Bwana Mohamed,nakupongeza sana kwa kufichua historia ya ukweli,hakika muda ni mwalimu mzuri......Leo tumepata waziri anayeienzi historia ya kweli ya wapigania uhuru akiwamo bibi titi,
Bila shaka Kuna siku tutampata rais atayeenzi historia ya kweli ya wapigamia uhuru
Rozela,
Hakika Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni Baba wa Taifa.
Ikiwa wengine waliopigania uhuru huwatambui hii ni bahati mbaya sana.
Mathalan ikiwa huwatambui wale waasisi tisa walioasisi African Association mwaka wa 1929 huu ni msiba kwani TANU iliasisiwa kutokana na African Association.
Waasisi wa African Association ni hawa: Cecil Matola (President), Kleist Abdallah Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Suleiman Majisu, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Rawson Watts na Raikes Kusi.
Huu ni mfano mfupi lakini ikiwa wewe huwatambui wazalendo hawa historia ya Tanganyika inawatambua.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.