Side Makini Entertainer
Member
- Jan 19, 2020
- 37
- 76
Mungu yupo na sababu za kuamini zipo. Sababu zimeandikwa mbinguni na duniani kwa herufi kubwa kiasi kwamba kila aaminiye aweza kuzisoma; nimesema, kila aaminiye aweza kuzisoma. Nikwambie mapema, sina ushahidi wa kumthibitishia asiyeamini uwepo wa Mungu hata asiweze kuutafsiri vinginevyo; kama vile nisivyoweza kumwaminisha asiyetaka kuniamini ninampenda hata asiweze kunichukulia tofauti. Katika mahusiano ya kuamini na kuaminia (iwe Mungu au mtu), imani hutangulia ushahidi jinsi msingi unavyoanza chini kabla ya nyumba kuja juu yake. Pasipo msingi wa imani hakuna ushahidi unaosimama. Katika ulimwengu wa asili zipo alama za mikono ya Mbunifu zinazoonesha uumbaji umebuniwa kwa kusudi na haukuibuka kwa bahati. Unataka uzione? Kwa ufupi wa wakati na udogo wa nafasi, niruhusu nikuoneshe kumi tu. Hizi hapa.
1. Kilichoanza huanzishwa na Muanzilishi
Kila kitu ulimwenguni kina mwanzo ulioanzishwa. Aya hii ipo hapa kwa kuwa mwandishi alimwaga wino juu ya ukurasa huu. Nani aliye hai ambaye hakupokea uhai toka kwa wazazi? Ni mama yupi anayepasisha kwa wanawe uhai ambao hakuupokea kutoka kwa waliomtangulia? Mwanzoni mwa mapokezano hayo ya uhai yupo nani kama si Yeye Aliye na uzima, uzima usio wa kupewa au kuazimwa? Pasipo Mwenye-kitabu hakuna kitabu cha kuazimwa. Tuna uhai wa kuazimwa kwa kuwa yupo Mwenye uhai aliyetuazima. Yeye daima “hapatikani na mauti” (1Tim 6:16); na “ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu”
(Matendo 17:28)
2. Mabadiliko huletwa na Mbadilishaji
Vitu vyote hubadilika: iwe mata (matter) au nguvu (energy), wakati (time) au nafasi (space). Mwenye hekima mmoja alisema vizuri, ‘hakuna kisichobadilika isipokuwa badiliko lenyewe.” Kwa kutazama kwa macho au darubini, vitu vina uwezekano wa kubadilika na si uwezo wa kubadilika. Mchanga huhamishwa na upepo na ua ukaushwa na jua. Uwezo wa kubadilika hutoka nje ya kitu husika. Kwa kuwa ulimwengu katika ujumla wake unabadilika, basi yupo Mleta-mabadiliko nyuma yake. Kama hayupo Mbadilishaji basi ulimwengu ungebakia ulivyokua daima. Mleta-Mabadiliko Mkuu wa ulimwengu yupo, yeye habadilishwi na habadiliki. Biblia inamtaja huyo kama,”Baba wa mianga; [ambaye] kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka” (Yakobo 1:17; lingasha na Malaki 3:6; Waebrania 3:18; Zaburi 102:24-27)
3. Sanaa humtangaza Msanii
Ulimwengu ni sanaa iliyobuniwa. Tupia macho nyota za angani au maua ya kondeni. Ni nini mbele yako? Si uzuri huo? Aidhaa uzuri huo umebuniwa na mbuni aliyejipanga au umeibuliwa na mlipuko usiokusudiwa (wanafizikia wauita, “big bang”). Lakini, iweje mlipuko usiopangilika uzue maumbile yaliyopangilika? Waweza kuamini herufi hizi usoni mwako ni matokeo ya wino uliojimwagikia badala ya binadamu aliyefikiria? Daima, sanaa hubuniwa na kubakia mali halali ya msanii. Kufurahia uvumbuzi na kutomtambua mvumbuzi ni nini kama si ubakaji wa sanaa, ukatili kwa msanii, na ukiukwaji wa haki ya msanii kutambulika? “Kwa sababu mambo yake [Mungu]….yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru” (Warumi 1:20
4. Hali ya kutambua/ kutambulika yatoka kwa Mwasisi-Mtambuzi
Ulimwengu uliobuniwa unatambulika. Kilimanjaro ya theluji au ngorongoro ya kijani yatambulika kwa macho. Ijapokuwa tunautambua ulimwengu lakini wenyewe haujitambui. Mata (matter) na nguvu (energy), mwamba na umeme, kompyuta na roboti havijitambui. Havina utambuzi wa nafsi. Haviwezi kutambua nafsini kwa kufikiri, kusikiliza, kukumbuka, kuongea, kuhisi, kuhiari, na hapo hapo kung’amua walichokitambua. Mwanadamu anatoa wapi utambuzi huo? Kama gesi iliyojilipukia (“big bang”) ilizua wanadamu wenye utambuzi, iweje chanzo kisichojitambua (mlipuko) kitofautiane na zao lake linalojitambua (mtu)? Hakika, wanadamu wenye ufahamu wametoka kwa Muumba mwenye-ufahamu. Mtu anamtambua Muumba na Muumba anamtambua mtu—wawili wanafahamiana hata kama wachukua muda kujuana. Mungu ndiye “akiisha kuwawekea walimwengu nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.” (Matendo 17:26b,27)
5. Wazo lenyewe linaakisi uhalisia wake
Wanadamu wote wanamuwazia Mungu. Waumini, wasioamini, au wanaodai hawajui kuwa Mungu yupo huwa wanachukua msimamo wao baada ya kuingiwa na kupambana na wazo lenyewe. Lakini, wazo linatua kichwani likitokea wapi? Aidha wazo limetoka ndani ya mtu au nje. Tujuavyo, chanzo huwa kikuu kupita matokeo yake (Mjapani ni mkuu kuliko Toyota). Kwa kuwa “Mungu” wa vichwani mwao hufikiriwa kuwa mkuu (katika wema, uweza na busara) kuliko yeyote wanayemjua (kuliko baba au mama), basi dhana ya uwepo wa Mungu ni akisi ya uhalisia uliopo nje ya vichwa vyao. Dhana haikuibuka vichwani mwao kama uyoga. Kutoka nje, Mungu ameweka, “milele ndani ya mioyo” yao. Ndiyo maana, pamoja na mahangaiko ya kitambo na wakati uliopo, kwa kujua au kutokujua, watu wote huangaikia umilele, hatima yao baada ya maisha yao duniani (Mhubiri 3:11; Matendo 17:26,27).
6. Usemi ‘Mungu yupo’ hudai uwepo wa Mungu
Usemi wowote uletao maana hupangika kisarufi bila kugongana kimantiki. “Duara ni pembe tatu” Sarufi? Sawa. Maana? Hakuna. “Mungu hayupo” huangukia hukumu hiyo hiyo. Vichwani mwetu, “Mungu” ni Yeye astahiliye kuabudiwa kwa kuwa ni Mkamilifu katika uweza na uadilifu. “Mungu” ataitwa Mungu kwa kuwa yupo. Mrembo aliyeko kwenye jeneza si mrembo, na “Mungu” asiyekuwepo si “Mungu.” Kusema, ‘”Mungu” hayupo’ ni kumhesabu Aliye hai miongoni mwa wasio hai. Mtu huthubutu vipi kusema “Mungu hayupo” kama hajateleza ulimi pasipo kujitambua? (Zaburi 51:1-2;14:1-2). “Duara ni nyuzi 360” na “Mungu yupo” ni tungo mbili sahii kwa muundo na maana zake.
7. Kufahamika kwa maadili hutangaza Mtunzi wake
Yapo maadili-msingi yanayotambuliwa na watu wa kila zama na kila mahali. Japo wanaishi mbele ya utisho wa kutoweka na kila huyo akipambana abakie, watu wote wanajua nafsini mwao kutunza uhai wa wengine ni muhimu kuliko kuupoteza, kuonesha huruma ni bora kuliko ukatili, urafiki kuliko usaliti. Wanaafiki heshima yafaa kuliko dharau, ushujaa kuliko woga, bidii kuliko uvivu, ukweli kuliko uongo, kutakiana heri kuliko kuoneana wivu, na kuridhika kuliko kutamani. Kufahamika kwa maadili yanayofanana ulimwengu kote ni uthibitisho wa uwepo wa mtunzi wake mmoja. Baba wa mema yote amewaachia wanadamu kanuni 10 za namna ya kuishi na akaziandika kwa wino usiofutika (Kutoka 20; Warumi 2:14,15). Maadili ya Bwana Mungu hutia mjinga hekima na kumpatia raha moyoni. Sheria yake ni kweli na haki. Tena ni tamu kuliko asali na hutamanika kuliko dhahabu safi (Zaburi 19:7-14). Kwa nini kizuri kisijitangaze?
8. Sauti ya dhamira inayohukumu ushuhudia hakimu anayehukumu
Tofauti na wanyama, mwanadamu mwenye ufahamu ana dhamira inayomsonda au “sauti ndogo” nafisini. Sauti hii hujuza mema (“fanya hivi”) na mabaya (“usifanye hivyo”). Kama ladha ilivyo kwa vyakula ndivyo dhamira ilivyo kwa maadili. Dhamira uhukumu: umtetea mtu na kumletea amani; pengine, umshutumu na kumletea huzuni. Hata isemaje, watu wote hukubali ni vema kutii dhamira yako. Lakini, dhamira imepata wapi mamlaka hayo ya kusikilizwa? Kutoka maumbile yangu asilia? Iweje asili iliyo chini yangu inikalie? Iweje nihuzunike ninapoiasi ikiwa mimi ndiye niliyeitunga? Kama imepewa mamlaka na jamii iliyonilea, iweje wana jamii walio sawa nami wawe juu yangu? Ni nani aliye na sauti ya mwisho kunipeleleza niliye chini, halafu kuniruhusu au kunikataza kabla sijatenda, kunitetea au kunishtaki baada ya kutenda? Hakika, “pumzi [neshamah kiebrania, au roho, dhamira,] ya mwanadamu ni taa ya Bwana; hupeleleza yote yaliyomo ndani yake” (Mithali 20:27)
9. Tamaa ya asili hutimizwa na kitu halisi
Kila hitaji asilia hutimizwa na kitu halisia. Njaa huzimwa na chakula. Upweke humalizwa na mpenzi. Kwa kila haja ya kimambile lipo jibu nje ya maumbile husika. Lakini ipo tamaa ya kibinadamu isiyoweza kutoshelezwa na mazingira ya mwanadamu. Elimu ya kidunia na ajira mali na madaraka na mapenzi haviwezi kukidhi haja hiyo. Nani asiyetamani kufurahia ua lisilonyauka, muziki usiochuja, na upendo usiopoa. Nani hana hamu ya kukutana na rafiki pasipo kuagana, kucheka pasipo kulia, na kuzaliwa pasipo kufa? Nani asiyependa kuongea na kusikilizwa, kugusa na kuguswa, kujua na kujulikana, na kupenda na kupendwa. Shauku ya kufaidi uzima katika ukamilifu wake ni kiu halisi ya ulimwengu huu na utimizo wake hupatikana katika uhalisia wake nje ya ulimwengu. Zaidi ya ulimwengu upo uhalisia, Mungu Baba halisi, utimilifu wa tamaa ya vizazi vyote. “Kila kipaji chema na kila zawadi kamilifu hutoka mbinguni; hutoka kwa Baba, Muumba wa mianga,…” (Yakobo 1:17)
10. Uzoefu wa wengi ni ushuhuda wa nguvu
Historia na anthropolojia hushuhudia kuwa uzoefu wa dini ni wa kiulimwengu. Watu wa kila zama na tamaduni wamedai kuwa na uzoefu na “Uungu.” Wamemkaribia “Mungu” kwa kusujudu, kuheshimu, kusifu, na kushukuru. Je! Yawezekana waabudu wote hao wanainama kiti kilicho tupu? Kwamba uzoefu wanaoujua sio halisia? Kweli, hapo kale walimwengu wengi walijua kimakosa kuwa jua linaizunguka dunia. Lakini uzoefu wao ulikuwa sahii. Kwa uzoefu walijua bila kukosea kuwa jua lipo, dunia ipo na mzunguko upo. Huenda waabudu wakakosea kujua Mungu yukoje, lakini haiwezekani wakakosea kujua yupo. Ikiwa wengine hawajui uzoefu unaojulikana sana, huenda shida ni mishipa ya fahamu, mishipa iliyopoteza uwezo wake wa kuhisi na kujua. “Kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.” (Warumi 1:21)
Hauko mwenyewe kama ungali unasita kuamini Mungu yupo. Lakini ikiwa yupo, Mungu aliye na uwezo wote na wema wote, basi utajiumiza mwenyewe usipomwamini. Ukimkataa, utakuwa unakataa uzima na upendo.
Wapo waliotafuta kumjua Mungu na kumpata; wakawa na hekima na furaha. Wapo waliotafuta kumjua na kumkosa; wakaonekana wana “hekima” lakini hawana furaha. Na wapo wasiomtafuta na wamepungukiwa hekima na furaha. Kuamini ni kuchagua. Ikiwa utachagua kuamini Mungu yupo, uwezekano wa kupata maana ya maisha upo. Yesu Kristo amekwisha sema, “tafuteni, nanyi mtaona” (Mathayo 7:7).
Kama unataka kumjua Mungu binafsi, lakini unaona woga, waweza kuomba ombi hili: “Mungu, sijui kama unaishi au la, lakini kama upo, tafadhali jifunue kwangu jinsi ulivyo.”
Hongera, ombi lako limesikiwa! Mungu amekwisha anza kujifunua kwako! Ili kupata masomo yanayofungua macho kwa ufunuo wa Mungu, tembelea daima Majaliwa Majaliwa. au tuma ujumbe mfupi (SMS) kwa 0783235234 (Whatsapp).