2012 miaka 28 basi 2024 utakuwa na miaka 40 siyo 36 acha kudanganyaWasalaam,
WanaJF wote.
Baada ya kuwa mwanaJF mtamazaji kwa muda wa miaka 8 hatimaye nimeamua kujisajili rasmi ili kuwa mwanachama hai ili nami niweze kuleta fikra zangu ambazo huenda zikawa msaada kwa watu wengine.
Kabla ya kuanza kueleza kilichonileta hapa, Kwanza naomba kutoa shukrani zangu za dhati kwa wanaJF wote kwa maandiko yenu katika JF. Hakika machapisho haya yamenijenga na kuniimarisha kifikra, kiroho na kimwili. Japo nilikuwa mwanachama mtamazaji kama nilivyoeleza hapo juu lakini nilikuwa nasoma, kufuatilia na kufanyia kazi machapisho yote muhimu ambayo nilihisi ama yananifaa au yananigusa moja kwa moja katika Safari yangu ya maisha nje ya ajira. Niseme tu kuwa huenda msiamini lakini maandishi haya yanaponya watu fulani, mahali fulani, na wakati fulani. Mungu awabariki sana.
Baada ya hapo, naomba kurudi kwenye mada yangu. Mara nyingi nimeona nyuzi mbalimbali zenye kukinzana juu ya kipi ni kizuri kati ya kuajiriwa au kujiajiri. Kwa miaka takribani 7 kama sio 8 nimekuwa nikifuatilia nyuzi hizi kwa umakini kwa kuwa zilinigusa kwa kiasi kikubwa kwa kuwa tayari nilikuwa nimeacha ajira Serikalini. Kwa hiyo mimi nitazungumzia upande wa kujiajiri kwa kutumia mfano wangu Mimi mwenyewe.
Leo imepita miaka 9 tangu niache kazi Serikalini na kuanza kujitafuta kupitia kujiajiri/ ujasiriamali. Mpaka hatua hii nimeona nina kitu kidogo naweza kuchangia lengo ikiwa ni kuwatia moyo na motisha watu wote wenye nia ya kujiajiri wenyewe na hasa kwa vijana.
Safari yangu kwa kweli imejaa mambo mengi sana ambayo siwezi kuelezea kwa siku, wiki, mwezi au mwaka. Ila nimeamua kuiweka hapa kwa ufupi tu kama muhtasari ili mbeleni nikipata muda nitakuwa naelezea hatua kwa hatua kiundani. Karibuni sana.
MIMI NI NANI?
Naitwa Emma. Jina maarufu kwa sasa Mwl. Mzazi. Miaka 36 nipo duniani navuta pumzi ya mwenyezi Mungu bure. Makazi kwa sasa mkoa X. Nina ndoto za kuwa MO Dewji au Bakhresa panapo majaliwa.
Mwezi May mwaka 2015 niliamua kuacha kazi ya ualimu serikalini. Hii ilikuwa ni miaka 2 tu tangu niajiriwe na serikali ya Tanzania yaani mwezi machi 2013 mara tu baada ya kumaliza shahada yangu ya ualimu pale DUCE mwezi Julai 2012. Nikiwa kijana wa miaka 28 niliamua kuacha kazi.
SABABU ZA KUACHA KAZI
i. Maslahi duni
Nilikuwa kijana mpambanaji kabla ya ajira. Hivyo tangu kumaliza chuo mwaka 2012 hadi kuajiriwa serikalini 2013 nilikuwa nishafanya kazi shule za private mbili kwa mishahara isiyozidi laki 5 bila makato. Nilipoajiriwa niliduwaa na nilichokikuta. Kweli kabisa niliduwaa.
ii. Mazingira mabovu ya kazi
Kijijini zaidi ya Kijiji. Hakuna umeme, hakuna mtandao, Kijiji kizima duka moja tu, hakuna hospitali, hakuna usafiri. Hii ilinishangaza.
iii. Ndoto zangu
Tangu kidato cha tano nilikuwa na picha fulani ya aina ya maisha niliyofikiria kuyaishi. Mara zote nilikuwa na picha ya kuishi maisha fulani mazuri sana mfano wa Mo Dewji au Bwana mkubwa Bakhresa. Nilipoingia tu kazini mwaka 2013 miezi miwili tu ilinitosha kufanya tathmini na kujua kwamba kwa njia ya ualimu niliyochukua hakika ndoto zangu kamwe hazitokaa zitimie. Hivyo ubongo ulinituma kwamba natakiwa kuwa na njia mbadala kama kweli nayataka aina ya maisha niliyofikiria.
iv. Majukumu ya kifamilia
Nikiwa kama kijana mkubwa katika familia ya watoto wanne iliyolelewa na mama baada ya baba kufariki, nilijiona nina jukumu la kumpokea mama mzigo wa watoto wengine. Mama huyu aliyepambana kwa kuuza dagaa mpaka mimi kupata elimu alikuwa na kila sababu ya kusaidiwa.
Hapa niliona jukumu langu kwa familia. Swali kubwa kwangu lilikuwa ni, "ikiwa huyu mama aliyeishia kidato cha pili ameweza kupambana hadi wewe kuwa hapo, je wewe unayejiita msomi unatakiwa kufanya nini?. Jibu likawa ni Mimi kubadilisha hatima na historia ya familia kutoka zero to hero.
MAZINGIRA YA KUACHA KAZI
Niliacha kazi nikiwa sina mtaji wa kutosha zaidi ya M.3, sina mpango unaoleweka, sina jina, sina connection, sina mtu wa kunishika mkono. Kiufupi nilikuwa sijajipanga ila niliamini nitajipanga mbele kwa mbele.
IMANI YA KUACHA KAZI
Pamoja na kutokujiandaa ila niliamua kuacha kazi kwa sababu ya kuamini katika mambo yafuatayo.
A. Mungu Kwanza
Niliamini na naamimini katika Mungu siku zote. Sikuamini kuwa Mungu alitaka niwe mwalimu masikini. Niliamini ananitakia mema hivyo huko ninapokwenda atasimama na mimi katika mapito yote.
B. Uwezo mkubwa katika ufundishaji. Hii niliamini nikishindwa hapo mbeleni hakuna private school itanikataa. Mimi ni mwalimu hodari sana katika somo la Kiswahili na Fasihi ya kiingereza (Literature)
C. Uwezo mkubwa katika uandishi. Hii ilinipa jeuri kwani nilijua kama ningezidiwa hapo mbeleni ningetumia kipaji hiki kuandika nakala za wanafunzi katika masomo hayo niliyobobea.
D. Uwezo mkubwa katika utendaji. Hii ni silaha kubwa sana hata sasa. Napiga kazi sio mchezo. Katika kazi sina mzaha, masihara wala uvivu hata kidogo.
E. Akili kubwa ya ubunifu na unyumbulifu wa vitu. Katika kitu najivunia ni akili yangu ya kipekee baada ya kuondoa elimu ya darasani(vyeti). Ni mdadisi, mbunifu na mwenye kufikiri nje ya box. Hii ni zawadi niliyotunukiwa.
F. Mtaji kidogo wa milioni 3 niliyojikusanyia ilinipa kiburi na jeuri ya kushinda huko niendako. Utashangaa niliipata wapi? Hapo juu nilidokeza kuwa kabla ya kuajiriwa Serikalini nilifanya private mbili kwa malipo si chini ya laki 5. (Kuanzia August 2012-May 2012). Nililipwa hii hela kutokana na uwezo mkubwa nilikuwa nayo katika masomo yangu(utaona hapo mbele)
SAFARI YA KWANZA 2015-2016
MWANZO WA MAPAMBANO
Niliikutana na dunia tofauti na ile niliyofikiria. Aisee asikwambie mtu, kujiajiri ni kazi sana. Hapa nilikutana na vita ya kupingwa na familia, ukoo, marafiki, jamaa, na wachumba kutokana na maamuzi yangu ya kuacha kazi.
Shughuli pevu ilikuwa kwa mama mzazi ambaye aliamini kazi yake ya kunisomesha ilizaa matunda baada ya kuajiriwa Serikalini. Aisee hii vita achana nayo asikwambie mtu yaani.
Jambo la pili ni kupoteza mtaji wangu takribani Milioni 2 kwa kukurupuka kuingia kwenye Biashara ya mazao bila utafiti. Biashara ya mahindi na mpunga iliondoka na milioni 2 zangu wajanja wa mjini wakinizidi kete na hatimaye kunufaika na mtaji wangu. Aseee! Haha! Hahaha! Haha! Hatari sana. Ngoma ya Giningi rha yake uingie kuicheza mwenyewe na sio kusimuliwa.
Sasa kwa kuona biashara ishaondoka na mtaji, milioni moja iliyobaki nikaigawa mara mbili. Laki 5 nikanunua desktop na printa ila sasa kutumia kipaji cha uandishi. Laki tano nyingine ikawa matumizi ya kujikimu huku nikitafuta plan B.
Hapa sasa akili ikaanza kukaa vizuri. Sina tena hela ya kumpa mchumba na kusapoti ndugu jamaa na marafiki kama pale awali. Hapa nilitamani kufa kwani hakuna rangi niliyoacha kuiona hapa duniani kutoka kwa wale niwapendao.(Wanawake Mungu anawaona)
Mwisho, niliipata akili nikajishikisha kwenye Tuition centre hizi zinazotoa huduma za QT, PC n.k. Daah! mshahara ikatamkwa sh. Elfu 70 ndio elfu 70 kwa mwezi. Nilikubali kupiga kazi kwa hela hiyo kwani niliona advantage ya population kubwa halafu pia nilitaka kujulikana kwani hapa nilipokuwa ni sehemu nyingine yaani mji mkubwa kwani kule porini nilishakimbia.
Niseme kwamba ni katika eneo hili hili, nikilipwa elfu 70, ndipo milango ya mapambano yangu yalizaliwa hapa. Nilipata fikra mpya ya kunifikisha Kaanani kule nilipotaka kwenda. Wazo la kumiliki Tuition Centre yangu ikazaliwa hapa( Nitakuja kueleza siku nyingine)
SAFARI YA PILI 2017-2020
DHIKI KUU: KILELE CHA MATESO
Mpaka mwaka 2017 nilikuwa nimefankiwa kufungua tuition centre yangu. Nilikuwa nimeamua kuibadili fani yangu ya ualimu kutoka kuwa huduma na kuwa Biashara. Bwana wee acha kabisa changamoto kibao. Uhaba wa mtaji, uhaba wa wataalamu( waalimu ukiwaajiri wanataka maslahi tu na sio kitu kingine), upinzani kutoka centre zingine, n.k ni miongoni mwa changamoto zilizonikabili. Korona ya mwaka 2020 ikaja kufunga kazi baada ya Serikali kufunga shule nchi nzima.
Changamoto zingine zilizotaka kunitoa roho na kutamani kufa kabisaa
A. Uhaba wa fedha kabisa. Kutokana na kipato duni kutoka tuition centre.
B. Kumpoteza mke(kuachwa) kwa sababu ya kuonekana sina dira ya maisha. Jukumu lingine ikiwa ni kusomesha ndugu zangu.
C. Kupata mtoto wa Kwanza kwa mwanamke wa pili na kisha kutelekezewa mtoto akiwa na miezi nane na hatimaye kukimbiwa na mwanamke huyo wa pili nikiachiwa kijana mdogo.
D. Kutengwa na familia(mama mzazi), ukoo na familia kwa ujumla kwa kudai kuwa niliyataka mwenyewe kwa kuacha kazi(nilionywa nikajidai mbishi)
E. Kufiwa na mtoto wangu wa Kwanza kutokana na kukosa malezi ya mama na pia uchumi mbovu. Kwa kweli hapa nililia kama mtoto mdogo. Kijana wangu niliyetelekezewa akiwa na miezi nane hatimaye akafariki akiwa na mwaka mmoja na miezi nane.
F. Mama kuanza kusumbuliwa na magonjwa ya mara kwa mara (presha, magonjwa ya uzazi) yaliyohitaji fedha nyingi kutibiwa. Kumbuka Mimi ndiye kijana mkubwa.
Katika nyakati nilianza kujuta na kujilaumu ni kwa nini niliacha kazi ilikuwa ni wakati huu. Nilikata tamaa hasa baada ya kumpoteza mtoto wangu wa kiume wa Kwanza(kufa) na pia kuachwa na wanawake wawili niliwaamini, kuwapenda na kuwathamini huku ninaona hivihivi(Jeraha la moyo. Maumivu ya mapenzi kwa natambua ya kwanza. Acha tu). Ni katika mwaka huu wa 2018 nikiwa Sina rafiki, ndugu, mshauri na huku nikibaki mpweke na kuwa kama kifaranga aliyekosa mama ndipo mbingu zinafunguka. Ardhi nayo inanikumbuka.
Imeandikwa Mungu sio Wanjara na wala sio Webiro, ni katika kipindi hiki cha maumivu, machozi na majuto ndipo napata moyo wa kishujaa kuliko wakati mwingine wowote ule. Mungu ananipa ujasiri wa hali ya juu na kupata matumaini mapya kupitia mambo haya.
A. Jamii Forums.
Mwanzoni nilikuwa najua JF ni mtandao wa kisiasa tu. Kwa kuwa hapo nyuma niliijua JF kupitia rafiki yangu mwanaharakati fulani, nilijua ni sehemu ya siasa. Sasa katika kipindi hiki kigumu napata familia mpya ya JF.
Nagundua kuna jukwaa la uchumi, siasa, michezo, burudani, mahusiano n.k. Daah! Hapa niwe mkweli nilianza kusoma vitu mpaka nikajuta nilikuwa wapi. Kufupisha, jukwaa la mahusiano yalinipa uponyaji juu ya kuachwa na wanawake (nilijifunza kutoka kuwa Alfa male na sio Beta male: kifupi kuwa mwanaume kauzu juu ya wanawake na mtazamo wangu kuhusu wanawake ilibadilika kabisa) hii imeniponya sana. Jukwaa la uchumi na Biashara likawa ni uwanja wangu wa mazoezi na chakula changu cha kila siku. Jukwaa la Burudani mkanisahaulisha matatizo yangu yote na mateso yangu. Tabasamu likarudi usoni pangu.
B. Kumpoteza mtoto wangu wa Kwanza.
Hii ilinizalishia hisia kali za kuuchukia umaskini. Niliamini nimempoteza kwa sababu ya umaskini na pia wanawake wameniacha kwa sababu ya umaskini. So kila siku asubuhi ya Jumamosi tangu Octoba 2018 (mwaka niliyompoteza kijana) basi ningeenda makaburuni na kumuapia kijana wangu marehemu kuwa wadogo zake kamwe hawatakuja kuteseka tena kama yeye, na kwamba lazima nije kuwa MO Dewji au Bakhresa siku moja.
Na kwamba mdogo wake (binti yangu: mtoto wa pili) lazima aje kuishi maisha ya juu sana( kumbuka hapa 2019 nilifanikiwa kupata mtoto wa pili). Kumbuka huyu mtoto wangu wa pili (binti) pia mama yake aliondoka naye. Kumbuka nimesema hapo juu nilikimbiwa na wanawake wawili, so kila mmoja nilizaa naye mtoto mmoja. Hii iliniongezea machungu ya kupambana kwani niliamini mtoto wangu alikuwa analelewa na baba mwingine. Hivyo, niliweka nadhiri ya kuwa tajiri ili siku moja binti yangu apate kunipongeza kwa mapambano niliyoyafanya.
C. Mama yangu.
Kutokana na mama yangu kupoteza upendo wake kwangu na kunichukia mazima na mimi kumchukia pia, mwishowe nilipata funzo kuwa njia pekee ya kufanya anipende tena ni kumuonyesha mafanikio kwa vitendo kuwa nilikuwa sahihi kuacha kazi. Hapa nilipata nguvu mpya ya kuinuka na kupambana tena.
D. Ndugu zangu
Pamoja na changamoto nilizopitia, kila senti niliyopata nilijinyima ili kusomesha ndugu zangu. Dada wa kwanza kunifuata alifanikiwa kumaliza form four na kuolewa na baadae akifariki huku akituachia vijana wawili. Dada wa pili alihitimu diploma ya uhasibu na kubarikiwa kupata ndoa. Mdogo wangu wa mwisho (kijana) alifanikiwa kumaliza form four na kufeli lakini nilipambana juu chini akaristi na kupata alama za kusoma cheti. Alisoma cheti na kuunganisha na diploma ya uhasibu. Hawa ndugu zangu waliokuwa wananitegemea nilipambana hasa kwa ajili yao.
SAFARI YA TATU 2021-2023
MAPAMBANO YANAANZA UPYA
Kutokana na maelezo hapo juu mwaka 2021 niliamka upya hasa baada ya kuvuna madini ya kutosha kutoka JF. Hakika nilikuwa nimezaliwa upya. Nilikuwa ni simba kwelikweli. Nikuwa nimeamua haswaa kuipigania Safari yangu na ndoto za utajiri. Zifuatazo ni baadhi ya hatua nilizochukua.
A. Niliamua kuipambania tution centre yangu kwa nguvu zote, nilipambana na washindani, niliongeza ubunifu wa hali ya juu, sikutaka mchezo tena. Hata hivyo nilikuwa nimeelewa gemu linaendaje sasa. Kidogo nilianza kupata vifedha kichele kupitia kituo hiki.
B. Niliamua kuoa tena mke wa tatu. Awamu hii sikutaka kuoa digrii wala diploma kama ilivyokuwa kwa wale wawili. Awamu hii nilioa form six. Hapa nilipatia asee. Kutokana na biashara nilizosoma humu JF nilianza kujaribu kila moja.
(Hapa Mimi nilikuwa naendesha kituo yaani ile tuition, vijisenti nikipata nawekeza kwenye Biashara huku mke wangu pamoja na mpwa: mtoto wa Dada aliyefariki wakiingia mzigoni). Kwa kuwa nilishajifunza kuwa JF kuna watu wa aina mbili (wakatishaji tamaa na watia moyo) niliamua kushikamana na hawa watia moyo(namaanisha kuna watu humu JF kila biashara lazima ianze na mamilioni kadhaa) Hawa sikuwajali.
Nilichofanya ni kuanzisha biashara kwa mtaji mdogo kadri niwezavyo. Nimeuza duka, nimeuza chipsi, nimeuza migahawa, nimefanya nafaka, nimeuza Mkaa, nimeuza duka la mitumba, nimeuza vitafunwa, nimeuza maji mtaani. n.k kiufupi nimepigana kufa na kupona. (N.B kila Biashara hapa nilikuwa naanza na mtaji wa laki 3 hadi 4 tu) hazijawahi kuzidi.
Katika hizi Biashara nilifeli na kufeli na kufeli na kufeli tena mpaka siku nilipopata kile nilichokuwa nakihitaji.(Muhimu sikuwahi kukopa ili kuwekeza kwenye biashara. Niliibana kila senti ya pesa niliyopata pale shule ikifika laki 2 au 3 nafungua biashara. Ikifeli mimi na mke na mpwa tunakaa na kuandika changamoto na mafanikio tuliyoyaona Kisha tunajipanga tena( kuna wanawake wapambanaji na wazuri asee. Huyu mama kwa kweli Mungu ambariki sana).
N.B: Katika Biashara hizo zote lengo ilikuwa ni kupata biashara inayoningizia faida ya elfu 10, 000 tu kwa siku. Niliamini nikipata hiyo biashara basi ndio utajiri wangu utaanzia hapo( hata hivyo mapambano yalikuwa makali sana. Pongezi ziende kwa cheupe wangu mdogo pamoja na mpwa wangu waliokubali kuwa maabara yangu ya kufanyia majaribio yangu bila kuhitaji malipo, wala kudai nguo nzuri au starehe) kama wale pasua vichwa wawili(wake) waliotaka kunitoa roho yangu.
c. Niliamua kuanza kuandika kitabu cha mapitio ya maisha yangu tangu kuacha kazi, na pia kuandaa kwa maandishi ramani ya kuwa tajiri wa kati kabla ya kufika 40 age. ( hapa namaanisha kuingiza kiasi cha sh. Milioni 10 kwa mwezi). Kwangu naamini nikiingiza kiasi hicho kwa mwezi kabla ya kufika 40 basi kuja kufika 50 age nitakuwa Mo Dewji hata kama sitokuwa bilionea ila kuwa milionea kwangu itakuwa mafanikio makubwa ukilinganisha na historia ya familia na ukoo niliotoka. ( Hapa naanda katiba/ramani ya maisha yangu hadi kufika 60 ambayo itatumiwa na kizazi hadi kizazi.( Mojawapo ya kitabu ni Namna ya kuingiza kipato/faida ya milioni 10 kwa mwezi). Kumbuka wakati huo naingiza faida ya laki 2 au 3 kwa mwezi kupitia tuition centre. But naandaa kitabu cha kuingiza milioni 10 baaday ya miaka mitano mbele.
SAFARI YA NNE 2014-2024
NIMEIPATA NJIA: NAIONA NURU
Ndugu zangu mpaka naandika waraka huu wakati huu kiukweli sina nyumba, sina gari, sina kiwanja, sina mashamba ila nina myoto mmoja wa like ambaye pia anaishi na mama yake. Nina mke wa tatu (cheupe mdogo) na mpwa wangu( greda ya kazi) tu.
Lakini katika umri huu wa miaka 36 ninaona nimefanikiwa tele kwani huko mbele naona kabisa jamii ya watanzania watanifahamu ikiwemo ninyi ndugu zangu JF. Mpaka sasa nina baadhi ya mambo ambayo kwangu Mimi nayaona ni mafanikio makubwa sana. Baadhi ya mmbo hayo ni.
A. Nina kituo cha tution centre inayotoa huduma ya QT, PC n.k ambayo nategemea kuitanua na kuifanya kuwa jina kubwa sana Tanzania hii ndani ya miaka mitatu ijayo.
B. Katika miaka 11 ya ualimu nimefanikiwa kujenga jina kubwa katika mkoa X niliopo kwa sasa. Siku ukisikia jina la Mwl. Mzaz basi ujue ni mimi. Usihofu panapo majaliwa ndani ya miaka 2 au 3 ijayo utalisikia popote pale ulipo ndani ya nchi ya Tanzania.
C. Sikuwa natambua kuwa mapito niliyokuwa napitia katika kituo changu hiki kwa miaka saba nilikuwa najitengenezea jina(Kumbuka baada ya kuona napata changamoto ya walimu) niliamua kuigeuza kituo changu kuwa cha masomo ya sanaa tu yaani HKL, HGL, HGK ambapo masomo yote nimekuwa nikiyafundisha mimi tu kwa miaka yote 7.
Nimekuwa nikifundisha QT masomo matano(Hist, Civ, Geog, Kisw, Engl), Form four wanaoristi masomo sita(Hist, Geog, Kisw,Engl, Civic, Liter) na pia advance(Hkl, Hgl, Hgk). Kutokana na imani waliyonayo Watanzania wengi kuwa mwalimu moja hawezi kufundisha masomo yote nimekuwa na darasa la wanafunzi wachache tu kwa miaka yote hiyo (wanfunzi 10-15) kwa kila darasa. Hii imenijengea heshima kubwa.
D. Kutokana na heshima hiyo nimejikuta nimekuwa pia lecture wa kujitegemea katika ngazi ya chuo kikuu ambapo nafaka mdiaha foundation course, certificate na diploma kwa wanafunzi wanaosoma Open University ( yaan Mimi nimewarisitisha wafanyakazi wengi hasa walimu, mapolisi, manesi n.k) ambao walipofika ngazi ya chuo na kusoma Open University wakanipendekeza kuwa lecture wao huku mtaani. Hivyo Mimi ni lecture wa kitaa japo ndio nimeanza mwaka jana. Hii nina mpango nayo kabambe na bab kubwa miaka miwili ijayo. Ndio ndugu zangu nimeweza kuwa mkufunzi wa kujitegemea licha ya GPA yangu ya 3.4 niliyopata huku wanakoita mlimani.
E. Nimefanikiwa kupata Biashara inayoniingizia faida ya sh. 10,000 kwa siku.
Hii nimefanikiwa mwaka huu mwezi Mei. Hapa ndipo nilikuwa napasubiri ili kuwa bilionea(nitaifanikishaje? Na je ni biashara ipi? Kwa sasa naiweka pending) kumbuka tangu naanza Biashara 2021 ni mwaka huu 2024 mwezi Mei ndio nimefanikiwa kugundua biashara ya kupata faida ya elfu kumi kwa siku. Yaani miaka 4 unaweka hela unaipoteza, unaweka nyingine unapoteza..(chukua hiyo)
F. Nimefanikiwa kuandika vitabu vya biashara katika masomo ya sanaa kuanzia form 1 hadi chuo kikuu. Nimeandika masomo ya English, Kiswah, literature, civics(general study na history( kwa olevel na Alevel) hapa neandika vitabu vya notsi pamoja na reviews). Kwa chuo nimeandika reviews za (Kiswahili, history, English, Development studies, special needs education, communication skills, vocational training for primary school, n.k).
N.B. Vitabu hivi nimeandika kwa miaka 10 hadi sasa (2014-2024)na bado naendelea sijamaliza. Aidha vitabu hivi sijaaviingiza sokoni hadi sasa kwani lengo langu, huu ni urithi nilioamua kuwaaachia watoto wangu hususani(binti yangu) endapo ningeshindwa/nitashindwa kufika nchi ya ahadi. Ni hazina ya watoto. Lakini kama nitafanikiwa kuwa hai nategemea mwaka 2016 kuziingiza sokoni ili kuanza kufaidi matunda ya kazi yangu kabla ya kufika 40 age. Kwa sasa nafanya kuvihariri ili kuendana na mahitaji ya sasa.
G. Katika umri wa miaka 36 na miaka 12 tangu kuhitimu chuo na miaka 9 tangu kuacha kazi na kujiajiri nimefanikiwa kuwa na watu/connection ya watu mbalimbali kupitia kazi ya ualimu. Wanafunzi niliowafundisha baadhi yao wako katika sekta mbalimbali. Wapo polisi, walimu, wafanyabishara, wakulima, wahasibu, madktari, n.k
H. Kwa upande wa familia, yule mdogo wangu wa kiume kwa sasa ni Afisa wa TRA, Dada yangu yule aliyeolewa kwa sasa ni Afisa wa Benki na mama sasa ameanza kuamini katika ndogo zangu na kuiombea sana baada ya kuona dogo yuko TRA. Shida yake kubwa ni kuwa ni kwamba nabii Mwamposa anammalizia hela zake tunazompa ale bata. Kila vijana tukijipanga tukampatia kitu kizuri mfano, nyumba yeye anaamini ni Mungu wa Mwamposa. Hahaha ! Hahaha ! Hajui kuwa hayo ni matunda ya process ya miaka kumi iliyopita. (Kumbuka nilipoamua kuachatu kazi aliamini nimerogwa). Kwa kweli Mungu ambariki tu.
SAFARI YA SITA: 2025-2026
MBELE NI USHINDI KWA IMANI
Ndugu zangu mwaka 2016 kama Mungu atapenda niwe hai nitakuwa na miaka 38. Niliacha kazi nikiwa na miaka 28 so nitakuwa nimetimiza miaka kumi tangu kuacha kazi.
Huu ni mwaka ambao naamini nitakuwa ninafika tamati ya lengu langu kuu la kuingiza milioni 10 kwa mwezi. So nina mapambano bado mzidi kuniombea. Panapo majaliwa nitakuwa nawapa mrejesho mdogo mdogo kuhusu huu uzi wangu. Ila mpaka sasa naamini kuna kitu unaweza kujifunza juu ya Safari yangu hii.
MAFUNZO NILIYOYAPATA MPAKA SASA ILI KUWA MTU WA MAFANIKIO.
a. Kanuni ya WH6.
Hii ni kanuni niliyopata kujifunza katika Safari yangu. Hii imekuwa falsafa yangu juu ya mtu yeyote anayeta kufanikiwa.
i. What? (Unataka nini/kuwa nani?)
ii. Why? (Kwa nini unataka kuwa huyo/hivyo?)
iii. How? (Kwa njia gani/mikakakati gani?)
iv. When?(lini/ muda/ kipindi gani?)
v. Where? (wapi/sehemu/eneo gani?)
vi. Who? (Nani mshirika/ wahusika gani?).
Siku nikipata muda nitakuja kuelezea kiundani
b. Kujitenga/upweke
Ukiwa na ndoto kubwa na ukataka kuifanikisha jiandae kwa upweke na kukataliwa kwanza. Utakuwa mwenye huzuni, maumivu, majeraha n.k. utawapoteza wapendwa(mke/mume, wazazi, watoto n.k) unatakiwa uwe na moyo mkuu.
c. Bidii na akili
Ndugu hapa namaanisha kama sio mchapa kazi usije kuacha kazi. Hapa unatakiwa uwe na nguvu ya kimwili , kiroho na kiakili. Kuwa mtu wa kutumia akili sana na huku unajituma kupita kawaida.
d. Kujikataa/ kujikana
Haloo lazima ujikane, ujikatae kwa kifupi uwe kama kichaa ikibidi. Naamanisha sahau starehe na anasa. Utatamani kula kuku hautaweza, utatamani wanawake wazuri utawala kwa macho tu( siku moja nitaelezea), utatani mavazi mazuri hautaweza. Yaani ni full kujizira. Kahela kadogo unakopata unawaza majukumu au uwekezaji. Ukikaaa vibaya hata kuoga unasahau (hahaha hahaha)
e. Usilaumu watu
Asee usije ukalaumu watu (mke, ndugu, marafiki n.k) kwa nini hawakusapoti, wanakutenga. Hii ilinitesa sana katika safari yangu ya pili mpaka pale Mungu aliponifungua. Ni hivi Mimi niliteseka kwa sababu ya maono niliyoyabeba. Mimi ndio niliamua njia hiyo kwa hivyo mpaka nilipogundua ni machaguzi yangu ndiyo yananitesa hivyo sipaswi kulaumu mtu kwa machaguzi yangu.
f. Maamuzi magumu
Hii kitu nilkuwa naisikia sikia tu wakati nikiwa kijana huko chuoni. Mara ooh Lowasa ana maamuzi magumu. Ndugu yangu ukitaka kufanikiwa lazima uwe mtu wa maamuzi magumu mno. Hapa simaanishi kwenda kwa waganda big No.
Nimaamuzi kweli kweli ( Mfano mdogo kwa upande wangu ni moja, kuamua kuacha kazi, pili, kuamua kuwa mwalimu mbobezi katika masomo yote ya sanaa na kufundisha shule nzima peke yangu). Yapo mengi hii siku nikipata wasaa nitaelezea kwa undani. Yaani ni maamuzi kweli.
g. Amini katika mchakato/process
Mafanikio ni mchakato ndugu. Kuna msemo kuwa "Roma haikujengwa kwa siku moja". Ni kweli kabisa. Amini katika malengo ya muda mrefu na mfupi.
h. Imani yako ndio mafanikio yako.
Unaamini nini kuhusu Mungu(nuru),shetani( giza) na wewe mwenyewe je(uwezo wako). Kwa upande wangu naamini katika nguvu ya Mungu( nuru) na Mimi mwenyewe ( uwezo wangu)
Ninayo mengi sana ya kuandika ila kwa kuwa ndio naanza ngoja niishie hapa kwa leo.
MWISHO
Ndugu zangu wanaJF asanteni sana kwa kusoma maandishi yangu. Mnisamehe kwa bandiko refu sikutaka kuwa na sehemu ya pili. Pia ni uzi wangu wa kwanza hivyo naamini penye makosa mtanirekebisha.
Watakaokwazwa na andiko langu mnisamehe na watakaobarikiwa nayo Mungu awape nguvu. Kwa maswali mtauliza na nitawajibu. Ila kumbuka hapa nimeandika kwa kifupi.
Emma
Tanzania
Jumapili 14. 07.2024
4: 00 AM
Asante kwa hii elimu nimejifunza kituWasalaam,

Kasome wewe vinzuriJamaa kasome upya uzi
Kasome wewe vinzuri
Asante sana mkuu. Barikiwa sanaAsante kwa hii elimu nimejifunza kitu
Aya bhanaKwenye nimesema mwaka huu nina 36.....pia nimesema niliacha kazi mwaka 2015 nikiwa na miaka 27..... Hiyo 2012 unayoisema nimeeleza kuwa ndio mwaka niliomaliza chuo nikiwa na miaka 25....So by 2026 nitakuwa na miaka 38 sio 40 mkuu.
By the way miaka sio ajenda kuu kwenye andiko langu. Lengo kuu la andiko ni kuwapa watu nafasi ya kujifunza kitu kutoka katika mapambano yangu.
Anaweza kujifunza makosa niliyofanya akayarekebisha na kufanya vema zaidi. Pia mwingine anaweza kujifunza ubora wangu na akafanya vema pia.
Samahani sana mkuu kama nitakuwa nimekuudhi.
Asante sana mkuu. Barikiwa sana
Ndio mkuuGrow rich au sio?
Hongera sana. endelea kupambana bila kukata tamaa. penye nia pana njia.Wasalaam,

Mkuu sijasema kuwa nimefanikiwa. Kwenye uzi nimesema watu wajifunze kupitia mimi. Ila nimesema katika kupata hiyo elfu 10 per day na kupitia uzoefu niliopitia miaka 9 nina uhakika wa kuwa Mo. Hiyo ni up to wewe uamini au usiamini but nakuhakikishia nitakuwa Mo. Mpya hapa mjini miaka sio mingi.Bado sijaona point ya utajiri hapa , miaka 7 bado unafundisha mwenyewe kwenye hiyo tuition centre 😁 hapa nilitegemea uniambie una walimu10 ambao unawalipa, , umefanikisha kuipata biashara ya kukuingizia elfu10 Kwa siku na unatupa miaka2 tutakuona level za akina Mo?? Seriously 😃 , huna nyumba, huna kiwanja , huna hata usafiri , then unakuja kuanzisha Uzi wa mafanikio😃😃
Nilichogundua kimoja hukujipanga wakati unacha Kazi urikurupuka Bila kujua nini exactly unaenda kufanya baada ya kuacha Kazi , Milion 3 sio ya kutukana mamba😂😂😂
Mkuu kitu kimoja uelewe ukiwa na maono makubwa ni ngumu sana watu wa kawaida au wenye mawazo madogo kukuelewa...wao wanaona boundaries tu like umri umeenda,, Hela hyo elfu kumi ndogo kwa siku,, sijui hujawah miliki mil 50, mara mawazo hayo hayawezekan.....nkKwenye nimesema mwaka huu nina 36.....pia nimesema niliacha kazi mwaka 2015 nikiwa na miaka 27..... Hiyo 2012 unayoisema nimeeleza kuwa ndio mwaka niliomaliza chuo nikiwa na miaka 25....So by 2026 nitakuwa na miaka 38 sio 40 mkuu.
By the way miaka sio ajenda kuu kwenye andiko langu. Lengo kuu la andiko ni kuwapa watu nafasi ya kujifunza kitu kutoka katika mapambano yangu.
Anaweza kujifunza makosa niliyofanya akayarekebisha na kufanya vema zaidi. Pia mwingine anaweza kujifunza ubora wangu na akafanya vema pia.
Samahani sana mkuu kama nitakuwa nimekuudhi.
Asante sana mkuu. Barikiwa sana
Awali ya yote nasema nimejitahidi kusoma uzi wote na kunameng sana.
Nikupe pole kwa yote magumu na changamoto ulizopitia.
Pongezi kwa uthubutu uloufanya.
Mengi ya kujifunza yako hapa
Asante sana mkuu kwa kuelewa kusudi la bandiko langu na kunitia moyo. Ushauri wako wa maombi usiku nitafanyia kazi vema. Asante sanaMkuu kitu kimoja uelewe ukiwa na maono makubwa ni ngumu sana watu wa kawaida au wenye mawazo madogo kukuelewa...wao wanaona boundaries tu like umri umeenda,, Hela hyo elfu kumi ndogo kwa siku,, sijui hujawah miliki mil 50, mara mawazo hayo hayawezekan.....nk
But ww keep focused na ulichopanga..watu wa hvo wapo kila sehem hata mm walinisumbua sana kipind naanza biashara na kuachana na mamb ya kuajiriwa..
All in all usisahau ibada kwa iman Yako ..amka usiku saa nane pakiwa tulivu jiconect na holy power daily,,mamb yatafunguka kwa uraisi zaid..
I pray for you comred!!
DuhNa hii ndio plan yangu
Mkopo huu ukiisha kwa daraja nililionalo nitakuwa na uwezo wa kukopa mil 45.
Wakati huo ukifika, nakopa halafu NAPOTEA mazimaaaaaa.
#YNWA
Nikwele kabisaMimi naamini mafanikio aliyonayo sasa ni sababu ya kuwa mwema na kusaidia watu wake wa karibu tena wakati anajitafuta ...