Anna Nkya
Member
- Oct 21, 2021
- 69
- 341
Nimesikiliza wimbo wa Roma Mkatoliki, napenda ila Chorus hasa kwa kuwa ameimba ABIUD ambaye wengi wanapenda anavyoimba mitaani. Roma amefanya vyema kumopa nafasi kuimba Chorus japo kweli Chorus na anachoimba Roma havifanani.
Katika wimbo huu Roma anaomba kupewa maua yake ayanuse kabla hajafa wakati sehemu kubwa ya huo wimbo ni kukata maua ya Rais Samia yaliyo ya wazi sana.
Kwa mara ya kwanza Roma ana mistari ya kuokoteza akijaribu kukata maua ya Rais. Kabla Roma hajapewa maua, atoe Maua ya Rais Samia, ayapange bustanini kama ifuatavyo;
Maua ya uhuru wa kujieleza. Haya ni maua ya wazi ya Rais Samia Suluhu kwamba sasa Roma na wenzanke wengine wanaweza hata kuropoka. Watu wako huru chini ya Mama na bila shaka hilo ni kubwa sana.
Maua ya kuboreshwa kwa huduma za kijamii kiasi kwamba Ivan (Mtoto wa Roma), mdogo wake Ivan, Mama yake Ivan na Bibi yake Ivan pale Tanga wanaishi vizuri. Shule, afya maji na huduma nyingine zinazidi kuboreshwa.
Maua ya Rais Samia Suluhu ni mengi, Roma ili usiwe mnafiki toa haya maua ya haki ndio tutafakari hayo yako ni yapi.