Role ya Vilabu Soka kwenye Historia ya Tanzania

HNIC

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
1,898
2,195


Hawa ni wadau wa soka wa mkoa wa Dar es Salaam enzi hizo . Mwaka 1986 walichangia kutuweka madarakani IDFA ya akina Mussa Shagow. Kutoka kushoto ni Margaret Bwana. Luke luhui. Afisa utamaduni wilaya ilala. Marehem Malik Chanzi. Amin Bakhressa. Chando. Hamisi Kissiwa. Abdallah Kisungura.Mstari wa pili viongozi walikuwa Saidi Kizega. Mussa Shagow. Abdallah Katungunya. Wadau wengine. Gerald Sewe Jaluo. (R.ip) Shabani Kinana(r.i.p)Shaaban Zembwela(r.i.p) Maharani Mkamba na wengineo

-Picha kwa Ihsani ya mzee wetu Mussa Shagow


Mohammed Said na wengineo

Tuaomba mtuleteee history ya namna vilabu vya soka kwenye historia ya Tanzania

Je ni kweli soka la Tanzania lilishuka baada ya Nyerere kuambiwa na Gama Abdel Nasser wa Misri awadhibiti vilabu vya soka kwa sababu za kisiasa?

Hivi ni kweli klabu ya YANGA ndio iliyozaa Klabu ya SIMBA?

Je ni kweli Yanga ilikuwa ni klabu ya the masses na simba ilikuwa na bado ni Klabu ya ma "UNCLE TOMS"? yaani Simba ni klabu ya ma middle class na watu waaliokuwa karibu na watawala wa kikoloni?

Je ni kweli Yanga ilikuwa ni klabu ya walalahoi, na watu wa hali za chini?

Je marais wetu walikuwa wanashabikia vilabu vipi?

Hebu tupatie historia ya akina ya akina Mussa Shagow, Captain Malik, Mzee Ugundo na wengineo
 



Hawa ni MZIZIMA UNITED iliyochanganya wachezaji wa cosmopolitan na usalama . Nawakumbuka baadhi yao. Waliosimama. Ahmad. Kuna Mohd Tall. Mohd Aden. Jumanne Masument. Katinko. Walochuchumaa namkumbuka Riisasi. Jalala. na Mbaraka Jingalao

Sasa kama kuna mwenye kukumbuka wengine atuletee majina hapa
 


Hii ni risiti ya uthibisho wa kununua tofali kwa ajili ya kujenga klabu ya Simba Sports Club(SUNDERLAND) miaka 80 iliyopita nimeeona nipost risiti hii iwe kumbukumbu kwa wale wasio jua na wale wanaojua wajikumbushe! UNDERLINE!
 


Mchezaji wa zamani wa timu ya Young Africans na Timu ya Taifa (Taifa Stars)Mzee Abdulrahman Lukongo amefariki leo.mazishi yanategemewa kuwa kesho! Katika picha hii iliyopigwa Ikulu ya Dsm 1965 wakiwa na Mwl.Nyerere baada kutwa kombe la Gossage(Challenge cup) Marehemu Lukongo anaonekana mstari wa nyuma wa tatu kutoka kulia baada ya Rashid Seif.Hamisi Fikirini(wote marehemu)wa tatu Lukongo anaecheka sana.INNA LILAH WA INNA ILLAH RAJUUN
 
Sidhani kama Mohammed Said alikuwa mtu wa mipira

Mtafute Dr Dau, Ramadhani Matimbwa, Mussa Shagow na hao wengine kwenye picha
 
Yanga iko direct na Uhuru wa taifa hili, inasemekana harakati za kisiasa zilididimizwa kipindi hicho. Ikaundwa timu ya mpira kwa madhumini ya kukusanyikia.

Dar young Africans ikaundwa, so Yanga ndo tokeo la Tanzania huru. Mwenye la nyongeza au pingamizi hapa aje nalo. Labda mi nasukumwa na unazi tu kwa hii klabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…