la Lissu: Wabunge wa Upinzani watoka nje ya Ukumbi wa Bunge

Good spirit. ni ujinga sana,coz naamini wakiwa na vikao,lazima spika apewe taarifa kwamba mbunge fulani anahitajika,sio kukamata kihunihuni
 
Wapinzani wamsusia Bunge Naibu Spika
Tuesday , 7th Feb , 2017
Wabunge wote wa vyama vya upinzani waliokuwa bungeni katika kikao kinachoendelea jioni hii wametoka nje ya Bunge, wakipinga wenzao kufukuzwa bungeni pamoja na kitendo cha Mbunge Tundu Lissu kukamatwa.

Tulia%20mdee%20bulaya.jpg

Wabunge waliokuwa wameamuliwa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge na Naibu Spika Dkt Tulia Ackson ni pamoja na mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya na Mbunge wa Serengeti Marwa Ryoba.

Wabunge hao watatu wamedaiwa kupinga uamuzi wa Naibu Spika kuhusu muongozo ulioombwa na mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, kuhusu utaratibu uliotumika kumkamata mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Mara baada ya Naibu Spika kutoa maamuzi ya kuwaondoa wabunge hao watatu bungeni, ndipo wabunge wengine wa upinzani pia wakaamua kutoka kama ishara ya kupinga maamuzi hayo, pia ikiwa ni ishara ya kupinga utaratibu wa kukamatwa kwa mbunge Tundu Lissu.

Nje ya ukumbi wa Bunge, Mbunge wa Kigoma Mjini Tundu Lissu, amesema wamefikia hatua hiyo kuonesha kuwa uataratibu unaotumiwa kukamata wabunge wakiwa bungeni siyo sahihi, na kwamba kesho wataendelea na vikao vya bunge lakini mapambano yataendelea.

"Kesho tunarudi bungeni, lakini mapambano yataendelea, tunataka kuonesha kuwa utaratibu huu wa kuvizia wabunge kwenye milango ya bunge bila taarifa rasmi ya Spika na bila kuwaeleza wabunge sababu za kukamatwa kwao siyo sawa. Tukilifumbia macho litakuwa kumtokea mbunge yoyote hata wa CCM" Amesema Zitto.
 
wana hoja ya msingi utaratibu wa kumkamata mbunge na mamlaka nyingine taratibu zifuatwe ,bunge ni mhimili.serikali na mahakama .
 
Mungu wabariki wapinzani , dunia inaona , Wala unga wanaitwa waje polisi na wanapewa soda lakini waheshimiwa wanadhalilishwa na koplo wa darasa la saba !
 
[TE="Ruttashobolwa, post: 19616246, member: 71917"]halafu kila leo wanafanya jambo lile lile[/QUOTE]


Tusha wachoka ,na wasirudi tu.
 
Wapinzani wajitafakari upya.Nahisi tangu aondoke Dr.Slaa upinzani umeshindwa kuitikisa Serikali.

Wajitafakari kwa lipi? Mtu anawindwa kama mwizi? Kwanini polisi hawakutoa taarifa kuwa Lissu anatakiwa kituoni badala yake walienda kumvizia bungeni? Endeleeni na biashara yenu ya madawa ya kulevya.
 
Hii tabia inaota mizizi sasa..........mi nadhani ni zamu ya UPINZANI nao kugoma kutoka ili wapambane humo humo.....ikibidi hao wengine ndio watoke.
wale wengine c wanapolisiccm hawawezi toka hawa wengine wakigoma kutoka na wakikomaa mjengoni watapelekwa nje mzogamzoga na askari wa chama dola,so hakuna namna,ila hatukati tamaa kitaeleweka ni suala la muda tu
 
Back
Top Bottom