Roman Abramovich Mmiliki wa Klabu ya Chelsea Ahamia Israel na Kupewa Uraia

African Believer

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
436
426
501990446.jpg

Kufuatia mgogoro kati ya Uingereza na Urusi uliotokana na jaribio la kuuwawa kwa kachero wa Kisuri, Sergei Skripal na binti yake Yulia, ambapo Uingereza iliituhumu Urusi kuhusika na jaribio hilo hivyo kuamua kufukuza wanadiplomasia wa nchi hiyo kutoka Uingereza.

Jambo hilo liliwaathiri raia mbalimbali wa Urusi waishio nchini Uingereza, moja kati ya watu hao ni Mrusi mwenye Asili ya Israeli na Mmiliki wa Klabu ya Kabumbu ya Chelsea ya Uingereza, Roman Abramovich ambae alishindwa kupata viza mpya ya kumwezesha kuendelea kuishi nchini Uingereza.

Kwa sababu hizo ilimlazimu kuomba uraia wa Israeli ambao alikidhi vigezo vya Law of Return na sasa ni raia kamili wa taifa la Israeli.

======

Bilionea wa Urusi ambaye ni mmiliki wa klabu ya soka ya Chelsea ya England Roman Abramovich, amesafiri kwa ndege hadi Tel Aviv baada ya kupata haki ya uraia wa Israel.

Maafisa wa uhamiaji wameiambia BBC kuwa alihojiwa wiki iliyopita kwenye ubalozi wa Israel mjini Moscow. Alikabiliwa na tatizo la kupata upya viza nchini Uingereza katika kinachoonekana kuwa na uhusiano na mzozo wa kidiplomasia kati ya Uingereza na Urusi.

Mzozo huo ulichangiwa zaidi na kupewa sumu kwa jasusi wa zamani na binti wake Sergei na Yulia Skripal.

Msemaji wa Abramovich hakutaka kuzungumza lolote kuhusiana na uraia wake mpya aliopewa katika taifa hilo la Mashariki ya Kati.

Bw Abramovich, mwenye umri wa miaka 51, atakua ndiye mtu tajiri zaidi nchini Israel sasa.

Viza yake ya uwekezaji nchini Uingereza inaripotiwa kuisha muda wake wiki kadhaa zilizopita, lakini serikali ya Uingereza imekataa kutoa kauli yoyote kuhusiana na 'suala lake binafsi'.

Kucheleweshwa kwa utoaji wa viza mpya ya Bw Abramovich kunakuja wakati kukiwa na uhasama wa kiplomasia baina ya serikali za London na Moscow Baada ya kupewa sumu kwa jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal kusini mwa Uingereza.

Bwn Abramovich hakuhudhuria fainali za Kombe la FA katika uwanja wa Wembley mapema mwezi huu wakati Chelsea ilipoichapa Manchester United 1-0.

Vyombo vya habari vya Israeli vinasema kuwa tayari amepewa kitambulisho cha uraia nchini Israeli chini ya sheria ya kurudi nyumbani, ambayo inawawezesha wayahudi popote pale walipo duniani kurudi na kuwa raia wa Israel.

Gazeti la The Times nchini Israeli limeandika kuwa Bw Abramovich aliwasili Israeli Jumatatu na kwamba amehamia nchini humo.

_100312852_forbes2017.png

Ni mtu ambaye amekuwa akiitembelea Israeli mara kwa mara na alinunua hoteli mjini Tel Aviv mnamo mwaka 2015 ambayo inasemekana ameigeuza kuwa makazi yake.

Wamiliki wa pasipoti ya Israeli wanaruhusiwa kuingia Uingereza kwa siku chake bila kuwa na visa.

Bw Abramovich ana utajiri wa thamani ya dola bilioni $11.5bn (£8.6bn), kulingana na jarida la Forbes.

Kuhamia kwake Israel kunaweza kumsaidia kifedha kwa sababu kama raia mpya wa Israeli ataweza kuondolewa ushuru unaolipwa na wawekezaji wa kigeni kwa muda wa miaka 10.

_101534405_presentational_grey_line464-nc.png

Roman Abramovich ni nani?
I
_101650518_roman_reuters.jpg


Mr Abramovich (right) has often been spotted at Chelsea's Stamford Bridge ground

  • Ni miongoni mwa watu tajiri zaidi Urusi, aliinunua klabu ya Chelsea FC mwaka 2
  • Inadaiwa aliuza midoli (wanasesere) kabla ya kuwekeza katika mafuta miaka ya 1990 baada ya kusambaratika kwa uliokuwa Muungano wa Usovieti
  • Bw Abramovich alikuwa wakati mmoja mshirika wa kibiashara wa tajiri wa zamani marehemu Boris Berezovky, rafiki wa rais wa zamani wa Urusi Boris Yeltsin
  • Wakosoaji wanasema wafanyabiashara hao wawili walitumia ukaribu wao na ikulu ya Kremlin kujipatia umiliki wa mashirika mengi ya serikali kwa 'bei ya kutupa'
  • Bw Abramovich alihudumu kama gavana wa jimbo la Chukotka, Urusi
  • Anaaminika kuwa na urafiki wa karibu na rais wa sasa wa Urusi Vladimir Putin
 
Report: Roman Abramovich lands in Israel for aliyah


Share
Russian-Jewish billionaire Roman Abramovich has landed in Israel in preparation for his absorption as a new immigrant, according to Channel 10 Television.

The Ministry of the Interior has confirmed the owner of England's Chelsea soccer team immigration application. The decision to immigrate to Israel was made after his visa in Britain was not renewed and not honored before it expired.
 
Hali tete England kanyimwa Resident permit ... Sasa kaishi miaka kibao kule kashindwaje kupata Uraia?

Ila Asili yake ndio inabeba zaidi kupewa Uraia wa Israel kirahisi bila kutumia coin yeyote ya Shekel Sheria za Israel zinawataka wenye Asili ya Israel kurejea home
 
Hali tete England kanyimwa Resident permit ... Sasa kaishi miaka kibao kule kashindwaje kupata Uraia?

Ila Asili yake ndio inabeba zaidi kupewa Uraia wa Israel kirahisi bila kutumia coin yeyote ya Shekel Sheria za Israel zinawataka wenye Asili ya Israel kurejea home
Haswaa, kupitia Sheria ya Kurudi (Law of Return)
 
View attachment 788500 Kufuatia mgogoro kati ya Uingereza na Urusi tangia kuuwawa kwa kachero wa Kisusi, Sergei Skripal na binti yake Yulia, ambapo Uingereza iliituhumu Urusi kuhisika na mauaji hayo na hivyo kuamua kufukuza wanadiplomasia wa nchi hiyo kutoka Uingereza.

Jambo hilo liliwaadhiri raia mbalimbali wa Urusi waishio nchini Uingereza, moja kati ya watu hao ni Mrusi mwenye Asili ya Israeli na Mmiliki wa Klabu ya Kabumbu ya Chelsea ya Uingereza, Roman Abramovich ambae alishindwa kupata viza mpya ya kumwezesha kuendelea kuishi nchini Uingereza.

Kwa sababu hizo ilimlazimu kuomba uraia wa Israeli ambao alikidhi vigezo vya Law of Return na sasa ni raia kamili wa taifa la Israeli.
Lilikuwa jaribio la kumuua hakuawa..!
 
Back
Top Bottom