Ruge ni mnyonyaji au mponyaji?

Bigbootylover

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
2,847
1,826
Ni muda sasa nimekuwa nikimsikia huyu jamaa hasa katika upande wa kuchukiwa, watu wanalalamika anawanyonya, anatembea na watangazaji wa redio yake wa kike n.k.

Juzijuzi hapa nikaja kumsikiliza akiwa katika kipindi cha mkasi na kutokana na kujieleza kwake me niliona kama jamaa hana makosa kama baadhi ya watu wanavyomsema, leo pia katoka kuongelea FURSA KUMI ambazo mtu yoyote anaweza kuzifanya hapa nchini kwetu na mtu akatoka kimaisha.

Binafsi nikimuangalia huyu jamaa naona ni mzalendo na taifa lake, anapenda watu wafanikiwe n.k lakini nikisikiliza story za watu nasikia huyu Jamaa sio mzuri, ni mpigaji.

Kwako unamchukuliaje huyu Jamaa MNYONYAJI AU MPONYAJI
 
Wengine hukilalamikia kituo chake kwamba ni cha kinyonyaji kumbuka album za ant virus

Hizo lawama mimi huwa sizichukulii kimaanani kivile kwa sababu hakuna sehemu ya kazi, biashara, au shughuli nyingine yoyote ihusishayo idadi kubwa ya watu halafu pakosekane lawama.

Lawama na manung'uniko ni mambo ambayo huja na kwenda na mazingira yake.
 
Kwani mishahara ikoje kina mchomvu wanalipwaje?tuanzie hapo...nakipanya aliondokaje hapo vile?

Tukumbushane tu. Na wale wasanii wa fiesta hivi huwa mikataba yao na bank receipt deposit huwa ni bei gani vile?

Na Ladjaydee sugu naye vipi? Vipi zile mixtape za DJ Choka bado zinagongwa kituoni pale mawingu?
 
Hajawahi kuajiriwa? Kwani Clouds anafanya nini hapo?

ni mmojawapo ya wamiliki.. ruge nilisikia interview yake baada ya kutoka chuo usa miaka ya 90.. san diego state univeristy sijui akarudi fasta na wazo la kuanzisha entertainment radio ndipo akashirikiana na rafiki yake kusaga kuanzisha clouds.. kusaga akichangia mtaji na ruge akachangia mtaji na akili ya ku manage biashara hiyo mpya aliyoipata chuoni usa....

kwa uzinzi na uhuni wa ruge kufukuza watu kazi... ingekuwa ameajiriwa na kusaga nae si angefukuzwa kazi... ila yeye ndio bosss... hakuna wa kumfanya chochote clouds... anafanya anachotaka..

kuna siku alisema hakuna kupiga bongo fleva clouds siku nzima... na haikupigwa kweli
 
Ruge Ni mtu WA media, ukiacha radio presenter watu ambao wanamjua Ruge vizuri Ni wasanii, all in all Ruge sio mtu mzuri! Unategea afanye interviews then aseme mabaya yake? Keshaiba Sana idea za watu, keshaharibu Sana ndoto za vijana, keshaua Sana vipaji vya watu, kawadhulumu sanna wasanii! Kuna kipindi ilikua ukiwa Na idea washirikishe clouds itatoka, hata ingeenda lets say kwenye kampun x kwamba idea yako inawahusu, wangekwambia nenda clouds kamuone Ruge, akiwa interesting kushirikiana Na ww! Wao Kama kampun x wapo tayari.....hapo ndo watu walipokua wanapigwa Na Ruge, baada ya cku moja idea ishakua yake! Kipindi hicho COSOTA haina lolote!
 
Watu kama, mapacha, dany msimamo, rama D, mkoloni, na yule Raisi wa mbeya wana mifano + antivirus volume zote.. Na asingesolve mapema ule mgogoro habari zake zote zingeisha.
 
Ulivyoongea vingi vina ukweli ila unakosea hapo unaposema Ruge ni moja wa wamiliki wa Clouds, ukweli ni kwamba Ruge Hana umiliki wowote, sema yeye Ndio 'mastermind', Kusaga Hana uthubutu wa kumfukuza kwakuwa Ruge Ndio kichwa, bila Ruge Clouds isingeweza kufika pale ilipo, so Kusaga anajua athari za kumfukuza Ndio maana hawezi kufanya hivyo hata Kama haendi Sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…