greater than
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 973
- 1,610
MAKALA YA 9
Leo tuangazie janga ambalo limekuwa likitokea katika nchi yetu kila baada ya miaka kadhaa. Kuanguka kwa Majengo1.Sababu kuu za Kuanguka kwa Majengo ni kama zifuatazo
MSINGI WA JENGO KUWA DHAIFU
- Tabia za ardhi za maeneo/Miji na mitaa hutofautiana.
- Maeneo ya kutuwamisha maji,Mfinyanzi huitaji msingi imara zaidi.
- Lakini kwa kukwepa gharama wala haifanyiki hivyo
- Jengo la ghorofa 4,mjini Kigali Rwanda ,liliporomoka kisa udhaifu wa msingi.
- Kutumia Nondo ,Nyaya za kufunga zisizo na ubora.
- Utumizi wa matofali,mabovu,mchanga wenye chumvi,kokoto zenye alkali.
- Jengo la ghorofa 6,Jijini Kampala lilianguka kisa utumizi wa matilio mbovu.
- Unakuta Ghorofa lilitakiwa Liwe na floor 4,Ila kwa tamaa tu,mmiliki anaamuru liwe la ghorofa 6.
- Hapa hatakama Msingi ulijengwa vizuri,utaelemewa na kuangusha Jengo.
- Jengo la Ghorofa ,Mtaa wa Indira Gandhi, lilianguka kisa hiki.
- Jengo lilikuwa la Ghorofa 12,mmiliki Bwana RAZA DAMJI akaamuru na kuhonga na kuongeza ghorofa zingine 4.
- Sheria zinataka Majengo yote yawe yanafanyiwa ukaguzi na vipimo katika kila hatua ya ujenzi
- Maghorofa mengi ya Kigamboni,Goba,Makabe,Chanika,Buyuni,Pugu, Toangoma hayafanyiwi ukaguzi.
- Mjenzi hutakiwa kuwasilisha sample ya zege kwenye ofisi za viwango,lakini haifanyiki hivyo
- Wakaguzi wa ujenzi kutoka manispaa, huenda site kupata hongo na kuondoka .
- Mteja anapakua Ramani mtandaoni anapita njia za panya kugonga muhuli na kupata kibali
- Ramani haijafanyiwa tathmini ya mfumo wa mhimili/structure
- Anampa kazi fundi,
- Jengo Laanza kujengwa bila hata kuwa na sanifu ya mhimili
- Aisee,siyo kila jengo huwa na aina sawa ya msingi
- Siyo kila jengo nguzo zitaachana kwa mita 4 au 5
- Jengo la ghorofa 1,Goba kwa awadhi lilianguka kisa hiki.
- Hapa Mtaalam/Fundi,wanaingia tamaa ,wanaanza kuiba matilio za ujenzi
- Wanabadilisha viwango vya ujenzi
- Utumizi wa vifaa duni vya kazi
- Kuwaisha ujenzi bila kujali ubora wa kinachojengwa.
- Zanzibar na Bagamoyo ndiyo wahanga wa Kipengele hiki.
- Hiji miji mikongwe, majengo yake mengi ni yana zaidi ya miaka 100.
- Hayafanyiwi ukarabati wa kutosha
- Yanakuja yanaagnuka yenyewe
8. Nini kifanyike kuondokana na Janga hili
- Mteja kusanifiwa Ramani yenye kuendana na eneo lake
- Kuandaliwa na nyara za mhimili
- Ujenzi ufanyike kwa kufuata viwango
- Wakaguzi wajitume na kufuata sheria
- Wato kutoishi katika magofu
- Kutakuwa na Tamaa
- Sheria na Taratibu zifuatwe katika hatua za ujenzi
-umakini wahitajika
10.Hata ukitumia fundi,basi tafuta mtaalam awe anakuja kukagua Ujenzi katika kila hatua kubwa ya Ujenzi,,,ole miaka minne/mitano ya shule usichukulie poa.....
Kwa yule mwenye huitaji wa ukaguzi wa jengo lake. Mwenye shaka juu ya tatizo lolote la jengo lake,asisiste kuwasiliana. Wahi kabla ya mwezi wa 5 kuingia
Nakaribisha maswali na Maoni.....