Sababu gani zilizo fanya kuanguka kwa Jamhuri ya watu wa Giningi?

Feb 13, 2024
63
151
Jamuhuri ya watu wa Giningi inasemekana ilianguka bahada ya Bibi Kilembwe kuingia madarakani, inasemekana mara bahada ya Bibi Kilembwe kuikamata ikulu ya Giningi ndipo alipofungua kucha zake mwanzo watu walikua na matumaini makubwa sana na huyu bibi.

Bibi Kilembwe alianza kwa kuwalisha wanaginingi unga wa ndele, unga huu unasemekana ulikua na nguvu ya kuwageuza vijana wa Giningi na kua machawa, hivyo vijana wa Giningi wakawa waimbaji wa mapambio ya kumsifu Bibi Kilembwe, inasemekana unga huu wa ndele ulikua na uwezo wa kuwapumbaza wananchi wa Giningi kiasi kwamba ukweli waliuona kama uongo na uongo ndio ukawa ukweli.

Inasemekana Bibi Kilembwe alipenda sana kusafiri kwenda kwenye nchi za wenzake, na gharama za ziara zake zilitokana na fedha za walipa kodi wa Giningi, japo Bibi Kilembwe alisafiri nchi mbalimbali hapa duniani na kujionea maendeleo makubwa yaliyofikiwa na hizo nchi alizozitembelea lakini Bibi Kilembwe hakuona kitu chochote cha kujifunza bali alichofurahi ni kuona vizawadi alivyopewa katika ziara hizo.

Zawadi alizopewa bibi Kilembwe zilifanya bibi Kilembwe kuanza kuuza rasilimali za wanaginingi kama mbuga za wanyama na bandari ili tu kulipa fadhira ya zawadi alizozipokea kutoka kwenye ziara zake alizozifanya Bibi Kilembwe.

Leo nimekumbuka mambo ya fasihi, hiki kitabu kilikua poa sana, kinaitwa kivuli kinaishi.
 
Jamani hii Hekaya ya Giningi nimeikumbuka nimelia sana hapa nilipo🥺
 
Back
Top Bottom