Jacob kalokola
JF-Expert Member
- Mar 26, 2022
- 884
- 2,713
Wakishilikiana na Kagame kuhujumu Taifa? Sijaelewa.Chadema ya Dr Slaa ilisimama na Kagame wakati Afande Jakaya alipokuwa anawashughulikia M23 kule Congo
Wakishilikiana na Kagame kuhujumu Taifa? Sijaelewa.Chadema ya Dr Slaa ilisimama na Kagame wakati Afande Jakaya alipokuwa anawashughulikia M23 kule Congo
Col. Mamadou Mustafa Ndala, huyu alikuwa kamanda wankikosi cha makomandoo.Walidai alipigwa ambush na M-23 lkn utata ni kuwa eneo alilokuwa lilikuwa ni mbali zaidi na walipo waasi (Km 156)
Maafisa aliowaacha waliouwawa ni 11 kwenye mazingira tata sasa
Muhusika inahisiwa ni vigogo walio ndani ya jeshi
Umeeleza vizuri Sana,wakubwa wake ndio walimuua mamadou Ndala.Col. Mamadou Mustafa Ndala, huyu alikuwa kamanda wankikosi cha makomandoo.
Huyu alizaliwa mwaka 1978 mpaka umauti unamkuta alikuwa na miaka 35. Kifo chake kilileta simanzi miongoni mwa wananchi waliokuwa wakisumbuliwa na uvamizi wa makundi kadhaa ya wahuni ikiwamo m23.
Huyu mwamba anakumbukwa sana miongoni mwa raia na wanajeshi wenzake Kwa akili kubwa ya kumsoma adui na kukabiliana naye bila uoga.
Mwaka 2013 wakati Rwanda ikiwaunga mkono m23 , aliekuwa mkuu wa majeshi wa Rwanda wakati huo gen. James Kabarebe aliwahi kuwafananisha FARDC na jeshi dhaifu ambalo haliwezi kuuwa hata panya.
Katika mapigano yaliyoanza mei 2013 maeneo ya Kibumba na Rutshuru Col Ndara akisaidiana na vikosi vya walinda Amani wa MONUSCO aliweza kuwalaza chini askari 721 wa m23 huku akikamata mateka 541 upande wa adui.
Kwa upande wake na walinda amani wa MONUSCO FARDC walipoteza askari 201 na 608 majerui ambapo walinda amani 3 wa MONUSCO pia walipoteza maisha.
Baada ya mission hii kukamilika, rais Kabila alimrudisha col Ndara Kinshasa.
Mwaka 2014 Januari, Ndala alipelekwa Jimbo la kivu kaskazini mji wa Beni Kwa lengo la kuendesha operation ya kuangamizi makundi mengine yaliyokuwa yanatishia usalama wa maeneo hayo na wakazi husika.
Akiwa amewahaidi wananchi wa Beni kuwasambaratisha makundi hayo popote walipo, alfajiri ya tarehe 2 January 2014 wakati akielekea msituni kuwasaka waasi mara ghafla gari lake la kivita lilipigwa roketi na kumwangamiza kamanda Ndala na askari wake kadhaa.
Msafara ulishambuliwa na waasi wa ADF-Nalu wenye mafungamano na Uganda.
Baada ya kifo cha Col Ndala, mapfisa kadhaa wa vyeo vya juu ndaninya FARDC walifunguliwa kesi ya mauaji ya col Ndala Kwa tuhuma za kupokea rushwa ya kiasi cha Dola za kimarekani 20,000 ambapo waliuza taarifa zilizosababisha mauaji ya col Ndala.
Kifo cha Ndala kilipokelewa Kwa majonzi makubwa miongoni mwa raia. Marehemu aliacha make na watoto 3.
Waźipìge tu. PENGINE itakuwa mwisho wà Kagame na Museveni na TshisekediRwanda imetuma wanajeshi kwenye mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, saa chache baada ya DRC kumfukuza balozi wa Rwanda kwa madai ya DRC kwamba serikali ya rais Paul Kagame inawaunga mkono waasi wa M23.
Msemaji wa serikali ya Rwanda, Alain Mukurarinda amesema kwamba “wakiamua kutangaza vita dhidi ya Rwanda, nasi tupo tayari kuchukua hatua kali, maana hata sasa wanapoendelea kuchukua hatua kama hizo, haina maana kwamba Rwanda imelala usingizi mzito.”
Taarifa ya Serikali ya Rwanda ilisema kwamba ‘inasikitishwa na hatua ya DRC kumfukuza balozi Vincent Karega.”
Taarifa hiyo imeendelea kusema kwamba “wanajeshi wa Rwanda wameimarisha usalama kwenye mpaka na DRC na wanaendelea kufuatilia hali ilivyo nchini DRC” kufuatia mapigano makali kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa Serikali.
Baraza la ulinzi la DRC linaloongozwa na Rais Felix Tshisekedi, lilimuamuru balozi wa Rwanda kuondoka nchini humo ndani ya muda wa saa 48, kufuatia ripoti kwamba Rwanda ilikuwa imetuma kikosi maalum cha kijeshi kuwasaidia waasi wa M23 katika sehemu za Kivu Kaskazini, Mashariki mwa DRC.
Ripoti za DRC pia zinadai kwamba Rwanda imetuma wanajeshi katika wilaya ya Rubavu, mpakani na DRC kuwasaidia waasi wa M23.
Rwanda imekuwa ikikanusha kila mara, ripoti za kusaidia waasi wa M23 na kusisitiza kwamba kinachoendelea DRC ni swala la usalama wa ndani ambalo lazima lishughulikiwe na serikali ya Kinshasa.
Madai ya serikali ya Rwanda
Rais wa Rwanda Paul Kagame
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, msemaji wa serikali ya Rwanda amesema kwamba “ushirikiano unaendelea kati ya jeshi la DRC na waasi wa FDLR, na jaribio lao la kulenga sehemu za mpakani na Rwanda kwa mashambulizi na kueneza habari za chuki kuhusu Rwanda.”
Rais wa DRC Felix Tshisekedi Tshisekedi ameamuru maafisa wa usalama kuhakikisha kwamba raia wa Rwanda wasiingie DRC, huku Rwanda ikitaka raia wake kutokwenda DRC.
“Mimi kama msemaji wa serikali ya Rwanda, nawashauri raia wa Rwanda kufikiria mara mbili kabla ya kuingia DRC,” amesema Alain Mukurarinda, msemaji wa serikali ya Rwanda.
Tshisekedi anatarajiwa kulihutubia taifa kuhusu uhasama kati ya DRC na Rwanda na mapigano ya M23.
Hivi karibuni, Tshisekedi alifanya mabadiliko makubwa katika uongozi wa jeshi la DRC na kutuma idadi kubwa ya wanajeshi na silaha katika sehemu za Kivu Kaskazini, kupigana na kundi la waasi la M23.
Mashambulizi ya M23
Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa walijeruhiwa Jumamosi kutokana na shambulizi la kundi la waasi wa M23 katika sehemu ya Kiwanja, Rutshuru, Kivu Kaskazini.
Waasi wa M23 wamekataa kuondoka mji wa Bunagana licha ya viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwataka kuondoka sehemu hiyo na kuacha mapigano.
source: Voice of America
Ustadi wa Ndala kuongoza mapigano Kwa weledi na ustadi wa hali ya juu vilimjengea Imani na ushawishi miongoni mwa raia na askari wa bataliani ya 42 ambayo ilikuwa ni kikosi cha makomandoo aliyokuwa akiongoza licha ya umri wake mdogo hivyo viongozi wakubwa wakaanza kupata hofu juu ya mustakabali wao wa siku za usoni.Umeeleza vizuri Sana,wakubwa wake ndio walimuua mamadou Ndala.
Hawakumpenda.
Hiyo Nchi haina suluhisho waache wapigane tu huku wakicheza sebene.
Maana ni vitu wanavyopenda.
Kabila alihusika kwa asilimia zote hata sio watu wa Western.Ustadi wa Ndala kuongoza mapigano Kwa weledi na ustadi wa hali ya juu vilimjengea Imani na ushawishi miongoni mwa raia na askari wa bataliani ya 42 ambayo ilikuwa ni kikosi cha makomandoo aliyokuwa akiongoza licha ya umri wake mdogo hivyo viongozi wakubwa wakaanza kupata hofu juu ya mustakabali wao wa siku za usoni.
Mara kadhaa Ndala alihusika pande za Kivu kutuliza uasi wa raia dhidi ya majeshi ya MONUSCO ambayo raia walitaka waondoke na kurejea kwao Kwa tuhuma za kushindwa kupambana na waasi.
Wakati diplomasia za serikali ziligoma,raia walimsikiliza na kumwelewa col Ndala na hivyo wakaacha kuwatishia walinda amani hao. Wakati raia wakiandamana mitaani Kwa hasira dhidi ya walinda amani wa MONUSCO,Col Mamadou Ndala alipata habari hizo na msafara wake wakawakaribia waandamanaji wenye hasira, col Ndala alishuka kwenye gari na kuwaendea waandamanaji wenye hasira, walipomwona kuwa ni yeye wakampokea kwa vifijo wakipiga kelele za furaha Mamadou.....Mamadou! Mwamba akawatuliza akawaachia na tabasamu na vicheko.
Mwakilishi wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa na kiongozi wa MONUSCO nchini DRC bwana Martin Kobler tayari alishatengeneza mafungamano ya karibu na col Ndala kuliko Maafisa wengine waandamizi kwenye jeshi la Congo kutokana na umahiri, na unyumbulifu wa Ndala killa alipo hitajika kukabili tishio lolote la usalama katika eneo.
Baada ya m23 kufurushwa, Ndala alirudishwa Kinshasa na rais Joseph Kabila. Baada ya mabadiliko hayo wananchi waliandamana waakiishutumu serikali kutaka kumdhoofisha Ndala lakini pia lengo la serikali kutoa fursa Kwa makundi ya kuhuni kunawili mashariki mwa DRC.
Ni ukweli ulio wazi kuwa mauaji ya Col Mamadou Ndala yalitengenezwa na viongozi wake ambao kimsingi wengi wao ni vibaraka wa mataifa ya nje yanayonufaika na mgogoro mashariki mwa DRC.
Wakati wa mazishi yake serikali ilimtunukia cheo cha Brig.Gen kwa kuheshimu mchango wake wa ulinzi wa nchi ya DRC.
Baada ya kifo cha Ndala Congo ilishuhudia maandamano makubwa ya raia na wanasiasa wakipinga mauaji ya Ndala huku hali ya usalama mashariki mwa Congo ikizidi kuwa tete kutokana na kushamiri Kwa harakati za makundi ya waasi na mauaji ya raia wasio na hatia.