Riwaya: Siri

SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 8: EPISODE 1
Kengele ya mlango wa
chumba cha Melanie Davis ililia
akainuka na kwenda mlangoni
akakutana na jamaa wawili
waliovalia suti nzuri
wakamtaka ajiandae kwani Rais
anahitaji kuonana naye usiku
ule
“Nadhani Jenerali Akiki
anataka kunipa mrejesho
kuhusiana na lile suala
tuliloliwasilisha kwake jana
kwani aliahidi kutupa mrejesho
leo” akawaza Melanie wakati
akijiandaa.Alivaa haraka haraka
suti ya rangi ya kijivu
akachukua mkoba wake na
kuongozana na wale jamaa hadi
katika gari wakaondoka
“Natamani sana kujua
maendeleo ya Gosu Gosu lakini
siwezi kumpigia Austin kwani
sitaki ajue kama niko
Uganda.Sitaki afahamu mambo
yangu.Ngoja nikamsikilize
kwanza Rais nijue kuna nini
anataka unieleza halafu nitajua
kama ntarejea nyumbani kesho
au nitaendelea kubaki hapa
hapa Kampala” akawaza
Melanie akiwa garini
“Kuna wazo limenijia
mchana wa leo na sijui lilitoka
wapi lakini ni wazo ambalo
naona kama lina
msingi.Ninampenda sana Gosu
Gosu na nimeumizwa na
kitendo cha kupigwa risasi
lakini ni vipi kama Gosu Gosu
atazinduka na kisha
akamueleza Austin kwamba
nilikuwa nimemtuma kwenda
Paris kuua mtu? Austin lazima
atakuwa na wasiwasi nami na
wanaweza wakaanza
kunichunguza na kama hilo
likitokea kuna uwezekano
wakanifahamu mimi ni
nani.Sitakiwi kuliruhusu hilo
litokee lazima niwe mwepesi
sana katika kuchukua tahadhari
mapema kabla mambo
hayajaharibika.Hapa kuna kitu
kimoja tu ambacho kinatakiwa
kifanyike nacho ni kumuua
Gosu Gosu” akawaza Melanie na
kufumba macho
“Oh my God ! akajikuta
ametamka kwa sauti na wale
jamaa aliokuwa nao garini nao
wakastuka
“Madam are you
okay?akauliza mmoja wao
“I’m okay” akajibu Melanie
“Kila ninapowaza na kufikia
katika sehemu ya kumuua Gosu
Gosu mwili wote
unanisisimka.Ni mtu ambaye
nilitaka kumtumia kwa kazi
mbali mbali za uuaji lakini
ndani ya moyo wangu ninajihisi
kumpenda pia hasa kwa mambo
anayonifanyia na
kinachonifurahisha zaidi ni
kwamba yuko tayari kufanya
kitu chochote kwa ajili yangu
kwa sababu ananipenda
sana.Nikimuua mwanaume Yule
nitaweza kweli kumpata
mwingine wa aina yake?
Akajiuliza Melanie
“Ngoja kwanza niliache
jambo hili nijielekeze katika
jambo la msingi la kumuua Rais
Patrice Eyenga.Kwa namna
yoyote ile lazima Patrice
auawe.Niliwaahidi wazazi
wangu hivyo kwamba wale
wote waliowakatili uhai wao
lazima nao waondoke duniani
hivyo lazima niitimize ahadi hii
kwa kutumia njia yoyote
ile.Sintawatendea haki wazazi
wangu kama nitashindwa
kuwaua watu hawa Patrice na
mwenzake Dr Fabian wakati
uwezo wa kufanya hivyo
ninao.Ufaransa na washirika
wake wamenipa uwezo
mkubwa wa kuweza kulipa
kisasi kwa wabaya wangu wote
kwa malipo ya kuivuruga Afrika
Mashariki na kuwatengenezea
njia ya kurejea kuinyonya nchi
ya Congo.Kwa hivi sasa
wanafurahia sana hiki
kinachoendelea Afrika
Mashariki laini laiti
wangeifahamu mipango yangu
katu wasingethubutu kunituma
kuja Afrika mashariki.Ngoja
niendelee kuwafurahisha huku
nikiendelea kutimiza ahadi
yangu ya kulipa kisasi na
nitakapomaliza hawataamini
macho yao kwa kile
nitakachowafanyia”akaendelea
kuwaza huku gari likienda
katika mwendo mkali
Waliwasili katika makazi ya
rais ndani ya kambi kubwa ya
jeshi nje kidogo ya jiji la
kampala.Melanie akashuka
garini na kukaribishwa ndani
“Melanie Davis ! akasema
Jenerali Akiki
“Mheshimiwa Rais”
akasema Melanie na
kusalimiana na Rais Akiki
“Karibu sana
Melanie.Samahani kwa
kukusumbua usiku huu”
akasema Jenerali Akiki
“Bila samahani
mheshimiwa Rais.Nimefurahi
sana kuja hapa kuonana nawe”
“Ahsante Melanie” akasema
Jenerali Akiki
“Vipi siku yako
imekwendaje?akauliza Jenerali
Akiki
“Siku yangu imekwenda
vyema mheshimiwa
Rais.Nashukuru ninahudumiwa
vizuri ninajiona kama nipo
nyumbani” akasema Melanie na
Jenerali Akiki akatabasamu
“Afrika Mashariki ni ndugu
moja.Ukiwa katika nchi yoyote
ndani ya jumuiya hii unajihisi
uko nyumbani” akasema
Jenerali Akiki
“Mheshimiwa Rais kwa hiki
kinachoendelea sasa hivi ndani
ya jumuiya hii hudhani kwamba
inakwenda
kusambaratika?akauliza
Melanie.Jenerali Akiki hakujibu
akachukua mkebe uliokuwa
mezani akaufungua na kutoa
sigara moja kubwa akawasha na
kuvuta
“Melanie hutajali twende
tukakae nje? akauliza
“Sawa mheshimiwa Rais”
akasema Melanie kisha
wakatoka na kwenda kuketi
katika kibaraza wakiyatazama
kwa mbali kidogo mataa ya
kambi ile kubwa ya kijeshi
“Usihofu Melani sehemu hii
ni salama sana” akasema
Jenereali Akiki
“Sina hofu mheshimiwa
Rais ninapokuwa nawe naamini
ulinzi uliopo ni mkubwa”
akajibuMelanie
“Uliniuliza kuhusu hofu ya
kusambaratika kwa jumuiya ya
Afrika Mashariki” akasema
Jenerali Akiki
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Kuna kila dalili kwamba
jumuiya ya Afrika Mashariki
inakwenda
kusambaratika.Uganda na
Rwanda hazielewani,Uganda na
Congo hazielewani,Tanzania na
Uganda zina mgogoro,unadhani
kwa mgogoro huu uliopo
jumuiya hii itaendelea kuwa
hai? Akauliza Melanie
“Ni kweli kuna hatari
kubwa kuhusu kusambaratika
kwa jumuiya ya Afrika
Mashariki.Yote haya ni matokeo
ya mipango ya
mabeberu.Wanataka
kutugawanya,wanataka
kuendelea kututawala na
kutunyonya ndiyo maana
mambo kama haya yanatokea.
Melanie mabeberu hawa
wanakutumia katika mipango
yao,wanatumia kigezo cha
kulipiza kisasi lakini kumbe
wana mipango yao.Pale Rais
Patrice Eyenga atakapokuwa
ameuawa basi utakuwa
umewatengenezea njia ya
kupita kuelekea Congo ndiyo
maana ninataka James Kasai
ashike madaraka ya Congo
kwani Yule ndiye kiboko
yao.Hakuna beberu atapeleka
pua yake Congo kama James
atakuwa madarakani. ” akasema
Jenerali Akiki.
“Ninafahamu mheshimiwa
Rais kwamba ninatumiwa na
mabeberu katika kufanikisha
mipango yao lakini sina namna
lazima kwanza nihakikishe
nimelipa kisasi kwani viongozi
hawa walimuua mama yangu
kikatili sana” akasema Melanie
“Usijilaumu
Melanie.Usiwaze kuhusu
jumuiya kuvunjika.Wewe
unachotakiwa kujielekeza ni
katika mpango wako wa kulipa
kisasi kwa wale wote
walioondoa uhai wa wazazi
wako na kukuacha yatima.Hiki
kinachotokea sasa ni matokeo
ya uovu wao na hakuna wa
kukulaumu” akasema Jenerali
Akiki na kunyamaza akaendelea
kuvuta sigara yake
“Melanie narudia tena
kukusisitiza kwamba jumuiya
ya Afrika Mashariki ivunjike au
isivunjike lakini lazima wale
wote waliotoa uhai wa wazazi
wako kikatili walipe uovu wao
na gharama ya kile
walichokifanya ndiyo hii hivyo
usirudi nyuma.Songa mbele na
mimi niko nyuma yako
ninakuunga mkono kwa kila
hatua unayochukua hadi pale
utakapohakikisha kwamba
wote wameuawa.Naamini pale
mtu wa mwisho atakapouawa
basi kila nchi itakuwa imebaki
peke yake hakutakuwa tena na
jumuiya.Unanisikia vizuri
Melanie?akauliza Jenerali Akiki
“Ninakusikia mheshimiwa
Rais”
“Vizuri.Fahamu hauko tena
peke yako katika mpango huu
tuko pamoja” akasema Akiki
“Nashukuru sana
mheshimiwa Rais”
Zilipita dakika mbili za
ukimya na Rais Akiki akasema
“Jioni ya leo nimetoka
kuzungumza na Jenerali Jean
Paul Mutombo mkuu wa
mejeshi wa jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo”
akasema Jenerali Akiki na
kunyamaza kama kawaida yake
ya kuzungumza kwa vituo
“Labda kwa kukupa tu
taarifa nina undugu na Jenerali
Mutombo na vile vile amewahi
kupata mafunzo katika jeshi la
Uganda hivyo basi ni
mwanafunzi wangu na
nilipomuita aliitika mara moja
akaja japo nchi zetu ziko katika
mgogoro hivi sasa” akanyamaza
tena kwa muda halafu akasema
“Kikubwa nilichomuitia ni
kuhusu ule mpango wako wa
kumuua Rais Patrice
Eyenga.Kama nilivyowaeleza
jana kwamba hatutaweza
kumuua Patrice Eyenga bila
kuwashirikisha watu wa ndani
ya nchi yake na watu wa karibu
yake ndiyo maana nikaanzakwa
kuzungumza na mkuu wa
majeshi” akasema Jenerali Akiki
na kunyamaza
“Kwa nini nimetaka
kuzungumza kwanza na mkuu
wa majeshi?akauliza Jenerali
Akiki
“Kuna mpango wa
mapinduzi unaandaliwa na
viongozi wa juu wa jeshi la
Congo.Wanataka kuiangusha
serikali ya Patrice Eyenga”
“Jeshi linataka kufanya
mapinduzi?akauliza Melanie
“Ndiyo Melanie.Makamanda
wa juu wa jeshi la Congo wana
andaa mpango kabambe wa
mapinduzi wanataka
kumuondoa Rais Patrice
madarakani.Machafuko
yaliyokuwepo nchini Congo
yaliwanufaisha sana
makamanda hawa wakuu wa
jeshi kwani walikuwa
wakifanya bishara ya kuwauzia
silaha waasi na kujipatia fedha
nyingi na madini kutoka kwao
lakini kwa sasa baada ya Patrice
Eyenga kumaliza uasi hawana
tena chanzo cha mapato hivyo
wanataka kumuondoa Patrice
madarakani ili kurejesha uasi
na waendelee kujipatia
fedha.Ninaufahamu mpango
huo na nilimuita Jenerali Paul
kumtaka tushirikiane naye
katika mpango huo wa
kumuondoa madarakani Patrice
Eyenga.Kikubwa nilichokuwa
nakitaka tuelewane naye ni
kumuweka James Kasai
madarakani baada ya
mapinduzi hayo kufanyika
lakini mambo yamekuwa
magumu kidogo” akasema
Jenerali Akiki na sura ya
Melanie ikaonyesha hofu
“Amekataa kushirikiana
nawe?akauliza Melanie
“Hapana hajakataa lakini
ugumu unakuja kuhusu James
Kasai.Hawako tayari kumpa
James Kasai madaraka yoyote
yale baada ya mapinduzi
kufanyika kutokana na sifa yake
mbaya.Sababu alizozitoa Paul
hata mimi nimezielewa.Kwa
ufupi ni kwamba James Kasai
ameharibu sana sifa yake baada
ya kuanzisha mashirikiano na
kikundi cha kigaidi cha IS.Kwa
sasa kila mtu anamjua kama
Gaidi na si mpiganaji kwa
maslahi ya Congo”akanyamaza
tena kidogo halafu akaendelea
“Melanie italazimu
kuendelea na mpango wetu wa
kumuua Patrice Eyenga bila ya
kumshirikisha James Kasai”
akasema Jenerali Akiki
“Unamuondoa James Kasai
katika mpango huu? Melanie
akauliza
“Ndiyo.Wakuu wale wa
jeshi la Congo hawataki
kushirikiana naye katika
mpango wa mapinduzi.James
Kasai ni mtu ambaye
amekwisha fanya mauaji ya
watu wengi nchini Congo na
hata nchi jirani na kwa sasa
anatafutwa na mahakama ya
kimataifa ya uhalifu wa kivita
kutokana na uhalifu mkubwa
uliofanywa na kikundi chake
cha waasi
anachokiongoza.Kama
utakumbuka jana nilimuahidi
James kwamba nataka awe Rais
wa Congo baada ya mapinduzi
lakini hilo halitawezekana
tena.Itabidi tumuweke James
pembeni.Hatafurahi lakini
hakuna namna lazima
tumuondoe katika mpango
huu.Wale wakuu wa jeshi
hawako tayari kushirikiana
naye katika mpango wowote wa
mapinduzi” akasema Jenerali
Akiki
“Mheshimiwa Rais wewe
mwenyewe umekuwa ukisema
mara kwa mara kwamba ni
James Kasai pekee ambaye
anapambana kwa maslahi ya
Congo ni wakati wa
kulithibitisha hilo kwa
kumsaidia aweze kuingia
madarakani .Umekiri wewe
mwenyewe kwamba ulikubali
kumsaidia James Kasai katika
harakati zake kwa kuwa
uliamini ndiye pekee anayefaa
kuiongoza Congo.Tembea
katika kauli yako hiyo” akasema
Melanie
“Melanie nilichokisema
kina ukweli.James
hakufadhiliwa na nchi yoyote
kubwa kutoka nje ya bAra ya
Afrika.Mimi ndiye niliyekuwa
mfadhili wake mkuu kwa kila
kitu kuanzia fedha za kujikimu
askari wake hadi silaha lakini
lazima niwe muwazi kwamba
James Kasai ameharibu sifa
yake baada ya kujiunga na
kundi la kigaidi la IS.Hata raia
wa Congo hawatakuwa tayari
kumuunga mkono au
kuongozwa na mtu mwenye sifa
ya kushirikiana na magaidi”
akasema Jenerali Akiki
“James hakuwafuata IS bali
wao ndio waliomfuata na
alikuwa katika shida kubwa ya
fedha na silaha ndiyo maana
akakubali kushirikiana
nao.Alihitaji kujenga jeshi lake
liwe imara ili akapambane na
jeshi la serikali ya
Congo.Haikuwa rahisi kukataa
kushirikiana na IS ambao
walimuahidi fedha nyingi na
silaha za kisasa.Mheshimiwa
Rais kwa namna yoyote ile
lazima James Kasai ashiriki
katika mpango huu wa
mapinduzi na kisha aingie
nchini Congo kushika
madaraka.Hao wakuu wa jeshi
la Congo lazima watakuwa
wanaandaa mpango huo kwa
kushirikiana na nchi za nje
ambao ni wazalishaji wakubwa
wa silaha hivyo hatutakuwa
tumeisaidia Congo badala yae
tutakuwa tumerejesha tena
matatizo na hicho ndicho
Ufaransa wamenituma kuja
kukifanya na mimi sitaki
kuirejesha Congo katika
machafuko baadaya kumuua
Patrice Eyenga” akasema
Melanie
“Melanie utake usitake
lazima machafuko yatatokea tu
baada ya Patrice
kuuawa.Majenerali wale lengo
lao kubwa ni kuanzisha
machafuko ili wapate sehemu
ya kuuzia silaha.Melanie kuna
mambo ambayo hatuwezi
kuyalazimisha.Ninaomba
unielewe” Akasema Jenerali
Akiki
“Mheshimiwa Rais
ninakuelewa sana lakini bado
naendelea kusisitiza kwamba
hatuwezi kuendelea na mpango
huu bila ya kumshirikisha
James” akasema Melanie
“Melanie shida yako ni
Patrice Eyenga auawe.Hata bila
ya James Kasai Patrice atauawa”
“Mheshimiwa Rais kwa
namna yoyote ile lazima James
ashirikishwe” akasisitiza
Melanie
“Kwa nini unasistiza sana
ushiriki wa James
Kasai?akauliza Jenerali Akiki
“Kwa sababu ninamuamini
anaweza akafanya vile
ninavyotaka.Siwezi kuwaamini
jenerali hao wa jeshi ambao
yawezekana mpango wao
ukashindwa kufanikiwa au
wanaweza wakafanya
mapinduzi bila kumuua Rais
Patrice lakini James Kasai kama
atashiriki atahakikisha Patrice
anauawa”
“Melanie usihofu bado
majadiliano na mkuu wa
majeshi wa Congo yataendelea
hivyo suala hilo la kuhakikisha
Patrice Eyenga anauawa
litazingatiwa”akasema Jenerali
Akiki
“Mheshimiwa Rais
sifahamu mazungumzo hayo
yatachukua muda gani na mimi
sina muda mrefu wa
kusubiri.Nahitaji jambo hili
lifanyike haraka kwani nina
mambo mengi ya kukamilisha
hivyo nashauri tuendelee na
mpango wetu wa kumuua
Patrice Eyenga bila kushirikiana
na jeshi la nchi hiyo” akasema
Melanie na Jenerali Akiki
akawasha sigara nyingine.
“Melanie una mpango
wowote kichwani mwako
ambao unadhani tunaweza
kuutekeleza bila kulihusisha
jeshi la Congo?akauliza Jenerali
Akiki.
“Ndiyo ninao mpango
mheshimiwa Rais” akasema
Melanie
“Nieleze tafadhali”
“Hivi sasa nchi yako na
Congo hazina maelewano
mazuri.Nataka kuitumia fursa
hiyo.Utampigia simu Rais wa
Tanzania na kumueleza
kwamba unataka kukutana na
kufanya mazungumzo naye
pamoja na Rais wa Congo
mazungumzo yanayolenga
kutafuta amani katika nchi za
jumuiya ya Afrika Mashariki na
mazungumzo hayo yafanyike
nchini Tanzania.Naamini Rais
wa Tanzania atakubali jambo
hilo na atamualika Rais Patrice
kuhudhuria mazungumzo
hayo.Kikubwa utakachowaeleza
utakaputna nao ni kwamba uko
tayari kutoa taarifa za mahala
alipo James Kasai.Wakati
mazungumzo hayo yakifanyika
litapandikizwa bomu ndani ya
ndege ya Rais Patrice na
atakapoondoka akiwa angani
bomu hilo litalipuliwa na
utakuwa ndio mwisho wa
Patrice Eyenga” akasema
Melanie na Jenerali Akiki
akamkazia macho huku
akipuliza moshi mwingi.
“Mpango huo”Melanie
akaendelea
“Hautawahusisha watu
kutoka ndani ya serikali ya
Congo lakini naamini
majenerali hao wa jeshi ambao
wanaandaa mpango wa
mapinduzi pindi watakaposikia
kwamba Patrice Eyenga
ameuawa basi watatangaza
jeshi kushika nchi na hiyo ni
fursa nyingine kwa James Kasai
kuanzisha mapambano na jeshi
la serikali na huku wewe
ukimuunga mkono na hiyo
ndiyo fursa yako kama unataka
James Kasai aiongoze Congo”
akasema Melanie.Baada ya
kutafakari kwa muda Jenerali
Akiki akasema
“Melanie mpango huo si
mbaya.Ni mpango mzuri lakini
ni wa hatari kubwa sana na
utekelezaji wake unaweza kuwa
mgumu mno” akasema Jenerali
Akiki
“Mheshimiwa Rais mpango
huu japo unasema ni mgumu
lakini ndio hasa mpango ambao
mimi nauona ni rahisi na
utakaotusaidia kumuua Patrice
Eyenga kwa haraka”
“Ugumu ninaouzungumza
mimi ni namna ya kuliingiza
hilo bomu ndani ya
ndege.Kuhusu kuwaita marais
hilo halina ugmu ninaweza
nikajishusha na nikaomba
kukutana nao lakini je hilo
bomu litaingizwa vipi ndani ya
ndege? Ni vipi kama
likagundulika mapema na
mpango ukashindwa
kufanikiwa?Sote tutakuwa
katika hatari kubwa”akasema
Jenerali Akiki
“Usihofu mheshimiwa
Rais.Ninao mtandao mkubwa na
nina uhakika suala la kuingiza
bomu katika ndege ya Rais
halitakuwa tatizo.Ninachohitaji
ni wewe kukubali kujishusha na
kuitisha kikao na marais hao wa
Tanzania na jamhuri ya
kidemokrasia ya
Congo”akasema Melanie
“Hata kama mpango huo
utafanikiwa na Patrice Eyenga
akauawa lazima lawama zote
zitaiangukia serikali ya
Uganda.Lazima dunia nzima
itaamini sisi ndio tuliomuua na
huo utakuwa ni mgogoro
mwingine unaoweza
kusababisha hata vita kati ya
Congo na Uganda ndiyo maana
nilitaka kuwatumia watu wa
ndani ya Congo ili hata kama ni
vita basi iwe ni baina yao
wenyewe sisi tusihusishwe na
lolote” akasema Jenerali Akiki
“Pamoja na faida zake lakini
mpango huo utachukua muda
mrefu.Majadiliano hatujui
yatachukua muda gani hadi
kufikia makubaliano na mimi
nataka jambo hili liende haraka
haraka kwani bado nina mambo
mengi ya kufanya.Naomba
mheshimiwa Rais kama kweli
una nia ya dhati ya kunisaidia
kubaliana na mpango wangu
huu nilioupendekeza” akasema
Melanie na ukimya ukatawala
mahala pale.Baada ya dakika
kadhaa za tafakari Jenerali Akiki
akasema
“Melanie endapo nitakubali
kufanya haya yote unayoyataka
niyafanye nini yatakuwa malipo
yangu? Nataka kujua namna
nitakavyofaidika kupitia
mpango huo. Wewe utakuwa
umelipiza kisasi na utajihisi
amani na mimi pia nahitaji
kufaidika” akasema Jenerali
Akiki
“Endapo tukiamua
kuukubali mpango wa
mapinduzi kwa kushirikiana na
jeshi wewe utafaidika na
nini?akauliza Melanie
“Zipo faida ambazo
ningezipata kupitia mpango ule
tena kubwa tu” akasema
Jenerali Akiki
“Wewe unahitaji nini
mheshimiwa Rais?Fedha? Kiasi
gani?akauliza Melanie na
Jenerali Akiki akatabasamu
“Sihitaji fedha.Ninazo fedha
za kutosha.Nahitaji kitu
kingine”
“Kitu gani? Melanie
akauliza
“Wewe” akajibu Jenerali
Akiki akiwa na macho
makavu.Melanie akatoa kicheko
kidogo na kusema
“Unanihitaji mimi?!
Akauliza Melanie
“Ndiyo”
“Unanihitaji kivipi
mheshimiwa Rais?Melanie
akauliza
“Melanie wewe si mtoto
mdogo wa kushindwa
kutambua ninamaanisha
nini”akasema Jenerali
Akiki.Ukapita ukjimya mfupi
Melanie akauliza
“Mheshimiwa Rais tafadhali
niambie kama humaanishi
hicho unachokisema” akasema
Melanie
“Ninaamisha
Melanie.Nakuhitaji
wewe.Nakuhitaji uwe mpenzi
wangu wa siri” akasema
Jenerali Akiki na Melanie
akacheka kidogo
“Mheshimiwa Rais jana
ulisema kwamba ulikuwa na
ukaribu mkubwa sana na
wazazi wangu hasa mama
ambaye alisoma na mke wako
na ukatamka kwa ulimi wako
kwamba kutokana na ukaribu
huo mimi ni kama mwanao kwa
nini leo unataka kulala na
mwanao?
“Sikiliza Melanie wewe
tayari ni mtu mzima na mambo
ya kupenda unayaelewa
vyema.Ni kweli nilikuwa na
ukaribu na wazazi wako lakini
nimeshindwa kuudhibiti moyo
wangu kufukuta toka nilipokuta
machoni.Melanie hakuna kitu
chochote kibaya kitatokea kama
mimi nawe tutakuwa wapenzi
wa siri.Nikubalie nikitakacho na
ninakuahidi utapata kila
unachokitaka” akasema Jenerali
Akiki
“Nimekutana na kigingi
kingine tena.Wanaume hawa
wakoje? Wameumbwaje?Mbona
wote wako sawa? Akawaza
Melanie
“Melanie unasemaje kuhusu
hilo nililokuomba?akauliza
Jenerali Akiki huku akiwasha
sigara nyingine tena
“Kwa nini unanifanyia hivi
mheshimiwa Rais?akauliza
Melanie
“Kuna ubaya gani mimi na
wewe tukiwa wapenzi wa siri
Melanie?Au ukinipa hicho
ninachohitaji utapungukiwa
nini?Ninachokiomba kutoka
kwako ni kidogo sana
ukilinganisha na kile ambacho
nitakifanya kwa ajili
yako.Ninakwenda kuubeba
mzigo mzito sana kwa ajili
yako.Wewe hautajulikana bali
ni mimi ambaye ninaweza
kutilia shaka kuhusika na
mauaji hayo hivyo sidhani kama
kuna haja ya kuwa na
majadiliano makubwa zaidi
katika suala hili” akasema
Jenerali Akiki
“Huyu anaweza
akanikwamisha mipango yangu
kwa kuwa anajua ninamuhitaji
sana.Ni kweli namuhitaji sana
katika suala hili lakini mzee
mzima naye amekwisha waka
tamaa na sasa anataka nimpe
mwili wangu.Sina namna ngoja
nimpe anachokitaka ili mambo
yangu yaende lakini ajue kila
mwosha huoshwa.Iko siku
yake” akawaza Melanie
“Mheshimiwa Rais sina
namna.Ninakuhitaji sana katika
mpango huu.Niambie lini
unanihitaji na wapi mimi
nitakuja” akasema Melanie na
Jenerali Akiki akatoa tabasamu
“Tunaanza usiku wa leo”
“Leo?
“Ndiyo.Hakuna anayejua
kesho yake hivyo ninakuhitaji
kuanzia usiku wa leo”
“Mpaka lini?Lazima kuwe
na ukomo hatuwezi kuendelea
na mchezo huu.Wewe ni rais wa
nchi una mke ambaye ni rafiki
wa mama yangu ambaye akijua
kama unatembea na mimi
ambaye ni sawa na mwanao
utaingia katika mgogoro
mkubwa wa familia yako”
akasema Melanie
“Ni kweli mimi ni Rais wa
nchi lakini vile vile ni binadamu
na nina mahitaji kama
wanadamu wengine hivyo
mambo yangu mimi na wewe
hayahusiani chochote na urais
wangu”
“Nimekuelewa mheshimiwa
Rais lakini usiku wa leo niache
niende na kesho nitakuwa
mgeni wako.Ninataka nije
nikiwa nimejiandaa vyema
kimwili na kiakili kwa siku ya
leo sikuwa nimejiandaa kwa
suala hilo” akasema Melanie
“Hakuna tatizo
Melanie.Nashukuru kwa
kunielewa.Nadhani kesho
tutapata wasaa mzuri zaidi wa
kujadili kwa kina hili suala letu
namna tutakavyoweza
kulikamilisha.Ninachokuomba
James Kasai asifahamu
chochote kuhusiana na haya
tuliyoyazungumza leo hadi pale
wakati muafaka utakapofika”
akasema Jenerali
Akiki.Hakukuwa na
mazungumzo mengine tena
akamsindikiza Melanie hadi
katika gari akaondoka.Jenerali
akiki akarejea ndani
“Melanie Davis ! akawaza
huku akiwasha sigara akavuta
mikupuo kadhaa huku akiachia
tabasamu pana sana
“Ningechekwa na dunia
kama mtoto Yule angeondoka
Uganda bila kumgusa hata
kidogo.Ni kweli mama yake
alikuwa ni rafiki wa familia yetu
lakini nimeshindwa
kuvumilia.Japo uzuri wake ni
wa kutegenezwa lakini
umenichanganya sana” akawaza
Jenerali Akiki.
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Ndege ya shirika la ndege la
Misri ilitua katika uwanja wa
ndege wa Julius Nyerere jijini
Dar es salaam saa nne za usiku
ikitokea jijini Cairo kupitia
Nairobi Kenya.Abiria walishuka
ndegeni na kuingia katika jengo
la uwanja ili kukamilisha
taratibu za kuingia
nchini.Mathew Mulumbi akiwa
miongoni mwa abiria waliokuja
na ndege hii alikuwa na hati ya
kusafiria inayomuonyesha
kuwa ni raia wa Saudi Arabia
mwenye jina la Abu Al Zalawi.
“Ninarejea nyumbani kama
mgeni wakati hii ni nchi yangu
ya kuzaliwa lakini imenilazimu
nirejee namna hii.Hapa
uwanjani wapo watu wengi
wanaonifahamu ila naamini
kwa mwonekano huu nilio nao
sasa hakuna
atakayenigundua.Nilifanya
jambo zuri kufuga hizi ndevu
nyingi.Kwa muonekano huu kila
mtu atadhani labda mimi ni
kiongozi wa kidini huko
nilikotoka” akawaza Mathew
akiingia ndani ya jengo la
uwanja.Hakuwa akizungumza
Kiswahili alizungumza
kiingereza akichanganya na
kiarabu kidogo.Aliwaona baadhi
ya watu kadhaa pale uwanjani
aliokuwa akifahamiana nao
akajitahidi kuwakwepa
asionane nao.
Baada ya kukamilisha
taratibu na kuruhusiwa kuingia
nchini Mathew akaenda katika
duka la kubadili fedha za kigeni
akabadili fedha alizokuwa nazo
na kupata fedha za Tanzania na
kutoka nje.Alitamani asujudu na
kuibusu ardhi ya Tanzania kwa
furaha aliyokuwa nayo.
“Natamani niibusu ardhi ya
nchi yangu kwani sikuwa
nimetegemea kuikanyaga tena
katika maisha yangu lakini leo
kwa nguvu ya Mungu nimerejea
nchini” akawaza akiendelea
kukokota torori lenye mabegi
yake hadi alipotoka
nje.Hakukuwa na mtu yeyote
aliyekuja kumpokea hivyo
akachukua taksi.
“Nikupeleke wapi
kaka?akauliza dereva taksi kwa
lugha ya kiingereza
“Ninaomba unipeleke
katika hoteli yoyote nzuri yenye
utulivu mkubwa lakini kabla
hujanipeleka huko nahitaji
kupita katika supermarket
yoyote kubwa kuna vitu
nahitaji” akasema Mathew na
dereva akaondoa gari
“Baada ya miaka mitatu
hatimaye niko tena ndani ya jiji
la Dar.Jiji limebadilika
sana.Maendeleo makubwa
yamefanyika katika kipindi
hiki” akawaza Mathew akiwa
amekaa kiti cha nyuma
akielekeza macho nje
Hatimaye baada ya
kuzunguka katika supermarket
kadhaa kubwa na kukuta
zimefungwa ,wakaipata ambayo
ilikuwa wazi.Mathew akashuka
garini na kuingia ndani ya duka
lile akaelekea katika upande wa
vifaa vya elektroniki akachukua
mashine ya kunyolea nywele
pamoja na vitu vingine kadhaa
akaenda kuilipia na kurejea
garini safari ikaendelea.Dereva
Yule alimfikisha katika hoteli
moja nzuri wakaagana huku
Yule dereva akimpa kadi yake
ya biashara.Mathew akapokewa
na wahudumu wachangamfu na
kupewa chumba
“Ni kama ndoto lakini ni
kweli niko Dar es salaam.Kwa
anayenifahamu atashangaa
sana kuniona hapa hotelini
kwani ninafahamika sana hapa
Dar es salaam kama mmoja wa
watu matajiri.Nimewekeza
katika majumba mengi tu lakini
kwa mujibu wa Habiba Jawad
Peniela ameuza mali zangu zote
zilizoko Dar es salaam hivyo
siwezi kujua katika mauzo hayo
nyumba ipi imeuzwa na ipi
imesalimika.Zipo baadhi ya
nyumba ambazo Peniela
hazifahamu anayezijua ni Gosu
Gosu.Mtu wa kwanza kabisa
ambaye natakiwa kumtafuta
kesho ni Gosu Gosu,nikimpata
huyu nitafahamu mengi kutoka
kwake” akawaza Mathew na
kuingia bafuni akaanza kunyoa
ndevu zote alizofuga
akajitazama na kutabasamu
“Hii ndiyo sura halisi ya
Mathew Mulumbi.Nilipotoka
kwa Ammar Nazari nilikuwa
nimechakaa sana lakini baada
ya kuanza kuishi na Najma
kidogo najiona nimeanza
kunawiri” akawaza huku
akipaka dawa katika kidevu
chake halafu akajitazama tena
katika kioo
“Welcome back Mathew
Mulumbi” akasema kwa sauti
ndogo akaoga kisha akaenda
kujilaza kitandani.
“Natakiwa kumjulisha
Habiba kwamba tayari nimefika
salama Dar es salaam” akawaza
Mathew.Hakuwa na simu
akachukua kompyuta yake
akaiunganisha na
intaneti.Hoteli ile ilikuwa na
huduma ya mtandao wa
intaneti.Baada ya kuunganisha
akamtafuta Habiba Jawad na
kumpigia simu kwa kutumia
mtandao wa skype.
“Mathew Mulumbi”
akasema Habiba baada ya
kupokea simu ya Mathew
“Mama Habiba” akasema
Mathew huku akitabasamu
“Naona uso wako una
furaha kubwa leo.Umenyoa
ndevu umebadilika
sana.Umerudi kuwa Mathew
Mulumbi na si Abu Zalawi”
akasema Habiba huku akitoa
kicheko kidogo
“Ni kweli mama nina furaha
ya kufika
nyumbani.Nimekupigia
kukujulisha kwamba tayari
nimefika Tanzania na hapa
nilipo nipo hotelini”
“Pole kwa safari
Mathew.Nashukuru umefika
salama.Kwa sasa endelea
kupumzika hadi kesho
tutazungumza zaidi.Jitahidi
upate simu kwa ajili ya
mawasiliano utakapokuwa
hapo kwani hatuwezi
kuwasiliana kila mara kwa
kupitia mtandao”
“Ni kweli mama.Kesho
nitashughulikia kila kitu na jioni
nitakupigia tuzungumze”
akasema Mathew na kuagana na
Habiba kisha akachukua juisi
aliyonunua supermarket
akanywa .
“Sasa nijipumzishe
nijiandae kwa siku ya
kesho.Nitakuwa na mizunguko
mingi” akawaza na kujilaza
kitandani
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 8: EPISODE 2
Sauti za watu waliopita
wakizungumza nje ya mlango
wa chumba alicholala ndizo
zilimstua Mathew kutoka
usingizini akafungua macho na
chumba kilikuwa na mwanga
wa kutosha.Akayaelekeza
macho ukutani kulikokuwa na
saa kubwa ambayo ilionyesha
ni saa mbili na dakika kumi na
nane
“Usingizi wa nyumbani
mtamu sana ndiyo maana
nimelala hadi nikapitiliza
namna hii.Kawaida yangu
huamka saa kumi na mbili za
asubuhi” akawaza Mathew
kisha akatoka pale kitandani
akavaa nguo za mazoezi na
kuelekea katika chumba cha
mazoezi.Hoteli ile aliyofikia
ilikuwa na chumba maalum cha
mazoezi.Alifanya mazoezi
kuuweka mwili sawa halafu
akaenda kuoga kujiandaa kwa
ajli ya kuikabili siku.Siku hii
alivaa suruali ya jeans rangi
nyeusi na fulana ya rangi
nyeupe kichwani akavaa kofia
ya rangi nyeusi ,macho
akayafunka kwa miwani myeusi
bila kusahau mkufu wa dahabu
kifuani akajitazama katika kioo
akaridhika kwa mwonekano ule
kisha akaelekea sehemu ya
chakula akaagiza kifungua
kinywa.Wakati akiendelea
kupata kifungua kinywa akapita
kijana muuza magazeti Mathew
akanunua magazeti matatu
akapitia kwa juu juu lakini
kubwa ambalo lilitawala
magazeti yale ni matukio ya
kushambuliana yanayoendelea
baina ya Uganda na
Rwanda.Alipomaliza kifungua
kinywa akaenda kulipa na
kumuachia chenji muhudumu
kisha akatoka nje akaanza
kutembea kwa miguu
“Sijui kwa nini nikiwa sina
silaha ninajiona mzito sana
lakini hata kama itatokea hatari
yoyote ninao uwezo wa
kukabiliana nayo bila kuwa na
silaha” akawaza huku akivuka
barabara kuelekea upande wa
pili ambako aliona taksi nyingi
zimeegeswa.Akakodisha taksi
moja akamtaka dereva
ampeleke sehemu Fulani
“Sehemu ya kwanza
ninakoanzia leo ni nyumbani
kwangu.Nataka nikamfahamu
aliyenunua ni nani na nijue vitu
vilivyokuwamo mle ndani
vimepelekwa wapi.Kulikuwa na
vitu vyangu vingi na vingine vya
siri kabisa.Nilijenga nyumba ile
kwa ajili yangu na ndiyo maana
nikaweka baadhi ya vitu kama
sehemu za siri za kuhifadhia
silaha n.k.Peniela alikosea sana
kuiuza nyumba yangu ile lakini
siwezi kumlaumu kwa sababu
anajua tayari nimefariki dunia
na yeye hana mpango wa kuja
tena kuishi Tanzania ndiyo
maana akaamua kuiuza.lakini
kwa nini Peniela akaamini
haraka namna hii kwamba
nimefariki dunia?Kitu gani
klichomuaminisha haraka
hivyo?Kwa nini hakutaka
kufanya uchunguzi kujua kama
kweli nimekufa? Anyway
nisiumize kichwa kwa hilo
majibu yote anayo yeye
mwenyewe” akawaza Mathew
huku gari likiendelea kukata
mitaa kuelekea katika nyumba
ya Mathew
“Natamani sana kumtafuta
Ruby na kujua maendeleo
yake.Najua nilimuacha katika
wakati mgumu
sana,nakumbuka ni siku moja tu
ilipita toka anieleze kwamba
ananipenda na anataka tuwe
wapenzi na nilimuahidi
kwamba baada ya kumaliza
operesheni ile basi
tungekwenda mahala sisi
wawili pekee kupumzika.Tayari
nilikwisha amua kuwa na
mahusiano ya siri na Ruby
lakini kwa bahati mbaya
sikurejea tena
Tanzania.Atakuwa aliumia
mno.Yuko wapi sasa
hi0vi?Anafanya nini?Ameolewa
au bado?Yote haya natakiwa
kujua.Nitamuuliza Gosu Gosu
nikionana naye” akaendelea
kuwaza Mathew
Hatimaye dereva wa ile
taksi aliyopanda alifika katika
mtaa ilipo nyumba ya Mathew.
“Huu mtaa wangu
nimeukumbuka
sana.Umejengeka mno sasa
hivi.Mimi ndiye muasisi wa
mtaa huu.Nilianza kujenga
wakati hakuna nyumba hata
moja” akawaza huku
akitabsamu na gari likienda
kwa mwendo wa
taratibu.Dereva akakata
kushoto kufuata barabara ya
zege iliyoelekea nyumbani kwa
Mathew.Mapigo ya moyo wake
yakaanza kumwenda kasi
walipokaribia geti la nyumba
yake.Kulikuwa na walinzi
wawili
wakawasimamisha.Mathew
akafungua mlango akashuka
akamlipa dereva akaondoka
halafu akawafuata
walinzi.Hakuwa akiwafahamu
walinzi wale akasalimiana nao
vizuri kisha wakamuuliza shida
yake
“Nahitaji kuonana na
wahusika wa nyumba hii”
akasema Mathew
Walinzi wale wakataka
kufahamu yeye ni nani na
katokea wapi akawajibu
kwamba ametokea nje ya nchi
na ni ndugu ya wanaoishi
pale.Mmoja wa walinzi akaingia
ndani na kupiga simu ndani ya
nyumba akieleza kwamba kuna
mgeni wao ametokea nje ya
nchi.
“Subiri kidogo kuna mtu
anakuja” akasema Yule mlinzi
aliyeingia ndani kupiga
simu.Baada ya dakika tatu
mlango mdogo wa geti
ukafunguliwa na msichana
mmoja akajitokeza
“Lucy !! akasema Mathew
huku akivua miwani na kofia
mara kikatokea kitu
kilichowashangaza wote.Lucy
aligeuka haraka akatimua mbio
kurudi ndani huku akipiga
kelele wale walinzi wakaanza
kumkimbiza.Mathew akavuka
geti akaingia ndani.Lucy
hakufika mbali akaanguka chini
na kupoteza fahamu.Walinzi
wale wakaungana na Mathew
wakaanza kumpatia huduma ya
kwanza
“Ana matatizo gani huyu?
Mathew akauliza
“Tukuulize wewe kwani
alipokuona tu ndipo alipoanza
kupiga makelele na
kukimbia.Wewe ni
nani?akauliza mlinzi mmoja
“Tusubiri azinduke tutajua
tatizo lake” akasema Mathew
huku walinzi wale wakionekana
kuwa na woga.
Baada ya muda Lucy
akaamka na mara tu
alipomuona Mathew yuko pale
sebuleniakaanza tena kupiga
kelele na kutaka kukimbia
lakini walinzi
wakamzuia,Mathew
akamuendea
“Jamani msimruhusu
anisogelee ni mzimu huyo !
akapiga kelele Lucy na wale
walinzi wakabaki wanashangaa
“Lucy ! akaita Mathew
lakini Lucy akapiga kelele
kubwa.Mlinzi mmoja akataka
kumzuia Mathew asimsogelee
Lucy lakini Mathew
akamsukuma akasogea
pembeni
“Lucy !! akaita Mathew na
kumshika Lucy
mabegani.Alikuwa anatetemeka
“Mimi si mzimu.Nitazame
vizuri ni mimi Mathew.Ni mimi
Yule Yule unayenifahamu”
akasema Mathew
“Mathew amekwisha fariki
miaka mitatu iliyopita !
akasema Lucy huku
akitetemeka
“Hapana Lucy
sikufariki.Mimi ni mzima ila
nilikuwa katika matatizo
makubwa na taarifa mliyoipata
kwamba nimefariki si taarifa ya
kweli.Mimi ni mzima
kabisa.Mimi si mzimu” akasema
Mathew lakini bado Lucy
aliendelea kutetemeka
“Lucy usiwe na wasiwasi ni
mimi Mathew nimerejea”
akasema Mathew na mara
mmoja wa walinzi akamsogelea
Lucy
“Lucy unahitaji msaada wa
polisi? Akauliza mmoja wa
walinzi
“Msijali ndugu zangu.Mimi
ni mwajiri wake wa zamani na
ndiye mmiliki wa nyumba
hii.Nilipotea kwa miaka mitatu
na taarifa waliyopata ni
kwamba nimekufa kumbe niko
hai”Mathew akajaribu kujieleza
“Ni kwel Lucy hayo
anayoyasema huyu
jamaa?akauliza mlinzi na Lucy
akatingisha kichwa kukubali
“Una hakika hatakuwa na
madhara tukikuacha naye humu
ndani?akauliza mlinzi
“Ndugu zangu msiwe na
wasiwasi na mimi hata
kidogo.Hii ni nyumba yangu na
huyu ni mfanyakazi
wangu.Hamnifahamu lakini
mimi ndiye mwenye nyumba
hii” akasema Mathew
“Nendeni msiwe na wasi
wasi hakuna tatizo” akasema
Lucy na walinzi wale wakatoka
lakini bado wakiwa na
wasiwasi.
“Lucy tafadhali nyamaza
kulia ni mimi Mathew
nimerudi” akasema Mathew
baada ya Lucy kuanza tena kulia
baada ya walinzi kutoka.
“Tafadhali usilie Lucy”
akasema Mathew na kutoa
kitambaa akamfuta machozi na
mara Lucy akamkumbatia kwa
nguvu.
“Mathew jamani kaka
yangu !! akasema Lucy huku
akiendelea kumwaga machozi
“Imetosha Lucy usiendelee
kulia” akasema Mathew
“Mathew niache nikulilie
kaka yangu hujui ni machungu
gani nimeyapata kwa kuamini
kwamba umefariki
dunia.Nimekulilia usiku na
mchana.Nimekuombea sana
upumzike kwa amani nikiamni
umekufa ndiyo maana
nilipokuona nilipatwa na
mstuko mkubwa sana.Niache
nikulilie kaka Mathew” akasema
Lucy.
“Nyamaza Lucy.Nimerudi
niko mzima wa afya.Hakuna
sababu ya kuendelea kumwaga
machozi.Ahsante kwa maombi
yako ambayo naamini
yamenisaidia sana hadi
tumekutana tena hapa”akasema
Mathew
“Nini kilikutokea
Mathew?Ulikuwa wapi?Nani
waliosambaza taarifa kwamba
umekufa? Lucy akauliza huku
akifuta machozi
“Tutazungumza hayo yote
baadae nitawaeleza nilikuwa
wapi lakini kwa sasa nataka
kufahamu nani wanaishi hapa?
“Tunaoishi hapa ni mimi na
Gosu Gosu”
“Gosu Gosu?
“Ndiyo”
“Hakuna watu waliouziwa
nyumba hii?
“Hakuna kaka.Nilisikia kuna
mali zako zimeuzwa lakini
nyumba hii
haikuuzwa.Tunaendelea
kuuishi mimi na Gosu Gosu”
“Ahsante Mungu” akasema
Mathew na kushusha pumzi
“Gosu Gosu yuko
wapi?akauliza Mathew na Lucy
akaanza tena kulia
“Imetosha Lucy usilie tena”
akasema Mathew
“Nieleze tafadhali mahala
alipo Gosu Gosu”
“Gosu Gosu…” akasema
Lucy na kushindwa kuendelea
akaendelea kulia
“Yuko wapi Gosu Gosu?
Mathew akauliza
“Yuko hospitali amepigwa
risasi juzi”
“Amepigwa risasi?
“Ndiyo?
“Nani kampiga risasi?
“Bado haifahamiki nani
waliompiga risasi” akasema
Lucy na Mathew akavuta pumzi
ndefu na kuuliza
“Vipi hali yake?
“Hali yake ni mbaya
anapumua kwa msaada wa
mashine”
“Oh my God ! akasema
Mathew
“Yuko hospitali
gani?akauliza
“Hospitali ya Mtodora”
akajibu Lucy na Mathew
akasimama
“Lucy vile vitu vilivyokuwa
chumbani kwangu vimewekwa
wapi?akauliza Mathew
“Hakuna kitu hata kimoja
kilichotolewa chumbani
kwako.Chuba chako kilifungwa
.Ni mimi tu ambaye huingia na
kufanya usafi”
“Ahsante sana Lucy naomba
ufunguo wa chumbani kwangu”
akasema Mathew na Lucy
akaenda chumbani kwake
akachukua funguo na kumpatia
Mathew wakaelekea katika
chumba cha
Mathew.Akaufungua mlango
wakaingia ndani
“Kila kitu ni kama
nilivyokiacha” akasema Mathew
“Nimekuwa nikiingia mara
kwa mara kufanya usafi”
“Lucy nakushukuru
sana.Naomba unipe dakika
chache nisubiri hapo nje”
akasema Mathew na Lucy
akatoka.Mathew akaenda kukaa
kitandani
“Chumba hiki sikutegemea
kukiona tena.Ahsante Mungu
kwa kunifikisha leo katika
chuba changu.Nawashukuru pia
hawa waliokitunza chumba hiki
kwa umakini mkubwa.Kila kitu
kiko vile vile nilivyokiacha”
akawaza Mathew na kufungua
chumba chake cha siri ambacho
hukitumia kuhifadhi silaha
mbali mbali
“Silaha zangu zote ziko vile
vile”akawaza na kuchukua
bastora moja akaijaribu ikiwa
haina risasi na kutabasamu
kisha akaweka risasi na
kuifutika kiunoni
“Nani kamshambulia Gosu
Gosu na kwa nini? Akajiuliza
Mathew
“Tayari nimepata pigo la
kwanza.Gosu Gosu
nilimtegemea sana katika
misheni hii hivyo sintaweza
kuwa naye.Kama anapumua
kwa msaada wa mashine basi
hali yake ni mbaya
sana.Ninamuombea aweze
kupona.Sitaki kumpoteza Yule
mwanajeshi.Hata kama
nitamkosa katika misheni hii
lakini nitamuhitaji huko
mbeleni.Kwa sasa ngoja
nielekee hospitali alikolazwa
nikajue maendeleo yake”
akasema Mathew na kutoka
akamuomba Lucy funguo za
gari.Kulikuwa na gari
limeegeshwa mbele ya nyumba
aina ya Mercedece benzi
alilokuwa analitumia
GosuGosu.Mathew akamuaga
Lucy kuwa anakwenda hospitali
kumtazama Gosu Gosu.
“Nimefurahi kwa Peniela
kutokuiuza nyumba
yangu.Nimefurahi pia kwa
namna Gosu Gosu alivyoitunza
hadi leo hii.Chumba changu
hakijawahi kuguswa kila kitu
kiko vile vile.Je Gosu Gosu
aliamini siku mojaninaweza
kurejea ndiyo maana
akakifunga chumba changu na
hakutaka kukitumia? akawaza
Mathew na kuingia katika kituo
cha mafuta akajaza mafuta ya
kutosha katika gari na kuelekea
hospitali
Geti la kuingilia hospotali
ya mtodora lilikuwa wazi
Mathew akapita na kwenda
hadi maegesho akafungua
mlango na kushuka akatazama
pande zote kuhakiki usalama
halafu akaanza kupiga hatua
kuelekea katika jengo la
mapokezi ambako aliwakuta
wahudumu kadhaa akawauliza
mahala alipo mgonjwa wake
Gosu Gosu,akaelekezwa
kwamba yuko katika jengo la
wagonjwa mahututi bila
kupoteza muda Mathew
akaelekea huko.Alipolikaribia
jengo hilo akasimama ghafla
baada ya kumuona mtu Fulani
kwa mbali
“Austin ?! akajiuliza
Mathew kwa sauti ndogo
“Ni yeye kweli au
nimemfananisha? Akajiuliza
akiendelea kumtazama
“Macho yangu bado yana
nguvu ya kutosha.Sina shaka na
kile ninachokiona.Yule atakuwa
ni Austin.He’s alive” akawaza
Mathew na kuanza kupiga hatua
kumsogelea.Mtu Yule alikuwa
ameinamisha kichwa akitazama
chini alionekana kuwa na
mawazo mengi sana
“Hallo brother” akasema
Mathew na kumstua Yule mtu
ambaye aliinua kichwa
wakatazamana.Mathew akavua
kofia na miwani.
“Mungu wangu !! akasema
Austin kwa mstuko
mkubwa.Alikuwa ameshika
karatasi kadhaa
zikamponyoka.Walitazamana
kwa muda wa sekunde kadhaa
“Hallo Austin ! akasema
Mathew
“Ma..mamamamath…”
Austin alitetemeka mdomo
akashindwa
kutamka.Akatazama kulia na
kushoto kama vile anataka
kukimbia
“Usiogope Austin ni mimi
Mathew Mulumbi” akasema
Mathew na kumpa mkono
“How’re you?akauliza
Mathew.Bado Austin aliendelea
kumtazama kwa hofu
“Austin usiwe na hofu.Ni
mimi Mathew.I’m not a
ghost.Nishike mkono tafadhali”
akasema Mathew akiwa
ameunyoosha mkono
wake.Taratibu Austin akauinua
mkono wake wa kulia na
kuushika mkono wa Mathew
akauminya kidogo na
kumtazama usoni
“This is unbelievable !!
akasema kwa sauti ndogo
halafu akamkumbatia Mathew
kwa nguvu.
“Ouh Mathew my brother !!
akasema Austin na Mathew
akahisi bega lake lilikuwa
linaloa machozi
“It’s okay
Austin.Imetosha.Hatuna sababu
ya kumwaga machozi.We cry
for the dead but I’m not
dead.I’m still alive” akasema
Mathew lakini Austin akajikuta
amechuchumaa chini akimwaga
machozi.Watu waliokuwepo
eneo lile wakawatazama
wakihisi labda Austin amepata
taarifa mbaya kuhusu mgonjwa
wake
“Austin usilie.Inuka
tafadhali” akasema Mathew na
kumnyanyua .
“Mathew Mulumbi !
akasema Austin na
kumkumbatia tena Mathew.
“Huu kwangu ni muujiza
mkubwa sana ambao sikuwa
nimeutarajia kabisa.Mathew !!
Bado Austin alikuwa katika
mshangao .
“Austin tutazungumza
mengi lakini kikubwa
kilichonileta hapa ni Gosu
Gosu.Nataka kujua maendeleo
yake”
“Hali yake si nzuri.Naamini
hadi umefika hapa tayari
umekwisha pewa taarifa
kwamba hata kupumua ni kwa
msaada wa mashine.Mathew
tunaweza kumpoteza Gosu
Gosu.Anything can happen!
akasema Austin akionekana
kukata tamaa.
“Dah ! hili ni pigo kubwa
sana.Nahitaji kumuona. I need
to talk to him” akasema Mathew
na Austin akazungumza na
wauguzi,Mathew akavishwa
mavazi maalum na kuingia
ndani ya chumba alimolazwa
Gosu Gosu.Akamtazama
“Please God don’t take him
yet.We still need him” Mathew
akaomba kimya kimya kisha
akavuta kiti akaketi karibu na
Gosu Gosu
“Papi Gosu Gosu it’s me
Mathew Mulumbi.I’m not dead
and I’m back home” akasema na
kuvuta pumzi ndefu
“Kwa mara ya kwanza
nilipokuja kukuchukua kutoka
kwa Kasu niliamini mimi nawe
tunaweza kuwa watu wa karibu
sana na ndivyo
ilivyokuwa.Sifahamu kwa nini
nilikuamini sana na baada ya
operesheni ile kumalizika
nikakuweka msimamizi wangu
wa miradi kazi ambayo
uliifanya kwa umakini na
uaminifu mkubwa
sana.Umekuwa si rafiki bali
ndugu yangu.Nikiwa njiani
nikirejea nyumbani wewe ndiye
mtu wa kwanza ambaye nilitaka
kukutana naye lakini kwa
bahati mbaya nimekukuta
ukiwa katika hali hii.Gosu Gosu
wewe ni mwanajeshi
usiyeogopa chochote.I know
you’re going to fight this.Please
fight my brother.I need you so
badly so don’t leave me yet.I
know you’re listening to me
right now so fight for your life.I
have a bigger mission and I
need you.Utakapoamka
nitakueleza nilikuwa wapi na
kwa nini ninakuhtaji sana”
akasema Mathew na kusimama
“Please fight Gosu Gosu and
wake up very soon ! akasema
Mathew na kutoka
“Umeona mwenyewe hali
yake ilivyo” akasema Austin
“Hali yake inakatisha tamaa
sana lakini Gosu Gosu ni
mpiganaji nimemwambia
apambane aamke naamini
amenisikia” akasema Mathew
“Hata mimi nimekuwa
nikiamini hivyo kwamba
ataamka muda si mrefu
kutokana na ujasiri wake lakini
naona siku zinakwenda hakuna
maendeleo yoyote ya kutia
moyo.Usiku unapita unakuja
mchana unaingia tena usiku
lakini bado Gosu Gosu hana
dalili zozote za kuamka.Mathew
mimi ni jasiri sana lakini katika
hili nimeanza kukata
tamaa.Tunakwenda kumpoteza
Gosu Gosu” akasema Austin
“Austin usiruhusu hata siku
moja roho ya kukata tamaa
ikakuingia.Unatakiwa uwe na
imani hata pale ambapo hakuna
matumaini.Kuwa na moyo
mgumu kama wa jiwe usikubali
kushindwa.Kwa hili la Gosu
Gosu bado hatuna sababu ya
kukata tamaa.Tuendelee
kusimama imara karibu yake na
atazinduka.Akiwa katika hali ile
anaweza akakaa hata mwaka na
hatupaswi kukata tamaa.Ni
wajibu wetu kumkumbusha kila
mara kwamba tuko karibu yake
na tunamuhitaji
azinduke.Atatusikia na
atazinduka.Gosu Gosu is our
brother,we love him and we
don’t give up on people we
love.You understand me Austin
? akasema Mathew
“I understand Mathew”
akasema Austin.Baada ya muda
kidogo Mathew akauliza
“Tukio hili
limetokeaje?Nani waliompiga
risasi Gosu Gosu?
“Mpaka sasa haifahamiki
nani waliofanya tukio
hili.Taarifa za Gosu Gosu
kupigwa risasi nilizipata kutoka
kwa mchumba wake anaitwa
Melanie.Alinipigia simu usiku
na kunijulisha kwamba Gosu
Gosu yuko hospitali amepigwa
risasi ndipo nikaja hapa mara
moja na kumkuta akiwa
ametoka kufanyiwa upasuaji na
alikuwa anaendelea vyema
lakini usiku hali yake
ikabadilika akalazimika
kuwekwa katika mashine ya
kumsaidia kupumua” akasema
Austin
“Gosu Gosu tayari ana
mchumba?Yuko wapi? Mathew
akauliza
“Hata mimi sikuwa
nikifahamu alifanya siri.Baada
ya tukio hili kutokea ndipo
nikamfahamu.Aliniaga juzi
kwamba atakuwa na safari
lakini hakunieleza anakwenda
wapi na toka wakati huo
sijamuona tena hapa hospitali
wala kupiga simu kuulizia hali
ya mchumba wake ikoje”
akasema Austin
“Kwa maelezo aliyonipa
Melanie ni kwamba Gosu Gosu
alikuwa anatoka ofisini kwake
nyakati za jioni na wakati
akijiandaa kuingia katika
barabara kuu ikatokea piki piki
ikiwa na watu wawili wenye
silaha wakaanza kulishambulia
gari la Gosu Gosu kwa
risasi.Walikuwa na lengo la
kumuua kabisa lakini
kilichomsaidia akanusurika ni
fulana isiyopenya risasi
aliyokuwa ameivaa.Ilimsaidia
kuzuia risasi nyingi kuingia
mwilini.Nimekuwa nikifuatilia
kwa jeshi la polisi kama kuna
mtuyeyote amekamatwa
kuhusiana na suala hili lakini
mpaka leo hii hakuna
aliyekamatwa ila uchunguzi
unaendelea” akasema Austin
“Kikubwa kwa sasa ni
kumuombea ili apone.Yeye
ndiye mwenye majibu yanani
waliompiga risasi na
yawezekana labda aliwaona
kwa macho.” akasema Mathew
na ukimya mfupi ukapita
“Nimefurahi kukuona
Austin.Vipi maendeleo yako?
Akauliza Mathew
“Mimi ninaendelea vyema
lakini bado niko kwenye
mstuko mkubwa.Sikutegemea
kabisa kukuona hapa” akasema
Austin lakini Mathew
“Hata mimi sikutegemea
kabisa kama ningekukuta
hapa.Sikujua kama ulisalimika
usiku ule” akasema Mathew
“Nilisalimika Mathew lakini
tulipoteza watu wengi sana
usiku ule na wote
tuliamin………..” akasema Austin
lakini Mathew akamkatisha
“Austin tuna mengi ya
kuzungumza na mazingira haya
si rafiki sana.Tutafute sehemu
nzuri tutulie tuzungumze”
akasema Mathew na haraka
haraka Austin akaenda
kuzungumza na wauguzi kisha
akamfuata Mathew akamtaka
waondoke.
“Jaribu kumpigia simu huyo
mchumba wa Gosu Gosu
ninataka kuonana naye”
akasema Mathew na Austin
akapiga simu lakini simu ya
Melanie haikuwa ikipatikana
“Hapatikani simuni”
akasema Austin
“Unafahamu anakoishi?
“Hapana sifahamu.Kwa
ujumla simfahamu vyema huyo
mwanamke.Nimefahamiana
naye hapa hapa hospitali na
hatujapata nafasi ya
kuzungumza kujuana
vizuri.Nimeshangaa kwa Gosu
Gosu kutonijulisha kuhusu
suala hili la kuwa na mchumba
wakati masuala yake karibu
yote huwa ananijulisha”
akasema Austin.Mathew
akakata kona kuingia katika
hoteli iliyokuwa karibu na
hospitali.Wakatafuta sehemu
tulivu wakaketi muhudumu
akafika na kuagiza vinywaji
“Austin najua una maswali
mengi unataka kufahamu
kuhusu mimi.Nilikuwa wapi na
yote yaliyonitokea lakini
nakuomba usiniulize chochote
kuhusu suala hilo.Kitu cha
msingi ni kufahamu tu kwamba
niko hai inatosha” akasema
Mathew
“Ni kweli Mathew kuna
mengi ninataka
kuyafahamu.Kuanzia usiku ule
wa tukio hadi leo hii
ulipotokea.Hakuna aliyeamini
kama uko hai kufuatia
shambulio lile baya” akasema
Austin.Mathew akanywa
kinywaji chake kidogo kisha
akauliza
“Did you search for me?
Akauliza Mathew.Swali lile
lilimfanya Austin abaki kimya
“Answer me Austin.Baada
ya tukio la usiku ule mlijaribu
kunitafuta kujua mahala
nilipo?akauliza Mathew
“Rais alituma kikosi
maalum siku iliyofuta kwenda
kukutafuta lakini ni kikosi hicho
kilichorejea na majibu kwamba
kuna uwezekano mkubwa
uliuawa na kuliwa na fisi”
akasema Austin
“Siulizi kuhusu Rais nauliza
kuhusu wewe.Did you search
for me? Akauliza Mathew na
Austin akabaki kimya
“Wewe ndiye uliyeongoza
kikosi cha pili ambacho jukumu
lake kubwa lilikuwa ni kulinda
kikosi cha kwanza ambacho
nilikuwa nakiongoza
mimi.Baada ya shambulio lile
kutokea ukiwa kama kiongozi
ulijaribu kunitafuta? Akauliza
Mathew na Austin akafikiri
kidogo kisha akasema
“Baada ya shambulio lile la
ghafla kukoma tulianza
kukusanya miili ya watu wetu
na karibu kikosi chako chote
ulichokuwa unakiongoza
kiliuawa na miili ikapatikana
lakini ni wewe pekee
uliyekosekana.Niliwaelekeza
watu wangu tuendelee
kukutafuta tukagundua pia
kwamba watu wa IS nao karibu
wote walikuwa wameuawa
lakini Edger Kaka hakuwa
miongoni mwao.Tuliamini
labda umejificha sehemu Fulani
karibu na pale lakini wakati
tukiendelea kukutafuta taarifa
zilimfikia Rais ambaye kwa
wakati huo alikuwa kambini
akifuatilia kwa karibu tukio lile
na akaamuru tuondoke haraka
sana eneo lile.Nilimueleza
kwamba wewe umekosekana
lakini akaamuru niondoe kikosi
mhala pale kwani tayari ilikuwa
ni hatari kwetu.Kama
tungeendelea kukaa pale
kukutafuta tungeendelea
kuwaweka hatarini hata wale
mateka tuliowakomboa hivyo
nikaondoa kikosi.Samahani
sana Mathew mzigo wote wa
lawama nastahili kuubeba
mimi” akasema Austin
“Hustahili lawama.Ulitimiza
amri uliyopewa na mkuu
wako.Najua usingekubali
kuniacha porini kwani siku zote
kiongozi unapopewa kikosi
ukiongoze katika misheni
Fulani unapaswa kuwarejesa
watu wako wote nyumbani
wakiwa wazima au wamekufa”
“Ahsante Mathew kwa
kulitambua hilo lakini ni jambo
ambalo limekuwa likinitesa
sana moyoni kwamba sikufanya
juhudi za kutosha usiku ule
kukutafuta”
“Austin usibebe lawama
ambazo hustahili.Tuachane na
hayo vipi kuhusu wale mateka
tuliokwenda kuwakomboa
walifika nyumbani salama?
“Wote walifika nyumbani
salama”
“Pamoja na yote yaliyotoea
lakini kumbe misheni
ilifanikiwa.Vipi kuhusu Olivia
huwa mnaonana?
“Mara chache sana huwa
tunaonana.Taarifa za kifo chako
zilimumiza mno” akasema
Austin
“Vipi kuhusu Ruby
mnawasiliana?akauliza Mathew
“Ruby amekuwa
akiwasiliana na Gosu Gosu mara
kwa mara na kwa sasa anafanya
kazi katika mamlaka kuu ya
mawasiliano ya kiintelijensia
nchini Uingereza GCHQ”
“Anafanya kazi GCHQ?
“Ndiyo.Mahusiano yangu
naye si mazuri toka wakati ule
ulipopotea na ananilaumu mimi
kwa kile kilichotokea na
kusababisha kile ambacho
wengi tuliamini kifo chako.Mara
ya mwisho kuwasiliana naye ni
miezi kadhaa imepita.Mimi na
Gosu Gosu tulihitaji msaada
wake katika misheni Fulani
muhimu sana”
“Misheni ipi?akauliza
Mathew
“Ilikuwa ni misheni moja
muhimu sana kwa nchi na
ambayo ilileta kiza zaa
kikubwa” akasema Austin
“Ilihusu nini hiyo misheni?
Mathew akauliza
“Tulitakiwa kumuua
mwanasiasa mmoja wa kutoka
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo” akasema Austin
“Nini ilikuwa sababu ya
kutaka kumuua?Nieleze kwa
undani zaidi jambo
hilo”akasema Mathew
“Mheshimiwa Rais Dr
Fabian alipewa taarifa na Rais
Patrice Eyenga wa Congo
kwamba kuna mwanasiasa
mmoja anatumiwa na mataifa
ya nje katika mpango wa
kuisambaratisha jumuiya ya
Afrika mashariki.Rais wa sasa
wa Congo Patrice Eyenga
amefanikiwa kumaliza
mchafuko yaliyoitawala nchi
hiyo kwa muda mrefu na hilo
halijawapendeza nchi kubwa
waliokuwa wakifaidika na
machafuko hayo ndiyo maana
wakataka kumtumia
mwanasiasa huyo ili awe daraja
la kuwavusha kurejea tena
kuendelea kuinyonya
Congo.Baada ya kupewa taarifa
hiyo Ras Dr Fabian alitupa sisi
kazi ya kumuondoa
mwanasiasa huyo aliyeitwa
Lucy Muganza”
“Mwanasiasa huyo alikuwa
ni mwanamke?Mathew akauliza
“Ndiya alikuwa ni
mwanamama
bilionea.Nikishirikiana na Gosu
Gosu na vijana wengine
tulifanikisha misheni hiyo na
kumuua Lucy Muganza na
mume wake Laurent
Muganza.Baada ya mauaji hayo
kuna makosa
yalifanyika.Tulipomuua Lucy
Muganza na mumewe
tulitakiwa kwenda mbali zaidi
lakini tulijisahau na miili le
ikafanyiwa uchunguzi na
ikagundulika kwamba risasi
zilizotumika katika mauaji
hayoni kutoka katika bunduki
zinazotumiwa na wadunguaji
na taarifa hiyo ikamfikia balozi
wa umoja wa Ulaya hapa nchini
ambaye aliendelea kuishinikiza
serikali kuruhusu wachunguzi
wa kutoka umoja wa ulaya kuja
chini kuchunguza mauaji
yale.Balozi huyo alikuwa na
taarifa kwamba bunduki
ambazo zilitumika kuwaua Lucy
Muganza na mumewe
zinamilikiwa na jeshi na hapo
ndipo Rais akatutaka
tumchunguze balozi huyo tujue
anapata wapi taarifa nyeti kama
hizo za kuhusiana na silaha za
nchi.Ilitulazimu kumuomba
msaada Ruby katika
kumchunguza balozi huyo na
ndipo nilipofahamu kuwa
anafanya kazi katika mamlaka
kuu ya mawasiliano ya
kiintelijensia nchini
Uingereza.Tulifanikiwa
kugundua kwamba balozi huyo
alikuwa na mawasiliano ya
karibu na mkurugenzi wa idara
ya siri ya usalama wa ndani wa
nchi aliyejulikana kama
Tamar.Kwa bhati mbaya kabla
ya kupiga hatua kubwa
kumchunguza balozi huyo
aliuawa” Austin akaendelea
kumueleza Mathew kwa undani
namna misheni ilivyokuwa hadi
pale ambapo mambo yalikuja
kutulia
“Dah ! hongereni sana kwa
kazi kubwa
mliyoifanya.Nimefurahi kwa
namna mlivyoendesha misheni
hiyo.Umeniambia kwamba
mlimshauri Rais amuite Ruby
nyumbani ili awe mkurugenzi
wa ile idara ya SNSA”
“Ndiyo.Tulimshauri hivyo
mheshimiwa Rais na aliahidi
kulitekeleza hilo suala lakini
mpaka leo hatujapata mrejesho
wowote kutoka kwake amefikia
wapi katika suala hilo la
kumshawishi Ruby aweze kuja
hapa nchini” akasema Austin
“Ahsante sana kwa
kumshauri Rais jambo
hilo.Idara ile ni muhimu sana
kwa nchi lakini tayari mabeberu
wamekwisha pandikiza watu
wao.Naamini hata baada ya
Tamar kuondoka bado kuna
mapandikizi yamebaki kwani
hawezi kuwa peke yake lazima
wawepo watu aliokuwa
anashirikiana nao ambao
wataendeleza kufanya kile
wanachokitaka mabeberu.Ruby
ni chaguo zuri na anafaa sana
kuongoza idara kama ile.Kuna
ulazima wa kufuatilia kujua
Rais amefikia wapi katika suala
hilo.Una namba za simu za
Ruby?akauliza Mathew
“Hapana sina nanba zake.Ni
Gosu Gosu ndiye aliyekuwa
akiwasiliana naye”
“Simu ya Gosu Gosu iko
wapi?
“Sifahamu mahala ilipo
simu hiyo” akajibu Austin.
“Unafahamu anakoishi Rais
mstaafu Dr Evans?akauliza
Mathew
“Ndiyo ninafahamu.Anaishi
katika nyumba yake mpya”
akajibu Austin
“Nipeleke huko nahitaji
kuonana naye” akasema
Mathew huku akisimama
wakaondoka kuelekea katika
gari la Mathew ambaye
alimtaka Austin aendeshe kwa
kuwa yeye hakuwa na
leseni.Austin akaondoa gari
wakaondoka kuelekea katika
makazi ya Rais mstaafu Dr
Evans.
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 8: EPISODE 3
Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dr
Fabian Kelelo aliwasili katika
uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Julius Nyerere akitokea
mkoani Mbeya katika mazishi
ya mke wake Millen
Kelelo.Kutoka katika uwanja wa
ndege wa Julius Nyerere Dr
Fabian alielekeza apelekwe
katika nyumba yake aliyokuwa
akiishi kabla ya kuwa Rais.
Ruby akiwa amepumzika ndani
ya chumba chake alistushwa na
muungurumo wa magari
akainuka kuchungulia nje
kupitia dirishani akayaona
magari ya msafara wa Rais
yakijipanga
“Rais amekuja” akasema
Ruby na haraka haraka
akaelekea katika meza ya
vipodozi akaanza kurekebisha
uso wake kabla ya kukutana na
Rais.Akiwa katika kujiandaa
mlango wake
ukagongwa.Akajitazama katika
kioo halafu akaenda mlangoni
akaufungua akakutana na
walinzi wawili ambao
walimtaka aongozane nao
wakaelekea hadi sebuleni
ambako alimkuta Rais Dr
Fabian akiwa ametulia
sofani.Akasimama baada ya
Ruby kuingia
“Ruby ! akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
shikamoo”
“Marahaba Ruby vipi
maendeleo yako?
“Ninaendelea vyema
mheshimiwa Rais” akasema
Ruby na Rais akamfanyia ishara
aketi
“Pole sana mheshimiwa
Rais” akasema Ruby
“Ahsante Ruby nimekwisha
poa.Ni mapito ya mwanadamu
na sote njia yetu ni hiyo
isipokuwa mwenzetu
ametutangulia.Japo nina
majonzi lakini nimefurahi
kukuona Ruby karibu sana.Jana
nilishindwa kurejea kama
nilivyokuahidi niliombwa na
wazee nibaki kwa ajili ya
kukamilisha mambo ya
kimila.Naamini umekuwa
ukihudumiwa vizuri” akasema
Dr Fabian
“Usijali mheshimiwa
Rais.Nafahamu unapitia kipindi
kigumu hivyo hata kama
ingenichukua mwezi mzima
kukusubiri hakuna tatizo kwa
upande wangu kwani hapa niko
nyumbani” akasema Ruby
“Ruby napenda kwanza
kabla ya yote kukupa pole
nyingi sana kwa yote uliyopitia
katika safari ya kuja hapa.Najua
mimi ndiye sababu ya mambo
yale yote kutokea kwa kukutaka
uache kazi uliyokuwa unaifanya
uje nyumbani.Umepitia mambo
magumu sana hata kunusurika
kifo.Nilipoona jina lako katika
orodha ya watu waliofariki
katika ile ajali ya ndege
nilijilaumu mno kwa kukuomba
uje nyumbani lakini
nakushukuru kwa namna
ulivyopambana kuhakikisha
unafika salama
Tanzania.Naamini hii yote ni
mipango ya Mungu kwani
umefika katika kipindi ambacho
unahitajika sana” akasema Dr
Fabian
“Ni kweli mheshimiwa Rais
nimepitia mambo magumu hadi
kufika hapa.Kazi niliyokuwa
naifanya nchini Uingereza
iliniwezesha kufahamu mambo
mengi sana ya siri hivyo
nilipowasilisha maombi ya
kuacha kazi walistuka na
walifanya kila mbinu
kunishawishi nibatilishe
mpango wangu huo wa kuacha
kazi lakini niliendelea kushikilia
msimamo wangu na ndipo
walipoamua kupanga mpango
ule wa kuniua.Ulikuwa ni
mpango wa siri sana na
ninamshukuru mmoja wa
marafiki zangu ambaye aliweza
kunijulisha kile kilichokuwa
kimepangwa dhidi yangu na
akanisaidia hadi nimefika
hapa.Ilikuwa ni safari ndefu na
ngumu kwangu lakini
namshukuru Mungu nimefika
salama nikiwa na afya njema”
akasema Ruby
“Kwa nini walikuwa na hofu
ya wewe kuacha kazi?akauliza
Dr Fabian
“Edward Snowden wa
Marekani amewapa fundisho
ndiyo maana walistuka sana na
walihisi labda na mimi nina
mpango kama ule wa kutoa siri
zao.Waliamini nimelipwa pesa
nyingi ili niweze kuuza siri
ndiyo maana suluhisho pekee
walilokuwa nalo ni
kuniua.Ninasikitika kwamba
maisha ya watu wengi yalipotea
kwa sababu yangu” akasema
Ruby
“Pole sana
Ruby.Ninakuahidi kukulinda
kwa kila namna dhidi ya hawa
jamaa ambao mpaka sasa
wanaamini tayari umekwisha
fariki”
“Nashukuru sana
mheshimiwa Rais”
“Mimi ndiye ninayepaswa
kukushukuru wewe kwa niaba
ya watanzania.Kitendo
ulichokifanya ni cha
kizalendo.Umeacha kazi
uliyokuwa ukiifanya ambayo
ilikuwa na maslahi manono na
ukakubali kuja kuitumikia nchi
yako.Ni uzalendo wa hali ya juu
sana” akasema Dr Fabian
“Tanzania ni nchi yangu na
lazima niitike ndiyo kila pale
ninapoitwa
kuitumikia.Mheshimiwa Rais
niko tayari kwa ajili ya kazi ya
kuitumikia nchi yangu”
akasema Ruby
“Karibu sana Ruby.Kwa
kuwa kwa sasa nina ratiba
nyingine nitakuomba jioni ya
leo ikulu kwa ajili ya chakula
kisha tutazungumza kwa kirefu
sana kuhusiana na kazi ambayo
nimekuita uje kuifanya”
akasema Dr Fabian
“Nitafika mheshimiwa Rais”
akasema Ruby na Dr Fabian
akasimama na kumpa mkono
“Ruby kwa mara nyingine
tena karibu Tanzania.Karibu
nyumbani” akasema Dr Fabian
kisha akaagana na Ruby
akaondoka.
KAMPALA – UGANDA
Gari nne aina ya range
rover zenye rangi nyeupe
zilifika katika nyumba ambayo
alifikia Melanie.Ulikuwa ni
msafara wa James Kasai
ambaye alishuka na kuingia
ndani ya jumba lile.Melanie
akiwa chumbani kwake
akafuatwa na mmoja wa
wahudumu akaitwa akatoka
kwenda kukutana na James
Kasai aliyekuwa sebuleni.
“James Karibu sana”
akasema Melanie
“Nashukuru sana
Melanie.Habari za toka
juzi?akauliza James Kasai
“Ninaendelea vizuri sana
sina tatizo lolote.Unapendeza
sana ukivaa suti kuliko yale
mavazi yako ya kijeshi”akatania
Melanie na wote wakaangua
kicheko
“Nashukuru kusikia
hivyoMelanie lakini nimezoea
sana kuvaa mavazi yale ya jeshi
kwa kuwa muda wote niko
katika mapambano.Samahani
kwa kutokuja kuonana nawe
siku ya jana”
“Usijali James
ninaelewa.Nimekupigia simu ili
tuje tuzungumze kuhusiana na
lile suala letu.Umekwisha pata
mrejesho wowote kutoka kwa
Rais?akauliza Melanie
“Hapana sijapata mrejesho
wowote bado kutoka kwa
Rais.Alituahidi angewasiliana
nasi jana lakini hakufanya
hivyo.Wewe hujapata chochote
kutoka kwake? Akauliza James
na Melanie akatoa kicheko
kidogo
“Hawezi kuwasiliana nami
kabla hajakujulisha kwanza
wewe.Hata hivyo dhumuni la
kukuita hapa kuna jambo
nataka tulijadili kuhusiana na
ule mpango wetu wa kumuua
Patice Eyenga”
“Karibu”akasema James
“Juzi tulipokwenda
kuzungumza na Rais alitueleza
kwamba anataka kushirikiana
nawatu kutoka ndani ya serikali
ya Congo katika mpango wa
kumuua rais Patrice
Eyenga.Anachotaka kukifanya
Rais Akiki si kitu kibaya lakini
tatizo la huo mpango wake ni
kwamba utachukua muda
mrefu kwanza kuwashawishi
watu waweze kukubaliana na
mpango huo na vile vile upo
uwezekano kwamba watu hao
ambao anataka kuwashirikisha
wakakataa kushirikiana
naye.Kama ikitokea watu hao
wakakataa kushirikiana naye
mpango utakuwa umekwama
na siri itakuwa imevuja
kwamba Rais Patrice anataka
kuuawa.Nimelitafakari sana hilo
nikaamua kuja na mpango
mpya ambao tutauwasilisha
kwa Rais Akiki” akasema
Melanie na kunyamaza kidogo
“Mpango gani umekuja
nao?akauliza James
“Kwa hivi sasa Uganda na
Congo hazina maelewano
mazuri.Hii ni fursa ambayo
tunatakiwa kuitumia.Jenerali
Akiki atawasiliana na Rais wa
Tanzania ambaye ndiye
mwenyekiti wa jumuiya ya
Afrika Mashariki kwa sasa na
atamuomba wakutane pamoja
na rais wa Congo ili kutafuta
suluhu ya mgogoro
unaoendelea hivi sasa na kikao
hicho kifanyike jijini Dar es
salaam.Wakati kikao hicho
kikiendelea tutapandikiza bomu
katika ndege ya Rais Patrice na
pale atakapokuwa angani
akirejea Congo tutailipua ndege
yake.Ni mpango ambao
hautahitaji mtandao mkubwa
kama anaotaka kuutengeneza
Rais Akiki na vile vile
hautachukua muda
mrefu.Unauonaje mpango
huo?akauliza Melanie.James
akafikiri kidogo na kusema
“Ni mpango mzuri japo nao
una changamoto
yake.Changamoto kubwa ni
namna ya kulipandikiza hilo
bomu katika ndege ya Rais
ambayo inakuwa na ulinzi mkali
wakati wote” akasema James
“Ndiyo maana nikauita
hapa ili tuweze kujadiliana
suala hilo.Mimi kwa upande
wangu ninaweza kutengeneza
mtandao ambao unaweza
ukatusaidia kuingiza bomu
katika ndege hiyo ya Rais
Patrice ”akasema Melanie
“Hilo ndio hasa kubwa
tunalolihitaji katika huo
mpango.Kama unao uwezo wa
kutengeneza mtandao
unaoweza kutusaidia basi
hakuna tatizo tunaweza
kuendelea na mpango
huu”akasema James
“Katika huo mpango
tutawahitaji watu wa IS.Baada
ya mlipuko kutokea na Patrice
kuuawa IS watajitokeza na
kudai kwamba wao ndio
waliohusika katika shambulio
hilo bila kutoa sababu
yoyote.Hakuna ambaye atajua
umehusika bali mzigo wote
wataubeba IS.Baada ya kifo cha
Patrice jeshi naamini linaweza
kutangaza kuchukua nchi na
hapo ndipo machafuko
yatakapoanza na wewe
utaendelea na mapambano na
serikali na safari hii ukiwa na
jeshi lenye nguvu na zana za
kisasa.”akasema Melanie
“Kweli ni mpango mzuri na
hata mimi nimeupenda sana
hivyo basi tuanze
maandalizi.Kwanza tuanze kwa
kuzungumza na Rais
Akiki.Nitawasiliana naye
kumueleza kwamba tunahitaji
kuzungumza naye na
tukikutana nitajaribu
kumshawishi aukubali mpango
huu ambao naamini hataweza
kuukataa hivyo jambo kubwa ni
kuandaa namna bomu hilo
litakavyoweza kuingizwa katika
ndege ya Rais.Hata hivyo kuna
kitu ninakiwaza.Kwa nini bomu
hilo lisiingizwe ndegeni jijini
Kinshasa? Tunaweza
kumchagua rubani mmoja wa
ndege ya Rais tukaiteka familia
yake na kumlazimisha aliingize
sanduku lenye bomu ndani ya
ya ndege ya Rais wakati
akijiandaa na safari ya kuja
Tanzania na Rais Patrice auawe
kabla hajafika Dar es
salaam.Unaonaje wazo hilo?
“Ni wazo zuri
pia.Tutayajadili haya yote na
Rais Akiki pale tutakapokutana
naye.James mimi ninafanya hivi
kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa
wazazi wangu lakini wewe
fanya kwa ajili ya harakati zako
za kuiomboa Congo.Kama
alivyosema Jenerali Akiki
kwamba ni wewe pekee
ambaye unapambana kwa
maslahi mapana ya Congo lakini
wengine wote wanapambana
kwa maslahi yao na wakubwa
wanaowafadhili hivyo hakikisha
mapambano yanandelea na siku
moja unafanikiwa kuingia hadi
Kinshasa”
akasema Melanie
“Melanie ahsante kwa
ushauri huo mzuri.Ni kweli
kama alivyosema Rais Akiki
kwamba ninapambana kwa ajili
ya maslahi ya Congo na ndiyo
maana siungwi mkono na taifa
lolote la Ulaya bali anayeniunga
mkono ni Rais Akiki pekee
ambaye anafahamu nia yangu
ya dhati ya kuikomboa
Congo.Ninakuahidi kwamba
mapambano yataendelea hadi
pale nitakapohakikisha
nimeitawala Congo” akasema
James
“Kuhusu IS umepanga
kushirikiana nao hadi lini?
Melanie akauliza
“IS nitaendelea
kushirikiana nao kwa ajili ya
kuniwezesha kijeshi.Kwa sasa
ninahitaji kikosi chenye nguvu
kubwa hivyo basi nategemea
kupata silaha kali na za kisasa
kutoka kwao.Mkataba wa
mashirikiano yangu nao ni kwa
ajili ya kuwasaidia kujenga
kambi yao ya mafunzo katikati
ya misitu”
“Ni vipi kama baadae
likawa jeshi kubwa na wao pia
wakaanza kupigana na serikali?
Akauliza Melanie
“Wanachokitaka wao ni
sehemu ya kufanyia mafunzo
kwa watu wao ambao
watawatuma sehemu
mbalimbali duniani.Hawana
mpango wowote wa
kushambulia Congo” akasema
James
“James nimeuliza swali hilo
kwa sababu watakapopata
sehemu ya kuweka kambi ya
mafunzo wataanza kujiimarisha
taratibu na pale watakapokuwa
na jeshi kubwa basi
wataanzisha mapigano na
serikali na kama unavyojua
hawa jamaa wakikita mizizi yao
sehemu Fulani kuwaondoa
huwa vigumu sana” akasema
Melanie
“Usiwe na hofu
Melanie.Nimekwisha kubaliana
nao kuwasaidia kupata kile
wanachokitaka na mimi niweze
kupata kile
ninachokitaka.Tuachane na
suala hilo una taarifa zozote za
Gosu Gosu?
“Sijapiga simu nyumbani
kuuliza hivyo sijui
kinachoendelea kuhusu hali
yake” akasema Melanie
“Melanie unatakiwa
kumjulia hali mpenzi wako.Piga
sim…” akasema James na
Melanie akamkatisha
“Nitawasiliana nao kujua
maendeleo yake usihofu”
akasema na James akamuaga
kwa ahadi ya kumpa mrejesho
baadae pale atakapokuwa
amezungumza na Jenerali Akiki.
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Gari la akina Mathew
lilisimamishwa na askari
waliokuwa wakilinda geti la
kuingilia nyumbani kwa Rais
mstaafu wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dr
Evans.Hawakuwa na miadi ya
kuonana na Dr Evans hivyo
mmoja wa askari akapiga simu
ndani ikapokelewa na mtumishi
wa ndani akamuomba
azungumze na Dr Evans
akamjulisha kuwa kuna wageni
wake ambao ni Austin January
na mwenzake wamefika
kuonana naye.Baada ya
kuzungumza na simu askari
Yule akaelekeza geti lifunguliwe
na akina Austin wakaruhusiwa
kuingia ndani.
“Umewahi kuja
huku?akauliza Mathew
“Ndiyo nimekuwa nikifika
mara kadhaa kumsalimu mzee”
akajibu Austin.
Waliegesha gari na
kushuka.Mmoja wa watumishi
wa Dr Evans akaenda
kuwapokea na kuwaongoza
kuelekea ndani.Austin
alitangulia mbele na Mathew
akamfuata
nyuma.Aliwakaribisha sebuleni
akawahudumia vinywaji halafu
akaenda kumuita Dr
Evans.Baada ya dakika chache
Dr Evans akatokea akiwa
ameshika gazeti mara gazeti
alilolishika likaanguka chini
baada ya kukutanisha macho na
Mathew Mulumbi.
“Jesus Christ ! akasema
huku akigeuka na kutazama
nyuma kama vile alitaka
kukimbia
“Shikamoo mzee” akasema
Austin
“Mar..marahaba Austin !
akaitika Dr Evans huku macho
yake akiwa bado ameyaelekeza
kwa Mathew.
“Shikamoo mzee”akasema
Mathew na Dr Evans
akamtazama Austin
“Is this real?akauliza
“It’s real mr President”
akajibu Austin.
Mara Dr Evans akashika
kifuani na kunza kupepesuka
akataka kuanguka.Austin
akamuwahi akamdaka na
kumkalisha sofani
“My pills” akasema Dr
Evans kwa taabu.Mathew
akamuita mtumishi wa Dr
Evans na kumtaka aonyeshe
zilipo dawa za mzee.Mtumishi
Yule akakimbia na kwenda
kuleta kichupa kidogo cha dawa
akatoa dawa mbili na kumpa
Mathew ambaye alimpa Dr
Evans akanywa haraka haraka
kisha akalazwa sofani.
“Mzee amekuwa
akisumbuliwa na matatizo ya
moyo na tatizo kama hili
limekuwa likimtokea mara kwa
mara” akasema Yule mtumishi
wake.Mathew akamuelekeza
ampigie simu daktari wake.
“Mathew utaua watu kwa
mstuko.Kila anayekuona
anapatwa na mstuko
mkubwa.Hakuna anayeamini
kama bado uko hai mpaka
sasa.Hata mimi nilipatwa na
mstuko mkubwa na
nilichuchumaa chini kwa kuwa
miguu iliniisha nguvu” akasema
Austin
“Naomba ujio wangu usije
ukasababisha maafa” akasema
Mathew.
Daktari wa Dr Evans alifika
akampima na kumkuta
anaendelea vizuri.
“Hakuna tatizo anaendelea
vyema” akasema Daktari na
kumpa maelekezo Yule
mtumishi kisha akaondoka
“Mlinzi wa mzee yuko
wapi?Alipaswa kuwa naye
hapa” akasema Mathew
“Mlinzi wa mzee amepata
dharura ndiyo maana leo
hayupo” akajibu Yule
mtumishi.Dr Evans akainuka
sofani na kuketi
“Mzee unajisikiaje?
Akauliza Austin
“Najisikia vizuri” akajibu Dr
Evans
“Pole sana mzee” akasema
Mathew
“Mathew ..” akasema Dr
Evans na kutaka kunyanyuka
lakini Mathew akamtaka
aketi.Akaendelea kumtazama
kwa macho yaliyojaa hofu.
“I can’t believe this.Ni wewe
kweli Mathew Mulumbi?
Akauliza Dr Evans
“Ni mimi mzee.I’m still
alive” akajibu Mathew
“I’m so sorry Math……”
“Usijali mzee.Austin tayari
amekwisha nieleza kila kitu
kilichotokea” akasema Mathew
“Mathew ninatamani hata
niyapofue macho yangu
nisiweze kukutazama
usoni.Ninaona aibu.Ulifanya
jambo kubwa sana kwa nchi na
kwangu pia.Uliwakomboa
watoto waliokuwa wametekwa
na magaidi na vile vile
ukamkomboa mwanangu
aliyekuwa mikononi mwa
magaidi lakini kama
alivyokueleza Austin usiku ule
lilipotokea lile shambulio baya
kabisa nilifanya maamuzi
magumu ya kumtaka akiondoe
kikosi kile na miili yote
iliyopatikana.Nilihofia
kungekuwa na shambulio
lingine na yawezekana
tungeweza hata kupoteza kikosi
kizima.Nakiri yalikuwa ni
maamuzi magumu sana
kuyafanya katika kipindi
changu chote cha
urais.Nilikubali kikosi kiondoke
na kumuacha mtu muhimu
kabisa kwa taifa.Siku iliyofuata
nilituma tena kikosi kingine
kwenda eneo la tukio kutafuta
kama wangeweza kukupata
walau hata mwili wako lakini
hawakupata kitu chochote na
taarifa waliyoirejesha ni
kwamba utakuwa ulifariki
dunia na maiti yako kuliwa na
fisi kwani walikuta kuna
mabaki kadhaa ya maiti
zilizoliwa na fisi eneo
lilipofanyika lile
shambulio.Baada ya kupewa
taarifa ile nilituma ujumbe kwa
mke wako Peniela jijini Paris
Ufaransa kumfahamisha
kilichotokea na kumpa pole
sana.Hakuna aliyejua kama uko
hai Mathew tusamehe sana”
akasema Dr Evans
“Mheshimiwa Rais
nafahamu yalikuwa ni maamuzi
magumu kabisa uliyafanya na
siwezi kukulaumu kwani hata
mimi ningekuwa mahala pako
ningefanya hivyo hivyo lakini
unapotuma watu katika misheni
Fulani lazima uhakikishe wote
wanarejea nyumbani wawe
wazima au wamekufa.Watu
wanapotumwa misheni Fulani
wanakwenda kupambana kwa
ajili ya nchi hivyo lazima hata
kama wamefariki wazikwe
kishujaa katika ardhi ya
nyumbani kwao.Kilichofanyika
kwangu kiwe somo wakati
mwingine kuwathamini wale
wanaotumwa kupambana kwa
maslahi ya nchi.Hata hivyo
ninataka kujua baada ya taarifa
kurudi kwamba nimeliwa na fisi
mlichukua hatua
zipi?Mlithubutu hata
kutengeneza kaburi mkazika
hata kiatu changu kuonyesha
kunithamini? Akauliza Mathew
“Hatukufanya hivyo”
akasema Dr Evans
“Hukuwa na mawazo hayo
kwa kuwa kile ulichokuwa
unakihitaji ulikwisha
kipata.Mwanao alikombolewa
na hukujisumbua tena kuhusu
Mathew Mulumbi.Hukutaka
hata kutuma timu ya kufanya
uchunguzi wa kina kufahamu
nini kilitokea.Ulifanya hivyo?
“Hatukufanya hivyo”
akajibu Dr Evans
“Mpaka leo hamjui nini
hasa kilitokea usiku ule! Hamjui
nani walitushambulia na kwa
nini! Hukutaka kusumbuka kwa
sababu mwanao alikuwa
amepatikana.Katika orodha ya
watu waliofariki dunia kwenye
ile misheni mlithubutu hata
kuliweka jina langu? Akauliza
Mathew na wote wakawa kimya
“Mheshmiwa Rais
ninaipenda sana nchi yangu
lakini ninyi viongozi
mnakatisha tamaa wazalendo
kama mimi ambao wako tayari
kumwaga damu yao kwa ajili ya
nchi.Licha ya mchango mkubwa
nilioutoa kwa nchi yangu lakini
bado thamani ninayoipata ni
ndogo mno.Hata hivyo siko
hapa kuomba nithaminiwe
kwani ni Mungu pekee
atakayeweza kunilipa lakini
ninataka kuwaeleza mtambue
makosa mliyoyafanya.Najua
hauko katika uongozi hivi sasa
lakini unayo sauti na unasikika
ukiongea hivyo basi nataka
uwashauri walio katika
madaraka hivi sasa
kuwathamini watu kama
mimi,kama Austin watu kama
Gosu Gosu ambaye hivi sasa
yuko mahututi akipigania
maisha yake.Hatuombi litokee
kwani Mungu ndiye mpanga
yote lakini anaweza akapoteza
maisha na akifariki ndiyo
anasahaulika kabisa.Nataka
uwabadilishe viongozi walio
madarakani wawe na uthubutu
wa kuthamini mchango wa wale
wanaojitolea kwa ajili ya nchi
yao.Wapo wanajeshi,askari
polisi na wengine kutoka
vyombo mbali mbali vya ulinzi
na usalama.Mnawajali vipi pindi
wakistaafu utumishi au
wakiumia wakiwa kazini?
Fikisha ujumbe huu kwa
wenzako walio madarakani
”akasema Mathew kisha akavua
fulana aliyokuwa ameivaa
akafungua fulana ya kuzuia
risasi aliyokuwa ameivaa ndani
na kuwaonyesha Austin na Dr
Evans makovu yaliyoko mwilini
mwake
“Dah ! akasema Austin
“Haya ndiyo
niliyopitia.Mwili wangu wote
umechafuliwa na makovu ya
vidonda” akasema Mathew
“Pole sana
Mathew.Unaweza ukatueleza
nini hasa kilichotokea?Ulikuwa
wapi? Akauliza Dr Evans
“Lengo la kuja hapa si
kueleza mahala nilikokuwa na
yapi nimepitia.Ukurasa huo
umekwisha fungwa lakini
nilitaka tu kuwapa somo
kwamba mlichokifanya
kilikuwa ni kitu kibaya kabisa”
akasema Mathew
“Mathew ninakosa maneno
ya kusema kijana wangu”
akasema Dr Evans
“Usiseme chochote.Sikuja
hapa kwa malumbano au kwa
hasira kwa nini mlinicha porini
lakini kubwa lililonileta hapa ni
kukujulisha kwamba niko hai
na sijafa kama mlivyoamini”
akasema Mathew na Dr Evans
akavuta pumzi ndefu
“Mathew hapa nilipo
sijitambui kama nina furaha au
majonzi lakini kikubwa
ambacho ninataka kukwambia
kwamba watu kama wewe
huzaliwa wachache sana katika
dunia ya sasa.Kwa nini
ninasema hivyo? Ni kwa sababu
kwa sasa nchi yetu iko katika
mgogoro mkubwa na kati kati
ya mgogoro huo umeibuka
kutoka kusikojulikana.Mathew
unaongozwa na roho wa Mungu
ndani yako ndiyo maana
umetokea kwa wakati huu
ambao nchi hii inakuhitaji sana”
akasema Dr Evans
“Sijakuelewa mzee nchi
inanihitaji kivipi?Walijua
nitarejea?Wanafahamu mahala
nilikokuwa?Wanafahamu
niliyoyapitia hadi umeniona
hapa leo?akauliza Mathew
“Hakuna aliyefahamu
mahala ulipo,hakuna aliyekuwa
anafahamu kama utakuja lakini
nchi ilikuhitaji sana mtu kama
wewe.Umetokea wakati ambao
ni muafaka kabisa.Mathew
Mungu amekuleta kwa wakati
huu isikie sauti yake na uisaidie
nchi” akasema DrEvans
“Mzee sijakuelewa nini
unakimaanisha” akasema
Mathew
“Mathew naamini Austin
amekwisha kueleza kile
ambacho kimetokea hapa
nchini siku chache zilizopita
kama bado hujasikia katika
vyombo vya habari huko
ulikokuwa”
“Ninafahamu kilichotokea
mzee.Ninafuatilia kila siku
taarifa za nyumbani kujua kila
tukio linalotokea hapa”
akasema Mathew
“Nashukuru kama
unafuatilia habari za nyumbani.
Kinachoendelea hivi sasa ni
mpango wa kuisambaratisha
jumuiya ya Afrika
Mashariki.Huu ni mpango wa
nchi kubwa
kutugawanya.Kikubwa
wanachokitaka ni kuvuruga
umoja wetu kila nchi ikae peke
yake ili wapate nafasi nzuri ya
kutunyonya.Huu ni mkakati
mzito san…..”akasema Dr Evans
na Mathew akamkatisha
“Mzee ninafahamu kila kitu
kinachoendelea hapa nchini na
kila kitu kuhusiana na mpango
huu wa kuigawanya afrika
Mashariki.Ninafahamu nchi
inayolengwa zaidi katika
mpango huu ni jamhuri ya
kidemokrasia ya
Congo.Wanataka machafuko
yarejee nchini Congo ili wapate
nafasi ya kurejea kuchuma mali
za nchi hiyo.Ninafahamu kila
kitu mzee huna hja ya kuelezea
sana” akasema Mathew.
“Where have you been
Mathew?akajiuliza Dr Evans na
ukimya ukatawala pale
sebuleni.
“Mzee najua nyote mko
katika mstuko mkubwa kwa
kuniona.Nafahamu mnayo
maswali mengi mngependa
kuniuliza,mngetaka kujua
nilikuwa wapi muda huu wote
lakini kitabu kile kilikwisha
malizika kwa mimi kutoweka
hivyo hakuna tena haja ya
kuendelea kuulizana maswali
kuhusiana na suala
hilo.Kikubwa ambacho
mnapaswa mkifahamu ni
kwamba niko mzima na
nimerejea nyumbani” akasema
Mathew na kunyamaza kidogo
halafu akasema
“Mzee umezungumza
maneno fulani kwamba Mungu
amenileta kwa wakati huu
ambao ni muafaka.Nakubaliana
nawe mzee kwa sababu hata
mimi sikutegemea kama
ningekuwa hapa muda huu
nikizungumza nanyi lakini kwa
uweza wa Mungu niko tena
katika ardhi ya
nyumbani.Nimekuja nyumbani
kumaliza kile ambacho
kinaendelea hivi sasa” akasema
Mathew na mstuko mkubwa
ukaonekana katika nyuso za Dr
Evans na Austin
“Huyu ni binadamu kweli
au ni mzimu? Alikuwa wapi
huyu hadi akaibuka kwa wakati
huu?akajiuliza Dr Evans
“Bado mpaka sasa inaniwia
ugumu kuamini kama kweli
huyu ndiye Yule Mathew
halisi.Nina wasiwasi tusije
kuwa tunachezewa na mzimu
hapa” akawaza Austin.
“Naona nyuso zenu
zimepatwa na mshangao lakini
narudia tena kuwahakikishia
kwamba nimekuja kumaliza
hiki kinachoendelea hivi sasa
hapa nchini.Nimekuja kuiokoa
jumuiya ya Afrika Mashariki
isisambaratike.Nimekuja
kummaliza James Kasi na
kuung’oa mzizi wa ugaidi hapa
Afrika mashariki” akasema
Mathew
“Mathew unaniogopesha
kwa maneno hayo
unayoyatamka” akasema Dr
Evans
“Usiogope mzee.Ulisema
mwenyewe kwamba nimekuja
kwa wakati muafaka.Ninaweza
kusema kwamba Afrika
Mashariki imeniita na siwezi
kusema hapana.Mimi ni mtoto
wa Afrika na Tanzania ambayo
iko ndani ya Afrika Mashariki
inaponihitaji lazima niitike
haraka sana.I’m back guys.I’m
the same Mathew
Mulumbi.Yawezekana mkaona
nimebadilika kidogo lakini mimi
ni Yule yule mliyenifahamu”
akasema Mathew na
kuwatazama akina Austin
ambao wote bado walikuwa
kimya wakimsikiliza.Dr Evans
akasimama
“Come here my son.I need
to hug you ! akasema Dr Evans
na Mathew akainuka akamfuata
Dr Evans wakakumbatiana
“Karibu tena nyumbani
mwana Tanzania.Sasa moyo
wangu una amani baada ya
kukuona wewe na nimepata
faraja kubwa kwa maneno yako
kwamba umekujwa kuiokoa
Afrika mashariki.Baada ya
shambulio lile la kigaidi kutokea
na kuuawa kwa wake za marais
nilikesha nikitafakari dhumuni
la shambulio lile na nikagundua
kwamba ule ulikuwa ni mtego
na viongozi wetu tayari
wamenasa katika mtego huo
kwa kuamsha hasira baada ya
wake zao kuuawa na kutaka
kuanza kushambuliana wao
kwa wao.Kila nchi kwa sasa
inaweka majeshi yake katika
utayari.Hakuna tena nchi
inayomuamini
mwenzake.Rwanda na Uganda
zinashambuliana japo
mapambano si makubwa lakini
amani baina ya nchi hizo mbili
haipo.Kitendo cha nchi mbili
ndani ya jumuiya kurushiana
risasi ni kiashiria kikubwa
kwamba jumuiya hiyo inaelekea
ukingoni.Uganda imewarejesha
nyumbani mabalozi wake
kutoka nchi za Rwanda na
Congo na kuwatimua mabalozi
wa nchi hizo walioko
Uganda.Nilimfuata Rais wetu Dr
Fabian na kuzungumza naye
nikamuonya kuhusiana na
hatua za kijeshi mbazo
wanataka kuzichukua dhidi ya
Uganda.Wanaandaa kikosi cha
jeshi ambacho kitakwenda
Uganda kumsaka James
Kasai.Uganda imekwisha onya
kuhusu kitendo chochote cha
kutuma kikosi cha jeshi katika
ardhi yake kwamba ni kitendo
cha kichokozi na imeapa kujibu
kwa nguvu zote uchokozi
wowote utakaofanywa na nchi
yoyote ya ndani au nje ya
jumuiya ya Afrika
mashariki.Nilijaribu kumueleza
kuhusu hatari ya kusambaratika
kwa jumuiya ya Afrika
Mashariki lakini inaonekana
Rais ameyapuuza mawazo
yangu na kwa taarifa niliyoipata
ni kwamba tayari wanajeshi
kutoka katika nchi za Rwanda
na Congo wamekwisha wasili
nchini na maandalizi ya kikosi
cha jeshi cha umoja kwa ajili ya
kwenda Uganda
yanaendelea.Viongozi wetu
wametanguliza hasira mbele
bila kujali maslahi ya nchi zao
na jumuiya.Wameungana
pamoja na wanachokitaka ni
kulipa kisasi kwa wake zao
kuuawa” akasema Dr Evans
“Mzee ukilitazama jambo
hili utakuta kati kati yake
anasimama mtu anaitwa James
Kasai.Yeye ndiye aliyesababisha
haya yote yakatokea.Kama
asingefanya shambulio nchini
Tanzania kusingekuwa na hofu
iliyoko hivi sasa ya nchi zetu
kufikia hatua ya kutaka
kushambuliana.Misheni yangu
ya kwanza ni kumuondoa James
Kasai.Huyu jamaa kama
akiondolewa hakuna nchi
ambayo itaendelea na mpango
wa kuishambulia
nyingine.Tanzania,Rwanda na
Congo wanajiandaa kufanya
operesheni ya kijeshi nchini
Uganda kumsaka James.Kama
ulivyosema mzee wameingia
mtegoni bila wao kujua kwani
hawataweza kumpata James
Kasai kwa kutumia nguvu za
kijeshi hivyo James
akiondolewa hakutakuwa tena
na ulazima wa kutuma kikosi
hicho cha jeshi” akasema
Mathew
“Jambo la pili ni kwamba
James Kasai hayuko peke
yake.Anashirikina na kikundi
cha igaidi cha IS na kwa pamoja
ndio waliotekeleza shambulio
lile na kuua wake za marais na
mabalozi.Baada ya kummaliza
James Kasai itafuata operesheni
nyingine ya kuung’oa kabisa
mzizi wa IS hapa nchini na
Afrika Mashariki.Hizi mbili si
operesheni nyepesi nitahitaji
sana msaada wenu” akasema
Mathew.
“Sema chochote
unachokihitaji Mathew.Mimi
niko tayari kukusaidia”
“Nitahitaji kuonana na Rais
wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania .Mimi naye
hatufahamiani.Ameingia
madarakani wakati sipo hivyo
nahitaji mtu wa kuniunganisha
naye.Nataka nikamshauri
aachane na operesheni za
kijeshi anazotaka kuzifanya na
mimi nitamuhakikishia
kummaliza James Kasai”
akasema Mathew
“Nitakuunganisha na Rais
wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania.Alikwenda Mbeya kwa
ajili ya mazishi ya mke wake
nitampigia simu baadae kujua
kama amerejea Dar es salaam”
“Sawa mzee.Suala hili
nililokueleza naomba iwe ni siri
yako” akasema Mathew
“Usihofu Mathew siwezi
kumueleza mtu bila ridhaa
yako”
“Kwa sasa sina mawasiliano
yoyote utawasiliana nami kwa
kutumia simu ya Austin”
akasema Mathew wakaagana na
Dr Evans wakaondoka.
“Austin kama
nilivyowaeleza kwamba
nimerudi hapa nchini kwa
kusudi maalum.Nina misheni
nzito ya kumuondoa James
Kasai na ninakutaka uungane
nami katika misheni hiyo”
akasema Mathew
“Mathew unafahamu jibu
lake.Katu siwezi kusema
hapana.Tulikula kiapo cha
kuilinda nchi dhidi ya adui wa
ndani na wa nje kwa hiyo kila
pale linapotokea jukumu la
kuilinda nchi siwezi kusema
hapana” akasema Austin
“Ahsante sana
Austin.Ningefurahi sana kama
Gosu Gosu angekuwa mzima
ajiunge nasi lakini kwa bahati
mbaya haitawezekana.Ruby
naye angekuwepo ni mtu
muhimu sana.Misheni za sasa
zinakwenda sambamba na
teknolojia.Tutahitaji kuongeza
watu wawili katika timu yetu
badala ya Gosu Gosu na Ruby”
akasema Mathew
“Wapo vijana wawili Tom
Denzel na mwingine anaitwa
Aidan Kengele.Hawa ni vijana
mahiri sana ambao wametoka
mafunzoni hivi karibuni.Wana
uwezo mkubwa sana”akasema
Austin
“Utanipa mafaili yenye
taarifa zao niyapitie” akasema
Mathew na ukimya ukapita
halafu Mathew akauliza
“Unazo taarifa zozote za
mali zangu kuuzwa?
“Mali zako kuuzwa?Austin
naye akashangaa
“Ndiyo.Una taarifa zozote?
“Hapana sina taarif zozote
za mali zako kuuzwa.Nani
kauza?Gosu Gosu?akauliza
Austin
“Hapana si Gosu Gosu.Mke
wangu Peniela” akasema
Mathew
“Sina taarifa zozote za
jambo hilo.Kwa nini kachukua
maamuzi hayo? Mbona Gosu
Gosu hajanieleza chochote?
Tufuatilie tufahamu undani wa
suala hili” akashauri Austin
“Usijali Austin.Kama kauza
siwezi kumlaumu sana kwani
yeye kama wengine wote
aliamini nimekwisha fariki
dunia.Isitoshe sikuja kwa ajili
ya hilo.Nimekuja kwa misheni
maalum kabisa” akasema
Mathew ukapita ukimya kidogo
Austin akauliza
“Peniela hajakueleza
chochote kuhusu jambo
hilo?akauliza Austin
“Sina mawasiliano
naye.Hafahamu kama niko hai”
akasema Mathew
“Where were you Mathew?
Akauliza Austin
“Austin let’s focus on our
mission” akasema Mathew na
kumuelekeza Austn waelekee
katika hoteli aliyokuwa
amefikia ili akachukue mizigo
yake.
Mara tu baada ya akina
Mathew kuondoka,Dr Evans
akampigia simu Rais Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais”
akasema Dr Evans baada ya Dr
Fabian kupokea simu
“Mzee shikamoo”
“Marahaba Dr Fabian.Vipi
maendeleo yako?
“Tayari nimekwisha rejea
Dar es salaam.Nilishindwa
kurejea jana.Nashukuru kila
kitu kimekwenda vizuri na
tumerejea salama”
“Dr Fabian najua mambo ni
mengi sana lakini nakuomba
nipate nafasi ya kuonana nawe
jioni ya leo.Kuna jambo la
muhimu sana nataka
kuzungumza nawe” akasema Dr
Fabian
“Mzee kwa siku ya leo
utanisamehe sana.Ratiba yangu
imebana sana.Mambo ni mengi
.Kuna mengi ya kuzungumza
nawe mzee wangu naomba iwe
kesho ili tupate nafasi ya
kutosha kuzungumza.Samahani
sana mzee” akasema Dr Fabian
“Usijali Dr Fabian.Hata
kesho tunaweza kuonana”
akasema Dr Evans wakaagana
na Dr Evans akampigia simu
Austin akamjulisha kuwa kikao
kitakuwa siku ya kesho
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 8: EPISODE 4
Saa moja za jioni Ruby
aliwasili katika makazi ya Rais
ikulu Dar es salaama.Mlango wa
gari lake ukafunguliwa na
mmoja wa walinzi aliokuwa
ameongozana nao akashuka na
kupokewa na msaidizi wa Rais
akamkaribisha ndani akamtaka
amsubiri Rais alikuwa
anamalizia mazungumzo na
watu waliokuja kumpa
pole.Dakika arobaini baadae
Rais wa jamhuri ya muungano
wa Tanzania Dr Fabian Kelelo
akaingia sebuleni akiwa
ameongozana na walinzi
wake.Ruby akasimama kwa
heshima
“Ruby ! akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais”
akasema Ruby na Dr Fabian
akampa mkono
“Karibu sana Ruby”
akasema Dr Fabian na kuketi
“Samahani kwa
kuchelewa.Nilikuwa na kikao na
mabalozi waliokuja kunipa pole
hivyo nikashindwa kuwaacha
peke yao”
“Usijali mheshimiwa Rais”
akasema Ruby
“Ruby nimefarijika sana
kukuona hapa” akasema Dr
Fabian na kumtaka Ruby
waelekee katika chumba cha
chakula ambako kulikuwa
kumeandaliwa chakula maalum.
“Ruby karibu
sana.Nimeandaa hiki chakula
kwa heshima yako” akasema Dr
Fabian
“Ahsante sana mheshimiwa
Rais” akasema Ruby na kila
mmoja akajisaidia chakula
alichohitaji
“She used to sit there”
akasema Dr Fabian
akimuonyesha Ruby kiti
ambacho mke wake Millen
alipenda kukaa wakati wa
chakula
“Pole sana mheshimiwa
Rais”akasema Ruby
“Itanichukua muda mrefu
kuizoea hali hii ya maisha bila
Millen.She was everything to
me” akasema Dr Fabian na
kuweka kijiko mezani
“Mheshimiwa Rais hili ni
jaribu kubwa ambalo unapitia
hivyo itakulazimu kuwa jasiri
sana kulikabili.Najua unaumia
moyoni lakini jitahidi
kuirejesha akili katika jukumu
kubwa la kuongoza watu zaidi
ya milioni hamsini ambao wote
wanakutazama wewe.Utalia
siku utakapomaliza urais lakini
kwa sasa bado una kazi kubwa
ya kuongoza so focus ! akasema
Ruby kwa sauti kavu.Dr Fabian
akamtazama halafu akainua
kijiko
“Ahsante Ruby.Katika wote
waliokuja kunipa pole wewe ni
wa kwanza kunieleza maneno
kama hayo na uko sahihi
ninatakiwa kuielekeza akili
yangu katika masuala ya msingi
ya uongozi wa nchi” akasema Dr
Evans
“Watoto wako
wapi?akauliza Ruby
“Wamebaki Mbeya na
ndugu wengine kuna ibada
itafanyika kesho.Watarejea
baada ya wiki moja.Tuliweke
hilo pembeni.Pamoja na yote
yaliyotokea Ruby nimefurahi
sana kukuona.Ujio wako
umenifarji sana” akasema Dr
Evans na kuendelea kula
walipomaliza wakaenda katika
chumba cha mapumziko
“Ruby naomba nianze kwa
kukueleza sababu iliyopelekea
kukuita hapa nyumbani”
akasema Dr Evans na kuanza
kumuelezea Ruby kila kitu toka
mauaji ya Lucy Muganza hadi
walipogundua kwamba Tamar
aliyekuwa mkurugenzi wa idara
ya siri ya usalama wa ndani wa
nchi kushirikiana na balozi wa
umoja wa Ulaya aliyeuawa na
watu wasiojulikana.
“Baada ya Tamar kuuawa
ndipo Austin aliponifuata na
kunieleza kwamba kuna mtu
ambaye anafaa sana na
anaweza kuiongoza SNSA na
akakupendekeza wewe.Sikuwa
nikikufahamu na ilikuwa ni
mara ya kwanza kusikia jina
lako” akanyamaza kidogo
“Nilipoingia madarakani
nilikumbana na changamoto
moja ambayo ni kuamini watu
wanaonizunguka.Nilipata somo
kutoka kwa rais aliyenitangulia
Dr Evans ambaye aliyekuwa
waziri mkuu wa serikali yake
alikuwa ni mfuasi wa mtandao
wa kigaidi wa IS.Nilipata taabu
kidogo kupata watu
nitakaowaamini kwa ajili ya ile
misheni ya kumuua Lucy
Muganza na ndipo Dr Evans
akanitambulisha kwa Austin
ambaye alinihakikishia ni mtu
ninayeweza kumuamini.Toka
wakati huo nimekuwa na imani
kubwa kwa Austin ndiyo maana
aliponieleza kwamba unafaa
kuiongoza idara nyeti kama ya
SNSA sikumuhoji mara mbili
moja kwa moja nikamtaka
anielekeze mahala
ulipo.Nashukuru sana kwa
kulikubali ombi langu na
ukafanya kila jitihada
kuhakikisha unafika Tanzania
kuifanya kazi hiyo
niliyokuomba.Sina neno zuri
zaidi la kukushukuru Ruby kwa
hiki ulichokifanya”akasema Dr
Evans
“Mheshimiwa Rais naamini
Austin alikueleza historia
yangu.Mimi ni mtanzania lakini
kwa sasa nina uraia wa
Uingereza.Kwa muda mrefu
sikuwahi kurejea nyumbani na
sikuwa na mpango huo hadi
pale nilipokutana na mtu
mmoja anaitwa Mathew
Mulumbi ambaye ndiye
aliyenifundisha kwamba
japokuwa nina uraia wa nchi
nyingine lakini nina deni kubwa
kwa nchi walikotoka wazazi
wangu ambako ndiko asili
yangu” akasema Ruby
“Mathew Mulumbi hili si
jina geni katika masikio
yangu.Who is he?akauliza Dr
Fabian
“Mathew Mulumbi aliwahi
kufanya kazi katika idara ya
ujasusi.Anatajwa mmoja wa
majasusi mahiri kabisa kuwahi
kutokea hapa nchini.Ni yeye
ndiye aliyenirejesha nyumbani
Tanzania na kunishirikisha
katika misheni mbali mbali
alizokuwa akizifanya.Misheni ya
mwisho kushrikiana naye ni
miaka mitatu iliyopita ambapo
tulishirikiana kuwakomboa
mateka waliokuwa wametekwa
na kundi la kigaidi la IS”
akasema Ruby
“Where is he now?
“Alifariki katika misheni
hiyo.Alikwenda nchini Kenya
katika misheni ya kuwakomboa
mateka waliokuwa
wanashikiliwa na kundi la IS na
miongoni mwao alikuwemo
mtoto wa Rais Dr
Evans.Walifanikiwa
kuwakomboa mateka lakini
Mathew hakurejea tena
nyumbani.Alifia huko” akasema
Ruby na kuinamisha kichwa
“Dr Evans hajawahi
kunieleza chochote kuhusiana
na suala hilo” akasema Dr
Fabian
“Mheshimiwa Rais,Mathew
Mulumbi ndiye hasa
aliyenifundisha kuipenda nchi
nilikotoka na ndiyo maana
uliponipigia simu kunitaka nije
Tanzania kufanya kazi
sikujiuliza maswali bali nilianza
mara moja mchakato wa
kuondoka kule Uingereza
kurejea huku.Haikuwa rahisi
kama nilivyokueleza kwamba
waliamini nimenunuliwa ili
nikatoe siri zao na ndiyo maana
wakapanga mpango ule wa
kuniua.Kwa bahati nzuri
nilijulishwa juu ya mpango ule
na kuukwepa.Haikuwa safari
rahisi hadi kufika hapa lakini
nashukuru Mungu ameniongoza
nimefika salama na niko tayari
kwa kazi” akasema Ruby
“Kweli haya ni maongozi ya
Mungu kwani hata mimi
sikutegemea kama ungeweza
kufika Tanzania salama.Kama
nilivyokueleza wakati
ninakupigia simu kwamba kazi
unayokuja kuifanya ni
kuongoza idara nyeti ya
usalama wa ndani wa nchi
ambayo inafanya kazi zake kwa
siri”
“Ninaifahamu idara hiyo na
majukumu yake” akasema Ruby
“Nashukuru kama
unaifahamu lakini idara hii ina
umuhimu mkubwa sana kwa
nchi tofauti na unavyoifahamu
ndiyo maana ninahitaji mtu wa
kuiongoza ambaye atakuwa ni
mzalendo wa kweli ambaye
hataitumia idara hii kwa ajili ya
manufaa yake kama
walivyofanya waliotangulia”
akanyamaza kidogo na kusema
“Kufuatia Tanzania
kuchafuka kimataifa kutokana
na kifo cha Lucy
Muganza,Millen alinishauri
tufanye kitu kwa ajili ya
kuirejesha tena sifa ya Tanzania
kama kisiwa cha amani na
akashauri kuandaa mkutano
mkubwa wa wake za marais wa
dunia nzima kupitia taasisi
yake.Tulitumia gharama kubwa
kuandaa mkutano huo muhimu
na wiki moja kabla ya mkutano
kufanyika balozi wa jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo hapa
nchini alimfuata Millen
akamueleza kwamba anataka
kuwakutanisha wake za marais
wa Rwanda na Congo na
akamtaka Millen kumsaidia
katika mpango huo.Millen
alikubali kwa kujua kwamba ni
jambo jema na maandalizi ya
hafla ya kuwakutanisha wake
hao za marais ikaandaliwa na
siku ilipofika wakakutana kwa
ajili ya hafla hiyo na ndipo
mabomu matatu
yakalipuka.Mke wangu
Millen,wake za marais wa
Rwanda na Congo,mabalozi
wanaoziwakilisha nchi hizo
hapa Tanzania pamojana
familia zao na raia wengine wa
kutoka nchi hizo waliokuwa
wamealikwa walipoteza
maisha”
“Pole sana mheshimiwa
Rais.Nilikuwa melini na sikujua
chochote kilichotokea” akasema
Ruby
“Ninafahamu ndiyo maana
nilikwambia nitakuja kukueleza
nitakaporejea” akanyamaza
kidogo
“Baada ya shambulio
kutokea alijitokeza mtu mmoja
anaitwa James Kasai akadai
kuhusika na lile shambulio
akisaidiana na kikundi cha
kigaidi cha IS”
“James Kasai.Who is
he?akauliza Ruby
“Huyu anaongoza kikundi
cha waasi ambacho kwa muda
mrefu wamekuwa
wakipambana na serikali ya
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo lakini wa sasa baada ya
kufurushwa nchini Congo
inaaminika ameenda kuishi
nchini Uganda”
“Katika maelezo aliyoyatoa
alidai nini sababu ya kufanya
shambulio hilo? Ruby akauliza
“Alidai ni kulipiza kisasi
kwa Rais Patrice Eyenga”
akasema Dr Fabian na
kunyamaza akatazama na Ruby
kwa muda halafu akasema
“Kwa hvi sasa Tanzania
ikiungana na Rwanda na Congo
tuko katika maandalizi ya
kuandaa kikosi cha jeshi
kitakachokwenda nchini
Uganda kumsaka James Kasai
na kuhakikisha anapatikana
akiwa mzima au
amekufa.Mazoezi ya kikosi
hicho yanaendelea na pale
watakapokuwa tayari
wataelekea nchini Uganda
kumsaka James Kasai” akasema
Dr Evans na kunyamaza kwa
sekunde chache
“Tunaamini balozi
Germinus Mapupu hakuwa
peke yake lazima kuna watu
alioshirikiana nao katika
kuandaa hafla ile.Nimewapa
jukumu hilo SNSA la
kuhakikisha wanachunguza na
kujua nani waliokuwa
wanashirikiana na balozi
Mapupu lakini hadi sasa hakuna
taarifa yoyote ya maana kutoka
kwao.Umefika kwa wakati
muafaka kabisa ninataka uanze
na jambo hili.Ninataka
uhakikishe tunafahamu nani
walioshirikiana na balozi
Mapupu.Tunajua James Kasai
ndiye aliyefanya shambulio
lakini lazima wapo watu wa
hapa nchini ambao
walishirikina naye na hao ndio
tunaotaka kuwafahamu.Jambo
lingine ninataka kufanya
mabadiliko makubwa katika
idara ile na nitategemea sana
ushauri wako.Utakapoanza kazi
rasmi utaisoma ile idara na
kutoa mapendekezo ni wapi
panahitaji mabadiliko na mimi
nitafanya bila kusita” akasema
Dr Fabian
“Nimekuelewa mheshimiwa
Rais na ninakuahidi utendaji
uliotukuka” akasema Ruby
“Ahsante Ruby naamini
utaweza kwani wenzako
wamekusifia sana na
kukupendekeza kuwa
unafaa.Tafadhali naomba
ukarejeshe heshima ya idara hii
ambayo ina umuhimu mkubwa
sana.Kwa kuwa umesafiri safari
ndefu naamini bado una uchovu
hivyo basi ninakupa wiki moja
ya mapumziko ili kujiweka
tayari kwa kazi.Wiki ijayo
nitakutangaza rasmi kama
mkurugenzi mpya wa SNSA”
akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais.Mimi
nimezoea kufanya kazi usiku na
mchana hivyo hata sasa
ukiniambia nikaanze kazi niko
tayari” akasema Ruby na Dr
Fabian akatabasamu kidogo
“Ninapenda sana watu
kama wewe Ruby wenye ari ya
kazi walio tayari kufanya kazi
usiku na mchana kwa ajili ya
nchi yao lakini ninakupa
mapumziko hayo ya wiki moja
ili kujiandaa kwa sababu kazi
unayokwenda kuifanya si kazi
ndogo.Unakwenda kuongoza
idara kubwa sana na nyeti
kabisa.Nimekwisha toa
maelekezo kwa wasaidizi
wangu wakuandalie nyumba
utakayoishi yenye hadhi
yako,utapata pia walinzi wa
kukulinda kila uendako na
kuhakikisha unakuwa
salama.Mambo hayo yote
yatakapokamilika
utafahamishwa” akasema Dr
Evans
Waliendelea na
mazungumzo na ilipofika saa
nne za usiku Ruby akaondoka
kurejea katika makazi yake ya
muda.
KAMPALA – UGANDA
Gari tatu ziliwasili katika
nyumba alimofikia
Melanie.Tayari ilikwisha timu
saa mbili za usiku.Rais wa
Uganda Jenerali Akiki
Rwamirama akashuka na
kuelekea ndani akiwa na
walinzi wake.Moja kwa moja
wakaelekea katika mlango wa
chumba cha Melanie mmoja wa
walinzi wake akagonga mlango
na baada ya sekunde kadhaa
mlango ukafunguliwa na
Melanie akiwa na tabasamu
akajitokeza.Jenerali Akiki
akawaelekeza walinzi wake
wampe nafasi akaingia ndani na
kuufunga mlango.Kabla hajaketi
Melanie ambaye usiku huu
alikuwa amevaa gauni jepesi
lililoonyesha kila alichokivaa
ndani akamkumbatia na
kumbusu
“Karibu sana mheshimiwa
Rais” akasema Melanie na
Jenerali Akiki akatabasamu
“Nashukuru sana Melanie”
akasema Jenerali Akiki na
kuketi sofani,Melanie
akamkaribisha kinywaji
“Umeshindaje leo Melanie?
“Nimeshinda salama
kabisa.Pole na mihangaiko ya
siku nzima”akasema Melanie
huku akimvua koti Jenerali
Akiki akalitupa pembeni
akachukua glasi ya pombe kali
akamnywesha
“Melanie mapokezi yako si
ya kawaida.Ni miaka mingi
sijawahi kupokelewa namna
hii” akasema Jenerali Akiki
“Mke wako hakupokei
namna hii?Melanie akauliza
“Hapana.Mambo kama haya
amekwisha yasahau
kabisa.Yawezekana umri ukawa
kigezo.Tumekwisha kuwa watu
wazima sasa.Wanawake wana
tatizo hilo wakifikia umri Fulani
yale manjonjo yote waliyokuwa
nayo mwanzo wa ndoa
yanatoweka mnabaki mkiishi
kwa mazoea”
“Usiseme wanawake.Wewe
umechukua hatua gani
kuboresha penzi
lenu?.Mheshimiwa Rais
mapenzi hayana umri.Ili
muyafurahie hata pale
mtakapokuwa mmezeeka
lazima kila mmoja aweke juhudi
za kuyaboresha”akasema
Melanie
“Ahsante kwa somo hilo
Melanie nitalizingatia” akasema
Jenerali Akiki na Melanie
akamnywesha tena kinywaji
kisha akaanza kufungua vifungo
vya shati la Akiki akaanza
kukichezea kifua chake.
“Mimi ni wako kwa usiku
wa leo ninajiweka katika
mikono yako” akasema Melanie
na kumbusu Jenerali Akiki
ambaye tayari mashetani yake
yalikwisha amka akashika
hatamu.Maandalizi ya mechi
yalifanyika kisha wakaingia
uwanjani.
“Hili jamaa linatumia nguvu
kana kwamba hii ni mara yake
ya mwisho kufanya
mapenzi.Hakuna raha yoyote
ninayoipata hapa zaidi ya
karaha.Ndiyo maaana
ninampenda GosuGosu.Ni
mwanaume wa aina yake.Ana
nguvu lakini anajua kuzitumia
na si kama huyu jamaa.Ngoja
nimuache ajiridhishe
ninachotaka ni mambo yangu
yafanikiwe.Ninaamini baada ya
kuonja asali hataacha atataka
tena na tena na hapo ndipo
nitampeleka kama ng’ombe”
akawaza Melanie wakati
Jenerali Akiki akiendelea
kujishughulisha kwa nguvu
Akiki alifika mshindo na
kujitupa pembeni akihema
kama amekimbia kilometa elfu
moja.
“Keshamaliza hoi
kabisa.Muone kwanza.Yale
maguvu yote alikuwa
anakimbilia wapi? Akawaza
Melanie na kumkumbatia Akiki
“Ahsante sana mheshimiwa
Rais.Sikutegemea u mjuzi hivi
wa haya mambo.Umenipeleka
mbio..” akasema Melanie.
“Ahsante pia Melanie.Huu
umekuwa ni usiku wangu wa
kipekee kabisa” akasema
Jenerali Akiki huku Melanie
akiendelea kumchezea kifua
kwa mkono wake.
“Melanie nina ombi moja
kwako” akasema Jenerali Akiki
“Omba chochote
mheshimiwa Rais.Unataka nini?
“Ninaomba tusiishie
hapa.Nataka tuendelee.Nataka
tuwe wapenzi kwa siri na mimi
nitakufanyia kila kitu
unachokitaka.Hata ukitaka
nikununulie ndege uwezo ninao
lakini tafadhali naomba
tuendelee” akasema Jenerali
Akiki .Melanie akatabasamu na
kumbusu kisha akasema
“Una maneno matamu sana
mheshimiwa Rais.Mimi sina
tatizo na ombi lako ili mradi tu
unihakishie kwamba mkeo
hatajua”
“Usihofu Melanie mke
wangu hatatafahamu
chochote.Itakuwa ni siri yetu
kubwa” akasema Jenerali Akiki
“Kama unanihakikishia
hivyo mimi sina kipingamizi
chochote.Tuendelee na
mahusiano ya siri”
“Ahsante
Melanie.Nakuahidi kukupa kila
unachohitaji.Nitakufanyia
mambo hadi utashangaa
mwenyewe” akasema Jenerali
Akiki huku Melanie akifanya
juhudi za kuamsha mambo
ikulu bila mafanikio
“Ikulu kumelala
kabisa.Haamki tena” akawaza
Melanie akainuka kitandani na
kumimina pombe kali katika
glasi na kumpa Jenerali Akiki
wakakaa kitandani
“Leo nimekutana na James
Kasai” akasema Melanie
“Umekutana naye wapi?
“Nilimpigi simu akafika
hapa.Nilimueleza kuhusiana na
ule mpango wangu niliokueleza
jana”
“Akasemaje ulipomueleza?
“Aliukubali ni mpango
mzuri lakini akashauri hadi
tukutane nawe kwanza tujadili
kwa kina.Tafadhali kubali
kukutana nasi pale
atakapokupigia simu
kukuomba”akasema Melanie
“Usijali Melanie kesho
tutakutana sisi watatu kulijadili
hili suala na tutalijadili lile suala
lako.Kwa sasa ushirikiano na
wale majenerali wa jeshi
hakuna tena”
“Nakushukuru sana
mheshimiwa Rais kwa namna
unavyonijali na kukubali
kunisaidia katika mpango
wangu huu” akasema Melanie
“Melanie nimekwisha
kueleza kwamba niko tayari
kukufanyia kitu chochote
unachokitaka ili mradi kiwe
ndani ya uwezo
wangu.Nimekwambia hata
ukitaka ndege nitakununulia”
akasema Jenerali akiki ambaye
tayari macho yake yalianza
kuwa mazito akionekana kuwa
na usingizi
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Ilikuwa siku ndefu kwa
Mathew Mulumbi.Saa tatu za
usiku alikuwa chumbani kwake
amekaa kitandani.
“Imekuwa siku ndefu
nashukuru imekwenda vizuri
na sasa ni wakati wa
kuwasiliana na Habiba
Jawad”akawaza na kuchukua
kompyuta yake akajiunga na
matandao wa intaneti kisha
akampigia simu Habiba
“Habari yako Mathew
Mulumbi” akasema Habiba
Jawad
“Nzuri mama shikamoo”
“Marahaba habari za Dar es
salaam?akauliza Habiba
“Dar es salaam kwema
ninaendelea vizuri”
“Nafurahi kusikia hivyo”
“Vipi maendeleo ya Najma?
“Anaendelea
vyema.Usimpigie simu sitaki
ajue uko wapi” akasema Habiba
“Nitafanya hivyo mama”
“Vizuri.Tayari umekwisha
anza kufanya maandalizi ya
operesheni?
“Ndiyo mama nimekwisha
anza maandalizi”
“Vizuri.Ukisha kuwa tayari
unijulishe.Jitahidi ndani ya
kipindi kifupi uwe
umekamilisha maandalizi yote”
“Nadhani baada ya kesho
kila kitu kitakuwa tayari”
“Ukishakuwa tayari
nijulishe ili niweze kukupa
taarifa za kuhusina na James
kasai’ akasema Habiba na
kuagana na Mathew.
“Baada ya miaka mitatu
hatimaye leo ninalala katika
kitanda changu” akawaza
Mathew wakati akijiandaa
kulala.
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 8: EPISODE 5
Saa kumi na mbili za
asubuhi ilimkuta Mathew
Mulumbi akiwa hospitali ya
Mtodora alikoenda kumtazama
Gosu Gosu.Pale hospitali
alikutana na Austin ambaye
alilala pale pale na kumjulisha
kwamba hali ya Gosu Gosu bado
haikuwa na mabadiliko
yoyote.Mathew akaomba
kuingia ndani ya chumba kile
alimo Gosu Gosu akavishwa
mavazi na kuingia akavuta kiti
na kumsogelea
“Gosu Gosu najua
unanisikia.It’s me Mathew
Mulumbi again.I’m back and I
need you.Please wake up.Fight
and wake up.Please don’t force
me to switch off this machine.If
you want to live my brother
please fight and wake up !You
hear me?Please fight ! Don’t
quit ! akasema Mathew kisha
akatoka mle ndani.Tayari
Austin alikwisha muita mmoja
wa vijana kutoka katika kikosi
chake kukaa pale hospitali
kuhakikisha Gosu Gosu
anakuwa
salama.Akamtambulisha kijana
Yule kwa Mathew
“Austin we need to go.Saa
tano leo tuna miadi ya kwenda
kuonana na Rais.Tunatakiwa
kujiandaa” akasema Mathew
wakaelekea katika gari na
kuondoka
“Umewasiliana na
mchumba wa Gosu
Gosu?Mathew akauliza wakiwa
garini
“Bado simu yake
haipatikani”
“Inanipa taabu kidogo.Ni
mwanamke wa aina gani huyo
ambaye anaweza akamuacha
mchumba wake katika hali ile
na kuondoka.Kweli ni mchumba
wake? Mathew akauliza
“Kwa mujibu wa Lucy ni
kwamba Gosu Gosu alikwenda
Ufaransa na aliporejea ndipo
alipoanza kuonekana na huyo
mwanamke.Lucy anadai
kwamba mwanamke huyo
amekuwa akienda karibu kila
siku nyumbani kwa Gosu Gosu
lakini hajawahi kulala
pale.Wakimaliza mambo yao
huondoka zake.Hata Lucy
mwenyewe hana taarifa za
kutosha kuhusiana na huyo
mwanamke”akasema Austin
“Unasema Gosu Gosu
alikwenda Ufaransa? Mathew
akauliza
“Ndiyo.Kwa mujibu wa
Lucy ni kwamba Gosu Gosu
alisafiri ya kwenda Ufaransa na
aliporejea akaanza kuonekana
na huyo mwanamke”
“Alikwenda kufanya nini
Ufaransa?Mathew akauliza
“Hata mimi
sifahamu.Hakuwahi kunieleza
chochote kama anasafiri na hata
suala la kuwa na mchumba
alinificha pia.Nimeyafahamu
haya yote baada ya kupigwa
risasi.Mathew unahisi labda
mwanamke huyo anaweza
akahusika na tukio hili?akauliza
Austin
“Siwezi kusema moja kwa
moja kwamba anahusika but
something is not right about
this woman.How she looks
like?akauliza Mathew
“She’s pretty.Very pretty”
akasema Austin
“Austin tunatakiwa
kumtafuta huyo
mwanamke.Nahitaji kumfanyia
mahojiano” akasema Mathew
“Tutamuuliza zaidi Lucy
kwani yeye ndiye
anayemfahamu zaidi.Anaweza
akatusaidia kufahamu mahala
tunakoweza kumpata huyo
mwanamke” akasema Austin na
ukimya mfupi ukapita
“Gosu Gosu alipokwenda
Ufaransa alifanikiwa kuonana
na Peniela? Akauliza Mathew
“Natamani Gosu Gosu
afumbue macho hata sasa.Kuna
maswali mengi ambayo
anatatakiwa kuyajibu” akasema
Mathew
“Mathew I’m sorry to say
this.Hudhani kama Peniela
anapaswa kufahamu kwamba
uko hai?akauliza Austin na
Mathew akatafakari kwa
sekunde chache halafu akasema
“Hapana.Hapaswi
kufahamu chochote kuhusu
mimi.Tayari anafahamu kuwa
nimekwisha kufa na itaendelea
kubaki hivyo.Wamekwisha
kubaliana na ukweli na sitaki
kuvuruga maisha yao” akasema
Mathew
“Vipi kuhusu watoto?
“Austin sitaki tuongelee
suala hilo.Tuna mambo mengi
ya kufanya tujielekeze huko
kuliko kujadili kuhusu masuala
yangu” akasema Mathew
“Sorry” akasema Austin na
safari ikaendelea kimya kimya
“Mathew alikuwa
wapi?Kwa nini hataki
kuongelea chochote kuhusiana
na mahala
alikokuwa?Ameibuka tu kutoka
kusikojulikana na hataki
kuzungumza chochote.Amekuja
moja kwa moja akijielekeza
katika misheni ya kutaka
kumuua James Kasai.Amekuja
akiwa anafahamu kila kitu
kilichotokea hapa
nchini.Amefahamuje mambo
haya? Kurejea kwake kunaibua
maswali mengi lakini hataki
kuulizwa chochote” akawaza
Austin.
Walikwenda kwanza
nyumbani kwa Austin
akajiandaa kisha wakaondoka
hadi nyumbani kwa Mathew
akajiandaa haraka haraka
akajitazama
“Mwonekano huu
unaruhusu kuingia ikulu”
akawaza na kutoka chumbani
kwake na kukutana na Lucy
mtumishi wake
“Lucy naomba kwa dakika
chache unieleze kuhusu
mchumba wa Gosu Gosu”
akasema Mathew
“Simfahamu vyema.Gosu
Gosu hakuwa na mazoea ya
kuleta mwanamke hapa
nyumbani hadi hivi majuzi
aliporejea kutokea Paris
Ufaransa ndipo nilipoanza
kumuona na huyo mwaname
akamtambulisha kwangu
kwamba anaitwa Melanie na
amekuwa akija hapa mara kwa
mara”
“Unaweza kufahamu
mahala anakoishi?
“Hapana sifahamu hajawahi
kunieleza”
“Kuna kingine chochote
unachoweza kukikumhuka
kuhusu huo mwanamke?
“Simfahamu kiundani na
kila ajapo huwa wanajifungia
chumbani kwa Gosu Gosu na
hajawahi kulala
hapa.Simfahamu vyema”
akajibu Lucy
“Gosu Gosu alikwambia
anakwenda Ufaransa kufanya
nini?akauliza Mathew
“Aliniambia kwamba
anakwenda katika mambo ya
kibiashara.Hakunieleza zaidi”
akasema Lucy
“Ahsante Lucy.Nitakuomba
kitu kimoja.Ingia katika chumba
cha Gosu Gosu jaribu kutafuta
picha ya huyo mwanamke
ninataka kumuona” akasema
Mathew wakaingia garini na
kuondoka kuelekea kwa Rais
mstaafu Dr Evans.Wakati safari
ikiendelea Mathew alikuwa
akiyapitia mafaili mawili
aliyopewa na Austin kuhusiana
na wale watu wawili
ambaoMathew alitaka
waongezwe katika timu
anayoiandaa kwa ajili ya
operesheni ya kumuondoa
James KasaiAkayapitia kwa
makini halafu akayafunika
“Si
wabaya.Wameiva.Tunaweza
kuwatuia” akasema
“Itakuwa ni misheni yao ya
kwanza toka wametoka
mafunzoni” akasema Austin na
safari ikaendelea
“Mathew kuna kitu nataka
ukifahamu” akasema Austin
“Kitu gani Austin?akauliza
Mathew na Austin akameza
mate kulainisha koo na kusema
“Watu wote waliamini
kwamba umekufa except me
and Gosu Gosu.Hatukuamini
hilo jambo na tuliwahi
kujadiliana tufanye uchunguzi
wetu kuufahamu ukweli ”
akasema Austin na Mathew
akatabasamu
“Kwa nini mliamini
sijafariki dunia?
Mathew akauliza
“Binafsi kuna kitu ndani
mwangu kilinifanya niamini
hivyo.Hakuna hata usiku mmoja
umewahi kupita bila
kukukumbuka” akasema ustin
“Thank you so much.I
appreciate that.You are true
brothers” akasema Mathew na
safari ikaendelea hadi
walipofika nyumbani kwa Rais
mstaafu Dr Evans.Walinzi
wakawafungulia geti wakaingia
ndani na kupokewa na mlinzi
wa Dr Evans.Siku hii Dr Evans
alikuwa na walinzi
watatu.Baada ya muda DrEvans
akatokea na kusalimiana na
akina Mathew
“Hatuna muda vijana
tuanze safari”akasema Dr Evans
wakaingia katika magari na
kuondoka.
“Ulipozungumza na Rais
kuomba kuonana naye
ulimueleza jambo
linalotupeleka huko?akauliza
Mathew
“Hapana sikumueleza
chochote” akajibu Dr Evans
ambaye alionekana bado
anamuogopa Mathew
“Taarifa nilizozipata
asubuhi ya leo ambazo
haijatangazwa ni kwamba usiku
wa kuamkia leo ndege za
Uganda zimeshambulia vijiji
vilivyo karibu na mpaka wao na
Rwanda na inasemekana watu
kadhaa wameuawa.Bado taarifa
rasmi haijatolewa lakini hiyo ni
taarifa ya kweli kabisa.Taratibu
jumuiya ya Afrika Mashariki
inamomonyoka.Kinachoniumiz
a ni kwamba wakati wa uongozi
wangu niliweka nguvu kubwa
sana pamoja na marais wengine
kuiimarisha jumuiya hii.Zipo
faida nyingi za jumuiya hii
ambayo kwa sasa imefikia
hatua nzuri na kubwa ya kuwa
na sarafu moja kwa hiyo haya
yanayoendelea hivi sasa
yananisonnesha mno” akasema
Dr Evans
“Usihofu mzee.Jumuiya
haitaweza kusambaratika
wakati vijana wa kusimama
kuitetea tupo.Ninakuahidi
tutasimama imara kuhakikisha
kwamba jumuiya inaendelea
kuwepo na kustawi.Wale wote
waliopandikiza chuki na kuleta
chokochoko baina ya
wanachama ili wapigane
wanakwenda kushindwa
vibaya.Si muda mrefu wale
makuwadi wa mabepari
watakwenda kukiona cha
mtema kuni.Siku zao
zinahesabika” akasema Mathew
na Dr Evans akatabasamu
“Mathew hujabadilika.Bado
ni Mathew yuleyule mwenye
maneno mazito ya
kizalendo.Nilifanya kos……”
akasema Dr Evans na Mathew
akamkatisha
“Mzee tumekwisha toka
huko.Kitabu kile tumekwisha
kifunga na kama kuna makosa
yalifanyika yote tumeyafukia
sasa tunajielekeza katika
mambo mengine ya msingi.By
the way how’s your
daughter?.akauliza Mathew
“She’s fine.Kwa sasa anaishi
nchini Afrika kusini amepata
kazi huko.Huwa ninakwenda
kumtembelea mara kwa mara
na haachi kukushukuru kwa
ushujaa uliouonyesha siku
ulipowakomboa” akasema Dr
Evans Mathew na safari
ikaendelea
Waliwasili ikulu na
kupokewa na msaidizi wa Rais
wakakaribishwa ndani ambako
wakamkuta Dr Fabian
akiwasubiri.
“Mzee karibu sana”
akasema Dr Fabian akipeana
mkono na Dr Evans
“Ahsante sana mheshimiwa
Rais”
“Nilidhani uko peke yako
kumbe umekuja na ugeni”
akasema Dr Fabian huku
akisalimiana na Austin
“Austin.Sikujua kama
unakuja na mzee.Vipi hali ya
Gosu Gosu? Sikuweza kukupigia
kujua hali yake kutokana na
kutingwa sana na mambo
mengi ya mazishi ya mke
wangu.Utanisamehe usije
ukaona kama nimewatupa
vijana wangu” akasema Dr
Fabian
“Usijali mheshimiwa Rais
tunaelewa kipindi unachokipitia
na sisi tuko pamoja nawe”
akasema Austin
“Anaendeleaje
mwenzako?akauliza Rais
“Hali yake bado iko vile vile
hakuna mabadiliko”
“Poleni sana.Nimekwisha
wasiliana na uongozi wa
hospitali kufanya kila lililo
ndani ya uwezo wao kuokoa
maisha yake na mimi nikipata
wasaa nitakwenda
kumtembelea vile vile
nimemuagiza mkuu wa jeshi la
polisi kuhakikisha jeshi la polisi
linawapata watu waliofanya
kitendo hicho” akasema Dr
Evans
“Tunashukuru sana
mheshimiwa Rais’ akasema
Austin na kukaa Dr Evans
akajikuta akitazamana na
Mathew
“Karibu sana ndugu”
akampa mkono.Hakuwa
akimfahamu
“Anaitwa Mathew
Mulumbi.Aliwahi kufanya kazi
katika idara yetu ya ujasusi” Dr
Evans akamtambulisha Mathew
kwa Rais ambaye alishindwa
kuzuia mstuko usionekane
katika uso wake
“Mathew Mulumbi?!!
Akauliza kwa mshangao
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Ninaitwa Mathew
Mulumbi” akasema Mathew na
bado Dr Fabian akaendelea
kumtazama kwa woga
“Mathew Mulumbi yupi?
Kwa taarifa nilizonazo ni
kwamba Mathew Mulumbi
amefariki dunia.Ni jana tu
nilikuwa na Ruby hapa
tukizungumza akanieleza
kwamba ni Mathew Mulumbi
ambaye alimfundisha kupenda
nchi alikotoka na akasikitika
kwamba huyo Mathew
amefariki dunia lakini leo
ninaletewa Mathew Mulumbi
mbele yangu.Dr Evans what is
this?akauliza Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
umesema ulikuwa na
Ruby?akauliza Mathew
“Ndiyo nilikuwa naye jana
na tulizungumza kuhusu
marehemu Mathew Mulumbi”
“Oh my God ! Ruby is
here?akauliza Mathew kwa
furaha Dr Fabian akabaki
anashangaa
“Dr Evans what’s going
on?akauliza DrFabian
“Mheshimiwa Rais
utanisamehe kwa mkanganyiko
huu uliotokea.Tunaweza
kuzungumza faragha
kidogo?akauliza Dr Evans
“Excuse us guys” akasema
Dr Fabian akatoka mle sebuleni
na Dr Evans
“Ahsante Mungu.Ruby
amekuja nchini ! akasema
Mathew kwa furaha
“Austin ahsante sana kwa
kumshauri Rais amuite Ruby
nyumbani.Ulifanya jambo
kubwa na zuri sana.I can’t wait
to see her ! akasema Mathew na
kumpa Mathew mkono wa
pongezi
“Haya ni maajabu.Nyote
wawili watu muhimu mmefika
kwa wakati mmoja” akasema
Austin
“Hii ni mipango ya
Mungu.Ni yeye ambaye ametaka
iwe hivi ilivyo.Sasa unaweza
ukaamini kwamba kwa namna
yoyote ile Afrika Mashariki
haitaweza kusambaratika”
akasema Mathew
Dr Fabian na Dr Evans
waliingia katika chumba Fulani
ambacho hakikuwa na mtu
ndani.
“Dr Evans nini hiki
kinaendelea?I real don’t
understand.Mathew Mulumbi
ambaye nilielezwa na Ruby
kwamba alifariki dunia ni huyu
uliyeongozana naye hapa au
kuna mwingine?akauliza Dr
Fabian
“Dr Fabian kuna Mathew
Mulumbi mmoja tu ambaye ni
huyu niliyeogozana naye”
akasema Dr Evans
“Haya ni
maajabu.Niliambiwa amefariki
sasa ametokea wapi tena?Ni
yeye kweli au ni mzimu ule?
Akauliza DrFabian
“Ni yeye mwenyewe
Mathew Mulumbi” akasema Dr
Evans.Ukapita ukimya mfupi Dr
Fabian akauliza
“Kwa nini ikadaiwa
amefariki dunia?
“Kuna hadithi ndefu hapa
nitakueleza lakini ukweli ni
kwamba Mathew hakufariki
dunia kama
tulivyodhani.Mathew ni mzima”
“Alikuwa wapi?
“Hajasema chochote
kuhusu mahala
alikokuwa.Ameibuka tu toka
kusikojulikana.Dr Fabian mimi
nawe tutakuwa na
mazungumzo marefu kidogo
baadae na nitakueleza kila kitu
lakini nakuomba nimekuja na
hawa vijana tuna mazungumzo
nawe” akasema Dr Evans na Dr
Fabiana akaonekana kusita
“Tafadhali Dr Fabian
tunahitaji kuzungumza na hawa
vijana”
“Kuna nini? Akauliza Dr
Fabian
“Kuna jambo kubwa la
kujadili.Tafadhali sana”
akasema Dr Evans
“Mzee naomba liwe ni
jambo lenye maslahi kwa
sababu dalili ninazoziona si
njema”
“Niamini mimi Dr Fabian”
akasema Dr Evans kisha
wakatoka na kurejea mahala
walikowaacha Mathew na
Austin
“Samahani tuliwakimbia
kidogo.Tulikuwa na
mazungumzo ya
faragha.Karibuni sana
vijana.Mathew Mulumbi karibu
sana.Ni furaha yangu kukutana
nawe leo” akasema Dr Fabian.
“Hata mimi nafurahi
kukutana nawe mheshimiwa
Rais” akasema Mathew
“Mzee wangu hapa
anasema kwamba kuna
mazungumzo muhimu.Naomba
tuelekee katika chumba cha
maongezi” akasema Dr Fabian
na kuwaongoza akina Mathew
kuelekea katika chumba cha
mazungumzo ya faragha
“Karibuni sana vijana
wangu.Mtanisamehe kwa
mkanganyiko uliotokea awali”
akaanzisha maongezi Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
nimekuja na hawa vijana wangu
kwa ajili ya mazungumzo
muhimu yanayohusiana na kile
kilichotokea na kinachoendelea
hivi sasa katika nchi yetu na
Afrika Mashariki kwa
ujumla.Nisiwe mzungumzaji
mkubwa naomba nimpe nafasi
Mathew Mulumbi aendelee”
akasema Dr Evans
“Karibu Mathew” akasema
Dr Fabian na bila kupoteza
muda Mathew akasema
“Mheshimiwa Rais,kama
rais mstaafu Dr Evans
alivyokwisha nitambulisha
kwako naitwa Mathew
Mulumbi,niliwahi kufanya kazi
katika idara ya ujasusi Tanzania
kabla ya kuanza
kujishughulisha na biashara
lakini hata wakati ninafanya
biashara zangu bado niliendelea
kushiriki katika misheni mbali
mbali kubwa zenye maslahi
mapana kwa nchi
yetu”akanyamaza kidogo
“Sitaki kuongelea tukio la
mimi kupotea na kujulikana
nimefariki dunia na
nisingependa kuulizwa
nilikuwa wapi.Ninaomba
nijielekeze moja kwa moja
katika suala la msingi lililotuleta
hapa” akanyamaza tena kidogo
“Japokuwa sikuwepo hapa
nchini lakini ninafahamu kile
kilichotokea na kinachoendelea
na baada ya kufika hapa nchini
nikapata tena taarifa nyingine
ambazo sikuwa nikizifahamu
kuhusiana na hiki
kinachoendelea hivi
sasa.Ambacho sikuwa
ninakifahamu ni mauaji ya Lucy
Muganza na mumewe” akasema
Mathew na kunyamaza huku
wote mle ndani wakimsikiliza
kwa makini sana
“Mheshimiwa Rais
kinachoendelea hivi sasa ni
mpango mkubwa wa nchi
kubwa tajiri kuisambaratisha
jumuiya ya Afrika Mashariki
nadhani unalifahamu hilo ndiyo
maana Lucy Muganza akauwa”
akasema Mathew na Dr Fabian
akatikisa kichwa kukubaliana
naye.
“Baada ya kifo cha Lucy
Muganza mambo hayakuishia
pale.Mpango ule bado
uliendelea na hiki
kinachoendelea hivi sasa ni
muendelezo wa kile
alichotakiwa kukifanya Lucy
Muganza lakini akawahi
kuuawa.Mataifa walioandaa
mpango huu wanailenga zaidi
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo lakini hawawezi kuingia
nchini Congo bila kuiondoa
kwanza nchi hiyo katika
jumuiya ya Afrika Mashariki na
ili kuiondoa nchi ya Congo
katika jumuiya ya Afrika
mashariki lazima kwanza
kuisambaratisha jumuiya hiyo
na kile kilichotokea juzi hapa
nchini ni mkakati wa mabeberu
kuisambaratisha jumuiya ya
Afrika Mashariki na
kutengeneza njia kuelekea
Congo.Tayari mpango wao huo
umeanza kuonyesha matunda
kwani umetokea mvurugano
mubwa baina ya nchi
wanachama na kuna kila dalili
kwamba uhai wa jumuiya hii
uko mashakani” akanyamaza
kidogo na kumtazama Dr
Fabian aliyekuwa ameweka
mkono shavuni akisikiliza kwa
makini sana
“Wametumia akili kubwa
kumtumia James Kasai
kutekeleza shambulio lile na
kuamsha hasira kali na sasa kila
nchi inataka kuishambulia
Uganda kwa kigezo cha
kumsaka au kulipiza kisasi kwa
James Kasai.Utaniwia radhi
mheshimiwa Rais lakini sina
lugha nyingine ninayoweza
kuitumia kulisema hili lakini
mlikurupuka sana kuanza
kuchukua hatua za
kijeshi.Hamkutakiwa
kuishambulia au kupanga
mipango ya kuingia Uganda
kijeshi kwa ajili ya kumsaka
James Kasai.Wewe mheshimiwa
Rais ukiwa kama mwenyekiti
wa jumuiya ya Afrika mashariki
ulitakiwa kuwa mstahimilivu na
kutafuta njia muafaka ya
kulimaliza hili suala lakini
ulikuwa mstari wa mbele
kuwaunganisha Rwanda na
Congo kuunda kikosi cha jeshi
kwenda nchini Uganda.Naweza
kusema kwamba kuna mkono
wako katika mvurugano huu
unaoendelea hivi sasa katika
eneo la Afrika Mashariki”
akasema Mathew na
kunyamaza baada ya sura ya Dr
Fabian kubadilika
“Dr Evans nini hasa
kimekuleta hapa? Umewaleta
vijana hawa waje waanze
kunifundisha uongozi? Akauliza
Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais nadhani
ungeendelea kumsikiliza
Mathew Mulumbi bado
hajamaliza kile anachotaka
kukueleza” akasema Dr Evans
“Huu ni upotevu mkubwa
wa muda wangu ..” akasema Dr
Fabian huku akitaka
kunyanyuka
“Sir,we’re not wasting any
of your time” akasema Mathew
“Yes you are. Nimekaa
nanyi hapa kwa heshima ya
huyu mzee wangu lakini kumbe
mambo mnayokuja kunieleza ni
upuuzi mtupu”
“Si upuuzi mheshimiwa
Rais” akajibu Mathew naye
akasimama
“Mathew please sit down”
akasema Dr Evans
“Ndiyo ni upuuzi
mtupu.Unadiriki kunifundisha
mimi namna ya kuongoza nchi?!
Who are you?Unadiriki
kumtetea gaidi muuaji ambaye
ameua watu kikatili
kabisa.Wewe ni nani kuhoji
maamuzi yangu?Mimi ni rais wa
Jamhuri ya muungano wa
Tanzania ninayeogoza watu
zaidi ya milioni hamsini ambao
natakiwa kuhakikisha usalama
wao wewe ni nani wa kuhoji
hatua ninazozichukua? Akafoka
Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
nafahamu umeumizwa na kifo
cha mke wako na hata sisi sote
tumeumizwa pia likini hatua
zile ulizozichukua wewe na
wenzako wa Rwanda na Congo
kukabiliana na suala hili si
hatua sahihi.Narudia kusema
tena na utanisamehe kwamba
mlikurupuka ! akasema Mathew
na Dr Fabian akamtazama kwa
hasira
“Dr Evans ninakuheshimu
sana mzee wangu na
nilitegemea una kitu kikubwa
unakuja kunieleza lakini kumbe
umeniletea huyu mgonjwa wa
akili.Narudia tena kukuuliza
Mathew Mulumbi wewe ni nani
wa kuhoji maamuzi ya Rais?
Unadhani katika watu milioni
hamsini ninaowaongoza wewe
pekee ndiye mwenye akili
kubwa kuliko wote? Akauliza Dr
Fabian akiwa amewaka hasira
“Dr Evans nashukuru kwa
kuja kunitembelea.Tumemaliza
kuna mambo mengine natakiwa
kuyafanya” akasema Dr Fabian
na kugeuka kuanza kuelekea
mlangoni
“Mr President we’re not
finished yet. You have to listen
to me ! akasema Mathew
“Siongei na wagonjwa wa
akili mimi ! akafoka Dr Fabian
akipiga hatua kuelekea
mlangoni
“You’re not going to find
James Kasai ! akasema Mathew
na Dr Evans akageuka
“What ?akauliza
“Umenisikia vizuri
mheshimiwa Rais.Hamtaweza
kumpata James Kasai ! Mathew
akasisitiza na Dr Fabian akatoa
kicheko kidogo
“Dr Evans hiki kituko gani
umeniletea mzee wangu?
Akauliza Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais naomba
umsikilize Mathew kile
anachotaka kukueleza.Ana kitu
cha muhimu sana” akasema Dr
Evans
“Dr Evans nakushangaa
sana.Unamuaminije huyu mtu?
Ameibuka kutoka
kusikojulikana na halafu
unamuamini? Ni vipi kama…oh
my God ! akasema Dr Fabian
“Mr president I know
Mathew Mulumbi and I trust
him.Nisingeweza kuja naye
hapa kama hana kitu cha maana
cha kukueleza ! akasema Dr
Evans
“Please Mr president !
akasema Dr Evans
“Kwa heshima ya huyu
mzee ambaye ninamuheshimu
sana nakupa dakika tatu
unieleze hicho unachotaka
kukisema lakini ukiendelea na
upuuzi wako wa kuhoji
maamuzi yangu kikao hiki
kitakuwa kimefika mwisho”
akasema Dr Fabian
“Thank you Mr President”
akasema Mathew
“Samahani kwa maneno
niliyoyatumia awali
yawezekana yalikuwa makali
lakini ninaendelea kusisitiza
kile nilichokisema kwamba
hatua za kijeshi dhidi ya Uganda
kwa kigezo cha kumsaka James
Kasai hazitakuwa na manufaa
yoyote badala yake zitakuwa ni
kama kuongeza mafuta katika
moto”
“Mathew unaniudhi mno
kwa kauli hiyo ya kwamba
maamuzi yetu ya kutumia
nguvu za kijeshi hayakuwa
maamuzi sahihi.Hatukuwa
wajinga tuliofanya maamuzi
haya ya kuunda kikosi cha
pamoja kwenda Uganda
kumsaka James Kasai !
akasema kwa ukali Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
ninasema kwamba hayakuwa
maamuzi sahihi kwa sababu
hamtaweza kumpata James
Kasai kwa nguvu za kijeshi”
“Kwa nini tusimpate?
Wewe unafahamu sana kuliko
sisi?Mimi ni Rais wa nchi na
nina kila taarifa za kila
kinachoendelea hapa nchini
hivyo hatukukurupuka narudia
tena kusema kwamba iwe mvua
iwe jua lazima James Kasai
apatikane ! akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais ni kweli
una kila taarifa ya kila
kinachoendelea hapa nchini
lakini kwa bahati mbaya wewe
na wenzako hamna taarifa
sahihi kuhusiana na James
Kasai ndiyo maana mkachukua
maamuzi yale lakini kama
mngekuwa na taarifa sahihi
msingeandaa kikosi kwenda
Uganda kumsaka”
“Wewe unazo hizo taarifa
za James”
“Hicho ndicho hasa
kilichonirejesha nyumbani”
akasema Mathew na
kunyamaza kidogo halafu
akasema
“Nimekuja kwa lengo moja
tu kummaliza James Kasai na
kuiokoa jumuiya yaAfrika
mashariki katika hatari ya
kusambaratika” akasema
Mathew na Dr Fabian akatoa
kicheko
“Wewe ! akasema Dr Fabian
kwa mshangao
“Unataka kumuondoa
James Kasai? Unajua
unachokizungumza Mathew
Mulumbi? Akauliza Dr Fabian
na kumgeukia Dr Evans
“Dr Evans nilikwambia
umeniletea mgonjwa wa
akili.Hajui anachokizungumza
ni kitu gani”
“Dr Fabian ninakuheshimu
sana na ninakuomba
uniheshimu pia.Huyu
anayezungumza si mgonjwa wa
akili na anajua anachokisema”
akasema Dr Evans
“Mheshimiwa Rais
ninamaanisha kile
ninachokisema kwamba
nimekuja kummaliza James
Kasai na kuinusuru jumuiya ya
Afrika Mashariki.Ningeweza
kumuondoa James kima kimya
bila kukueleza chochote kwani
ninazo taarifa zote za kuhusiana
naye lakini nimekuja kwako
kukueleza kuhusiana na kile
ninachotaka kukifanya na
kukuomba usitishe operesheni
zote za kijeshi mlizopanga
kuchukua kuhusu kumsaka
James Kasai na vile vile
uwashauri wenzako wa Rwanda
na Congo waondoe majeshi yao
katika mipaka ya nchi zao na
Uganda” akasema Mathew na
Dr Fabian akazama mawazoni
kisha akauliza
“Taarifa gani unazo kuhusu
James Kasai ambazo unadhani
sisi hatuna?
“Mnachofahamu ni kwamba
James Kasai amejificha katika
misitu ya Kaskazini mwa
Uganda.Siyo Sahihi.James Kasai
hayuko huko”
“Kama hayuko huko
msituni yuko wapi?akauliza Dr
Fabian
“Siwezi kusema kwa sasa
yuko wapi lakini hayuko
msituni na mkipeleka kikosi
msituni utakuwa ni upotevu wa
muda na uchokozi kwa Uganda”
“Kama hujui mahala alipo
James Kasai unataka
kumuondoa vipi? Dr Evans
huyu mtu anacheza na akili
zetu.Anasema anao uwezo wa
kumuondoa James Kasai lakini
hajui mahala alipo”
“Hata kama ningekwambia
usingeniamini.Umetanguliza
hasira mbele unataka kulipiza
kisasi kwa kifo cha mkeo bila
kuzingati maslahi mapana ya
nchi na jumuiya ya Afrika
mashariki.James Kasai amezidi
kujitanua na kwa sasa
amejiunga na kundi la kigaidi la
IS ambao wanamfadhili kwa
fedha na vifaa vya kijeshi na ana
nguvu kubwa hivyo
mnapofikiria kupambana na
James Kasai mfikirie pia kuhusu
kupambana na kundi la kigaidi
la IS.Mheshimiwa Rais tafadhali
nakuomba uniamini hiki
ninachokwambia kwamba
ninao uwezo wa kumuondoa
James Kasai na vile vile
kuuondoa mzizi wa kundi la IS
ambalo kwa miaka ya karibu
limeendelea kujiimarisha katika
ukanda huu wa Afrika
Mashariki na kati.Mimi si
mwanasiasa na sina maneno
matamu ya kukushawishi lakini
nilichokueleza hapa ni ukweli
mtupu.Ni juu yako kufanya
maamuzi aidha kufuata yale
niliyokushauri au kuendelea
kuibomoa jumuiya ya Afrika
mashariki kwa kuendelea na
mipango ya kijeshi dhidi ya
Uganda” akasema Mathew.Dr
Evans akakohoa kidogo na
kusema
“Mheshimiwa Rais kijana
ameweka wazi kila
kitu.Ninamfahamu Mathew
Mulumbi na ninasimama
upande wake.Alichokueleza ni
sahihi na maamuzi yote ni juu
yako.Mimi kwa ushauri wangu
badala ya kuendelea kumpinga
na kumuona kama mgonjwa wa
akili ungekubali kushirikiana
naye kwani anahitaji sana
kuungwa mkono kwa kitendo
hiki cha kizalendo anachotaka
kukifanya.Imekuwa ni kawaida
ya Mathew kuyaweka hatarini
maisha yake kwa maslahi ya
taifa lake hivyo ni mtu
anayehitaji kupongezwa na si
kubezwa.Lakini kama bado
unamuona ni mwendawazimu
basi endelea na mipango yako
ya kijeshi na wenzako na
utauona mwisho wake.Mimi na
vijana wangu tunaondoka lakini
pale maji yatakapofika shingoni
usijaribu kunitafuta au
kuwatafuta vijana hawa”
akasema Dr Evans na kusimama
“Mheshimiwa Rais kabla
hatujaondoka nataka kuuliza
swali.Nani alitoa wazo la
kuundwa kwa kikosi cha umoja
kwenda kuivamia Uganda
kumsaka James Kasai?akauliza
Mathew Dr Fabian akabaki
kimya
“Lilikuwa ni wazo lako
mheshimiwa Rais? Dr Evans
naye akauliza
“Lilikuwa ni wazo la
pamoja”
“Nani aliyelileta
mezani?akauliza Mathew na Dr
Fabian akabaki kimya
“Ukimya huo unaonyesha
kwamba si wewe uliyebuni
wazo hilo la kuundwa kwa
kikosi cha jeshi cha pamoja kwa
ajili ya kwenda Uganda
kumsaka James Kasai.Wazo hilo
lilitoka aidha kwa Rais wa
Rwanda au Congo.Mheshimiwa
Rais utanisamehe kwa mara
nyingine tena kwa lugha
ninayotumia lakini labda
nizungumze kwa kiingereza
they’re using you.Rwanda na
Congo kila moja kwa muda
mrefu imekuwa na mahusiano
yasiyo mazuri na nchi ya
Uganda na wanataka kutumia
nafasi hii kuiadhibu
Uganda.Wote wamejificha
ndani ya koti lako la inaonekana
kwamba ni Tanzania ndiyo
inayoongoza kikosi hicho
kinachoandaliwa kwenda
Uganda.Mheshimiwa Rais tunao
uwezo wa kumuondoa James
Kasai kimya kimya bila hata
kutumia nguvu za kijeshi na
kuinusuru jumuiya hii ya Afrika
Mashariki kusambaratikia
katika mikono yako.Kama ni
kulipiza kisasi kwa kile
alichokifanya James kumuua
mke wako nakuahidi ninaweza
kumleta akiwa hai na wewe
ukamfanya kile utakacho ili
kumaliza hasira yako” akasema
Mathew na Dr Fabian
akainamisha kichwa kafikiri
kwa muda na kusema
“Mathew una hakika unao
uwezo wa kumuondoa James
Kasai? Akauliza Dr Fabian
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Ninao uwezo wa
kumuondoa James Kasai na
ndicho ambacho nimekuja
kukifanya na nitaendelea na
mipango yangu hiyo hata kama
hautakubaliana nami kwa
sababu kwa mipango yenu
hamtaweza kumuondoa James
Kasai na ataendelea kuwa mtu
hatari kwa eneo hili la Afrika
mashariki ” akasema Mathew
“What do you
need?akauliza Dr Fabian na Dr
Evans akaonyesha tabasamu
usoni
“Kitu cha kwanza
ninachokihitaji ni kuwasiliana
na marais wenzako wa Rwanda
na jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo na kuwataka waondoe
vikosi vyao vya jeshi katika
mipaka ya nchi zao na
Uganda.Tunataka kwanza
kuondoa hatari ya kutokea
machafuko makubwa katika
ukanda wa Afrika Mashariki na
hilo litawezekana pale ambapo
vikosi vya jeshi vitaondolewa
mipakani na wewe kama
mwenyekiti wa jumuiya ya
Afrika Mashariki ndiye mwenye
uwezo wa kulifanya hilo na si
mimi wala Dr Evans” akasema
Mathew na Dr Fabian akaguna
“Mathew suala hilo si rahisi
kama unavyodhani.Mataifa
haya mawili wote wamekwisha
athirika na James
Kasai.Amefanya ukatili mkubwa
Congo na hata Rwanda pia na
kwa muda refu nchi hizi mbili
zimekuwa zikiishinikiza Uganda
kumfukuza James katika misitu
ya nchi hiyo lakini Uganda
imekuwa ikipuuza na kwa sasa
wameamua kuchukua
hatua.Nafahamu kama
ulivyoeleza kuwa nchi hizi
zimekuwa na migogoro yao ya
muda mrefu lakini kwa sasa
wote wamepata chanzo cha
kutaka kuishambulia
Uganda.Wazo la kuundwa kwa
kikosi cha pamoja halikuwa
langu bali la Rais wa
Rwanda.Kwa upande Fulani
ninaanza kukubaliana nawe
Mathew kwamba yawezekana
tuliharakisha sana kufanya
maamuzi yale ya kutumia nguvu
za kijeshi kutafuta James Kasai
na sasa inaniwia ugumu namna
ya kuanza kuwashawishi hawa
wenzangu kutokutumia nguzu
za kijeshi.Lazima watajitenga
nami na kujiunga wao wenyewe
wakaendelea na operesheni
zao.Kitu cha msingi ambacho
kinaweza kunipa hata mimi
nguvu ya kuwataka waondoe
majeshi yao mpakani ni kama
tukifanikiwa kumuua James
Kasai .Hawatakuwa tena na
sababu nyingine ya kuendelea
na mapambano na Uganda
hivyo Mathew Mulumbi kama
kweli unataka kusaidia katika
jambo hili muue James Kasai na
mambo yote yatakuwa
yametulia”
“Ahsante mheshimiwa Rais
kwa kuanza kunielewa.Narudia
kukuhakikishia tena kwamba
uwezo wa kumuua James Kasai
ninao na nitamuondoa lakini
naomba japo kwa kipindi hiki
ambacho nitakuwa
nikilishughulikia suala hilo
operesheni zozote za kijeshi
zisifanyike nchini Uganda ili
kutokuharibu mambo”
“Ninakupa siku saba
Mathew uwe umempata James
Kasai na kama ukishindwa
ndani ya siku hizo saba basi
kikosi cha umoja kitaendelea na
kazi yake bila kujali athari
zitakazojitokeza kwani
hatuwezi kuendelea kumuacha
huyu mtu mmoja aendelee kuua
watu hovyo wakati uwezo wa
kumuondoa
tunao.Ninakuruhusu ukafanye
operesheni yako ndani ya siku
saba uwe tayari umempata
James”
“Ahsante mheshimiw
Rais.Nakuahidi kabla ya siku
hizo saba hazijamalizika
nitakuwa nimempata James
Kasai”
“Kitu gani unahitaji
nikusaidie?akauliza Dr Fabian
“Kitu cha kwanza
ninachokihitaji ni kuunda timu
ambayo tutaifanya hiyo
operesheni.Tayari ninaye
Austin.Nilimtegemea Gosu Gosu
lakini kwa bahati mbaya
amepigwa risasi lakini tayari
tumekwisha pata vijana
wengine wawili ambao
tutasaidiana nao vile vile
ninamuhitaji Ruby”
“Ruby? Akauliza Dr Fabian
“Ndiyo.Ninamuhitaji sana
Ruby katika operesheni hii”
“Ruby nimemuita hapa
nchini kwa ajili ya kazi nyingine
kabisa.Operesheni hiyo ni
hatari na siwezi kuruhusu
akajiunga na timu hiyo na
kuhatarisha maisha yake”
akasema Dr Fabian
“Ninamuhitaji Ruby pamoja
na idara anayokuja kuiongoza”
akasema Mathew
“SNSA? Unaifahamu idara
hiyo?akauliza Dr Fabian
“Ndiyo ninaifahamu vyema”
akasema Mathew
“Ruby bado sijamkabidhi
rasmi nafasi ya ukurugenzi wa
SNSA na nimempa nafasi ya
kupumzika kwa wiki moja kabla
ya kuanza kazi rasmi” akasema
Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais hii ni
vita na hakuna muda wa
kupumzika.Ruby anatakiwa
aanze kazi mara
moja.Tunaihitaji ile idara ikiwa
chini yake.Nakuomba
ikiwezekana hata kesho
ukamkabdhi ofisi.Ruby ni
mchapkazi hachoki hata
ukimuita hapa sasa hivi na
kumkabidhi ofisi ataanza kazi
hivyo hakuna haja ya kumpa
mapumziko ya wiki
nzima”akasema Mathew
“Mathew unanilazimisha
kufanya jambo ambalo sikuwa
nimelikusudia.Ruby amepitia
mambo mazito hadi kufika hapa
ndiyo maana nimempa muda
wa kupumzisha akili yake”
“Mheshimiwa Rais najua
unalo tatizo la kuamini watu
lakini nakuomba katika hili
ujaribu kuniamini”
“Mheshimiwa Rais hata
mimi nakusisitiza kwamba
mtimizie Mathew kila
anachokitaka na hutajutia”
akasema Dr Evans
“Kwa ajili yako Dr Evans
nitafanya lakini roho yangu
haitaki kabisa” akasema Dr
Fabian na Mathew akainuka
“Mheshimiwa rais ahsante
kwa kulikubali ombi langu.Sina
kingine ninachohitaji toka
kwako.Ninachoomba kwa sasa
ni kuonana na Ruby” akasema
Mathew na Dr Evans akamuita
mmoja wa wasaidizi wake
akamtaka awapeleke akina
Mathew katika nyumba yake
aliko Ruby.Mathew na Austin
wakawaaga Dr Fabian na Dr
Evans wakaondoka kuelekea
anakoishi Ruby.
“Dr Evans nini hiki
umenifanyia leo? Sikutegemea
kabisa ! akasema Dr Fabian
baada ya akina Mathew
kuondoka
“Fabian leo umefanya kitu
kibaya sana.Umeonyesha
dharau kubwa kwa Mathew
Mulumbi.Sikutegemea
kabisa.Taifa linamuhitaji sana
Mathew kwa wakati huu na
ninaweza kusema kwamba ni
Mungu ndiye
aliyemleta.Hukupaswa
kumtamkia maneno kama yale”
akasema Dr Evans
“Utanisamehe mzee wangu
lakini Yule kijana aliniudhi
sana.Kuibuka kutoka kusiko
julikana halafu anaanza kuhoji
maamuzi yangu.Anataka
kunifundisha namna ya
kuongoza nchi.Sikupenda jambo
lile”
“Hakuwa anakufundisha
kuongoza bali alikuwa anasema
kitu cha kweli.Makosa
makubwa yamekwisha fanyika
Fabian japokuwa hamtaki
kukubali na ulipaswa
kushukuru kwani Mathew
Mulumbi ndiye ambaye
amekuja kurekebisha pale
ulipokosea.Hakukosea kusema
kwamba mliongozwa na hasira
kufanya maamuzi yale ya
kuandaa kikosi cha jeshi
kumsaka James Kasai.Alitumia
lugha kali kidogo ya
kukurupuka na mimi ninarudia
kusema kwamba
mlikurupuka.Fabian
kinachoendelea hivi sasa Afrika
mashariki kinawafanya
mabeberu wafungue chupa za
shampeni wakifurahia.Muache
Mathew Mulumbi akamuondoe
James Kasai.Mpe kila
anachokihitaji na utaona
matokeo yake” akasema Dr
Evans.
Walikuwa na mazungumzo
marefu kisha Dr Evans akaaga
na kuondoka
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 8: EPISODE 6
Mathew na Austin
waliwasili katika nyumba ya
Rais anakoishi
Ruby.Walikaribishwa ndani
kisha mmoja wa watumishi
akaenda kumjulisha Ruby
kwamba kuna wageni wake
wamekuja kumtembelea.Ruby
hakupoteza muda akatoka
chumbani kwake na kuelekea
sebuleni huku akijua wageni
wale lazima watakuwa
wametumwa na Rais.Alipoingia
sebuleni mtu wa kwanza
kumuona alikuwa ni Austin
“Austin ! akasema kwa sauti
ndogo ya mstuko na kuanza
kupiga hatua ndogo mara
akapawa na mstuko wa mwaka
baada ya kugonganisha macho
na Mathew.Mstuko alioupata
ulikuwa mkubwa akataka
kuzungumza kitu sauti
haikutoka midomo
ikamtetemeka.
“Hallo Ruby ! akasema
Mathew lakini Ruby hakujibu
kitu alishindwa kuzungumza
“Ruby it’s me
Mathew.Please say something !
akasema Mathew
“I…I…I.don…I don’t
kn………..”akasema Ruby
akitetemeka mdomo kisha
akajikuta ameangukia mikononi
mwa Mathew nakuanza kulia
machozi mengi
“Nyamaza Ruby” akasema
Mathew
“Why Mathew ?!! Why ?!!
akauliza Ruby huku akiendelea
kumwaga machozi
“Ruby please.I know this is
a surprise to you and you have
so many question to ask but
right now you and I we need to
go somewhere” akasema
Mathew na Ruby akainua
kichwa akafuta machozi na
kumtazama Mathew
“Oh my God ! Why
Mathew?Kwa nini umenitesa
namna hii?akauliza Ruby na
kukilaza kichwa chake kifuani
kwa Mathew akiendelea kulia
“Ruby tutazungumza
nitakueleza kila kitu lakini kwa
sasa nakuomba ujiandae
tuondoke”
“Sina haja ya kujiandaa
Mathew.Twende kokote
unakotaka hivi hivi nilivyo”
akasema Ruby kisha wakainuka
na kuelekea katika gari
wakaondoka.Ndani ya gari bado
Ruby aliendelea kumwaga
machozi hadi walipofika
nyumbani kwa Mathew ambako
walishuka kisha akampa Austin
maelekezo kadhaa na
kumuachia gari akaondokanalo
wao wakaingia ndani na
kuelekea moja kwa moja hadi
chumbani kwa Mathew.
“Ruby there is only one
thing I need right now !
akasema Mathew na
kumkumbatia Ruby akaanza
kumbusu.Ruby alisisimka
unyayo hadi
unyweleni.Hatimaye
mwanaume Yule aliyempenda
kwa moyo wake wote leo hii
ametua tena katika mikono
yake.Bado Ruby alijihisi kama
yuko ndotoni.Kadiri sekunde
zilivyozidi kwenda ndivyo
alivyozidi kuona mabadiliko
katika mwili wake na kugundua
kile ambacho kilikuwa
kinaendelea.Akamkumbatia
Mathew kwa nguvu na kuanza
kumporomoshea mabusu
mengi.Mathew akaivua fulana
akaitupa na Ruby akastuka
baada ya mkono wake laini
kukutana na makovu makubwa
ya vidonda mgongoni kwa
Mathew
“Mathew what’s
this?akauliza
“Utauliza baadae..” akasema
Mathew huku akiendelea na
zoezi.Ruby alishindwa
kuvumilia zaidi akamtaka
Mathew kuanzisha
mpambano.Filimbi ikapulizwa
na mpambano wa kukata na
shokaa ukaanza.
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 8: EPISODE 7
“Mathew is this real?Au
niko ndotoni?akauliza Ruby
akiwa amemkumbatia Mathew
baada ya kumaliza mzunguko
mmoja
“Ruby hii si ndoto.Ni kweli
tuko wote” akasema Mathew
“Mathew ninashindwa
niseme nini ndiyo maana
ninabaki tu ninalia”
“Usilie Ruby ni mimi
Mathew Mulumbi Yule Yule
unayemfahamu.Usiwe na
wasiwasi wowote” akasema
Mathew
“Ulikuwa wapi?What
happened to you? Nimelia
machozi mengi sana kwa ajili
yako Mathew lakini leo Mungu
amesikia kilio changu na
amekuleta tena.Naamini haya ni
maongozi ya Mungu kwani
nimepitia magumu mengi hadi
kufika hapa Tanzania lakini
kumbe yale yote niliyokuwa
nayapitia ni kwa ajili ya kuja
kukutana tena nawe Mathew”
akasema Ruby na machozi
yakaanza tena kumtoka
“Ruby huu si muda wa
kulia”
“Mathew niache nilie
tafadhali nimeteseka
sana,nimelia sana baada ya
kupata taarifa ya kufariki
kwako.Nashindwa hata
nikueleze vipi” akasema Ruby
“Naelewa Ruby.Hata mimi
haukuwahi kubanduka katika
mawazo yangu.Ruby kuna
mengi ya kuzungumza.Naamini
unataka sana kujua nini
kilinitokea na nilikuwa
wapi.Mimi pia nina hamu sana
ya kutaka kufahamu mengi
kuhusu wewe katika kipindi
hiki chote ambacho sikuwepo
lakini hayo ni baadae kwa sasa
kuna kitu cha muhimu nataka
kukufahamisha” akasema
Mathew
“Niambie Mathew”
akasema Ruby
“Kuna misheni nzito
imenirudisha hapa nyumbani
na ninakuhitaji sana katika
misheni hiyo muhimu” akasema
Mathew na Ruby akaonyesha
mstuko kidogo
“Mathew hata baada ya
masahibu yote kukutokea bado
unaendelea na hizi
kazi?akauliza Ruby
“Ni misheni muhimu sana
kwa nchi Ruby”
“Misheni ipi hiyo? Akauliza
Ruby
“Nadhani Rais amekwisha
kufahamisha kuhusiana na kile
kilichotokea hapa nchini siku
chache zilizopita”
“Ndiyo nilikutana na Rais
jana ikulu tukawa na
mazungumzo marefu kuhusiana
na kazi aliyoniita nije
kuifanya.Rais ameniita hapa
nyumbani kwa ajili ya
kuiongoza idara ya siri ya
mambo ya ndani ya nchi ile
ambayo alikuwa anaiongoza
Devotha” akasema Ruby
“Ninafahamu.Austin
amekwisha nieleza kila kitu na
Rais pia ameniambia hivyo”
“Umeonana na Rais tayari?
“Ndiyo nimeonana na
Rais.Nilitoka ikulu kuonana
naye ndipo nikakufuata”
“Umekuja lini hapa nchini?
“Nimekuja juzi usiku”
akajibu Mathew
“What a coincidence”
akasema Ruby
“Nadhani utaona namna
sote wawili tulivyorejeshwa
nyumbani katika muda ulio
karibu sawa.Sikujua kama
nitakutana nawe huku na wewe
hukujua kama utakutana
nami.Kukutana huku kuna
sababu kubwa.Nchi yetu kwa
sasa inapitia kipindi kigumu
sana kufuatia shambulio lile
lililotokea hivi majuzi na kuua
wake watatu wa
marais,mabalozi na raia
wengine.Sitaki kurudia kwani
Rais amekwisha kueleza kila
kitu”
“Ndiyo amenieleza kila kitu
jana.Ni tukio baya kabisa
kutokea”akasema Ruby
“Aliyefanya tukio lile
anaitwa James Kasai ambaye
ameshirikiana na kundi la
kigaidi la IS na kuleta
mvurugano mkubwa katika nchi
za jumuiya ya Afrika
mashariki.Hivi sasa nchi
hazielewani na nyingine
zinashambuliana.Huu ni
mpango mkubwa
kuisambaratisha jumuiya ya
Afrika Mashariki ulioandaliwa
na nchi kubwa na lengo kuu la
kufanya hivyo wanailenga
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo.Shambulio lile ulikuwa ni
mtego kwa nchi za Afrika
mashariki na kwa bahati mbaya
nchi zetu zimenasa katika
mtego huo na hivi sasa amani
imeanza kutoweka na jumuiya
ya Afrika mashariki iko hatarini
kusambaratika na mabeberu
wanaelekea kupata
ushindi.Misheni iliyonileta ni
kumuondoa James Kasai na
kuutegua mtego wa mabeberu
wa kuisambaratisha jumuiya ya
Afrika Mashariki.Vile vile
nimekuja kuung’oa mzizi wa IS
uliopo hapa nchini.Ni misheni
kubwa na nzito ndiyo maana
ninakuhitaji sana uuungane
nami katika misheni hiyo”
akasema Mathew
“Mathew Mulumbi sijawahi
kusema hapana kila pale
uliponiita kwa ajili ya misheni
yoyote toka tumefahamiana na
hata sasa siwezi kusema
hapana.Lakini Mathew huyu
James Kasai anaongoza kundi
kubwa la waasi na wanaishi
msituni.How are we going to
end him?Rais Dr Fabian na
wenzake wa Rwanda na Congo
tayari wameandaa kikosi cha
jeshi ambacho kitakwenda
kumsaka James Kasai msituni
na kuhakikisha kinamtia
nguvuni”
“Huo ndio mtego ambao
viongozi wetu hawa walitegewa
na wamenasa.Kutuma kikosi
cha jeshi Uganda ni kosa kubwa
wanataka kulifanya kwani
kutaongeza machafuko badala
ya kumsaka James.Uganda
tayari imekiita kitendo hicho ni
uchokozi mkubwa na imeahidi
kukisambaratisha hicho kikosi
endapo kitakanyaga ardhi yake
na huo utakuwa ni mwanzo wa
machafuko makubwa sana na
hicho ndicho mabeberu
wanakihitaji.Ninasema kwamba
nguvu za kijeshi hazitafaulu
kwa kuwa James Kasai haishi
msituni kama inavyodaiwa bali
anaishi maisha ya kifahari
sehemu Fulani jijini Kampala”
“James Kasai haishi
msituni? Ruby akashangaa
“Ndiyo.James haishi
msituni.Kwa muda mrefu
serikali ya Uganda imekuwa
ikimfadhili James katika
mapambano yake dhidi ya
serikali ya Congo na wakati
dunia nzima wakifahamu James
anaishi msituni lakini ukweli ni
kwamba James anaishi kifahari
jijini Kampala.Watu wengi hata
ndani ya Uganda yenyewe
hawajui kama James Kasai
anaishi kifahari katika ardhi
yao” akasema Mathew
“Unafahamu anakoishi
James ?Ruby akauliza
“Nitafahamu muda si mrefu
mahala alipo na ndiyo maana
nilimfuata Rais leo na kumtaka
asitishe mipango yote ya kijeshi
ya kumsaka James Kasai kwani
nimerejea nyumbani kwa ajili
ya kazi hiyo”akasema Mathew
“Rais amekubali?
“Amenipa siku saba niwe
nimefanikiwa kumpata James
Kasai au atapeleka kikosi cha
jeshi cha umoja ambacho
kinaendelea na mazoezi hivi
sasa.Tayari nimeandaa timu
kwa ajili ya operesheni
hiyo.Mimi,Austin vile vile
tutawaongeza vijana
wawili.Gosu Gosu hatakuwepo
kwa kuwa yuko hospitali
amepigwa risasi na watu
wasiojulikana” akasema
Mathew
“Gosu Gosu amepigwa
risasi?! Ruby akashangaa
“Ndiyo.Hali yake si
nzuri.Kwa hivi sasa anapumua
kwa msaada wa mashine”
“Oh jamani” akasema Ruby
kwa masikitiko
“Nimezungumza na Rais
tumekubaliana kwamba kesho
ataenda kukukabidhi rasmi ofisi
ili kazi ianze mara
moja.Tutaihitaji sana ofisi ile
kwani ina msaada mkubwa
kwetu katika misheni hii.Baada
ya kumaliza misheni ya James
Kasai tutaingia katika misheni
nyingine ya kuung’oa mzizi wa
IS hapa nchini” akasema
Mathew
“Mathew kama
nilivyokwambia awali kwamba
siwezi kusema hapana.Niko
nawe katika misheni
hii.Ninakuahidi kufanya kila
niwezalo kukusaidia kuweza
kufanikisha misheni hii”
“Ahsante sana Ruby”
akasema Mathew na kuanza
tena maandalizi kwa ajili ya
kuingia katika mzunguko wa
pili.
KAMPALA – UGANDA
Saa moja za jioni,katika
makazi ya Rais wa Uganda
yaliyo ndani ya kambi ya
jeshi,kulikuwa na kikao
kinaendelea kati ya Jenerali
Akiki Rwamirama Rais wa
Uganda.James Kasai na Melanie
Davis
“Mheshimiwa Rais jana
nilikutana na James.Nilimuita
mimi na kubwa nililomuitia ni
kujadili kwa kina kuhusiana na
ule mpango wetu niliouleta
kwenu wa kumuua Rais Patrice
Eyenga.Tulipokutana mara ya
mwisho ulituahidi kutupa
mrejesho baada ya kuzungumza
na mkuu wa majeshi wa Congo
lakini baada ya kutafakari sana
nikaona kuungana na wanajeshi
wa Congo kutakuwa na
changamoto kubwa ambayo ni
kuchelewa kwa mpango
wenyewe ambao mimi nataka
ufanyike haraka.Baada ya
kukutana na James tumekuja na
mpango mpya” akanyamaza
kidogo na kusema
“Utampigia simu Rais wa
Tanzania na kumtaka aitishe
kikao kati yako na Rais wa
Congo kwa ajili ya mazungumzo
ya kutafuta muafaka kwa njia ya
amani.Naamini Rais Patrice
Eyenga lazima atakubali
kukutana kwa ajili ya
mazungumzo
hayo.Atakapokuwa Dar es
salaam wakati mazungumzo
yakiendelea bomu litawekwa
katika ndege yake na
atakapoondoka kurejea
Kinshasa bomu hilo litalipuliwa
na utakuwa ni mwisho wa
Patrice atakuwa amebaki mtu
mmoja katika orodha yangu Dr
Fabian Kelelo” akasema
Melanie.Baada ya kutafakari
kidogo Jenerali Akiki akasema
“Ni mpango mzuri na mimi
ninauunga mkono lakini ugumu
wa mpango huo ni namna ya
kuliingiza bomu katika ndege
hiyo ya Rais” akasema Jenerali
Akiki
“Kwa upande huo
hakutakuwa na ugumu
wowote.Mimi nitalishughulikia
suala hilo.Ninao mtandao
mpana jijini Dar es salaam
hivyo hakutakuwa na tatizo
katika kuingiza bomu hilo ndani
ya ndege ya Rais” akasema
Melanie
“Mimi nina wazo lingine
lakini halijaenda mbali na
mpango huo wa kumuua Patrice
Eyenga.Badala ya kupandikiza
bomu ndani ya ndege ya
Rais,kwa nini tusiandae
shambulio la kujitoa mhanga na
kuwamaliza marais hao wote
wawili kwa wakati mmoja yaani
Rais Patrice Eyenga na Rais Dr
Fabian Kelelo? Kwa kuwa tayari
unao mtandao mkubwa
tunaweza kumuandaa mtu
atakayebeba bomu na pale Rais
Fabian atakapokuwa
anamsindikiza Rais Patrice basi
mtu huyo atajilipua na
kuwauwa marais hao wote
wawili kwa mara moja na
orodha yako itakuwa
imekamilika utaendelea na
maisha yako kama kawaida”
akasema James Kasai
“Huu nao unaonekana ni
mpango mzuri sana James”
akasema Melanie
“Hata mimi naona huu ni
mpango mzuri” akasema
Jenerali Akiki
“Kama nyote mnakubaliana
na mpango huu nitazungumza
na watu wa IS ili wanipatie
mtaalamu wa kuunda mabomu
ya kujitoa mhanga ambaye
atakuja Dar es salam kwa ajili
ya kutengeneza bomu hilo hivyo
basi Melanie unatakiwa ufanye
mpango ili niweze kuingia Dar
es salaam kwa ajili ya jambo
hilo.Unao mtandao mkubwa na
nina imani kwa mimi kuingia
Dar es salaam hakutakuwa na
tatizo” akasema James
“Ndiyo ninao mtandao
mkubwa na unaweza ukaingia
na kutoka Dar es salaam bila
matatizo yoyote.Kuna idara
inaitwa SNSA.Hii ni idara ya siri
ya usalama wa ndani wa
nchi.Mkurugenzi wa idara hii
yupo katika mtandao wangu na
amewekwa pale makusudi
kabisa kwa ajili ya kunisaidia
mimi kufanikisha operesheni
zangu hivyo basi kwa kumtumia
yeye na idara yake utaingia
Tanzania na kutoka salama”
akasema Melanie
Waliendelea na kikao na
kukubaliana namna
watakavyofanikisha suala lile
kisha James akamrejesha
Melanie mahala alikofikia na
yeye akaondoka kuelekea
katika makazi yake.Nusu saa
baada ya Melanie kurejea
mahala alikofikia,Jenerali Akiki
akawasili
“Mheshimiwa Rais”
akasema Melanie kwa
mshangao kidogo hakuwa
ametarajia kama Jenerali Akiki
angeweza kumfuata usiku ule.
“Melanie siwezi kupitisha
usiku huu bila kuwa nawe ndiyo
maana nimekuja.James
hajagundua chochote kama
mimi nawe tulionana na
tukazungumza?
“Hajafahamu chochote”
“Vizuri sana.Naomba
usihofu kila kitu kitakwenda
sawa kabisa .Pale mtakapokuwa
mmekamilisha mipango yote
kuhusiana na hilo bomu basi
mtanijulisha na mimi nifanye
yala ya upande wangu yaani
kuwaita mezani marais hao
wanaotakiwa
kuuawa.Nitakuunga mkono
Melanie katika kila unachotaka
kukifanya.Hata hivyo nina wazo
moja kwa nini usiingie katika
siasa? Mimi nitakupigania na
utafika mbali sana.Unaweza
hata kuwa Rais” akasema
Jenerali Akiki
“Hapana mheshimiwa
Rais.Sitaki kuwa
mwanasiasa.Nina mipango
mingine kabisa”
“Mipango ipi? Akauliza
Jenerali Akiki
“Siwezi kuisema kwa sasa
ngoja kwanza nimalize mpango
wangu wa kulipiza kisasi halafu
nitakwambia nini kinafuata”
akajibu Melanie
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Mathew na Ruby walirejea
nyumbani kwa Mathew baada
ya kutoka hospitali kufuatilia
maendeleo ya Gosu Gosu
ambaye bado hali yake haikuwa
na mabadiliko.Ruby alipitiliza
moja kwa moja bafuni kisha
Mathew akafungua kasiki
akatoa kompyuta yake na
kuelekea katika chumba cha
ofisi akamtafuta Habiba Jawad
mtandaoni na kumpigia
“Mathew Mulumbi habari
za Dar es salaam?
“Huku kwema
mama.Mnaendeleaje
huko?akauliza Mathew
“Huku tuko salama.Vipi
wewe maendeleo yako?
Mipango yako inakwendaje?
“Leo nimekutana na Rais
wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania nikazungumza naye
nikamueleza kuhusu misheni
yangu ya kumuondoa James
Kasai nikamtaka asitishe
operesheni zozote za kijeshi
wanazotaka kuzifanya nchini
Uganda kumsaka
James.Hakuonekana
kufurahishwa na ombi langu
hilo ila amenipa siku saba niwe
nimempata James Kasai ama
sivyo wataendelea na
operesheni zao za kijeshi kama
walivyopanga.Tayari nimeunda
timu maalum kwa ajili ya
operesheni hiyo na sasa
ninasubiri maelekezo yako
mama ili kazi ianze mara moja”
akasema Mathew
“Vizuri sana” akasema
Habiba na kunyamaza kidogo
“Usiku huu nimepata taarifa
kwamba kuna mtu anaitwa
Khalid Sultan Khalid.Huyu
anatokea nchini Syria.Ni
mtaalamu mkubwa sana wa
milipuko.Taarifa niliyoipata ni
kwamba Khalid anakuja
Tanzania.Ameelekezwa na
viongozi wa IS kwenda
Tanzania na kwa taarifa
nilizozipata ni kwamba Khalid
anakuja kukutana na James
Kasai jijini Dar es salaam”
“James Kasai anakuja Dar es
salaam?
“Ndiyo anakuja kukutana
na Khalid.Inaonekana IS kwa
kushirikiana na James Kasai
wanataka kufanya shambulio
lingine kubwa jijini Dar es
salaam.Kazi yako ni
kuhakikisha mipango hiyo
haifanikiwi na uhakikishe
unamuua Khalid na James
Kasai.Mathew kama kuna
shambulio linaandaliwa basi
litakuwa ni kubwa sana kwani
Khalid hushiriki katika
mashambulio makubwa
makubwa.Taarifa hiyo
nimekupa ni jukumu lako wewe
na timu yako kuhakikisha
mnafahamu ni kitu gani Khalid
na wenzake wanakipanga na
kama ni shambulio basi
mhakikshe halifanyiki na
mwisho kabisa Khalid na James
Kasai hawapaswi kutoka hai
nchini Tanzania.Umenielewa
Mathew? Akauliza Habiba
“Nimekuelewa
mama.Nitatekeleza kama
ulivyoagiza .Lini Khalid
anatarajiwa kuingia nchini?
Akauliza Mathew
“Khalid anatumia hati ya
kusafiria ya Saudi Arabia yenye
jina Nassor Khalid.Kwa taarifa
nilizonazo Khalid ataingia
nchini Tanzania kesho
kutwa.Nitakupa taarifa zote
kuhusiana naye kesho usiku”
“Vipi kuhusu James Kasai
amekwisha ingia Tanzania? Au
anatarajiwa kuingia nchini lini
na kwa njia gani?akauliza
Mathew
“Bado sijajua.Mathew
siwezi kujua kila kitu.Ni jukumu
lako sasa kutafuta James Kasai
ataingiaje nchini Tanzania
lakini nitakapofahamu chochote
nitakujulisha.Nitakutumi vile
vile picha za Khalid Khalid ili
uanze kumfuatilia” akasema
Habiba
“Sawa mama nashukuru
sana kwa taarifa hizi
ulizonipa.Nitaanza kuzifanyia
kazi mara moja” akasema
Mathew akaagana na Habiba
Jawad akaifunika kompyuta
yake
“Mambo yameanza
kupamba moto.IS na James
Kasai wanapanga tena
shambulio lingine.Safari hii
wameliekeza wapi hilo
shambulio? Akajiuliza Mathew.
“James Kasai ni mtu mweye
roho ya jiwe.Pamoja na kujua
kwamba anatafutwa sana na
serikali ya Tanzania kufuatia
shambulio kubwa alilolifanya
siku chache zilizopita lakini
bado anataka kuingia nchini na
kupanga tena shambulio
lingine.Kwa nini anajiamini
kiasi hiki? Akajiuliza
“James hawezi kuingia hapa
nchini kama hakuna watu
wanaomsaidia.Lazima anao
mtandao wake wa watu ambao
wanamuwezesha kuingia nchini
na kutoka atakavyo.Hana wasi
wasi hata kidogo kama anaweza
akakamatwa.Lakini ni nani hao
wanaomuwezesha kuingia
nchini mtu kama
huyu?akajiuliza
“Ameungana na kundi la
kigaidi la IS.Kwa namna yoyote
ile hawa ndio
wanaomuwezesha kuingia hapa
nchini na kutoka bila
wasiwasi.Lazima IS wana
mtandao mrefu sana hapa
nchini na ndiyo maana Habiba
alinitaka nije
niung’oe.Nakumbua wakati ule
hadi waziri mkuu wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania alikuwa
ni mmoja wa watu wao hii
inaonyesha ni namna gani hawa
jamaa walivyodhamiria
kujijenga katika ukanda huu wa
Afrika Mashariki”akawaza
Mathew na kuvuta pumzi ndefu
“Mwisho wa James Kasai
umewadia.Atakapoingia nchini
hatatoka salama” akawaza
Mathew na kuifungia kompyuta
yake katika droo kisha akarejea
chumbani na kumkuta Ruby
akiwa amejilaza kitandani.
“Are you okay
Mathew?akauliza Ruby
“Kuna taarifa nimeipata
kwamba James Kasai anakuja
hapa Dar es salaam”
“James anakuja Dar es
salaam? Ruby naye akashangaa
“Ndiyo anakuja Dar es
salaam”
“He mus be
crazy.Anawezaje kuthubutu
kuja Dar es salaam huku akijua
kwamba anatafutwa kwa nguvu
zote kufuatia shambulio lile
alilolifanya?akauliza Ruby
“Hata mimi nashangaa
anajiamini nini”
“Taarifa hiyo uliyopata
imetoka katika chanzo
kinachoaminika?Ruby akauliza
“Ndiyo ni chanzo cha
kuaminika sana.Si James Kasai
pekee anayekuja Tanzania bali
pia kuna mtu anaitwa Khalid
Sultan Khalid ambaye ni
mtaalamu wa milipuko
mikubwa ndani ya kundi la IS
naye anakuja Tanzania na
anakuja kuonana na James
Kasai hapa Dar es
salaam.Inaonekana kuna
shambulio lingine kubwa
linaandaliwa na hawa jamaa
ndiyo maana wanakuja
kukutana hapa Dar es salaam”
akasema Mathew na
kukumbuka kitu
“Habiba alinituma Dubai
kushuhudia IS wakisaini
makubaliano ya kumtumia
James Kasai kiasi kikubwa cha
fedha ambacho kilitoka kwa
Habiba ndiyo maana Najma
alikuwepo
kumuwakilisha.Sikumbuki jina
la Yule mwanamke mrembo
aliyemuwakilisha James lakini
nakumbuka alitokea
Tanzania.Sura yake bado
haijanitoka kichwani,bado
ninamkumbuka. Fedha ambazo
IS wanampatia James zinapita
Tanzania kwa Yule
mwanamke.Nina uhakika
mkubwa kama James anakuja
Tanzania lazima ataonana naye
hivyo tukimpata Yule
mwanamke tutakuwa
tumempata James Kasai”
akawaza Mathew na kutoa
tabasamu
“Sasa nimepata picha kwa
nini Habiba Jawad alinituma
Dubai nikashuhudie
makubaliano yale kati ya IS na
James Kasai.Yule mwanamama
ana akili sana” akawaza Mathew
na kutoka akaelekea katika ofisi
yake akachukua kalamu na
karatasi Akakaa mezani na
kuanza kuikumbuka sura ya
Yule mwanamke ambaye
alimuwakilisha James Kasai
Dubai huku akiichora katika
karatasi.
“Namshukuru Mungu
aliyenipa pia kipaji kikubwa cha
uchoraji’akawaza Mathew
wakati akiendelea kuichora
sura ya Yule
mwanamke.Alipomaliza
akaitazama picha ile na
kutabasamu.
“Alikuwa hivi hivi” akawaza
Mathew kisha akatoka na
kurejea chumbani
“Ruby kuna kazi ambayo
nahitaji unisaidie” akasema na
kumpa Ruby ile picha
aliyoichora
“Huyu ni nani? Ruby
akauliza
“Ninataka unisaidie
kumfahamu mwanamke huyu ni
nani.Kesho utakapokwenda
SNSA kitu cha kwanza ambacho
ningetaka ukifanye ni kuingia
katika kumbu kumbu zote za
usajili hapa Tanzania na
umtafute mwanamke huyu.Ni
muhimu sana” akasema
Mathew
“Anahusiana na James
Kasai?akauliza Ruby
“Nitakueleza hapo kesho
tutakapokuwa tumepata taarifa
zake ndiyo maana nilimtaka
Rais akukabidhi ofisi kesho
kwani ukiwa ndani ya SNSA una
uwezo wa kupata kila aina ya
taarifa tunayohitaji” akasema
Mathew
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 8: EPISODE 8
Sa kumi na mbli za asubuhi
tayari Mathew alikuwa amefika
katika nyumba ya Rais alikofikia
Ruby akimrejesha baada ya
usiku mzima kuwa naye
nyumbani kwake.Waliagana
kwa miadi ya kuonana tena
baadae kisha moja kwa moja
akaelekea hospitali alikolazwa
Gosu Gosu.Mara tu alipofika
hospitali alikutana na Austin
ambaye alikuwa na sura yeye
tabasamu kubwa
“Austin tabasamu hili la
asubuhi nashindwa kulielewa”
akasema Mathew
“Hali ya Gosu Gosu
imebadilika ghafla usiku wa leo
na kwa sasa ameondolewa
katika ile mashine ya kumsaidia
kupumua.Madaktari wanasema
mifumo yake yote imeanza
kufanya kazi vyema na sasa
anapumua kama kawaida”
“Ahsante Mungu” akasema
Mathew na kugonganisha
mikono na Austin kisha
akaingia katika chumba
alichokuwa amelazwa Gosu
Gosu.Hakuwa amerejewa na
fahamu bado lakini kwa mujibu
wa madaktari hali yake ilikuwa
inaendelea vizuri na
walitegemea haingechukua
muda mrefu kabla hajarejewa
na fahamu zake
“Ahsante sana Papi kwa
hatua hii nzuri.Umezifanya
nyuso zetu zitabasamu asubuhi
ya leo.Naamini muda si mrefu
utafumbua macho.Natamani
sana tuonane uso kwa uso
Papii” akasema Mathew na
kunyamaza kidogo
“Mambo yameanza Gosu
Gosu.Mji unakwenda kuwaka
moto natamani sana
ugekuwepo ndugu yangu lakini
usijali ninakuhitaji sana katika
misheni nyingine
zinazokuja.Endelea
kupambana,nataka
nitakapokuja tena hapa jioni ya
leo nikukute ukiwa tayari
umefumbua macho na
tuzungumze” akasema Mathew
kisha akatoka na kumfuata
Austin
“Mathew nilikuona jana
ukimtamkia Gosu Gosu maneno
Fulani kwa hisia
kubwa.Naamini amekusikia”
akasema Austin
“Tumshukuru Mungu kwa
maendeleo haya mazuri ya Gosu
Gosu” akasema Mathew na
kumtaka Austin waelekee garini
“Ulifanikisha maelekezo
yangu ya jana?akauliza Mathew
“Ndiyo Mathew.Jana
tulipoachana nilikamilisha kila
kitu” akasema na kushuka
katika gari la Mathew akaenda
katika gari lake akachukua
mkoba mdogo na kurejea kwa
Mathew
“Nilifanikiwa kusajili laini
tatu za simu kama ulivyokuwa
umeelekeza” akasema Austin na
kumpatia Mathew simu tatu
“Good.Mimi nitakuwa na
moja,wewe pia utakuwa na
moja na itakayobaki atatumia
Ruby.Mambo yameanza
Austin.Kwa taarifa nilizo nazo
ni kwamba James Kasai
anatarajia kuingia hapa nchini
sijafahamu lini na ataingia vipi ”
akasema Mathew
“James Kasai anakuja Dar es
salaam? Austin naye
akashangaa
“Ndiyo Austin.James Kasai
anakuja Dar es salaam.Anakuja
kuonana na mtu anaitwa Khalid
Sultan Khalid ambaye ni
mtaalamu mkubwa wa milipuko
kutoka katika kundi la IS.Kuna
shambulio lingine wanakuja
kulipanga hapa Dar es salaam”
akasema Mathew
“Nimeshangaa sana kusikia
huyu gaidi ana mpango wa kuja
Tanzania wakati bado vidonda
vya shambulio alilolifanya hivi
majuzi havijapona” akasema
Mathew
“Kwa bahati nzuri
atakapokuja hatarejea tena
Uganda.Utakuwa ndio mwisho
wake na kama ananisikia huko
aliko labda aahirishe safari
lakini kama akija Tanzania
ndipo roho yake itakapoachana
na mwili” akasema Mathew
“Tatizo ni kufahamu ni
namna gani ataingia nchini.Je
atakuja kwa ndege,atapita
kiwanja gani?Hivi sasa video
yake imesambaa kila mahala na
kila mtu anamjua ni gaidi
atapita wapi?Austin akauliza
“James anao mtandao wake
katika nchi hizi za Afrika
Mashariki ndiyo maana mpaka
leo imeshindikana kumkamata
anaweza akaingia katika nchi
yoyote na kutoka vile atakavyo
lakini safari hii kiama chake
kimefika hatatoka
salama”akasema Mathew na
kumtaka Austin akawachukue
wale vijana wawili waliopanga
kuwa nao katika operesheni ile
na kupanga wakutane
nyumbani kwake ambako ndiko
kutakuwa ofisi kuu
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 8: EPISODE 9
Msafara wa Rais wa
jamhuroi ya muungano wa
Tanzania uliwasili katika jengo
la makao makuu ya idara ya siri
ya usalama wa ndani wa
nchi.Hakuwa ametoa taarifa
kama atafika pale hivyo kufika
kwake ulikuwa ni mshangao
kwa kila mtu.Edwin Mbeko
mkuu wa idara ile alitoka mara
moja ofisini kwake na kwenda
kumpokea Rais akamkaribisha
ndani.Rais hakuwa peke yake
alikuwa ameambatana na Ruby
wakaingia ndani na
wafanyakazi wote wakaacha
kazi zao wakasimama mara Rais
alipoingia.Akawasalimu kisha
akaongozana na Edwin hadi
katika ofisi yake
“Karibu sana mheshimiwa
Rais” akasema Edwin
“Nashukuru sana
Edwin.Utanisamehe kwa kuja
bila taarifa”
“Usijali mheshimiwa Rais
hapa ni nyumbani kwako huna
haja ya kubisha hodi” akasema
Edwin
“Edwin sitaki kuchukua
muda mrefu sana.Nimekuja kwa
jambo moja tu la muhimu”
akasema na kumgeukia Ruby
“Huyu mwanamama
niliyeongozana naye anaitwa
Annabel Jones.Nimemteua
kuwa mkurugenzi mpya wa
idara hii kuanzia leo na wewe
utaendelea kuwa msaidizi
wake.Atatumia ofisi iliyokuwa
ya Tamar kwa muda wakati
ofisi yake mpya
ikiandaliwa.Ahsante sana kwa
kukaimu nafasi hii muda mrefu
umefanya kazi nzuri na sasa
nimempata mtu ambaye
atachukua nafasi ya
ukurugenzi.Natagemea utampa
ushirikiano mkubwa” akasema
Dr Fabian na Edwin akajenga
tabasamu
“Karibu sana mama
Annabel.Mimi ni Edwin Mbeko
kama alivyosema mheshimiwa
Rais nimekuwa nikikaimu
nafasi hii ya ukurugenzi kwa
zaidi ya miaka
mitatu.Ninamshukuru sana Rais
kwa kukuteua na ninakuahidi
ushiriano mkubwa kutoka
kwangu na kwa wafanyakazi
wote” akasema Edwin.Baada ya
kumaliza kile kilichompeleka
pale Dr Fabian akaondoka
zake.Baada ya Rais kuondoka
Edwin akawataka wafanyakazi
wote wakusanyike katika
ukumbi mkubwa kisha akaenda
kumtambulisha Ruby kama
mkurugenzi mpya wa idara
ile.Baada ya utambulisho ule
akaenda kumfungulia Ruby ofisi
ambayo ataitumia na Ruby
akaanza rasmi kazi kama
mkurugenzi mkuu wa SNSA.
Wakati Ruby akiwa ofisini
kwake Edwin akatoka na
kwenda sehemu ambako alitoa
simu na kumpigia simu Devotha
“Edwin habari za
Tanzania?akauliza Devotha
“Habari za huku ni njema
lakini kuna jambo limetokea
asubuhi hii nimeona nikujulishe
mara moja”
“Kumetokea nini?akauliza
Devotha
“Mheshimiwa Rais ametoka
hapa muda si mrefu”
“Amekuja kutafuta nini?
“Amemleta mkurugenzi
mpya wa SNSA”
“Mkurugenzi mpya?
“Ndiyo Devotha”
“Kwa nini amekuacha
wewe ambaye umekaimu kwa
muda huu wote na akamteua
mtu mwingine?
“Sifahamu hayo ni maamuzi
yake.Nimekupigia kukujulisha
kwamba kuna baadhi ya
mambo ambayo nitashindwa
kuyatekekeleza kwa kuwa
sintakuwa na nguvu niliyokuwa
nayo awali”
“Usijali kuhusu hilo.Tuko
karibu sana kumaliza misheni
yetu.Umewasiliana na Melanie?
“Ndiyo nimewasiliana naye
na amenitaka nifanye
maandalizi jioni ya leo niende
kumpokea kwani anakuja na
James Kasai.Tayari nimekwisha
fanya maandalizi yote ndege
yetu ndogo iko tayari na baadae
leo nitaelekea Bukoba
kumpokea”akasema Edwin
“Una hakika ujio wa huyo
mkurugenzi mpya hautaathiri
kitu chochote katika mipango
yetu?akauliza Devotha
“Hapana haitaathiri kitu
chochote.Bado ni mgeni na
hafahamu kitu chochote”
“Vizuri.Tunakutegemea
sana Edwin na hakikisha
hakuna kitu kitakachoharibika
hata kama amekuja mkurugenzi
mpya lakini endapo utaona
anakuwa ni kikwazo katika
kufanikisha mambo yetu basi
hakuna haja ya kumchelewesha
tumuondoe mara moja”
akasema Devotha
“Usiwe na hofu Devotha
hakuna kitu kitakachoharibika”
akasema Edwin
“Muda wowote kama kuna
tatizo lolote nijulishe haraka
sana” akasema Devotha na
kuagana na Edwin.
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 8: EPISODE 10
Austin aliwasili katika
makazi ya Mathew akiwa
aeongozana na vijana wawili
Tom Denzel na na Aidan
Kengele.Mathew aliyekuwa
akiwasubiri kwa hamu
akawakaribisha na kuwapeleka
moja kwa moja katika ofisi yake
“Karibuni sana Ton na
Aida.Mimi naitwa Mathew
Mulumbi.Naamini tayari
kiongozi wenu Austin
amekwisha wajulisha mimi ni
nani hivyo naomba tuokoe
muda na tuelekee moja kwa
moja katika suala la msingi”
akasema Mathew kisha akaenda
mezani kulikokuwa na
makaratasi mengi pamoja na
picha akaichukua picha moja
akaenda kuibandika katika
ubao
“Mtu anayeonekana pichani
anaitwa James Kasai.Huyu ana
umri wa miaka arobaini na
nne.Ni mzaliwa wa Kivu
Kaskazini na amepata elimu
yake ya msingi,sekondari hadi
chuo kikuu nchini Congo.Ana
shahada ya sheria kutoka chuo
kikuu cha Kinshasa.Baada ya
kumaliza chuo kikuu alijiunga
na jeshi.Baba yake pia alikuwa
mwanajeshi katika jeshi la
serikali mwenye cheo cha
Jenerali lakini baadae aliasi na
kuanzisha kundi lake ambalo
lilianza kupambana na
serikali.Jenerali Kasai baba yake
James aliuawa na majeshi ya
serikali na ndipo James
alipochukua uongozi wa
kukiongoza kikundi cha waasi
kilichoanzishwa na baba
yake.Baada ya makundi yote ya
waasi kukubali kuweka silaha
chini na kumaliza machafuko
yaliyodumu kwa miaka mingi,ni
James Kasai pekee aliyegoma
kuweka silaha chini hivyo
akatimuliwa kutoka katika
misitu ya Congo na kukimbilia
nchini Uganda ambako
inadaiwa amekuwa akiishi
katika misitu iliyo Kaskazini
mwa Uganda.Hivi majuzi James
Kasai amefanya shambulio hapa
nchini na kuua wake za marais
wa Tanzania,Congo na
Rwanda.Huyu ndiye mtu
ambaye tunamsaka.It’s a
capture or kill mission”
akasema Mathew akawatazama
watu wale waliokuwa
wakimsikiliza kwa makini sana
kisha akaendelea
“James Kasai haishi msituni
kama inavyodaiwa bali anaishi
jijini Kampala.Kwa muda mrefu
amekuwa akifadhiliwa na
serikali ya Uganda na kwa
miaka ya hvi karibuni hali yake
kifedha haikuwa nzuri hivyo
alilazimika kuingia
makubaliano na kundi la kigaidi
la IS ambao wanamfadhili kwa
fedha na zana za kijeshi.Kwa
nini IS wameingia makubaliano
na James Kasai na si mtu
mwingine?akauliza Mathew
“IS wana mpango wa
kujitanua barani Afrika na
wamechagua kujikita katika
eneo la Afrika Mashariki na
kati.Kwa sasa wanataka kupata
sehemu ya kuweka kambi yao
ya mafunzo ya ugaidi na
wamekusudia kuweka kambi
hiyo katika misitu ya Kaskazini
mwa Congo ndiyo maana
wanamuhitaji James
Kasai.Wanamuwezesha kwa
fedha na zana za kijeshi ili
aweze kurejea katika misitu ya
Congo na kudhibiti eneo
hilo.Wataweka kambi yao ya
mafunzo ya kigaidi kati kati ya
misitu ambayo itakuwa
inadhibitiwa na James Kasai na
ambaye ndiye atakayekuwa
akiwalinda hivyo basi James
Kasai ni mtu hatari sana kwa
eneo zima la Afrika
mashariki.Endapo IS
watafanikiwa kujenga kambi
yao ya mafunzo ya kuwandaa
magaidi basi eneo zima la Afrika
Mashariki na kati halitaweza
kukalika litakuwa katika hatari
kubwa ya mashambulio ya
kigaidi hivyo basi kwa namna
yoyote ile lazima James Kasai
akamatwe au auawe”
“Umesema James Kasai
haishi msituni bali anaishi jijini
Kampala,unafahamu anapoishi?
Iwapo tutalazimika kwenda
Kampala Uganda kumfuata
James ni vipi endapo serikali ya
Uganda watagundua kwamba
tunafanya operesheni ndani ya
Uganda hivyo tukawa
tumeanzisha mgogoro?
Akauliza Tom Denzel
“Swali zuri Tom.Hatuna
haja ya kwenda Kampala
kumfuata James kwani anakuja
hapa hapa nchini”
“James anakuja
nchini?akauliza Aidan
“Ndiyo anakuja hapa
nchini.Anakuja kukutana na
huyu mtu” akasema Mathew na
kuchukua picha nyingine
akaibandika ubaoni
“Anaitwa Khalid Sultan
Khalid.Huyu ni mtaalamu wa
milipuko katika kundi la kigaidi
la IS.Kukutana kwao jijini Dar es
salaam ni kiashiria kwamba
kuna shambulio lingine kubwa
wanaliandaa kwani Khalid
hushirikishwa pale
panapotakiwa kufanyika
shambulio kubwa” akasema na
kunyamaza kidogo
“Naamini mtakuwa
mnajiuliza James Kasai
anafahamu kabisa kwamba
anatafutwa kwa shambulio lile
alilolifanya kwa nini haogopi
kuja Tanzania?Jibu ni kwa
sababu tayari anao mtandao
wake hapa Tanzania.Fedha
ambazo James anapewa na
kundi la IS zinapita hapa
Tanzania.Kwa sasa mwenzetu
mmoja anaitwa Ruby ambaye
ameanza kazi leo katika idara
moja nyeti ya serikali
anashughulikia kumtambua
mtu huyo ambaye ndiye IS
wanapitishia kwake pesa
kwenda kwa James Kasai.Pale
atakapokuwa amepata chochote
basi atatujulisha.Tom na Aidan
nimeambiwa na kiongozi wenu
hii itakuwa ni misheni yenu ya
kwanza toka mmemaliza
mafunzo.Naomba niwaweke
wazi wadogo zangu kwamba hii
si misheni rahisi hata kidogo.Ni
misheni ngumu na ya hatari
kwani watu tunaowatafuta ni
hatari pia.Kabla ya misheni
kuanza rasmi ninawataka kama
kuna yeyote anataka
kutoendelea na misheni hii awe
wazi ili tutafute mtu mwingine
wa kushika nafasi
yake.Remember we’re doing
this for our country” akasema
Mathew na vijana wale
wakamuhakikishia kwamba
wako tayari kuendelea na
misheni ile kisha Mathew
akawataka wakaanze kujiandaa
kwani muda wowote wanaweza
wakahitajika.Tom na Aidan
wakaondoka kwa kutumia gari
la Austin.
Dakika chache baada ya
akina Tom kuondoka Mathew
akajulishwa na walinzi kwamba
kuna mgeni wake
getini.Akatazama katika
runinga iliyounganishwa na
Kamera akaliona gari jeusi aina
ya Mercedece benz.Hakujua
nani alikuwa ndani ya gari lile
akaruhusu liingie kisha
akashuka kwenda kumtazama
mgeni Yule ni nani.Gari lile
lilifika hadi karibu na kibaraza
kisha mlango ukafunguliwa
akashuka Ruby.
“Ruby ! akasema Mathew
na kuachia tabasamu.Ruby
akamfuata akamkumbatia
“Karibu sana.Sikutegemea
kama ungekuja mida
hii”akasema Mathew
“Imenilazimu nije kuna kitu
cha muhimu” akasema Ruby
kisha Mathew akamuongoza
wakaelekea ndani
“How’s your first day at
work?Mathew akauliza
“Kikubwa nilichokifanya
baada ya kupewa ofisi ni
kujikita katika misheni
yetu.Masuala mengine yatafuata
baadae.Vipi nyie
mnaendeleaje?Vipi Gosu
Gosu?akauliza Ruby
“Mungu mkubwa kwani hali
yake imebadilika usiku na sasa
mifumo yake yote ya mwili
inafanya kazi vyema amekwisha
ondolewa katika mashine ya
kumsaidia kupumua” akasema
Mathew
“Ahsante
Mungu.Namuombea apone kwa
haraka” akasema Ruby
“Tunamuhitaji sana”
akasema Mathew na kuufungua
mlango wa ofisi ambamo
alikuwemo Austin akasalimiana
na Ruby
“Ruby karibu sana.Muda
mfupi uliopita tulikuwa na
vijana ambao tutashirikiana nao
katika misheni hii nikijaribu
kuwapa picha ya misheni
itakavyokuwa.Vijana
wameelewa na wako tayari kwa
misheni.Kwa upande wako
kuna taarifa gani?akauliza
Mathew
“Nilipokabidhiwa ofisi
nilianza mara moja
kushughulikia ile picha
uliyoichora.Sijafanikiwa
kumpata mwenye ile picha
lakini nimefanikiwa kuipata
picha ya mtu mwingine ambaye
anafanana mno na hii picha
uliyoichora.Mwanzoni niliamini
ni mwenyewe lakini baada ya
kuichunguza hii picha uliyonipa
na hii niliyoipata nimekuta
kuna utofauti.Picha hii ambayo
nimeipata ni ya mwanamke
anaitwa Melanie Chuma
ambaye ni mfanya
biashara.Hana taarifa nyingi na
haionyeshi anaishi wapi wala
biashara gani anayoifanya.Picha
ya Melanie chuma
inamuonyesha akiwa na kidoti
chesi chini ya jicho na ana kovu
katika kidevu chake.Hizo ni
tofauti nilizozipata katika picha
hizi mbili lakini sura ni ile
ile.Mathew kwa kuwa wewe
ndiye unayemfahamu vyema
huyo mwanamke jaribu
kuitazama vyema picha hii ya
Melanie Chuma na uthibitishe
kama kweli ni yeye.Yawezekana
katika mchoro wako ulisahau
kuweka vitu hivyo viwili
nilivyovitaja” akasema Ruby na
kutoa picha katika mkoba wake
akampatia Mathew akaitazama
picha ile halafu akafumba
macho kama vile kuna kitu
anakikumbuka “What’s goig
on here.Sura hii ni ile ile ya Yule
mwanamke niliyemuona kule
Dubai akimuwakilisha James
Kasai lakini kama Ruby yuko
sahihi kuna
utofauti.Ninaikumbuka vyema
sana sura ya yule mwanamke
na hakuwa na kidoti cheusi
kwenye jicho lake wala hakuwa
na kovu kidevuni vitu ambavyo
huyu Melanie Chuma anavyo.Je
wawili hawa ni mapacha?
Akawaza Mathew na kustuliwa
na Ruby
“Mathew ! akaita Ruby
“Najaribu kuvuta kumbu
kumbu zangu kama nilikosea
katika ile picha niliyochora
lakini sikukosea.Mwanamke
Yule niliyemchora hakuwa na
kidoti wala kovu” akasema
Mathew
“Ni vipi kama alifuta kidoti
hicho na hilo kovu kwa kutumia
poda wanazopaka akina mama”
akasema Austin huku
akimtazama Ruby
“Make up” akasema Ruby
“Exctly.Ni vipi kama
atakuwa amefunika alama hizo
kwa make up? Austin
“Kwa nini afanye
hivyo?Kuna sababu yoyote
inayoweza kumfanya afunike
alama hizo kwa make up?Ruby
akauliza
“Hata kama angetumia
make up kufunika hizo alama
alizonazo lazima hili kovu la
kidonda lingeonekana kwani
linaonekana ni kovu kama la
kuungua lakini sikuona kovu
lolote usoni kwake.Ngozi yake
ilikuwa nyororo kama
malaika.Kila kitu unachokiona
katika picha hii ni yeye
isipokuwa alama hizo mbili.It’s
real confusing” akasema
Mathew na kuiweka picha ile
mezani Austin akaichukua
akaitazama na kupatwa na
mshangao mkubwa.
“Nini Austin?Mbona
umestuka?akauliza Mathew
“Huyu ndiye mchumba wa
Gosu Gosu ! akasema
“What?
“Huyu ndiye mchumba wa
Gosu Gosu.Alijitambulisha
kwangu anaitwa Melanie”
akasema Austin
“Austin are you
sure?akauliza Mathew
“Ndiyo.Nimekutana naye
zaidi ya mara moja ni huyu
huyu lakini……” akasema Austin
na kusita kidogo
“Lakini nini Austin?Mathew
akauliza
“Nikijaribu kuvuta picha ya
sura yake hana hili kovu
linaloonekana pichani wala hiki
kidoti chini ya jicho.Lakini naye
alijitambulisha kwangu kwa
jina la Malanie ila hakunitajia
jina la ukoo wake lakini kila kitu
ni hivi hivi”akasema Gosu Gosu
“Austin mtazame vizuri
kama kweli huyu ndiye
mchumba wa Gosu Gosu”
akasema Austin
“Mathew sina shaka hata
kidogo.Nimekutana naye zaidi
ya mara moja hivyo siwezi
kumpotea.Ni mwenyewe kabisa
isipokuwa hizi alama sijawahi
kumuona nazo”akasema Austin
“Huyu Melanie Chuma ni
nani hasa? Je ni ndugu na huyu
mwanamke ambaye niliichora
sura yake? Akauliza Mathew
“Kuna taarifa chache sana
kuhusiana na Melanie Chuma
ambazo nimezipata” akasema
Ruby na kutoa karatasi akampa
Mathew akalisoma kisha
akalitupa mezani
“Taarifa ni chache sana
kama alivyosema Ruby ambazo
haziwezi kuwa na msaada
wowote kwetu.Kwa nini
amekuwa na taarifa chache
namna hii? Akauliza Mathew
lakini hakuna aliyekuwa na
jibu.Baada ya muda Ruby
akauliza
“Mathew huyu mwanamke
uliyemchora sura yake ambaye
anafanana na Melanie Chuma
umekutana naye wapi?
Anaingia vipi katika misheni
hii? akauliza Ruby.Mathew
akainamisha kichwa akafikiri
kidogo na kusema
“Nimewaeleza akina Austin
kwamba James Kasai baada ya
kufurushwa kutoka katika
misitu ya Congo hali yake ya
kifedha si nzuri na alihitaji
kukiimarisha kikosi chake kabla
ya kurejea tena msituni
kupambana hivyo akaingia
makubaliano na kundi la kigaidi
la IS na katika makubaliano
hayo IS walimuahidi kumpa
fedha nyingi pamoja na silaha
za kisasa kuimarisha kikosi
chake.IS wanataka kumtumia
James Kasai kwa ajili ya kupata
sehemu ya kuweka kambi yao
ya mafunzo ya kigaidi katika
misitu ya kaskazini mwa
Congo.Huyu mwanamke
ambaye nimeichora picha yake
na kumtaka Ruby amtafute
tumfahami ni nani na yuko wapi
ndiye alisaini makubaliano ya
fedha kati ya IS na James Kasai
na fedha kutoka kwa IS zinapita
kwake kabla ya kufika kwa
James Kasai.Ninaamini kama
tungeweza kumpata huyu
mwanamke tungepata mambo
mengi kuhusiana na James
Kasai lakini sasa naona mambo
yamejichanganya.Amejitokeza
mwanamke ambaye anafanana
kwa kila kitu na huyu
muwakilishi wa James Kasai
lakini kuna tofauti ndogo”
akasema Mathew
“Mathew kuna kitu
ambacho kinazunguka kichwani
kwangu.Unasema huyu
mwanamke uliyeichora sura
yake ndiye anayepokea fedha
kutoka IS kwa niaba ya James
Kasai? Akauliza Ruby
“Ndiyo” akajibu Mathew
“Kwani umemfahamu vipi
huyo mwanamke? Ruby
akauliza.Mathew akatafakari
kidogo halafu akasema
“ I was there and I
witnessed everything” akasema
Mathew.Austin na Ruby
wakabaki wanamtazama
“I don’t understand
Mathew.You witnessed what?
Akauliza Ruby
“Guys” akasema Mathew na
kuvuta pumzi ndefu
“Hamtaweza kunielewa
kwa sasa.Ukweli ni kwamba
nilikuwepo na nkashuhudia kila
kitu wakati mwanamke huyu
Melanie Chuma akisainiana
makubaliano na wawakilishi
kutoka kundi la IS ya kupokea
fedha kwa niaba ya James
Kasai.Tafadhali naomba
nisiulizwe maswali ilikuaje
nikashuhudia jambo kama hilo”
akasema Mathew
“So you knew about James
Kasai and yet you let him do
what he did? Akauliza Ruby
“Yes I did ! akajibu Mathew
“Why Mathew? That’s not
Mathew Mulumbi we all
know.Mathew Mulumbi katu
hawezi kukubali magaidi
wakafanikiwa mipango yao !
akasema Ruby
“Ndiyo maana nikasema
kwamba hamtaweza
kunielewa” akasema Mathew
“Make us understand !
akasema Ruby
“Let’s not talk about that
okay? Akasema Mathew na
ukimya ukapita
“Mathew mahala tulipofika
tumekwama na wewe unazo
taarifa ambazo zinaweza
kutukwamua.Tafadhali
tushirikishe na sisi pia kile
unachokifahamu ili tusaidiane
mawazo namna ya kuweza
kulikabili jambo hili linalozidi
kuwa gumu” akasema Austin
“I didn’t do anything
because I was
undercover.Please don’t ask me
more okay?akasema Mathew
“Austin unasema kwamba
mchumba wa Gosu Gosu
ambaye alijitambulisha kwako
kwa jina la Melanie hana alama
hizi alizonazo Melanie Chuma?
Mathew akauliza
“Ndiyo hana alama hizi
alizo nazo Melanie
Chuma.Nimekutana naye zaidi
ya mara moja na sijawahi
kumuona na alama hizi japo
sura na kila kitu ni Melanie
Chuma” akasema Austin
“Mwanamke Yule ambaye
nilimuona Dubai akisaini
makubaliano na IS naye
anafanana kwa kila kitu na
Melanie Chuma isipokuwa ni
hizo alama.Kwa hiyo
yawezekana huyo mchumba wa
Gosu Gosu ndiye Yule
mwanamke ambaye
anashirikiana na James Kasai”
akasema Mathew
“Kwa maelezo haya
uliyoyatoa hata mimi naweza
kuamini hivyo” akasema Austin
“Kama ikiwa hivyo je
kupigwa risasi Gosu Gosu kuna
mahusiano yoyote na James
Kasai?Kuna kitu alikigundua
ndiyo maana wakataka
kumuua?Mathew akauliza
“Lakini mwanamke Yule
alionekana kuguswa sana na
kitendo kile cha
GosuGosukutaka kuuawa.Ni
rahisi kumtambua mtu
anayeigiza au anayeumia
kutoka moyoni,Melanie
alionekana kuumia kutoka
moyoni.Anaonekana kumpenda
Gosu Gosu” akasema Austin
“Gosu Gosu alikutana vipi
na huyo mwanamke? Mathew
akauliza
“Kwa maelezo aliyoyatoa
Lucy ambaye anaishi humu
ndani na Gosu Gosu anadai
kwamba Gosu Gosu alikwenda
Ufaransa na aliporejea ndipo
alipoanza kuonekana na huyo
mwanamke.Swali linalokuja ni
kwamba je alikutana nae
Ufaransa?Je walikuwa na
mahusiano kabla ya hapo?
Mwenye majibu ya maswali
haya ni Gosu Gosu ambaye bado
yuko hospitali na hawezi
kutujibu maswali yetu”
akasema Austin ukapita mfupi
ukapita halafu Mathew akatoka
akamuita Lucy mtumishi wa
ndani
“Lucy samahani kwa
kukusumbua.Nilikupa kazi ya
kuchunguza katika chumba cha
Gosu Gosu kutafuta picha ya
mpenzi wake je
umeipata?akauliza Mathew
“Hapana kaka sijafanikiwa
kupata chochote.Hakuna picha
yoyote ya Yule mwanamke
chumbani kwa Gosu Gosu”
“Unaweza ukakumbuka lini
ilikuwa mara ya mwisho kwa
Yule mwanamke kufika hapa
nyumbani?
“Alifika hapa nyumbani
asubuhi ya siku ile ambayo
Gosu Gosu alipigwa risasi.Siku
hiyo Gosu Gosu hakwenda
kabisa kazini walijifungia
chumbani baadae mwanamke
huyo akaondoka.Ilipofika jioni
Gosu Gosu akaondoka lakini
hakuniambia anakwenda wapi
hadi baadae nilipopata taarifa
za kuwa amepigwa risasi”
akasema Lucy
“Ahsante Lucy unaweza
kwenda” akasema Mathew
“Lucy ameweka wazi
kwamba siku ya Gosu Gosu
kushambuliwa mwanamke
huyo alifika hapa asubuhi.Kuna
kamera za ulinzi tupitie kumbu
kumbu tujue gari alilotumia ili
tuanze kulifuatilia” akasema
Mathew na kuanza kupitia
kumbu kumbu za kamera katika
siku ambayo Gosu Gosu
alipigwa risasi.
Gari moja la kifahari lenye
rangi nyekundu lilionekana
likiingia katika geti na Mathew
akasimamisha picha ile ili
waweze kuipata namba ya
gari.Ruby akaiandika namba ile
kisha akaitoa kompyuta yake
katika mkoba na kuanza
kazi.Mathew akahamia katika
kamera iliyo mbele ya
nyumba.Gari lile likaenda hadi
mbele ya nyumba ile na
kusimama kisha mwanamke
mmoja akashuka.Aliinamisha
sura yake chini wakati
akielekea ndani
“Inaonekana alifahamu
kuna kamera hapa ndiyo maana
akainamisha kichwa ili asiweze
kuonekana.She’s very smart !
akasema Mathew
“Ruby kuna chochote
umekipata kuhusiana na hilo
gari?akauliza Mathew na Ruby
akaguna kidogo
“Kuna tatizo hapa.Namba
hii imesajiliwa kwa jina la Stella
kasamaki lakini jina hili halipo
sehemu yoyote.Namaanisha
halijasajiliwa katika taasisi
yoyote ile” akasema Ruby
“Kwa lugha rahisi tunasema
ni jina hewa” akasema Austin
“Exactly ! Ni hewa.Halipo”
akasema Ruby na wote
wakatazamana.Mara simu ya
Austin ikaita akaipokea
akazungumza na aliyempigia na
mara sura yake ikabadilika
“Austin kuna nini?akauliza
Mathew
“Gosu Gosu ! akasema
Austin kwa wasi wasi
“Kafanya nini Gosu
Gosu?akauliza Mathew
“Aliyenipigia simu ni kijana
ambaye nimemuweka pale
hospitali kumlinda Gosu
Gosu.Anasema hali ya Gosu
Gosu imebadilika ghafla na
ameondolewa haraka katika
chumba alimokuwa amelazwa
muda mfupi uliopita na hana
uhakika kama ni mzima”
akasema Austin
“Nini kimetokea
tena?Mbona hali yake tayari
ilikwisha kuwa nzuri?akauliza
Mathew na wote wakatoka
haraka wakaingia katika gari la
Mathew wakaondoka kuelekea
hospitali.Ukimya mkubwa
ulitawala ndani ya gari.
“Listen to me guys”
akasema Mathew
“Chochote kinaweza
kutokea kwa Gosu Gosu hivyo
nawaomba muwe na moyo
mgumu.Kumbukeni tunayo kazi
kubwa mbele yetu tujielekeze
huko.Bado tunaendelea
kumchunguza huyu mwanamke
ambaye anashirikiana na Jame
Kasai.Kabla ya kupata taarifa ya
Gosu Gosu tulikuwa tumepata
watu wawili wanaofanana
karibu kwa kila kitu isipokuwa
alama mbili.Mmoja anaitwa
Melanie Chuma ambaye ana
alama tofauti na mwenzake
ambaye naye jina lake ni
Melanie lakini hana alama kama
za Melanie Chuma.Kiwango cha
kufanana cha watu hawa ni
kikubwa sana hivyo kunifanya
nihisi yawezekana wakawa ni
mapacha lakini huyu Melanie
mchumba wa Gosu Gosu
nashawishika kuamini kwamba
ndiye Yule hasa tunayemtafuta
kwani yeye hana alama hizi
alizonazo Melanie Chuma.Lakini
wapi pa kuanzia
kumtafuta?Hapo ndipo
tumekwama” akasema Mathew
akiwa amekaa kiti cha nyuma
na Ruby huku Austin akiwa
katika usukani
“Mathew kuna kitu
ninajiuliza.Ni vipi kama huyu ni
mtu mmoja?akauliza Ruby
“Una maanisha nini
Ruby?Austin akauliza
“Ninamaanisha ni vipi kama
huyu Melanie mchumba wa
Gosu Gosu na Melanie Chuma ni
mtu mmoja?Kama alivyosema
Mathew kiwango cha kufanana
kwao ni kikubwa sana
isipokuwa tofauti hizo
mbili.Ninawaza yawezekana
akawa ni mtu mmoja ambaye
anatumia majina tofauti ili
kutuchanganya” akasema Ruby
“Hilo linawezekana
kabisa.Hata mimi ninahisi hivyo
yawezekana huyu Melanie
ndiye huyu huyu Melanie
Chuma.Wamefanana karibu kila
kitu na hata majina yao ni
Melanie.Yawezekana kama
alivyosema Ruby akawa ni mtu
mmoja lakini mwenye sura
mbili tofauti”akasema Mathew
“Gosu Gosu angeweza
kuzungumza angeturahisishia
sana kulifumbua fumbo hili”
akasema Austin
“Gosu Gosu is not
here.Tunatakiwa kujitahidi sisi
wenyewe kuhakikisha
tunampata huyu mwanamke”
akasema Mathew na
kunyamaza kidogo
“I have an
idea.Ninaikumbuka tarehe
ambayo Yule mwanamke
aliwekeana saini na IS
makubaliano ya kupokea fedha
kwa niaba ya James Kasai.Ingia
katika kumbu kumbu za
wasafiri waliosafiri kupitia
uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere kati ya tarehe hizi
tuone kama tunaweza kupata
chochote” akasema Mathew na
kumpatia Ruby tarehe ambazo
alitaka achunguze wasafiri
waliosafiri kupitia uwanja wa
ndege wa Julius Nyerere.
“Ninaamini kama alisafiri
kutokea Dar es salaam kwenda
Dubai basi lazima itakuwa ni
katika terehe hizo na lazima
alipita katika uwanja huu”
akasema Mathew na Ruby
akiwa na kompyuta yake
akaanza kufanya kile
alichoelekezwa na Mathew
Austin akiwa katika
usukani alijitajidi kupita njia
ambazo hazikuwa na
msongamano mkubwa wa
magari ili wawahi kufika
hospitali
“Aaaaghhh !! akasema
Austin kwa hasira baada ya
kusimama katika taa za
barabarani
“Relax Austin.”akasema
Mathew
“Tunatakiwa kufika haraka
hospitali kujua kilichomtokea
Gosu Gosu” akasema Austin
“Hatuwezi kubadilisha
chochote hata kama tukiwahi
kufika.Ruby umepata chochote?
“Nisubiri kidogo.Mtandao
unasumbua” akasema Ruby.Taa
zikawaka na safari
ikaendelea.Walipokaribia
kufika hospitali Ruby akasema
“Tayari nimeipata orodha
ya wasafiri waliosafri katika
tarehe hizi kupitia uwanja wa
ndege wa Julius Nyerere
kuelekea nchi
mbalimbali.Nataka niipitie
orodha hii kujua wale
waliosafiri kwenda Dubai”
akasema Ruby
“Good job Ruby.Keep
looking” akasema Mathew
wakati wakivuka geti la
hospitali na kuelekea katika
maegesho.Wote wakashuka na
kukimbia kuelekea katika jengo
la wagonjwa mahututi na
kukutana na Yule jamaa ambaye
Austin alimuweka kumlinda
Gosu Gosu
“Jerry nini
kimetokea?akauliza Austin
“Hata mimi
nashangaa.Mgonjwa alikuwa
anaendelea vizuri kabisa na
tayari alikwisha fumbua
macho.Timu ya madaktari
walifika wakampima na kusema
anaendelea vizuri wakashauri
asisumbuliwe tumuache
aendelee kupumzika ili arejewe
na fahamu kamili.Baada ya
kama nusu saa hivi akaja
daktari mmoja akampima na
kuchoma sindano katika chupa
ya maji aliyotundikiwa halafu
akatoka.Dakika chache baada ya
kutoka nilisikia king’ora kikilia
katika chumba cha mgonjwa
nikaingia ndani hakukuwa na
muuguzi nikakimbia kwenda
kuwatafuta wauguzi wengine
wakaja mbio na madaktari na
kumkuta mgonjwa akitapa tapa
kitandani na mara akatulia
wakasema moyo wake
umesimama.Wakatumia
mashine ya umeme ya kuustua
moyo na mapigo ya moyo
yakarejea halafu wakamuondoa
ndani ya kile chumba na
kumuingiza katika chumba hiki
na mpaka sasa hawajatoka
kunipa majibu yoyote.Nawaona
wakikimbia wakiingia na
kutoka” akasema Jerry
“Ee Mungu tafadhali
msaidie Gosu Gosu” akasema
Ruby kwa masikitiko
“Okay guys let’s not
panic.Hatujui kilichomtokea
mwenzetu na hatujui
kinachoendelea kuhusu hali
yake.Tusubiri madaktari
watakapomaliza kazi yao ya
kuokoa uhai wake watatueleza
nini kimetokea na vile vile tuwe
tayari kupokea taarifa zozote
ziwe nzuri au mbaya kwa
sababu kwa hatua hii chochote
kinaweza kutokea.Tumshukuru
Mungu kwa chochote
kitakachotokea” akasema
Mathew na kugeuka kutazama
watu wakikimbia kuelekea
sehemu Fulani
“Nini kimetokea kule watu
wanakokimbilia?akauliza
Mathew na mara mlango
ukafunguliwa na madaktari
watatu wakatoka wakikimbia
nao wakielekea kule ambako
watu walikuwa wanakimbilia.
“Kuna nini?Mbona wote
wanakimbilia huko?akauliza
Ruby.Wakati wakijiuliza
akatokea muuguzi akitokea
upande ule watu waliokuwa
wakikimbilia Mathew
akamsimamisha na kumuuliza
kumetokea nini kule ambako
watu wanakimbilia
“Kuna mfanyakazi
mwenzetu amejirusha
ghorofani amefariki dunia”
“Nini sababu ya kujirusha?
akauliza
“Hakuna anayejua”
akasema Yule muuguzi
aliyeonekana kuwa na haraka.
“Wakati tunaendelea
kusubiri taarifa ya madaktari
Ruby tuendelee na lile zoezi”
akasema Mathew na Ruby
akaikunjua kompyuta yake
akaendelea na kazi .Baada ya
dakika tano akamuita Mathew
aliyekuwa amesimama mbali
kidogo na Austin
wakizungumza.Wote wakaja
mbio
“Kuna kitu nimekipata”
akasema Ruby
“Nimempata mtu anaitwa
Melanie Davis .Huyu aliondoka
tarehe hii na ndege ya shirika la
ndege la Emirates kuelekea
Dubai”
“Melanie Davis ! Who is she
?Mathew akauliza na Ruby
akaendelea kubofya kompyuta
yake halafu akasema
“Huyu anatumia hati ya
kusafiria ya Ufaransa” akasema
Ruby
“Ni raia wa
Ufaransa?Mathew akauliza
“Ili kulijua hilo natakiwa
kuingia katika mtandao wa
GCHQ na kudukua taarifa za
Ufaransa kumtafuta huyu
Melanie Davis ili kujua kama ni
raia wa Ufaransa”akasema Ruby
“Hilo ni jambo la hatari
sana Ruby.Hawa jamaa
wanaamini tayari umekwisha
fariki katika ajali ya ndege
itakuwa ni hatari kubwa kwako
wakijua kama uko hai bado”
akasema Mathew
“Mathew usemacho ni
kweli.Ninachotaka kufanya ni
kitu cha hatari lakini tunahitaji
sana kupata taarifa za Melanie
Davis hivyo hatuna ujanja
lazima nifanye hivyo”
“Unadhani hakutakuwa na
tatizo kwa upande wako?
Mathew akauliza
“Nitajaribu kutumia njia
ambayo hawataweza
kunigundua” akasema Ruby
“Sawa fanya hivyo”
akasema Mathew na Ruby
akaanza kucheza na kompyuta
yake huku Mathew na Austin
wakishuhudia.Wakati Ruby
akiendelea na zoezi
lile,madaktari wawili wakatoka
akina Mathew
wakawafuata.Wakajitambulisha
kwamba wao ni ndugu za Gosu
Gosu.Daktari mmoja aliyevaa
kitambulisho kilichomuonyesha
anaitwa Dr Masawe akawataka
waelekee sehemu kwa ajili ya
mazungumzo.Ruby akakunja
kompyuta yake akaongoza na
akina Mathew hadi katika
chumba maalum kwa ajili ya
mikutano.Madaktari
wakaongezeka na kufika
wanne.Dr Masawe akasema
“Vijana wangu tumewaiteni
hapa kuwapeni taarifa za
kuhusiana na maendeleo ya
mgonjwa wenu na kile
kilichotokea.Usiku wa kuamkia
leo hali yake ilibadilika na kuwa
nzuri mifumo yake yote ilianza
kufanya kazi vizuri kama
kawaida hivyo tukamuondoa
katika mashine ya kumsaidia
kupumua.Saa tano na dakika
ishirini na moja tulijulishwa
kwamba mgonjwa amefumbua
macho tukaenda kumpima
alikuwa anaendelea vyema
tukatoa maelekezo aendelee
kupumzishwa.Muda mfupi
baadae tukaitwa tena kwamba
hali ya mgonjwa
imebadilika.Tukawahi na
kumkuta akiwa ana hali mbaya
na tukiwa pale moyo wake
ukasimama ikatulazimu
kuustua kwa kutumia mashine
ya umeme na kwa bahati nzuri
ukaanza kufanya kazi
tena.Tukamuondoa na
kumpeleka katika chumba
maalum tukaanza
kumchunguza nini
kimesababisha hali ile na
tumegundua mgonjwa
alichomwa sindano ya sumu
kali” akasema daktari Yule na
akina Mathew wakatazama
“Bado hatujajua ni sumu
gani ,sampuli ya damu iko
maabara hivi sasa
ikichunguzwa kujua ni aina gani
ya sumu alichomwa.Aliyefanya
kitendo hiki ni dhahiri
alidhamiria kumuua kwa
haraka lakini tunashukuru
tuliwahi na tukaokoa maisha
yake”
“Thank you lord ! akasema
Mathew kwa sauti ndogo
“Suala hili tayari
tumelifikisha katika kitengo cha
usalama hapa hospitali
wameanza kulifanyia kazi ili
tujue nani aliyemchoma
mgonjwa sindano yenye
sumu.Tutawajulisheni kila
hatua itakayochukuliwa”
akasema daktari na Mathew
akasimama
“Daktari kwanza kabisa
tunashukuru sana kwa jitihada
kubwa ambazo mmekuwa
mkizifanya kuokoa maisha ya
ndugu yetu.Kuhusiana na tukio
la leo tunaye kijana wetu
ambaye tulimuweka hapa kwa
ajili ya ulinzi wa mgonjwa wetu
ambaye ametueleza kwamba
muda mfupi baada ya timu ya
madaktari kutoka kumpima
mgonjwa na kuelekeza
apumzike, aliingia dakari
mwingine na kuchoma sindano
katika chupa ya maji aliyokuwa
ametundikiwa mgonjwa na
muda mfupi baadae ndipo hali
ile ikajitokeza.Kama mtaruhusu
tunaweza kumuita akaeleza nini
kilitokea” akasema Mathew na
daktari akaruhusu kijana Yule
aitwe.Austin akatoka haraka
akaenda kumchukua Jerry
akamleta katika kile
chumba.Jerry akaeleza
ilivyokuwa na kueleza
muonekano wa daktari
huyo.Ikalazimu mtu
anayeshughulika na masuala ya
wafanyakazi wote wa hospitali
ile aitwe akafika na kompyuta
yake na Jerry akamuelezea
muonekano wa huyo daktari
aliyemchoma GosuGosu
sindano ya sumu
“Kuna wafanyakazi mia nne
na ishirini katika hospitali
hii.Siwezi kuwafahamu wote
labda tujaribu kukaa na kupitia
mfanyakazi mmoja mmoja ili
aweze kumtambua huyo daktari
aliyefanya huo uhalifu” akasema
Yule meneja
“Kuna njia rahisi ya
kuweza kumtambua huyo
daktari” akasema Mathew na
kuomba apewe karatasi na
kalamu akaanza kuchora picha
ya huyo daktari aliyemchoma
sindano Gosu Gosu kwa kufuata
maelezo ya Jerry.Baada ya
dakika kumi picha ikawa tayari
Mathew akamuonyesha Jerry ile
picha
“Mungu wangu ! akasema
Jerry kwa mshangao
mubwa.Hakuamini kile
alichokiona
“Ni huyu huyu ambaye
aliingia na kumchoma sindano
mgonjwa” akasema
Jerry.Mathew akawaonyesha
madaktari wale picha ile
aliyoichora na wote wakabaki
na mshangao mkubwa.
“Dr Sebastian Makebu”
akasema Dr Masawe.
“Huyu ni daktari wetu
anayehusika na dawa za
usingizi.Kijana una uhakika ni
huyu?akauliza DrMasawe
“Ni yeye”akajibu Jerry bila
woga
“Kwa nini Dr Seba akafanya
kitendo kama hiki?akauliza Dr
Masawe na kupiga simu katika
idara ya usalama pale hospitali
na kuagiza Dr Sebastian
Makebu kutafutwa haraka sana
na kukamatwa kama yuko
katika maeneo ya pale hospitali
“Dr Masawe kuna kitu
kingine ninataka kuuliza.Karibu
muda wote huwa hapakosekani
muuguzi katika chumba kile cha
Gosu Gosu.Nini kimetokea leo
hadi daktari huyu akaweza
kuingia na kufanya kile
alichokifanya? Mathew akauliza
“Ni kweli.Mgonjwa wenu ni
mmoja wa wagonjwa
wanaopewa kipaumbele
kikubwa sana hapa hospitali
kwani Rais alipiga simu na
kuagiza kwamba kila juhudi
zifanyike kuhakikisha mgonjwa
huyu anahudumiwa vizuri na
maelekezo yakatolewa
kusikosekane muuguzi katika
chumba chake na ndivyo
inavyokuwa kila siku toka
ameletwa hapa.Hata mimi
nashangaa leo kumetokea nini
kusiwe na muuguzi mle
chumbani hadi akaingia huyu
kijana na kufanya hiki
alichokifanya.Kuna mtu mmoja
ambaye tungeweza kumuuliza
nini kimetokea hadi chumbani
kwa Gosu Gosu kusiwe na
muuguzi lakini kwa bahati
mbaya wakati tukiendelea
kumuhudumia mgonjwa wenu
tukapokea taarifa kwamba
mkuu wa wauguzi hapa
hospitali amejirusha ghorofani
na kufariki dunia.Sijui nini
kinaendelea hapa” akasema Dr
Masawe na simu yake ikaita
akaipokea akazungumza halafu
akawatazama akina
Mathew.Sura yake ilionyesha
wazi kuna kitu hakiko sawa
“Nimetaarifiwa na idaraya
ulinzi kwamba Dr Sebastian
tayari amekwisha toka nje ya
hospitali.Alipita getini na
akasaini kutoka.Nimejulishwa
pia kwamba muuguzi ambaye
alitakiwa kuwepo katika
chumba cha Gosu Gosu
amekutwa sasa hivi akiwa
amefariki chooni.Sifahamu ni
mambo gani yanaendelea hapa
hospitali. Vyombo vya dola
vitatusaidia katika suala hili
lakini ninawahakikishia
kwamba Dr Sebastian
atapatikana tu.Hawezi kukwepa
mkono mrefu wa
dola.Ahsanteni sana kwa
kutusaidia tumeweza kupata
mwanga wa nini kilitokea na
nani amefanya.Tukiliweka
pembeni suala hilo kwa muda
kuna suala lingine muhimu sana
ambalo mnatakiwa mlifahamu”
akasema Dr Masawe.
“Kufuatia sumu kali
aliyochomwa Gosu Gosu kuna
tatizo kubwa limejitokeza.Ini
lake linashindwa kufanya kazi
hivyo basi anahitaji
kupandikizwa ini haraka
iwezekanavyo ama sivyo
atapoteza maisha”
“Jesus ! akasema Ruby
“Najua nimewastua sana
vijana wangu lakini huo ndio
ukweli.Ili kuokoa maisha ya
mwenzenu lazima kumfanyia
upasuaji na kumpandikiza
ini.Bila kufanya hivyo
tutampoteza” akasema Dr
Masawe
“Daktari unadhani Gosu
Gosu ana muda gani wa kuweza
kuishi kuanzia sasa?Mathew
akauliza
“Kwa hali aliyo nayo sasa
ninaweza kusema kwamba ana
saa arobaini na nane kama
asipopandikizwa ini atakufa”
akajibu Dr Masawe.
“Ni muda mfupi sana huo
tutapata wapi ini la
kumpandikiza? Tunaweza
kupata ini hapa
hospitali?akauliza Mathew
“Hapa hospitali ni vigumu
kwani kuna orodha ndefu ya
wagonjwa wanaohitaji
kupandikizwa ini lakini idadi ya
wanaojitokeza kuchangia ini ni
ndogo sana au niseme hakuna
kabisa” akasema Dr Masawe.
“Unatushauri nini
mzee?Mathew akauliza
“Anatakiwa mmoja wenu
ajitolee kumchangia ini
mwenzu.Si lazima awe ni ndugu
wa damu mtu yeyote ambaye
yuko tayari kujitolea ini kwa
ajili ya huyu mwenzenu
atapimwa na akionekana ini
lake linafaa basi kitachukuliwa
kipande na kupandikizwa kwa
mgonjwa.Ni upasuaji ambao
unaweza kuchukua saa tano au
zaidi”
“Endapo ini hilo
likipatikana upasuaji huo
unafanyika hapa hapa hospitali
au nadi nje ya nchi?akauliza
Mathew
“Tunapandikiza hapa hapa
hospitali” akajibu Dr Masawe
“Vijana kujitolea ini kuokoa
maisha si kitu cha hatari kabisa
japo wengi
wanaogopa.Tunachukua
kipande kidogo cha ini safi
tunakipandikiza katika ini la
mgonjwa.Baada ya miezi mitatu
ini litarejea katika hali yake ya
kawaida” akasema Dr
Masawe.Mathew akawaomba
madaktari wale wawape dakika
mbili wakajadiliane
“Guys kwanza kabisa
tunashukuru kwa Gosu Gosu
kuwa hai mpaka sasa.Jaribio la
kumuua limeshindwa lakini
bado yuko kwenye hatari kama
asipopata ini.Sisi ndio ndugu
zake hivyo inabidi kufanya kila
tuwezalo kuokoa maisha
yake.Binafsi ninajitolea
kupimwa na kama nikikutwa
ninaweza kutoa ini basi
nitafanya hivyo kuokoa maisha
ya Gosu Gosu”akasema Mathew
“Hapana Mathew.Wewe
hupaswi kuwa kitandani.Wewe
ni mtu muhimu sana kwa
sasa.Niache mimi nikapimwe na
kama ikionekana ninafaa basi
nitolewe mimi ini ili wewe na
Ruby muendelee na
operesheni” akasema Austin
“Nadhani Austin yuko
sahihi.Mathew hutakiwi kulala
kitandani kwa muda
huu.Kumbuka una siku saba tu
za kuhakikisha unampata James
Kasai “ akasema Ruby
“Sawa Austin.Nalikubali
wazo lako.Wakati vipimo
vikiendelea mimi na Ruby
tutaendelea na operesheni
ambayo kwa sasa inazidi
kutanuka kwani tunatakiwa
kumpata huyo mtu aliyetaka
kumuua Gosu Gosu kwa sumu
ambaye nina uhakika mkubwa
ametumwa afanye hivyo”
akasema Mathew wakarejea
ndani ya kile chumba na
wakawajulisha madaktari
kwamba Austin amejitolea
kutoa ini litakalopandikizwa
kwa Gosu Gosu.
“Dr Masawe nahitaji
kufahamu huyu daktari
Sebastian anaishi wapi?akauliza
Mathew na kuelekezwa kisha
wakaondoka pale hospitali na
kumuacha Austin akijiandaa
kwa ajili ya kupimwa.
“Ruby kuna picha
inaendelea kujitengeneza
kufuatia hiki kilichomtokea
Gosu Gosu.Kuna watu wanataka
auawe.Naamini kuna kitu
anakifahamu ndiyo maana watu
hao hawataki apone na
wakamtumia huyo Dr Sebastian
ili akamchome sindano ya sumu
afe.Kifo cha muuguzi mkuu na
muuguzi aliyekuwa akimuuguza
GosuGosu vinahusiana na hiki
kilichomtokea Gosu
Gosu.Naamini kabisa kwamba
Dr Sebastian alimtumia
muuguzi mkuu kumuondoa
muuguzi katika chumba kile cha
Gosu Gsou ili aweze kupata
nafasi ya kwenda kumchoma
sindano ile ya sumu na wauguzi
wale wawili wameuawa ili
kuharibu uchunguzi” akasema
Mathew akiwa katika usukani
wakielekea nyumbani kwa Dr
Sebastian
“Kwa vyovyote vile lazima
mwanamke huyo ambaye
anadai ni mchumba wa Gosu
Gosu anahusika na hiki
kilichomtokea Gosu Gosu na
ndiyo maana ametoweka na
hajulikani alipo.Umefanikiwa
kupata taarifa za Yule Melanie
Davis?akauliza Mathew
“Nimekwisha sahau kama
nina kazi kubwa ya
kufanya.Nimejielekeza katika
suala la Gosu Gosu” akasema
Ruby na kuikunjua komputa
yake akaanza tena kazi.
“Melanie Davis na Melanie
Chuma ! akawaza Mathew
“Hawa ni watu wawili
tofauti au ni mtu mmoja?
Akajiuliza
“Ngoja tuendelee na
uchunguzi tutaupata ukweli”
akawaza Mathew akiendelea
kukanyaga mafuta
“Mathew unaweza
ukasimamisha gari?Kuna kitu
nataka uone” akasema Ruby na
Mathew akatafuta sehemu nzuri
akasimamisha gari .
“Kuna nini Ruby?akauliza
Mathew
“Nimepata taarifa za
Melanie Davis” akasema Ruby
na kumpa Mathew kompyuta ili
asome
“It’s her ! akasema Mathew
baada ya kuiona picha ya
Melanie Davis
“Huyu ndiye Yule
mwanamke niliyekuwa
ninamzungumzia.Huyu ndiye
ambaye nilimshuhudia Dubai
akisaini makubaliano ya
kupokea fedha kwa niaba ya
James Kasai. Hata ukitazama
sura yake haina kovu lolote ni
kama ile picha niliyoichora”
akasema Mathew
“Taarifa inaonyesha
anaitwa Melanie Davis.Ni raia
wa Ufaransa mwenye asili ya
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo”
“Melanie Davis ana asili ya
Congo ! Mathew akashangaa na
kuendelea kusoma ile taarifa na
kuimaliza
“Taarifa inaonyesha
Melanie Davis ana utajiri
mkubwa aliorithi kutoka kwa
wazazi wake waliofariki katika
ajali.Anatajwa kuwa miongoni
mwa mabilionea wenye umri
mdogo lakini haijaonyesha
anamiliki miradi au biashara
zipi nchini Ufaransa na hata
wazazi wake hawajatajwa kwa
majina ili tujue walikuwa
wanamiliki miradi ipi.Bado
kuna ukakasi kuhusu huyu
Melanie Davis”akasema Mathew
“Ninajiuliza kama anatajwa
kuwa miongoni mwa
mabilionea wakubwa nchini
Ufaransa amekuja kutafuta nini
Tanzania? Akauliza Ruby
“Yawezekana amewekeza
hapa Tanzania na ndiyo maana
IS wanapitisha fedha
kwake.Ninadhani hata vyombo
vya fedha havijaweza kuwa na
mashaka naye kwa vile ni mtu
mwenye utajiri mkubwa.Ruby
tutaendelea baadae
kuwachimba hawa watu wawili
Melanie Davis na Melanie
Chuma.Kwa sasa tuwahi
nyumbani kwa Dr Sebastian”
akasema Mathew na kuingia
barabarani wakaendelea na
safari
“Melanie Davis ambaye
ninaamini ndiye aliyesaini
makubaliano ya fedha na IS na
ndiye tunayeamini ni mchumba
wa Gosu Gosu anatokea
Ufaransa.Gosu Gosu naye
alikwenda Ufaransa na baada ya
kurejea ndipo akaanza
kuonekana na huyo
mwanamke.Ni vipi mahusiano
yao yalianza? Je walikutana
Ufaransa? Nini anakifanya huyu
mwanamke hapa nchini ?
Melanie Chuma amefanana naye
kwa kila kitu je wana undugu au
imetokea tu wakafanana? Au ni
mtu mmoja? Haya yote baadae
kwa sasa ngoja tumsake
kwanza huyu daktari aliyetaka
kumuua Gosu Gosu” akawaza
Mathew
Walifika katika nyumba
anakoishi Dr Sebastian kwa
mujibu wa maelekezo
waliyopewa kule hospitali.Ni
nyumba ambayo ilikuwa na
uzio wa maua na geti la
bati.Mathew na Ruby
wakashuka garini na kuliendea
geti kwa tahadhari
kubwa.Akajaribu kulisukuma
geti halikuwa limefungwa
wakaingia ndani.Taratibu
wakaelekea hadi katika mlango
mkubwa wa kuingilia ndani
ulikuwa umefungwa.Mathew
akazunguka nyuma ya ile
nyuma ambako kulikuwa na
mlango mwingine akajaribu
kuufungua nao ulikuwa
umefungwa.Akatoa vifaa Fulani
vidogo na kuvichomeka katika
kitasa akaufungua mlango
wakaingia ndani wakaanza
kukagua vyumbani.Katika
chumba kikubwa cha kulala
wakakuta vitu vimepanguliwa
hovyo..Kabati la nguo lilikuwa
tupu
“Tumechelewa.He’s
gone.Inaonekana baada ya
kufanya kitendo kile alikuja
hapa na kuchukua vitu
akaondoka haraka.Unaweza
ukajua mara ya mwisho
alizungumza na nani?akauliza
Mathew wakatoka na kurejea
katika gari Ruby akachukua
kompyuta yake na kuziingiza
namba za Dr Sebastian katika
program maalum na baada ya
dakika mbili akasema
“Aliwasiliana na mtu
anaitwa Salome Mtete” akasema
Ruby na kuufungua ujumbe huo
“Unaweza ukafuatilia na
kujua mahala alipo?akauliza
Mathew na Ruby akafungua
program nyingine akamtafuta
huyo mtu aliyewasiliana naye
mara ya mwisho akaweza kujua
mahala alipo.
“Samawati tower” akasema
Mathew kisha akaondoa gari
wakaondoka.
MPENZI MSOMAJI MATHEW
MULUMBI TAYARI AMEANZA
KAZI ILIYOMLETA TANZANIA
USIKOSE SEHEMU IJAYO….
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 9 : EPISODE 1
Baada ya kutoka katika
geti la hospitali ya Mtodora Dr
Sebastian alichukua simu na
kumpigia mpenzi wake Salome
Mtete
“Hallo Darling” akasema
Salome baada ya kupokea
simu
“Salome ninakuja hapo
kazini kwako muda si mrefu
naomba usitoke nisubiri
tafadhali” akasema Dr
Sebastian.
“Sawa nakusubiri mpenzi”
akajibu Salome na Dr
Sebastian akakata simu kisha
akaizima kabisa.
Kutoka hospitali anakofanya
kazi hadi nyumbani kwake
ilimchukua dakika ishirini na
tano.Alipofika nyumbani
kwake akashuka garini huku
akikimbia na kufungua mlango
akaelekea chumbani kwake
akachukua sanduku lake
kubwa akafungua kabati na
kuanza kupakia nguo haraka
haraka halafu akafungua ndoo
za kabati akachukua nyaraka
zake za muhimu.Akaangalia
mle chumbani kama kuna kitu
cha muhimu amekisahau na
aliporidhika kwamba kila kitu
kiko sawa akatoka akafunga
nyumba yake na
kuondoka.Moja kwa moja
akaelekea katika jengo la
kibiashaa lililojulikana kama
Samawati tower anakofanya
kazi mchumba wake
Salome.Alipofika akaegesha
gari na kushuka garini
akatembea haraka haraka
kuelekea katika katika duka la
kuuza vifaa vya electroniki
anakofanya kazi Salome
ambaye alipomuona akatoka
akamfuata.
“Seba kuna nini
leo?Mbona unaonekana una
haraka sana? akauliza Salome
wakati wakishuka ngazi kwa
haraka kuelekea chini
“Nimepata safari ya
dharura ya kikazi ndiyo maana
unaniona nikiwa na haraka
namna hii” akasema Sebastian
“Unasafiri kwenda
wapi?akauliza Salome lakini
Seba hakumjibu akampatia
funguo za nyumba yake
“Funguo hizi za nyumba
yangu utazitunza.Gari pia
ninakuachia utaendelea
kulitumia hadi pale
nitakaporejea” akasema Dr
Sebastian
“Seba mbona hutaki
kunieleza unakwenda
wapi?akauliza Salome
“Nitakupigia simu
nikifika” akasema Sebastian
huku akifungua buti ya gari na
kutoa sanduku lake akaita
taksi halafu akambusu Salome
“Baki salama
Salome.Nakupenda sana”
akasema Dr Sebastian na
kuingia katika taksi akaondoka
akimuacha Salome akiwa
ameduwaa.Hakuwahi
kumuona mchumba wake
akiwa katika hali ile.
“Seba amepatwa na
nini?Mbona ghafla namna
hii?Halafu mbona anaonekana
kuwa na wasiwasi
mwingi?akajiuliza Salome
wakati taksi aliyopanda
mpenzi wake ikitoka katika
geti la kuingilia Samawati
tower.
Dr Sebastin alimuelekeza
dereva wa ile taksi aliyopanda
ampeleke sehemu Fulani na
alipomfikisha mahala hapo
akamlipa fedha akashuka
halafu akaifuata gari moja
nyeusi iliyokuwa imeegeshwa
pembeni ya kibanda cha
kuuzia magazeti akaufungua
mlango na kuingia kisha lile
gari likaondoka.Kulikuwa na
mtu mmoja tu mle garini
ambaye hakumuuliza chochote
Dr Sebastian.Gari lile
alilopanda Seba lilikwenda
hadi katika nyumba
iliyozungushwa ukuta wa rangi
nyeupe na juu kukawekwa
seng’enge.Akapiga honi geti
likafunguliwa wakaingia
ndani.Yule dereva akashuka
akamfungulia mlango Dr
Sebastian na kulishusha
sanduku lake.Toka ndani ya ile
nyumba wakatoka watu watatu
na mmoja wao akiwa ni Edwin
Mbeko mkurugenzi msaidizi
wa SNSA.
“Dr Sebastian karibu
sana.Umefika kwa wakati
muafaka” akasema Edwin
Mbeko huku akiitazama saa
yake
“Ahsante sana Edwin”
akasema Dr Sebastian
“Dr Sebastain naiomba
simu yako” akasema Edwin na
kuichukua simu ya Sebastian
akaikanyaga ikasambaratika
halafu akamtazama
DrSebastian na kusema
“Dr Sebastian taarifa
niliyoipata kutoka kwa watu
wangu ni kwamba yule jamaa
yuko hai” akasema Edwin na
Dr Sebastina akastuka sana
“Yuko hai?akauliza
“Ndiyo yuko hai.Madaktari
wamefanikiwa kuokoa maisha
yake na hii inaashiria kwamba
hukuifanya vyema kazi yako”
“That’s impossible.Sumu
niliyomchoma ni kali sana na
inayoua baada ya muda
mfupi.Niliichoma sumu ile
katika chupa ya maji
aliyokuwa ametundikiwa na
niliamini ndani ya muda mfupi
angepoteza maisha kutokana
na ukali wa sumu ile na………”
akasema Dr Sebastian na
Edwin akamkatisha
“Dr Seba makubaliano
yetu yalikuwa ni kumuua Yule
jamaa Gosu Gosu lakini
hukufanya hivyo na Yule
jamaa ni mzima.Kibaya zaidi
ni kwamba tayari
umefahamika kuwa ni wewe
uliyetaka kumuua na tayari
suala hilo limefika katika
vyombo vya
uchunguzi.Tumeua watu
wawili muuguzi mkuu na
muuguzi aliyepangiwa chumba
cha Gosu Gosu lakini hakuna
manufaa yoyote tuliyoyapata
hivyo basi wewe ni mzigo
ambao hatuwezi kuubeba”
akasema Edwin Mbeko na kwa
kasi ya ajabu akachomoa
bastora iliyofungwa kiwambo
cha kuzuia sauti na kumpiga
Dr Sebastian risasi katika paji
lake la uso akaanguka katika
majani.Hakuwa na uhai tena
“Get rid of the body !
Edwin akawaamuru vijana
wake wawili halafu akaelekea
katika gari lake akaliwasha na
kabla ya kuondoka akampigia
simu Devotha
“Hello Edwin naamini kila
kitu kimekwenda vizuri”
akasema Devotha baada ya
kupokea simu
“Madam Devotha mambo
hayajaenda vyema.Kuna
makosa yamefanyika katika
lile zoezi la kumuua Gosu Gosu
na kwa taarifa niliyoipata ni
kwamba bado yuko hai”
akasema Edwin
“Nini kimetokea Edwin?
Suala lile lilikuwa la muhimu
sana kwani Yule jamaa endapo
akipona anaweza akawaeleza
wenzake mambo anayoyafanya
Melanie hivyo kumuweka
katika hatari kubwa na
Melanie akiingia katika hatari
sisi sote tunakuwa hatarini”
akasema Devotha
“Daktari niliyemtumia
alifanya makosa kidogo na
kusababisha hayo yakatokea
lakini tayari nimekwisha
mshughulikia.Nimemuua ili
kuondoa matatizo kwani suala
hili limekwisha fika katika
vyombo vya dola lakini
nitalimaliza endapo litataka
kuleta shida upande wetu”
akasema Edwin
“Edwin jitahidi sana
kusitokee tena makosa ya aina
yoyote ile.We’re so
close.Tumekaribia sana
kumaliza misheni
yetu”akasema Devotha
“Nitajitahidi madam
Devotha” akasema Edwin
“Vipi kuhusu huyo
mkurugenzi mpya
unamuonaje? Anaweza akawa
kikwazo katika mipango
yeu?akauliza Devotha
“Kama nilivyokwambia
asubuhi kwamba huyu bado ni
mgeni na hajui mambo mengi
hivyo hadi pale atakapoanza
kuielewa idara hii atakuta
tayari tumekwisha kamilisha
kila kitu.Kwa muonekano
wake haonyeshi kama atakuwa
kikwazo chochote kwetu.Kwa
muda huu mfupi toka amefika
nimejitahidi kujenga ukaribu
naye ili niweze kumsoma
vizuri.Hatakuwa na shida
usihofu”akasema Edwin
“Safi sana
edwin.Sikukosea kukuweka
hapo.Umekuwa ni msaada
mkubwa kwangu na
ninakuahidi kwamba
hautajutia hiki
unachokifanya.Matunda yake
ni makubwa sana.Tumebakiza
muda mchache tu na utaanza
kuyaona matunda.Kwa sasa
endelea kufuatilia kwa karibu
sana maendeleo ya Gosu Gosu
na kutafuta namna nyingine ya
kumuua kwani kitendo
alichokifanya huyo daktari leo
cha kushindwa kumuua tayari
kimewasha taa nyekundu na
wataanza kuchukua tahadhari
kubwa wakimlinda” akasema
Devotha
“Usijali madam
ninafuatilia kwa karibu sana
na tutamuondoa Gosu Gosu
kabla hajaleta hatari yoyote
kwetu” akasema Edwin
“Umekwisha wasiliana na
Melanie?akauliza Devotha
“Melanie nimewasiliana
naye asubuhi ya leo na hivi
sasa niko njiani ninaelekea
kupanda helkopta kuelekea
Kagera ambako ninakwenda
kuwapokea.Kila kitu
kinakwenda vizuri.Kwa kuwa
wataingia hapa Tanzania jioni
watalala Kagera na kesho
nitawaleta Dar es salaam”
“Edwin kuwa makini sana
kwani unajua namna James
Kasai anavyotafutwa kwa
nguvu kubwa.Hili ni moja ya
jambo gumu ambalo tumewahi
kulifanya na sikupenda wazo la
Melanie la kutaka James
aingie Tanzania kwani endapo
akigundulika kila kitu
kitakuwa kimekwisha.Serikali
za afrika mashariki
zimewekeza nguvu kubwa
katika kumsaka James”
akasema Devotha
“Nalifahamu hilo madam
Devotha na nimekwisha
jiandaa kikamilifu kuhakikisha
James anaingia hapa nchini na
kutoka bila matatizo
yoyote.Hilo lisikupe hofu
madam” akasema Edwin
“Sawa Edwi naomba
tafadhali unijulishe kila
hatua,kila kinachoendelea.Na
kama kuna tatizo lolote
tafadhali nijulishe haraka
sana”akasema Devotha na
kuagana na Edwin
“Sifahamu kwa nini
Melanie aliamua kuingia
katika mahusiano na Yule
jamaa Gosu Gosu wakati
akifahamu kwamba ni mtu
hatari.Matokeo yake ndiyo
haya tunalazimika kuanza tena
mipango ya kumuua na kama
tusipofanikiwa kumuua Yule
jaama anaweza akawa ni mtu
hatari sana
kwetu.Nitakaporudi toka
Kagera nitakaa na vijana
wangu tuone namna mpya ya
kuweza kumuondoa Gosu
Gosu” akawaza Edwin.
Aliwasili katika jengo la
ofisi zao,akashuka garini na
kuelekea katika ofisi
yake.Akampigia simu rubani
wa helkopta ya idara yao
akamtaka ajiandae kwa safari
ya kuelekea Kagera.Baada ya
dakika ishirini akajulishwa
kwamba helkopta iko tayari
akachukua baadhi ya vitu
vyake vichache muhimu
akatoka bila kuaga mtu na
kuelekea katika helkopta
akaondoka kuelekea Kagera.
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 9 : EPISODE 2
Mathew na Ruby
waliwasili Samawati Tower.Ni
jengo lililokuwa na biashara
nyingi hivyo watu walioingia
na kutoka walikuwa wengi pia.
“Bado yuko hapa hapa”
akasema Ruby aliyekuwa
akimfuatilia Salome kwa
kutumia program maalum
katika kompyuta yake
“Mpigie simu mtake
ashuke tuonane naye”
akasema Mathew na Ruby
akachukua simu akaziandika
namba za Salome akampigia
“Hallow” akasema Salome
baada ya kupokea simu
“Hallow Salome habari
yako” akasema Ruby kana
kwamba ni mtu
anayemfahamu vyema
“Nzuri dada habari yako
nawe”
“Salama kabisa.Samahani
Salome yawezekana
hunifahamu lakini mimi
ninaitwa Dr Prisca ninafanya
kazi na Dr Sebastian ndiye
aliyenipa namba zako za simu”
“Ouh sawa Dr Prisca
nikusaidie nini?akauliza
Salome
“Dr Sebastian amepatwa
na safari ya ghafla leo na
wakati akiondoka mimi
sikuwepo alinipigia simu
akanipa namba zako
niwasiliane nawe kuna vitu
Fulani ninavihitaji na
aliniambia nikuone wewe”
akasema Ruby
“Wewe uko wapi?akauliza
Salome
“Niko hapa chini katika
jengo ulimo.Unaweza
ukashuka tafadhali tukaonana
mara moja?akauliza Ruby
“Sawa ninakuja.Naomba
kama dakika tano tu nitakuwa
hapo chini” akasema Salome
na kukata simu.Wakashuka
garini na kwenda kusimama
karibu na mlango mkubwa wa
kuingilia ndani ya jengo.
“Huyu Salome lazima
atakuwa ni mtu wa karibu na
Dr Sebastian kwani baada ya
kuwasiliana naye akazima
simu kabisa.Tukimfuatilia
huyu anaweza akatusaidia
kujua mahala aliko Dr
Sebastian”akasema Mathew
“Nimeweka program
Fulani katika simu
yangu.Nitakapokuwa karibu
naye program hiyo itaitafuta
simu yake na kujiunganisha
nayo kisha tutaanza
kumfuatilia na kila pale
atakapowasilian na Dr
Sebastian tutafahamu”
akasema Ruby.Baada ya
dakika chache simu ya Ruby
ikaita.Alikuwa ni Salome
“Hallow dada uko
wapi?akauliza Salome.
“Niko hapa nimesimama
karibu na maua haya ya rangi
nyeupe” akasema Ruby
“Sawa nimekuona”
akasema Salome na kukata
simu.Baada ya dakika chache
mwanamke mmoja aliyevaa
suruali ya jeans rangi ya bluu
akajitokeza.
“Habari yako dada”
akasema Salome
“Nzuri Salome.Habari
yako?
“Karibuni sana” akasema
Salome.
“Ahsante.Huyu anaitwa Dr
Cosmas sote kwa pamoja
tunafanya kazi kitengo kimoja
na Dr Sebastian.Alinipigia
simu na kunieleza kwamba
amepatwa na safari ya dharura
akanieleza nije
nikuone.Amepatwa na dharura
gani? Ruby akauliza
“Hata mimi hakuniambia
amepatwa na dharura
gani.Alinipigia simu mchana
huu akaniambia kwamba
anakuja kuniona.Alifika hapa
nikaonana naye akaniambia
kwamba amepata safari ya
dharura ya kikazi akaniachia
gari na funguo ya nyumba yake
akapanda taksi na kuondoka”
“Alikueleza anakwenda
wapi? Akauliza Mathew
“Hapana hakunieleza
anakwenda
wapi.Aliponikabidhi funguo za
gari na za nyumba yake
akaondoka.Nilidhani nyie
wenzake mtakuwa mnajua ni
kazi gani ya dharura
iliyojitokeza”
“Alikuwa amebeba
nini?akauliza Mathew
“Alikuwa na sanduku
kubwa la nguo”
“Ni mara yake ya kwanza
kuondoka ghafla namna hii au
amekwisha wahi fanya hivyo
siku za nyuma?Mathew
akauliza
“Hajawahi kuondoka kama
alivyoondoa leo.Imekuwa
ghafla mno na alionekana
kuwa katika haraka kubwa”
akasema Salome na Mathew
akamtazama Ruby
“Hakuna mzigo mwingine
alikuachia?akauliza Ruby
“Zaidi ya gari na funguo za
nyumba yake hakuna kingine
chochote alichoniachia”akajibu
Salome
“Ahsante Salome.Kama
hakukuachia chochote basi
tutamsubiri hadi atakaporejea”
“Nini mlikuwa mnakihitaji
toka kwake? Yawezekana
amekiacha nyumbani kwake
akasahau kuniambia.Ninaweza
kwenda kuwatazamia
nyumbani kwake” akasema
Salome
“Ni vifaa vya kazi.Usijali
tutawasiliana naye na
kumuuliza mahala
alikoviweka.Ahsante Salome
tunashukuru kwa muda wako”
akasema Ruby wakamuaga
Salome na kuelekea katika gari
lao.
“Do you believe
her?akauliza Ruby
“Ndiyo.Hafahamu
chochote.Alichosema ni cha
kweli.Sebastin tayari
amekwisha toroka na hatujui
amekwenda wapi.Kwa kuwa
suala hili tayari liko katika
mikono ya polisi kama
amekimbilia mikoni lazima
atapatikana.These people are
very smart.Walikwisha jiandaa
kwamba baada tu ya kumuua
Gosu Gosu basi Dr Sebastian
aondoke haraka sana Dar es
salaam” akasema Mathew
huku akiliondoa gari
“Alichokifanya Dr
Sebastian ni kucheza na Yule
muuguzi mkuu ambaye
naamini ndiye aliyemuondoa
Yule muuguzi katika chumba
cha Gosu Gosu ndipo
Sebastian alipopata nafasi ya
kwenda kumchoma ile sindano
ya sumu.Kwa bahati nzuri
alikuwepo kijana wetu pale
hospitali ambaye aliweza
kusaidia sana kufikisha taarifa
kwa madaktari ambao
waliweza kuokoa maisha ya
Gosu Gosu.Huu lazima ni
mtandao mpana ambao unajua
nini wanakifanya”akasema
Mathew
“Ninachojiuliza kwa nini
GosuGosu awe ni hatari kwao
hadi watake kumuua? Hii ni
mara ya pili wanajaribu
kumuua na ninaamini
wataendelea kujaribu tena na
tena”akasema Ruby
“Ni kwa sababu kuna kitu
anakifahamu na wanaogopa
kwamba akipona anaweza
akaweka wazi na wao hawati
kijulikane.Naomba Mungu
amsaidie Gosu Gosu apone
kwani ni mtu anayeweza
kutusaidia sana kufahamu
kinachoendelea na hasa
kuhusu huyu Melanie Davis
ambaye tunaamini ndiye Yule
anayeshirikiana na James
Kasai.Natamani sana
kufahamu wawili hawa namna
walivyokutana na kuanza
mahusiano yao.Nataka kupata
taarifa za kutosha kuhusu
huyu Melanie Davis ambaye
anaendelea kuumiza vichwa
vyetu” akasema Mathew
“Nini kinafuata?Ruby
akauliza
“Tunarejea tena
hospitali.Wenzetu
wanatuhitaji kule” akasema
Mathew
Baada ya muda Ruby
akaita
“Mathew”
“Unasemaje
Ruby?akauliza Mathew
“Natambua ulisema hutaki
kuulizwa kuhusiana na wapi
ulikokuwa na nini hasa
kilikutokea lakini inaniwia
ugumu sana Mathew.Tafadhali
natamani sana kufahamu
kilichokutokea.Unaonekana
umepitia masahibu makubwa”
akasema Ruby na kuinamisha
kichwa kwa sekunde kadhaa
halafu akasema
“Hakuna siku ambayo
sikuwahi kudondosha chozi
kukulilia
Mathew.Ninakupenda Mathew
kiasi ambacho siwezi
kueleza.Nimefurahi
nimekuona tena.Nafsi yangu
imetulia lakini nahisi kuna kitu
kinaukata moyo wangu
taratibu.Natamani sana kujua
kinachoendelea Mathew katika
maisha yako. Sifahamu nini
kitatokea kesho.Utaondoka
tena na kuniacha hapa peke
yangu?” akasema Ruby na
kulengwa machozi.Mathew
akaendelea kuendesha gari
baada ya muda akasema
“Ruby kwa muda huu wote
niliopotea sikuwahi kupitisha
hata usiku mmoja bila kuileta
sura yako kichwani
kwangu.Umekuwa ukiishi
ndani mwangu” akasema
Mathew na kunyamaza kidogo
“Kama unakumbuka
nilikuahidi kwamba baada ya
kurejea kutoka kuwakomboa
mateka mimi na wewe
tungepata nafasi ya kwenda
sehemu tukapumzike.Nilikuwa
namaanisha kile nilichokisema
lakini kwa bahati mbaya
sikuweza kurejea tena
nikapotelea huko huko.Hata
nikiwa huko nilikokuwa bado
umeendelea kuwepo moyoni
na katika akili
yangu.Wanasema ili kujua
thamani ya kitu ni hadi pale
utakapokikosa.Nimekukosa
kwa miaka mitatu na nimeiona
thamani yako kwangu.Sitaki
kukukosa tena Ruby kwani
nakupenda pia.Lakini……...”
akasema Mathew na kutulia
kidogo.Ruby akamkazia macho
kusikia kile alichotaka
kukisema
“Uliniuliza kama
nitaondoka tena na kukuacha
peke yako” akasema Mathew
na kunyamaza baada ya dakika
moja akasema
“Ndiyo nitaondoka baada
ya operesheni hii kumalizika
lakini nitarejea tena kwa ajili
yako.Nafahamu unaumia
ukisikia hivyo lakini ni lazima
nipotee tena na nitakaporudi
itakuwa ni moja kwa moja
sintaondoka
tena.Ninachokuomba pale
nitakapoondoka usilie tena
bali uwe mvumilivu ukiendelea
kuniombea ili nirejee salama”
akasema Mathew na Ruby
akakiegemeza kichwa katika
kiti.
“Mathew neno lako ni
amri kwangu.Chochote
utakachokisema mimi
nitakitii.Nitakusubiri kama
ulivyoahidi kwani naamini
wewe hutembea katika
maneno yako.Ukiahidi kitu
lazima ukitimize.Niko tayari
kukusubiri hata kama
itanigharimu maisha yangu
yote kwa sababu wewe ni
mwanaume pekee uliyejaa
ndani ya moyo
wangu”akasema Ruby huku
macho yake yakilengwa na
machozi.Mathew akamtazama
na kutabasamu
“C’mon cry baby.Please
don’t cry “ akasema Mathew na
Rubyakafuta machozi
“Jambo lingine
nitakapoondoka tafadhali
usijaribu kunitafuta
nimekwenda wapi.Nafahamu
wewe unao uwezo mkubwa wa
kucheza na teknolojia na
unaweza ukataka kufahamu
mahala nilikoenda lakini
nakuomba usifanye
hivyo.Kuwa na imani nami
kwamba nitarejea” akasema
Mathew
“Sintafanya kitu ambacho
umenikataza kukifanya
Mathew”akasema Ruby
“Good” akasema Mathew
na ukimya ukatawala
“Natamani sana nijue kile
kinachoendelea katika maisha
ya Mathew lakini ninashindwa
namna ya kumshawishi
akanieleza.Hakuna
anayefahamu alikuwa
wapi.Ameibuka kutoka kusiko
julikana na hataki kusema
chochote.Ngoja niendelee
kuwa mvumilivu kama
alivyonitaka yawezekana siku
moja akanieleza kile
kinachoendelea katika maisha
yake” akawaza Ruby
“Mungu akinisaidia
operesheni hii ikamalizaka
salama nitarejea tena kwa
Habiba Jawad nikafahamu ni
kitu gani alinitaka nirejee
nikafanye na
nitakapokamilisha lazima
nirejee nyumbani kwa ajili ya
Ruby” akawaza Mathew
Waliwasili hospitali na
kumfuata Austin katika
chumba ambacho alikuwa
amelazwa akiandaliwa kwa
ajili ya kufanyiwa upasuaji ili
kutolewa kipande cha ini cha
kumpandikiza Gosu
Gosu.Mathew akamsimulia
kile walichofanikiwa kukipata
walikoenda kumfuatilia Dr
Sebastian
“Hawa watu lazima
watarejea tena kutaka
kummaliza Gosu Gosu na
hawatakata tamaa mpaka
wahakikishe Gosu Gosu
amekufa” akasema Austin
“Lazima kuna jambo
ambalo Gosu Gosu
analifahamu kuhusu hawa
jamaa na wanaogopa
akifumbua macho anaweza
akalisema ndiyo maana
wanataka kumuua.Ninahisi
anaweza kuwa amegundua
kitu kuhusu Mel……..”
akasema Mathew na
kunyamaza baada wauguzi
watatu kuingia mle ndani na
kuwataka akina Mathew
watoke kwani mgonjwa
alikuwa anapelekwa kufanyiwa
uchunguzi zaidi.Wakaagana
naye na kumuahidi kwamba
wataendelea kuwepo pale
hospitali kufuatilia kila
kinachoendelea.Walikwenda
kukaa nje ya wodi ya wagonjwa
mahututi alimokuwa
amelazwa Gosu Gosu.
“Natamani Gosu Gosu
aamke sasa na aseme hata
maneno mawili tu
kutufumbulia fumbo
hili”akasema Ruby
“Ruby usihofu hatujawahi
kushindwa katika operesheni
yoyote tuliyowahi kuwa
pamoja na hata misheni hii pia
tutaimaliza.Niamini” akasema
Mathew.Waliendelea kukaa
pale nje wakiwa kimya kila
mmoja akiwaza lake.
Wakiwa pale nje mara
akatoka Dr Masawe na
alipomuona Mathew akamuita
“Sikujua kama uko hapa”
akasema Dr Masawe
“Vipi maendeleo ya
mgonjwa wetu?akauliza
Mathew
“Mgonjwa maendeleo yake
siwezi kusema ni mabaya sana
wala mazuri.Ni hamsini kwa
hamsini.Bado tunaendelea
kufuatilia kwa karibu sana
maendeleo yake.Austin
anaendelea kufanyiwa vipimo
ili tuone kama anaweza akafaa
kumpa mgonjwa ini.Naomba
msiwe na wasiwasi tunafanya
kila jitihada kuokoa maisha ya
Gosu Gosu na endapo ikitokea
akapoteza maisha basi ni
mapenzi ya Mungu lakini sisi
kwa upande wetu tunaweka
nguvu kubwa sana katika
kuhakikisha mgonjwa
anapona.Kuhusu suala la Dr
Sebastian tayari liko kwenye
vyombo vya dola
vinalishughulikia na lazima
atapatikana.Alichokifanya ni
kitu kib……..” Dr Masawe
akanyamaza baada ya
mwanamke aliyekuwa akipita
mbele yao kujikuta akiangusha
mkoba aliokuwa ameushika
mkononi kwa mstuko
alioupata.Mathew akageuka
kumtazama mwanamke Yule
naye akastuka
“Kisa ! akasema Mathew
kwa mshangao akimtazama
mwanamke Yule aliyekuwa
amesimama karibu yao huku
akionekana kuwa katika
mstuko mkubwa na mwili
ukimtetemeka
“Mathew ! Ni wewe kweli
au nimekufananisha? Akauliza
Yule mwanamama kwa uoga
“Hujanifananisha Kisa.Ni
mimi Mathew Mulumbi”
akasema Mathew
“No that’s not
true.Mathew is
dead.Samahani” akasema Yule
mwanamama huku akiinama
aokote mkoba wake Mathew
akamshika bega.
“Kisa ni mimi Mathew
Mulumbi.I’m not dead”
akasema Mathew.Taratibu na
woga mkubwa Yule
mwanamama akapiga magoti
akakaa chini na kuanza kulia
“Kisa tafadhali usipige
kelele eneo hili.Inuka
tafadhali” akasema Mathew
lakini bado Kisa aliendelea
kumwaga machozi.Mathew
akatumia nguvu akamuinua na
kumtoa eneo lile akampeleka
katika kiunga kilichokuwa na
majani mazuri
“Kisa tafadhali naomba
unisikilize ! akasema Mathew
“Mathew niambie
tafadhali kama kweli ni wewe”
“Ni mimi usihofu”
“Jamani nini hiki
knaendelea?! Akasema Kisa na
kuinua kichwa akamtazama
Mathew
“Ni mimi Kisa usiwe na
wasi wasi.Inuka tafadhali
twende kule mgahawani
tukazungumze” akasema
Mathew na kumsaidia Kisa
kunyanyuka akashika viatu
mkononi wakaelekea katika
hoteli iliyoko pale hospitali
“Ujio wangu huu unaweza
ukasababisha mtu kufa kwa
mstuko.Karibu watu wote
wanajua kwamba nimefariki
dunia ndiyo maana kila
anayeniona anastuka sana na
wengine wakitaka kukimbia
wakidhani mimi ni mzimu”
akawaza Mathew akitazamana
na Kisa aliyekuwa bado
akimtazama Mathew kwa
woga.
“Kisa naomba uvute pumzi
ndefu tafadhali” akasema
Mathew na Kisa akavuta
pumzi ndefu
“Pole sana Kisa kwa
mstuko ulioupata”
“Naomba unihakikishie
kama kweli ni wewe Mathew”
akasema Kisa
“Kisa ni mimi usiogope.Ni
mimi Mathew Mulumbi
unayemfahamu na si mzimu”
akasema Mathew na Kisa
akamwaga tena machozi.
“Tuliambiwa umefariki
dunia” akasema Kisa
akiendelea kulia.
“Nyamaza Kisa usilie
tena.Mimi sijafa niko hai kama
unavyoniona” akasema
Mathew
“Tumelia sana
Mathew.Tumekulilia mno
jamani kwa nini Mathew?Nini
kilitokea?akauliza Kisa na
kuanza tena kulia
“Kisa imetosha.Usilie
tena” akasema Mathew
“Niache nilie
Mathew.Machozi haya ni
furaha ya kukuona
tena.Sikutegemea kabisa.Bado
naona kama niko njozini”
akasema Kisa
“Hii si njozi Kisa.Ni kitu
cha kweli kabisa.Ni mimi
halisi” akasema Mathew
“Siamini.Haya ni maajabu
makubwa” akasema Kisa
akifuta machozi
“Sijui hata nianzie wapi
Mathew.Nahisi
kuchanganyikiwa”
“Pole sana Kisa.Vipi
maendeleo yako?akauliza
Mathew
“Ninaendelea vizuri
Mathew.Mimi na wote kazini
tunaendelea vyema
kabisa.Nini kilikutokea
Mathew?Ulikuwa wapi?Kwa
nini wakakuzushia umefariki
dunia? Akauliza Kisa
“Kisa naamini una
maswali mengi sana unataka
kuniuliza lakini hapa si mahala
pake.Nitatafuta nafasi
tutakutana tutazungumza
mengi sana kuhusiana na
mimi nini kilinitoea hadi watu
wakanizushia nimekufa”
akasema Mathew
“Ni kweli
Mathew.Nilikuwa nimekuja
hapa kufuatilia maendeleo ya
Gosu Gosu.Toka alipopatwa na
matatizo sikuwa nimekuja
kumtazama.Nilikuwa na vikao
vingi leo lakini kuna kitu
kilikuwa kinanisukuma kuja
hospitali kumbe ninakuja
kukutana na muujiza huu
mkubwa.Naamini hata wewe
pia uko hapa kwa sababu yake”
akasema Kisa
“Ndiyo niko hapa
kufuatilia hali ya Gosu
Gosu.Alikuwa anaendelea
vizuri na aliweza kufumbua
macho lakini kuna mtu alifika
na kumchoma sindano ya
sumu kwa lengo la
kumuua.Madaktari
wamejitahidi sana kuokoa
maisha yake na kwa sasa
kinachoendelea anahitajika
kupandikizwa ini ambalo
limeharibika kutokana na
sumu hiyo kali”
“Mungu wangu !! akasema
Kisa
“Ndiyo hali inayoendelea
sasa” akasema Mathew
“Mungu amsaidie aweze
kupona” akasema Kisa akiwa
ameiweka mikono kifuani
“Kwa hali aliyonayo
tunahitaji kumuombea sana
kwani lolote linaweza kutokea
lakini Mungu wetu ni mwema
atamsaidia” akasema Mathew
“Gosu Gosu jamani nani
lakini wanaotaka kumuua?Ni
mtu mzuri sana hana tatizo na
mtu.Hajawahi kugombana na
mtu yeyote.Kazini kila mtu
anampenda.Toka ilipokuja
taarifa umefariki yeye ndiye
ambaye amekuwa akisimamia
biashara zote na hakuna
aliyetegemea kama angeweza
kusimamia kwa ufanisi namna
ile lakini amefanya maajabu
kila mtu akabaki
anashangaa.Makampuni yako
yote yamefanya vizuri na
kuendelea kustawi hadi
tulipostuliwa na taarifa
kwamba
yameuzwa.Tulistushwa sana
na maamuzi yale ya kuamua
kuuza mali zako” akasema Kisa
“Nani ameuziwa
makampuni yangu?akauliza
Mathew na Kisa akaonekana
kushangaa
“Ina maana hufahamu
nani aliyenunua makampuni
yako?
“Hapana sifahamu
chochote”
“Mathew ni kweli
hufahamu chochote kuhusiana
na suala hili?akauliza Kisa
“Suala hili nimelikuta hapa
hapa Dar es salaam.Sifahamu
chochote” akasema
“Haya mbona maajabu !
akasema Kisa
“Tumetambulishwa
mwanamke mmoja bilionea
anaitwa Melanie Davis kuwa
ndiye mmiliki mpya wa
makampuni yako.Lakini kuna
kampuni kama mbili hivi
ambazo ziko bado chini ya
Gosu Gosu” akasema Kisa
Mathew alistuka baada ya
kusikia jina Melanie Davis
likitajwa
“Umesema Melanie Davis?
“Ndiyo unamfahamu?
“Hapana
simfahamu.Ametokea wapi?Ni
mtanzania?Mathew akauliza
“Hakuna anayemfahamu
vizuri huyo mmiliki mpya
lakini inasemwa kwamba ni
raia wa Ufaransa ila
anazungumza kiswahili vizuri
kabisa.Kwa ujumla kama
nilivyosema bado
hatumfahamu
vizuri.Hajajiweka wazi kwetu
tumfahamu.Ni Gosu Gosu
pekee ambaye yuko naye
karibu sana na ndiye
anayemfahamu vyema kwani
alisafiri kwenda Ufaransa na
aliporejea alikuja na huyo
mwanamke akatutangazia
kwamba ndiye mmiliki mpya”
akasema Kisa
“Dah ! akasema Mathew
“Mpaka leo hatufahamu
hata ofisi yake iko wapi kwani
kila kitu ameendelea
kushughulikia Gosu Gosu
kama ilivyokuwa awali”
akasema Kisa
“Unafahamu anakoishi
huyo Melanie Davis?akauliza
Mathew
“Hakuna anayejua.Kuna
mambo yanafumbwa fumbwa
sana hapa na ambaye
anafahamu kila kitu ni Gosu
Gosu pekee.Yeye ndiye
anayeweza kuwa na majibu
yote kuhusiana na huyo
Melanie Davis”
“Basi usijali Kisa ninyi
endeleeni na kazi kama
kawaida nitalifuatilia suala hili
kwa undani zaidi kujua nini
hasa kilitokea hadi
yakafanyika maamuzi haya ya
kuuza kampuni
zangu.Tuachane na hayo
wengine wote hawajambo?
“Wote wazima lakini
tumempoteza mzee Msimbo
na Julitha walipata ajali ya gari
mwaka jana”
“Poleni sana”
“Sipati picha wafanyakazi
watakapopata taarifa za kuwa
uko hai.Itakuwa ni mshangao
mkubwa sana lakini kila
mmoja atashangilia.Mathew
tulilia sana tulipopata taarifa
za kifo chako kwa sababu
wewe umetufanya tuishi kama
familia moja.Umemfanya kila
mtu afanye kazi kwa bidii na
kujituma.Umetufanyia mambo
mengi makubwa ambayo
siwezi kuyaeleza ndiyo maana
nasema kwamba taarifa za
kuwa upo hai zikiwafikia
itakuwa ni shangwe kubwa
sana na wengi hawataamini na
wengine wanaweza
wakapoteza hata fahamu kwa
mstuko” akasema Kisa
“Kisa kuna kitu kimoja
ambacho nataka tukubaliane”
“Kitu gani Mathew?
“Sitaki upeleke taarifa hizi
wamba niko hai.Muda
utakapofika mimi mwenyewe
nitakuja kuwatembelea lakini
kwa sasa sitaki mtu mwingine
yeyote afahamu labda kama
ikitokea tukakutana kama
tulivyokutana mimi nawe”
“Kwa nini Mathew hutaki
wajue kuwa uko hai?
“Nina sababu
zangu.Naomba unisaidie kwa
hilo”
“Lakini wanakuja sana
hapa hospitali kumjulia hali
Gosu Gosu ipo hatari
wakakukuta hapa”
“Ikitokea hivyo sawa lakini
usiwaeleze
chochote.Umenielewa Kisa?
“Nimekuelewa Mathew”
“Ahsante sana” akasema
Mathew
“By the way unamfahamu
mchumba wa Gosu Gosu?
Akauliza Mathew
“Mchumba wa Gosu Gosu?
Kisa akashangaa kidogo
“Ndiyo”
“Hapana simfahamu.Gosu
Gosu ana mchumba?Anataka
kuoa?akauliza Kisa
“Ndiyo.Nimeambiwa ana
mchumba lakini sijamuona
akifika hapa hospitali kujua
maendeleo ya mchumba wake”
akasema Mathew
“Huyo atakuwa si
mchumba lazima atakuwa ni
mwanamke wa kupotezea
wakati.Kama angekuwa kweli
ni mchumba wake angekesha
hapa hospitali akifuatilia
maendeleo ya mchumba
wake.Huyo lengo lake lilikuwa
ni kumchuna pesa na alipoona
Gosu Gosu amepata matatizo
haya akaamini hawezi kupona
akatokomea zake” akasema
Kisa
Waliendelea na
mazungumzo kidogo halafu
Mathew akasema
“Kisa imekuwa vizuri
nimekutana nawe
umenijulisha mambo mengi
ambayo sikuwa
nikiyafahamu.Kwa kuwa
tumekutana mahala hapa
kwenye matatizo nakuahidi
kutafuta tena nafasi nyingine
nzuri tukae tuzungumze.Kuna
mengi nataka kuyafahamu
kutoka kwako”
“Mathew hata mimi
nimefurahi mno kwa kuiona
sura yako tena.Naamini leo
sintapata usingizi nikiwaza juu
ya jambo hili” akasema Kisa na
Mathew akasimama
“Natakiwa kwenda
kufuatilia kwa karibu
kinachoendelea kuhusu zoezi
la kumpandikiza Gosu Gosu
ini.Endapo mtu aliyejitolea
kumpa ini Gosu Gosu vipimo
vitaonyesha kwamba
hawaendani basi tutakuja
kuomba msaada kwa
wafanyakazi kwani Gosu Gosu
ana saa 48 tu kwa mujibu wa
daktari kama asipopandikizwa
ini katika muda huo atakufa”
“Mathew endapo itatokea
hivyo nijulishe haraka sana na
mimi nitazungumza na
wafanyakazi.Nitawashawishi
wajitokeze kuokoa maisha ya
Gosu Gosu.Namba yako ya
simu ni ile ile?akauliza Kisa na
Mathew akacheka kidogo
“Sikuwepo kwa miaka
mitatu nimekuta kuna
mabadiliko mengi yametokea
hivyo nitahitaji kupata laini
mpya ya simu.Nipatie namba
zako tafadhali” akasema
Mathew na Kisa akampatia
kadi yake ya biashara kisha
wakaondoka kurejea kule
wodini ambako walimkuta
Ruby
“Ruby huyu anaitwa Kisa
Mwakalukwa ni mhasibu
mkuu wa yaliyokuwa
makampuni yangu,amefika
hapa kujua maendeleo ya Gosu
Gosu na kwa bahati nzuri
tukakutana.Kisa huyu ni rafiki
yangu anaitwa Ruby” Mathew
akafanya utambulisho Ruby na
Kisa wakasalimiana
wakazungumza kidogo kisha
Mathew akamtaka Kisa
akaendelee na shughuli zake
na endapo kutatokea kitu
chochote atamjulisha.Kisa
akaaga na kuondoka.
“Ruby tutafute sehemu
tukakae kuna watu wanakuja
kumtazama Gosu Gosu ambao
wanaweza kunikuta hapa na
yakatokea kama yale ya Kisa”
akasema Mathew
“Mathew hili suala la wewe
kuonekana hai linawastua
watu wengi ndiyo maana kila
anayekuona anastuka
mno.Wewe ni mtu mwenye
roho nzuri kwa watu ndiyo
maana wengi walikulilia
walipopata taarifa za kifo
chako na wanapokuja kukuona
ukiwa hai wengi wanaamini
labda wewe si Mathew halisi ni
mzuka” akasema Ruby
“Wewe unaamini
nini?Mimi ni halisi au
mzuka?akauliza Mathew
“Mzuka hauwezi kuwa na
nguvu kitandani kiasi
kile”Akasema Ruby na wote
wakacheka.
Mathew alimtaka Jerry
awajulishe kila kitakachokuwa
kinaendelea wakaenda kukaa
mbali kidogo na wodi ile ya
wagonjwa mahututi
“Kuna jambo lingine
nimelipata kutoka kwa Kisa”
akasema Mathew
“Ni kweli mali zangu
zimeuzwa na mtu aliyenunua
mali hizo ni bilionea Melanie
Davis”akasema Mathew
“Melanie Davis
again?akauliza Ruby kwa
mshangao
“Ndiyo”
“Mhh ! hili jambo mbona
linazidi kujichanganya !
akasema Ruby
“Nilistuka sana aliponitajia
jina hilo lakini sikutaka
agundue chochote”akasema
Mathew na ukimya ukapita
“Kwa mujibu wa Kisa”
Mathew akaendelea
“Gosu Gosu alisafiri
kwenda Ufaransa na aliporejea
ndipo alipowatangazia
wafanyakazi wote kwamba
makampuni yameuzwa na
akamtambulisha mmiliki
mpya ambaye ni Melanie
Davis.Kisa anadai kwamba
mpaka sasa hakuna
anayemfahamu kiundani
Melanie.Hakuna anayejua
ametokea wapi anaishi wapi ni
Gosu Gosu pekee.Nadhani hiki
kilichomtokea Gosu Gosu
kutaka kuuawa kina
mahusiano na Melanie
Davis.Kuna mambo ambayo
nadhani Gosu Gosu
ameyafahamu kuhusu yeye na
ndiyo maana anatakiwa
auawe” akasema Mathew na
kushika kichwa akawaza
kidogo halafu akasema
“Kama Gosu Gosu
alikwenda Ufaransa na
aliporejea ndipo alipoanza
kuonekana akiwa na Melanie
Davis basi mambo yote ya
mauziano yalifanyika huko
kwa Peniela na ndiyo maana
alimuita Gosu Gosu kwani
ndiye aliyekuwa akifahamu
biashara zangu nyingi.Naamini
Peniela atakuwa akimfahamu
vyema huyu Melanie Davis.Oh
God ! I didn’t want this to
happen.Sikutaka Peniela ajue
kama niko hai ! akasema
Mathew na kushika kichwa
“You want to call
her?Ruby akauliza
“Gosu Gosu ambaye
anaweza kutupa taarifa za
Melanie hali yake ndiyo
hii.Hawezi kutusaidia
chochote kwa sasa.Peniela
pekee ndiye anayeweza kutupa
taarifa za kumuhusu Melanie
Davis kwani ndiye aliyenunua
makampuni yangu.Hakuna
namna lazima nimpigie simu
Peniela nizungumze naye
kuhusu suala hili na
nimuombe anieleze kwa
undani kuhusu Melanie
Davis.Lazima atakuwa na
taarifa zake za kutosha”
akasema Mathew akafikiri
kidogo kisha akasema
“Twende tuondoke hapa”
“Tunaelekea wapi?
“Nyumbani”
akajibuMathew kisha
wakaenda kumuaga Jerry
wakaondoka
“Tunakwenda kufanya nini
nyumbani?Ruby akauliza
“Kuna jambo nataka
tukalifanye” akajibu Mathew
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 9 : EPISODE 3
Walifika nyumbani kwa
Mathew ambaye moja kwa
moja akaelekea chumbani kwa
GosuGosu akaanza kupekua
katika kabati na kuipata hati
ya kusafiria ya Gosu Gosu
akaichukua wakaelekea ofisini
“Nataka kujua tarehe
ambayo Gosu Gosu alirejea
kutoka Paris Ufaransa kisha
tujue kama Melanie Davis naye
aliingia nchini siku hiyo hiyo”
akasema Mathew na kumpa
Ruby tarehe ambayo Gosu
Gosu alirejea nchini akitokea
Paris Ufaransa na Ruby
akaanza kuifanyia kazi.Baada
ya dakika kadhaa akasema
“Gosu Gosu alirejea nchini
siku hiyo akitumia ndege ya
shirika la ndege la Ufaransa
ikipitia Nairobi Kenya.Melanie
Davis pia alikuwemo katika
ndege hiyo naye akitokea
Ufaransa”
“Kama wote waliingia
nchini siku moja na walikuwa
katika ndege moja ina
maanisha kwamba walikutana
nchini Ufaransa hivyo basi
mtu ambaye anaweza
akatusaidia kumfahamu
Melanie ni Peniela” akasema
Mathew na kuinamisha kichwa
akavuta pumzi ndefu
“Hakuna ujanja lazima
nimtafute Peniela” akasema
Mathew na kuchukua kitabu
ambacho aliandika namba za
simu za watu wengi akaitafuta
namba ya Peniela
“Sina hakika kama
atakuwa bado anatumia
namba hii ya simu ngoja
nijaribishe” akasema Mathew
na kuziandika namba zile
katika simu yake akapiga simu
ikaanza kuita
“Simu inaita”
akamwambia Ruby.Baada ya
muda ikapokelewa
“Hallow hapa ni nyumbani
kwa Peniela,nikusaidie nini
tafadhali?ikauliza sauti ya
mwanamke
“Ninaomba kuzungumza
na Peniela tafadhali”
“Nimwambie nani anapiga
simu?
“Mwambie kuna taarifa
muhimu kutoka Tanzania”
akasema Mathew
“Sawa naomba usubiri
kidogo” akasema Yule
mwanamama na Mathew
akaendelea kusubiri.Baada ya
dakika chache akasikia sauti
ambayo ilimfanya asite
kuitikia
“Hallow! Ikasema sauti
ambayo aliitambua ilikuwa ya
Peniela
“Hallow habari yako.Nani
mwenzangu?akauliza Peniela
“Hallo Penny ! akasema
Mathew na ukimya ukatanda
“Penny ! akaita Mathew
“Wewe ni nani?akauliza
Peniela
“Umeshindwa kuitambua
sauti hii? Mathew akauliza
“Niambie tafadhali wewe
ni nani ama sivyo nitakata
simu .Sipendi kuchezewa !
akasema Peniela kwa ukali
“Ni mimi Mathew
Mulumbi” akasema Mathew na
simu ikakatwa
“Amekata simu ! akasema
Mathew
“Haamini kama kweli ni
wewe ndiyo maana amekata
simu.Mpigie tena” akasema
Ruby na Mathew akapiga tena
lakini simu haikupokelea.
“Ngoja nijaribu kutumia
mtandao wa skype akiniona
ataamini” akasema Mathew na
kuchukua kompyuta yake
akampigia Peniela kwa
kutumia mtandao wa
Skype.Simu ikaita na
kupokelewa.Macho ya Peniela
yalijaa machozi
“Tafadhali wewe
unayetumia sura ya Mathew
shindwa ! akasema kwa ukali
Peniela
“Peniela tafadhali naomba
unisikilize ! akasema Mathew
“Nimekwambia shindwa !
Rudi huko huko kaburini
ulikotoka.Muache Mathew
apumzike kwa amani !
akasema Peniela
“Peniela mimi si mzimu
wala mchawi.Mimi ni Mathew
Mulumbi mume wako !
“Mume wangu amekwisha
fariki miaka mitatu
iliyopita.Tafadhali naomba
uniondokee mchawi mkubwa
wewe unayediriki kuvaa sura
za watu” akasema Peniela
“Peniela naomba
unisikilize.Nipe dakika chache
tu kuna kitu ninataka
kuzungumza nawe” akasema
Mathew lakini Peniela
hakujibu kitu aliendelea kulia
“Peniela kwanza nataka
ufahamu mimi sijafa.Mimi ni
mzima japo iliaminika
kwamba nimefariki dunia.Si
wewe tu uliyeamini hivyo bali
kila mtu alijua kwamba
nimekufa.Mimi ni mzima
kabisa na ni Mathew Yule yule
mume wako unayemfahamu”
akasema Mathew
“Nitazame vizuri Penny ni
mimi Yule Yule nimerudi”
akasema Mathew
“Haya mbona mauza uza !
akasema Peniela
“Si mauza uza Penny ni
kweli nimerejea”
“Ee Mungu naomba unipe
nguvu.Hili jambo limenizidi
uwezo wa kulibeba” akasema
Peniela na kuinamisha kichwa
“Peniela najua nimekustua
sana lakini naom…….”
Akasema Mathew na Peniela
akamkatisha
“Whoever you are please I
can’t talk right now ! akasema
Peniela na kukata simu
“Amekata simu.Ndiyo
maana sikutaka kuzungumza
naye.Nilijua angepatwa na
mstuko mkubwa sana”
akasema Mathew
“Mpigie tena simu.Suala
hili ni muhimu zaidi kuliko
mstuko wake.Akipokea nenda
moja kwa moja kumuuliza
kuhusu suala hili la Melanie
ambalo ndilo limekusababisha
ukampigia simu masuala ya
kifamilia huu si wakati wake”
akasema Ruby na Mathew
akapiga tena simu ikapokelewa
“Wewe ndugu
nimekwishakwambia niache
usinisumbue.Unan……….”
“Peniela kuna kitu nataka
kujua.Nimekuta mali zangu
nyingi hapa Dar es salaam
zimeuzwa ninataka kujua je ni
wewe uliyefanya jambo hili? Ni
wewe uliyeuza? akauliza
Mathew na Peniela
akaonekana kustuka.
“Mali ?akauliza
“Ndiyo.Naamini sasa
umekwisha anza kuamini
kwamba mimi si mzimu bali ni
Mathew halisi.Nimekuta mali
zangu nyingi zimeuzwa lakini
sifahamu nani ameuza na kwa
nini.Sina wa kumuuliza kwani
Gosu Gosu amepigwa risasi
yuko hospitali ndiyo maana
nikaona nikupigie nikuulize
jambo hili”
“Oh mon Dieu” akasema
Peniela kwa lugha ya kifaransa
akimaanisha oh Mungu wangu
kisha akafunika uso kwa
kiganja chake cha mkono
“Peniela tafadhali nahitaji
sana kujua kuhusu jambo hili !
“Hivi ni wewe kweli
Mathew?akauliza Peniela
“Ni mimi Peniela usihofu”
akajibu Mathew
“Ni ngumu kuamini”
“Peniela tutazungumza
mengi hapo baadae lakini
naomba kwanza unipe jibu
kuhusiana na hicho
nilichokuuliza” akasema
Mathew na Peniela hakumjibu
kitu akakata simu.
“Amekata simu” akasema
Mathew
“Tumekwama”
“Kuna kitu kimoja
ambacho nalazimika
kukifanya”
“Kitu gani?
“Natakiwa kwenda Paris
Ufaransa”
“Paris?! Ruby akashangaa
“Ndiyo.Natakiwa kwenda
Paris Ufaransa haraka sana
kuonana na Peniela.Amepatwa
na mstuko mkubwa na kama
nisipomuwahi anaweza
akaharibu mambo kwa
kuzungumza na Melanie
kwamba niko hai na ninaulizia
mali zangu”
“Mathew kwa wakati huu
haitakuwa rahisi kwani kuna
mambo mazito
yanayoendelea.Khalid Khalid
na James Kasai wanawasili
nchini na tunakutegemea sana
wewe katika zoezi
hili.Ninakushauri usiende
Paris bali mpigie simu tena
Peniela na umtake aje
Tanzania mzungumze na
atakueleza kila kitu” akasema
Ruby na Mathew akafikiri
kisogo na kusema
“Ushauri mzuri sana”
akasema Mathew na kumpigia
tena simu Peniela.
“Jamani ninakuomba
kakaangu usinisumbue tena
kwa kunipigia simu”
“Peniela naomba
unisikilize.Nakuhitaji uje
Tanzania nizungumze
nawe.Ningeweza kuja Paris
lakini sitaki kuleta mstuko kwa
watoto.Nakuomba tafadhali
uje Tanzania kama utaweza
siku ya kesho nataka sana
kuzungumza nawe.One more
thing usimweleze mtu yeyote
kuhusu mimi hasa
watoto.Tafadhali Peniela
nakuomba sana uje Tanzania
kesho” akasema Mathew na
kukata simu
“Amesemaje?Ruby
akauliza
“Sikutaka kumpa nafasi ya
kujibu chochote.Ninamfahamu
Peniela naamini
atakuja”akasema Mathew na
ukimya mfupi ukapita
“Ruby tupumzike kidogo
kabla ya baadae kurejea tena
hospitali kujua kile
kinachoendelea huo” akasema
Mathew
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 9 : EPISODE 4
Saa tano za usiku geti la
nyumba moja iliyozungukwa
na migomba mingi
likafunguliwa na gari mbili
zikaingia ndani ya jumba
lile.Lango la gereji
likafunguliwa gari moja
ikapitiliza hadi ndani ya gereji
“Tumefika mahala
tutakapopumzika kwa usiku
wa leo kabla ya kueleka Dar es
salaam hapo kesho” akasema
Edwin Mbeko huku akifungua
mkanda na kushuka
akwafungulia wageni wake
milango wakashuka.Kwa
kutumia mlango mdogo
uliokuwemo ndani ya gereji
wakaingia ndani ya ile nyumba
wakaenda sebuileni.
“Karibu sana” akasema
Edwin
“Edwin tunashukuru sana
kwa kazi kubwa uliyoifanya”
akasema mmoja wa wale
wageni wawili
“Usijali madam
Melanie.Ni jukumu langu
kuhakikisha unakuwa salama
muda wote” akasema Edwin
na kwenda kuleta chupa
kadhaa za mvinyo akaziweka
mezani akawakaribisha akina
Melanie waendelee kunywa
Edwin Mbeko alikuwa
ametoka kuwapokea Melanie
na James Kasai na kuwapeleka
katika nyumba moja mjini
Bukoba kwa mapumziko ya
usiku ule kabla ya kuelekea
Dar es salaam siku inayofuata.
“Sikuwepo Tanzania kwa
siku kadhaa.Mambo
yanakwendaje hapa?akauliza
Melanie
“Mambo yanakwenda
vizuri.Hakuna wasiwasi
wowote”akajibu Edwin
“Juhudi za kumsaka
James Kasai zimefikia
wapi?akauliza Melanie huku
akitoa kicheko kidogo na
kumtazama James ambaye
naye alitabasamu
“Kikosi cha umoja
kinaendelea na mazoezi kabla
ya kuelekea Uganda muda
wowote kitakapoamriwa
kufanya hivyo.Kwa idara
nyingine mpaka sasa
hawajapata kitu chochote”
akasema Edwin na James
Kasai akatoa kicheko kidogo
wakaendelea kunywa pombe
.Baada ya muda chakula
kikaletwa na kuwekwa mezani
wote wakajumuika.
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 9 : EPISODE 5
Mshale wa saa ulionyesha
ni saa saba za usiku pale
mlango wa chumba cha
upasuaji ulipofunguliwa na
vitanda kutolewa vikisukumwa
kuelekea wodini.Upasuaji wa
kumpandikiza ini Gosu Gosu
ulikuwa umemalizika.Saa
mbili za usiku ndipo upasuaji
ule uliochukua saa tano
ulioanza.Mathew na Ruby
walikuwepo hospitali
wakisubiri upasuaji ule
umalizike na muda mfupi
baada ya upasuaji kumalizika
Dr Masawe akatoka na kuwaita
akina Mathew ofisini kwake
akawajulisha kwamba upasuaji
ulifanyika kwa mafanikio
makubwa akawataka wasiwe
na wasiwasi tena.
Akina Mathew waliondoka
hospitali na kurejea nyumbani
kwa Mathew ilipata saa nane
za usiku.Wakati Ruby akioga
Mathew akaenda ofisini kwake
akachukua kompyuta yake na
kumpigia Habiba Jawad.
“Mathew
Mulumbi.Inakaribia saa tisa za
usiku sasa lakini bado sijapata
usingizi hata
kidogo.Nimekuwa na hofu
kubwa juu yako kwani
umezoea kunipigia simu saa
nne au saa tano.Nini
kimekutokea leo?Ulikuwa
katika hatari yoyote?Habiba
akauliza
“Samahani mama kwa
kukupa wasiwasi lakini sikuwa
katika hatari yoyote nilikuwa
hospitali” akasema Mathew na
kumsimulia Habiba kila kitu
kuhusu Gosu Gosu.
“Poleni sana.Naamini
mgonjwa wenu huyo atapona
inshallah” akasema Habiba
“Mama nimekupigia
kupata taarifa za kuhusiana na
ujio wa Khalid Sultan ambaye
uliniambia atawasili nchini
hapo kesho” akasema Mathew
“Umepata chochote
kuhusu James Kasai?akauliza
Habiba
“Bado sijafahamu ataingia
vipi nchini lakini kuna mtu
ambaye ninamfuatilia na
nikifanikiwa kumpata naamini
nitakuwa nimempata James
Kasai.Ulinituma Dubai
kushuhudia yakisainiwa
makubaliano ya fedha kati ya
IS na James kasai na
alikuwepo mwakilishi wa
James Kasai ambaye anatokea
Tanzania.Huyo mwanadada
anaitwa Melanie Davis na
ambaye ndiye nimeanza
kumtafuta.Naamini nikimpata
huyo basi nitakuwa karibu
sana kumpata James kasai”
akasema Mathew
“Una akili sana
Mathew.Nilikutuma Dubai
kwa kusudi kabisa
nikakwambia utulie ujifunze
na sasa umeona faida
zake.Sikutaka kukueleza
chochote kuhusu Melanie
Davis nilitaka nikuache
nikupime nione utafanya nini
lakini kumbe umefanya kile
ambacho nilitegemea
ukifanye.Melanie Davis ndiye
kiungo kati ya James Kasai na
IS.Kama James anakuja
Tanzania lazima atakutana
naye hivyo hakikisha
unampata.Kuhusu Khalid
Sultan atawasili kesho saa
moja za jioni na ndege ya
shirika la ndege la
Ethiopia.Picha zake unazo
naamini mtajipanga vyema
kumfuatilia kujua kilichomleta
Tanzania lakini ufunguo wa
hili fumbo ni Melanie
Davis”akasema Habiba
“Mama kuna chochote
unakifahamu kuhusu Melanie
ambacho unadhani kinaweza
kunisaidia kufahamu mahala
alipo?Mathew akauliza
“Mathew wewe ni mtu
mahiri sana katika kazi
hii.Hata kama ningekuwa
nikifahamu nisingekueleza
kwani nataka uumize kichwa
ili uweze kugundua mambo
mengine mengi.Mimi
nitakueleza yale mambo
makubwa tu na mengine ni juu
yako kuyafanyia
kazi.Umenielewa Mathew?
“Ndiyo nimekuelewa
mama”
“Vizuri.Nakutakia kazi
njema na kesho nipate
mrejesho wa nini
kinaendelea.Kumbuka Khalid
Khalid na James Kasai
hawapaswi kutoka salama
nchini Tanzania.Kumbuka vile
vie hakuna kuwaua watu hawa
wawili kabla kwanza ya
kufahamu nini wanakipanga
kukifanya”
“Nimekuelewa mama”
akasema Mathew na kuagana
na Habiba Mathew akashusha
pumzi
“Mambo yameiva.Habiba
naye anakiri kwamba Melanie
Davis ndiye mwenye ufunguo
wa fumbo hili.Wapi alipo huyu
mwanamke?Ngoja nitulize
kwanza kichwa na kujiandaa
kwa siku ya kesho” akawaza
Mathew na mara mlango wa
ofisi yake
ukagongwa.Akaifunika
komputa yake haraka haraka
na kwenda kuufungua
akakutana na Lucy mtumishi
wake wa ndani
“Karibu Lucy”
“Kaka samahani kwa
kukusumbua.Ruby
ameniambia kwamba nije
nikuone huku” akasema Lucy
na kunyamaza kidogo
“Kuna jambo ninataka
kukwambia.Nimepigiwa simu
na madam Peniela pale
ulipoondoka akaniuliza kama
kweli umerejea
nikamuhakikishia kweli ni
wewe na umerejea.Alikuwa
analia sana na akaniambia
kwamba nisikueleze
chochote.Nimeona nije
nikwambie kaka suala hilo”
“Ahsante sana
Lucy.Umefanya vyema
kunieleza”
“Sawa kaka.Vipi hali ya
Gosu Gosu?
“Tayari amekwisha
fanyiwa upasuaji wa
kupandikizwa ini na kwa
mujibu wa madaktari ni
kwamba kila kitu kilikwenda
vizuri.Usiwe na wasi wasi
kama kuna chochote kibaya
nitakujulisha” akasema
Mathew na kuagana na Lucy
“Kama Lucy
amemuhakikishia Peniela
kweli ni mimi nimerejea basi
lazima atakuja Tanzania .Huyu
ndiye atakayenipa ukweli wote
kuhusiana na Melanie Davis”
akawaza Mathew na kutoka
akarejea chumbani
“Khalid Sultan ataingia
nchini kesho saa moja za jioni
na ndege ya shirika la ndege la
Ethiopia” Mathew
akamwambia Ruby
“Hizi taarifa Mathew
anazipata wapi? Lazima kuna
mtu anawasiliana naye ambaye
ndiye anayempa taarifa
hizi.Natamani kumchunguza
kujua kinachoendelea lakini
naogopa akijua nitaharibu kila
kitu na mimi sitaki
kumkorofisha huyu jamaa”
akawaza Ruby
“Kuhusu Melanie Davis”
Mathew akaendelea
“Naamini kesho tutapata
kila kitu kuhusu yeye kwani
nina uhakika mkubwa Peniela
lazima atakuja.Alimpigia simu
Lucy kupata uhakika kama
kweli ni mimi niliyempigia
simu”akasema Mathew
“Do you miss her?akauliza
Ruby
“Not much” akajibu
Mathew
“Ni mke wko wa ndoa
nilidhani ungekuwa na hamu
sana ya kutaka kumuona”
akasema Ruby
“Nina hamu sana ya
kutaka kuwaona watoto
wangu”
“Kwa nini mama yao huna
hamu ya kutaka
kumuona?akauliza Ruby
“Ruby tusiongelee mambo
hayo tafadhali” akasema
Mathew
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 9 : EPISODE 6
Saa kumi na mbili za
asubuhi Mathew na Ruby
walipofika hospitali tayari
Austin alikwisha zinduka
kutoka usingizini na alikuwa
anaendelea vizuri.Taarifa ya
madaktari waliokuwa
wanafuatilia hali ya Gosu Gosu
toka alipotolewa chumba cha
upasuaji ilionyesha alikuwa
anaendelea vizuri.Saa moja za
asubuhi wakalazimika
kuondoka kurejea katika
makazi yao ambako Ruby
aliacha gari lake kwani
alihitajika kwenda ofisini
kwake asubuhi hiyo.Baada ya
Ruby kuondoka kwenda
kujiandaa Mathew naye
akajiandaa halafu akaondoka
kuelekea uwanja wa kimataifa
wa Julius Nyerere jijini Dar es
salaam.Alikuwa anamtafuta
mtu mmoja aliyeitwa Salim
Chongo.Huyu ni rafiki yake wa
muda mrefu.Aliwahi kufanya
kazi katika idara ya ujasusi
kabla ya kuacha baada ya
kupata kazi katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere katika idara ya
usalama.Aliekekezwa ofisi
mpya ya Salim na kuelekea
huko.Aligonga mlango wa kioo
na mwanadada aliyekuwamo
ndani akamkaribisha ndani
akaeleza shida yake ya
kuonana na Salim
akamuombwa asubiri kwani
Salim alikuwa katika kikao cha
kazi ambacho kilikaribia
kumalizika.
Ilipita saa moja na dakika
ishirini ndipo kikao
kilipomalizika na Salim
akaingia mle ofisini.Alistuka
alipomuona Mathew
“Mathew Mulumbi !
akasema Salim kwa mshangao
“Salim” akasema Mathew
huu akisimama
wakakumbatiana.
“Umepotelea wapi
Mathew?Nina zaidi ya miaka
mitatu hatujaonana”
“Nilikuwa nje ya nchi
ndiyo maana hatujaonana”
akasema Mathew na Salim
akamkaribisha ofisini kwake
“Mathew nimefurahi sana
nimekuona leo.Karibu sana”
akasema Salim
“Salim ninashukuru sana
lakini nimekuja nina shida
ndugu yangu nahitaji msaada
wako”
“Shida gani Mathew?
“Kuna kumbu kumbu ya
kamera nataka kuipitia”
akasema Mathew na Salim
akatoa kicheko kidogo
“Mathew usiniambie
mpaka sasa bado hujaacha ile
kazi”akasema Salim
“Hapana sijaacha.Bado
ninaendelea nayo”akajibu
Mathew
“Mulumbi wewe ni mtu wa
ajabu sana.Pamoja na utajiri
wote huu ulio nao lakini bado
unaendelea kufanya kazi hizi
za hatari.Waachie vijana ili ule
maisha.Uliyoyafanya
yanatosha” akasema Salim.
“Kuna yale maandishi
mgongoni kwangu uliwahi
kuyasoma ukacheka sana
unayakumbuka?Mathew
akauliza
“Kama sijasahau uliandika
People sleep peaceably on their
bed at night only because
rough men stand ready to do
violence on their
behalf.Nadhani umeandika
hivyo”
“Exactly.Kazi ile iko
damuni na kamwe siwezi
kuiacha” akasema Mathew
“Nini unahitaji nikusaidie
Mathew?akauliza
Salim.Mathew akachukua
karatasi akaandika tarehe
kisha akasema
“Ninataka kupitia kumbu
kumbu za kamera kwa tarehe
hiyo”
“Nini hasa unataka
kukitazama Mathew?Salim
akauliza
“Kuna mtu ninamfuatilia
ambaye aliingia nchini tarehe
hiyo akitokea Ufaransa kwa
kutumia ndege ya shirika la
ndege la Ufaransa kupitia
Nairobi” akasema Mathew na
Salim akatazama katika
kompyuta yake akasema
“Ni kweli tarehe hiyo
kulikuwa na ndege ya shirika
la ndege la Ufaransa”
Salim akamtaka Mathew
amfuate wakaingia katika
mlango uliokuwemo mle
chumbani wakaingia katika
chumba chenye kompyuta
runinga zaidi ya kumi kisha
akaitafuta tarehe ile
aliyoiandika Mathew na muda
ambao ndege ile ya Ufaransa
iliwasili nchini.Mathew
akawatambua Gosu Gosu na
Melanie ambao ni miongoni
mwa abiria waliokuja na ndege
ile
“Huyu mwanamke ndiye
hasa nataka kufuatilia”
akasema Mathew
Baada ya kukamilisha
taratibu akaruhusiwa kuingia
nchini Salim akabadili kamera
na kuhamia katika kamera ya
sehemu ya abiria
wanaowasili.Melanie
alionekana akiwa na Gosu
Gosu halafu mwanamke
mmoja akawasogelea
akasalimiana na Melanie
“Simamisha hapo”
akasema Mathew na
kumtazama Yule mwanamke
ambaye alimpokea Melanie
uwanjani.Nataka kupata picha
ya huyu mwanadada
aliyempokea huyu mgeni”
akasema Mathew na Salim
akamchapishia ile picha kisha
wakaendelea kufuatilia katika
kamera.Walihamia kamera
nyingine ya kwenye maegesho
ya magari na kuwaona
wakiingia katika gari.Mathew
akachukua namba za gari lile
akamshukuru Salimu
akamuaga na kuondoka.Baada
ya kuingia katika gari lake
akampigia simu Ruby
“Ruby vipi maendeleo
yako?akauliza Mathew
“Ninaendelea vizuri na
kazi.Vipi kuna habari yoyote
mpya?akauliza Ruby
“Nimetoka kuonana na
rafiki yangu mmoja wa muda
mrefu anaitwa Salim anafanya
kazi idara ya ulinzi uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere.Nimepitia kumbu
kumbu za kamera za ulinzi
zilizoko uwanjani pale siku
waliyorudi Gosu Gosu na
Melanie Davis.Nimemfuatilia
Melanie alipokewa uwanjani
na mwanadada mmoja
ninakutumia picha yake sasa
hivi ili umtafute ni nani”
akasema Mathew na
kumtumia Ruby ile picha ya
Yule mwanamke aliyempokea
Ruby uwanja wa
ndege.Akawasha gari na
kuondoka.Baada ya dakika
tano Ruby akampigia simu
“Anaitwa Felista Kabasa ni
mfanya biashara anaishi mtaa
wa Mwakisule nyumba 204”
“Ahsante Ruby ninaelekea
huko sasa hivi” akasema
Mathew
Mathew alifika mtaa wa
Mwakisule kama
alivyoelekezwa na Ruby
akaitafuta nyumba 204
akashuka garini na kuelekea
getini akabonyeza kengele ya
mlangoni baada ya muda
mfupi akatokea mama mmoja
mnene akamkaribisha Mathew
kwa tabasamu
“Karibu sana kaka”
“Ahsante mama yangu”
“Nikusaidie nini?akauliza
Yule mama
“Ninamtafuta dada mmoja
anaitwa Felista Kabasa”
akasema Mathew
“Felista?akauliza Yule
mama
“Ndiyo” Mathew akajibu
“Hapana haishi hapa huyo
dada” akasema Yule mama
“Nimeelekezwa anaishi
hapa”
“Waliokuelekeza au kama
ni yeye kakuelekeza
amekudanganya kaka
yangu.Haishi hapa huyo
mtu.Humu ndani ninaishi
mimi,mume wangu na watoto
wetu wawili na wala hatuna
mtoto anayeitwa Felista hata
mtumishi wetu wa ndani hana
jina hilo” akasema Yule mama
“Samahani sana
yawezekana nimekosea lakini
nimeelekezwa ni nyumba hii”
akasema Mathew na kutoa
picha akamuonyesha Yule
mama
“Unamfahamu huyu
dada?akauliza Mathew
“Hapana simfahamu na
wala sijawahi kumuona mtaa
huu” akasema Yule mama
“Una hakika hujawahi
kumuona mtaa huu? akauliza
Mathew
“Kwanini nikudanganye
kaka yangu?Huyu dada
sijawahi kumuona mtaa
huu.Kaka yangu kuwa makini
siku hizi wanawake wamekuwa
wadanganyifu sana” akasema
Yule mama
“Ahsante nakushukuru
sana” akasema Mathew na
kurejea katika gari lake
akaondoka.Akachukua simu
na kumpigia Ruby
“Ruby nimetoka katika
nyumba ile uliyonielekeza
kwamba anaishi Felista
nimekutana na mtu mwingine
kabisa.Felista nimemkosa”
akasema Mathew
“Lakini taarifa zake
zinaonyesha anaishi
hapo.Yawezekana labda
alikuwa akiishi hapo lakini
amehama.Ngoja niendelee
kumchimba zaidi kama
nitapata taarifa zake” akasema
Ruby
Baada ya kutoka mtaa wa
Mwakisule Mathew akarejea
nyumbani kwake na moja kwa
moja akamfuata Lucy
akamuonyesha ile picha ya
Yule mwanadada
“Melanie amekuwa akifika
mara kwa mara hapa umewahi
kumuona akiwa na huyu
mwanamke?akauliza Mathew
“Huyu ni dereva wake
anaitwa Joyce.Amekuwa akija
naye hapa kila ajapo.Akiwa
chumbani na Gosu Gosu Joyce
hubaki sebuleni na mimi ndiye
ninaye muhudumia” akasema
Lucy
“Una hakika jina lake ni
Joyce?
“Ndiyo.Jina lake ni Joyce
na hata Melanie humuita hivyo
Joyce”
“Amewahi kukueleza
mahala anakoishi?akauliza
Mathew
“Hapana hajawahi
kunieleza.Hatujawahi
kuzungumzia chochote kuhusu
yeye” akasema Lucy
“Ahsante sana Lucy”
akasema Mathew na kurejea
katika gari lake akaondoka
halafu akampigia simu Ruby
“Ruby nimetoka nyumbani
sasa hivi nimeelezwa na Lucy
kwamba huyu mwanamke
ambaye umepata taarifa zake
anaitwa Felista jina lake ni
Joyce.Ni dereva wa Melanie”
“Joyce?akauliza Ruby kwa
mshangao kidogo
“Ndiyo.Kwa mujibu wa
Lucy hilo ndilo jina lake”
akasema Mathew
“Mbona taarifa zake
hazisemi hivyo?akauliza Ruby
“Nimegundua hawa watu
wanatumia majina
bandia.Mtandao huu wa
Melanie ni mkubwa na
wamejipanga vyema.Wanajua
wanachokifanya.Kwa sasa
ninaelekea hospitali kujua
maendeleo ya wagonjwa kwani
kutokana na kazi
tutakayokuwa nayo baadae
yawezekana tusiweze tena
kupata nafasi ya kwenda
kuwaona wagonjwa” akasema
Mathew
“Nami pia ninakuja hapo
hospitali” akasema Ruby
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 9 : EPISODE 7
Helkopta ya idara ya siri
ya usalama wa ndani wa nchi
ikitokea Kagera ilitua katika
sehemu ya kutulia ndani ya
uwanja wa bohari la idara
ambako huhifadhiwa vitu
mbali mbali vya idara ya
SNSA vile vile kuna karakana
ya kutengeneza magari na
vifaa mbali mbali vya
idara.Edwin Mbeko alikwisha
mpa maelekezo dereva wake
ampelekee gari lake katika
bohari na tayari gari lilikwisha
fika.Helkopta ilipotua gari la
Edwin Mbeko likaanza
kusogea taratibu.Injini
ilipozimwa gari la Edwin
likasogezwa karibu zaidi na
helkopta mlango ukafunguliwa
akashuka Edwin Mbeko
akafuatiwa na James Kasai na
Melanie na wote wakaingia
katika gari la Edwin ambaye
alimtaka dereva wake aingie
katika helkopta wakutane ofisi
kuu.Akashika usukani na
kuondoka eneo lile.
“Karibuni Dar es salaam”
akasema Edwin Mbeko.James
Kasai hakuonekana kuwa na
wasi wasi wowote
Kutoka bohari kuu la
SNSA moja kwa moja
walielekea nyumbani kwa
Melanie.
“Karibuni ndani” Melanie
akawakaribisha ndani Edwin
na James
“Ahsante sana Melanie”
akasema Edwin Mbeko lakini
kabla hajaketi simu yake
ikaita.
“Hallo” akasema Edwin
“Edwin unaongea na
Annabel”
“Madam Annabel habari
yako?
“Nzuri.Sijakuona ofisini na
hakuna taarifa yoyote.Uko
wapi?akauliza Annabel
ambaye ni Ruby
“Ninakuja madam nilipata
dharura nje ya mkoa.Tayari
nimerejea na nitafika hapo
ofisini muda si mrefu”
akasema Edwin
“Sawa Edwin” akasema
Ruby na kukata simu.
“Melanie tayari mmefika
salama.Ninahitajika ofisini
.Nilikwambia kwamba kuna
mkurugenzi mpya ameletwa
na Rais ndiye huyo
ananihitaji.Nitawasiliana nawe
tena baadae kwa ajili ya zoezi
la kumpokea Khalid” akasema
Edwin
“Edwin ahsante sana kwa
kazi kubwa uliyoifanya ya
kutufikisha salama Dar es
salaam.Nakutegemea sana
hapo baadae katika
kuhakikisha Khalid anaingia
nchini salama bila matatizo
yoyote”akasema Melanie
“Jambo lingine Melanie
suala la Gosu Gosu ni kama
nilivyokueleza kwamba jaribio
la kumuua hospitali
lilishindikana hivyo basi hii ni
taa nyekundu kwa watu wake
wa karibu na kuwafanya
waimarishe ulinzi na vile vile
wanaweza wakaanza
kuchunguza nani wanaotaka
kumuua Gosu Gosu.Wakati
tunatafuta namna nyingine ya
kumuua Gosu Gosu tafadhali
usitumie zile simu zako zote
bali tumia simu mpya
niliyokupa na wala wala
usiende hospitali.Naamini
ndani ya siku mbili hizi tayari
tutakuwa tumepata mpango
mpya wa kumuua.Kama
alivyosema Devotha huyu
jamaa ana ukaribu na watu
hatari ambao wanaweza
wakaharibu mipango yetu
hivyo kwa sasa jiweke mbali na
Gosu Gosu”akasema Edwin na
kuondoka .
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 9 : EPISODE 8
Ruby aliwasili hospitali na
kukutana na Mathew ambaye
alimpa taarifa za maendeleo ya
Gosu Gosu na Austin.
“Mungu mkubwa.Naamini
Gosu Gosu atapona tu”
akasema Ruby
“Umechimba zaidi kupata
taarifa za Yule mwanamke
niliyekutumioa picha yake
Joyce?akauliza Mathew
“Ndiyo lakini sijaona
taarifa zake nyingine zaidi ya
zile
nilizokutumia.Nimeshangaa
uliponiambia eti anaitwa
Joyce” akasema Ruby
“Kwa mujibu wa Lucy ni
kwamba yule mwanamke
anaitwa Joyce na ni dereva wa
Melanie.Kama nilivyokueleza
simuni hawa watu
wanaonekana wanatumia
majina bandia.Sasa ninaanza
kuamini lile wazo lako
kwamba yawezekana kabisa
Melanie Davis na Melanie
Chuma akawa ni mtu
mmoja.Ruby huu ni mtandao
mkubwa na una watu makini
sana.Wanajua wanachokifanya
na ndiyo maana hata fedha za
kutoka IS zinapita kwao bila
vyombo vya fedha
kugundua.Kila aliyemo katika
mtandao huu inakuwa vigumu
sana kumfuatilia na kumpata”
akasema Mathew na
kumtazama Ruby
“Nadhani kwa sasa
tujielekeze zaidi kwa Khalid
Sultan ambaye atawasili nchini
jioni ya leo kwa ajili ya
kukutana na James
Kasai.Tukimfuatilia Khalid
atatufikisha kwa James lakini
kuna tatizo
limejitokeza”akasema Mathew
“Tatizo gani
Mathew?akauliza Ruby
“Kuna vijana ambao
Austin aliwaandaa kwa ajili ya
kutusaidia katika operesheni
hii na nilitegemea jioni ya leo
kuwa nao katika zoezi la
kumfuatilia Khalid lakini
wamenipigia simu wakati
nikija hospitali na kunieleza
kwamba wamepata safari ya
kikazi kwenda Morogoro hivyo
hawataweza kushiriki katika
operesheni yetu hadi pale
watakaporejea”Mathew
akanyamaza baada ya muda
akaendelea
“Ninataka tuwashirikishe
idara yako katika zoezi hili ili
waweze kumfuatilia Khalid
toka atakapoingia nchini hadi
pale atakapokuwa
amefikia.Pale SNSA mna kila
kitu kinachohitajika katika
zoezi hilo mnao watu na vifaa
vya kutosha hivyo itakuwa
vyema kama tukiwashirikisha
kufuatilia Khalid lakini
usiwaeleze kama anakuja
nchini kukutana na James
Kasai inaweza ikazua taharuki
kubwa.Ujio wa James Kasai
itabaki ni siri yetu kwa sasa”
akasema Mathew.
“Ni wazo zuri pia kwani
tunao watu wa kutosha wenye
mafunzo na ujuzi mkubwa pale
SNSA”akasema Ruby
“Nataka zoezi zima la
kumfuatilia Khalid
litakalofanywa na idara yako
liunganishwe katika ofisi
yangu nami pia nifuatilie lakini
asijue mtu yeyote kama
ninafuatilia.Can you do that?
akasema Mathew
“Nitakuwa pamoja nawe
wakati wa kufuatilia zoezi
hilo.Utanipa maelekezo nini
cha kufanya na mimi nitakuwa
nikiwasiliana na timu
itakayokuwa ikiendelea na
zoezi hilo la kumfuatilia
Khalid” akasema Ruby na
kunyamaza baada ya simu ya
Mathew kuita alikuwa ni Lucy
“Lucy” akasema Mathew
“Kaka Mathew samahani
kwa usumbufu.Nimekupigia
kukujulisha kwamba mama
Peniela yuko hapa nyumbani
amefika sasa hivi” akasema
Lucy
“Peniela amekuja?!
Akauliza Mathew akionyesha
mshangao kidogo.
“Ndiyo amekuja muda si
mrefu na amesema nikupigie
simu kuwa anakuhitaji hapa
nyumbani” akasema Lucy
“Sawa Lucy ninakuja hapo
nyumbani muda si mrefu”
akasema Mathew na kukata
simu akashusha pumzi
“Mambo yameiva.Peniela
amekuja” akasema Mathew
“Dah ! akasema Ruby
“Natakiwa nikaonane
naye.Usiogope hakuna
kitakachoharibika.Andaa timu
kwa ajili ya zoezi la jioni na
unijulishe kila
kinachoendelea”akasema
Mathew
“Kama Peniela atakuwepo
haitakuwa vyema mimi kuja
nyumbani kwako jioni lakini
nitakuunganisha na kila
kinachoendelea” akasema
Ruby
“Ruby lazima uje
nyumbani na tutaongoza zoezi
kutokea pale.Jambo hili ni
muhimu mno” akasema
Mathew na kuagana kila
mmoja akaingia katika gari
lake na kuondoka.
“Nilijua tu lazima Peniela
atakuja.Nashukuru kwa ujio
wake kwani utanisaidia
kufahamu mambo mengi
kuhusiana na Melanie Davis
lakini hata hivyo liko
tatizo.Lazima Peniela atataka
kufahamu kilichokuwa
kimenitokea.Nilikuwa
wapi,kwa nini nikatangazwa
nimekufa na mambo mengine
kadha wa kadha.Nitafuata
maelekezo ya Habiba
sintamueleza mtu yeyote hata
Peniela mahala nilikokuwa”
akawaza Mathew akielekea
nyumbani kwake
OFISI KUU SNSA
Ruby alirejea ofisini kwake
na muda mchache baadae
mlango wa ofisi yake
ukagongwa akaingia Edwin
Mbeko
“Habari yako madam
Annabel” akasema Edwin kwa
adabu
“Edwin ulikuwa
wapi?Toka jana hujaonekana
hapa ofisini na hakuna taarifa
zozote za mahala ulikokuwa”
akasema Ruby
“Madam kama
nilivyokueleza uliponipiga
simu kwamba nilikuwa
nimekwenda nje ya mkoa
kikazi” akasema Edwin
“Ninataka kupata orodha
ya kila operesheni
inayoendelea hivi sasa ndani
ya SNSA na kila pale
unapohitaji kwenda nje ya
mkoa nijulishe tafadhali.Mimi
hapa ni mgeni bado kuna
mmbo mengi siyafahamu
ninakutegemea sana wewe
hivyo usipokuwepo inanipa
ugumu katika kazi zangu”
akasema Ruby
“Sawa madam nitakupa
orodha ya operesheni zote
zinzaoendelea na samahani
sana kwa
kilichotokea.Hakitajirudia
tena” akasema Edwin kwa
adabu.
“Nataka kuzungumza na
wafanyakazi wote ndani ya
dakika tano.Kuna zoezi ambalo
linatakiwa kupewa uzito
mkubwa” akasema Ruby
“Sawa madam” akajibu
Edwin na kutoka kwenda
kuwakujulisha wafanyakazi
kwamba mkurugenzi
atazungumza nao muda mfupi
ujao.Zilipita dakika tano kama
alivyokuwa ameahidi Ruby
akatoka ofisini kwake
akaelekea katika ukumbi
mkubwa.Edwin akawataka
wafanyakazi wote kuacha kazi
zao kumsikiliza mkurugenzi
ambaye alianza kwa
kuwasalimu halafu akageukia
mbele kulikokuwa na runinga
kubwa
“Nafahamu zipo
operesheni mbali mbali
ambazo mmekuwa mkiendelea
nazo hapa ningependa
kuzifahamu zote na tayari
nimekwisha muelekeza Edwin
aniwekee mezani orodha ya
operesheni zote zinazoendelea
hivi sasa.Pamoja na kazi nzuri
mnazoendelea nazo sasa hivi
lakini kuna zoezi moja
muhimu sana ambalo nataka
wote tujielekeze huko kuanzia
sasa” akasema Ruby akageukia
runingani akabonyeza kitanza
mbali picha kubwa ikatokea.
“Anaitwa Khalid Sultan
Khalid” akasema Ruby na
kunyamaza kidogo
“Anatokea Syria.Ni mmoja
kati ya watu wa juu kabisa wa
kundi la IS ambaye anahusika
na milipuko mikubwa.Huyu
mtu anakuja nchini Tanzania”
Ruby akanyamaza kidogo
kisha akaendelea
“Ujio wake nchini
Tanzania unatufanya tuamini
kwamba IS wanapanga tena
shambulio lingine kubwa hivyo
ni jukumu letu kama idara
yenye dhamana ya kuhakikisha
nchi inakuwa salama kufanya
kila lililo ndani ya uwezo wetu
kuhakikisha hakuna tena
shambulio lingine ambalo
litatokea hapa nchini
Tanzania” akasema Ruby na
kunyamaza tena kidogo.
“Leo saa moja za jioni
Khalid ataingia nchini na
ndege ya shirika la ndege la
Ethiopia akitokea Cairo
Misri.Tutamfuatilia kuanzia
atakaposhuka katika uwanja
wa ndege wa Julius Nyerere
hadi atakapofikia.Tunatakiwa
kufahamu kila anachokifanya
hapa nchini,tumjue kila
anayekutana naye.Khalid haji
Tanzania kwa mapumziko
tunaamini kuna kitu kikubwa
kinachomleta hivyo basi zoezi
hili ni muhimu mno.Edwin
utapanga timu ya watu wetu
kuanzia uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere kwa ajili ya
kumfuatilia Khalid kila mahala
anakoenda hadi mahala
atakapofikia.Naomba
niwakumbushe kwamba hii ni
operesheni muhimu mno
hivyo tuwekeze nguvu kubwa
na ujuzi wetu wote katika
operesheni hii.Ninyi ni
wazoefu katika mambo haya
mmekwisha fanya operesheni
mbali mbali na kwa mafanikio
makubwa hivyo naamini hata
katika zoezi hili litafanyika
kwa ufanisi mkubwa
sana.Mkumbuke pia kwamba
IS wametekeleza shambulio
lingine baya sana hapa nchini
siku chache zilizopita na bado
machozi ya walichokifanya
hayajakauka hivyo tusiwape
nafasi hata ndogo ya
kutekeleza tena shambulio
lingine katika ardhi yetu ya
Tanzania.Ni wakati wa
kuung’oa mzizi wa IS hapa
nchini na zoezi hilo litaanza
usiku wa leo.Khalid
atatuongoza kuweza
kuwafahamu washirika wake
hapa nchini” akasema Ruby na
kuwatazama wafanyakazi wale
waliokuwa kimya
wakimsikiliza
“Mkumbuke pia kwamba
IS wanashirikiana na James
Kasai ambaye nchi zetu
zinamsaka kwa udi na uvumba
na nina uhakika kwa
kumfuatlia Khalid tunaweza
pia kupata taarifa za
kumuhusu James
Kasai.Narudia tena
kuwasisitiza ndugu zangu kwa
kiasi kikubwa sana usalama wa
nchi unatutegemea sisi hivyo
tukishindwa sisi tutakuwa
tumewapa IS ushindi na nafasi
ya kumwaga tena damu ya
watanzania.Tusikubali tena
damu yoyote ikamwagwa na
magaidi hawa.Tupambane
kufa na kupona kwa ajili ya
nchi yetu.Nadhani
mmenielewa.Kuna yeyote
mwenye swali kuhusiana na
zoezi hili la jioni ya leo?
Akauliza Ruby na kuwatazama
wafanyakazi waliokuwa kimya
wakimsikiliza.Hakuna
aliyeuliza swali lolote.
“Hakuna swali naamini
mmenielewa vizuri.Ahsanteni
sana.Sasa tuanze maandalizi”
akasema Ruby na kumtaka
Edwin waelekee ofisini kwake.
“Edwin kama ulivyosikia
kwamba mtu huyu anayekuja
Tanzania Khalid Sultan Khalid
ni mtu hatari sana.Ni
mtaalamu wa milipuko
mikubwa na IS wamekuwa
wakimtumia sana nchini
Syria.Ninaamini kwamba ujio
wake hapa Tanzania si bure
lazima kuna jambo anakuja
kulifanya.Lazima IS
wanapanga kufanya shambulio
lingine hapa nchini.Kama
nilivyoeleza kwamba tutaanza
kumfuatilia Khalid toka
atakaposhuka ndegeni.Nataka
upange vijana mahiri kabisa
wenye ujuzi na uozefu wa
kutosha katika kazi
wamfuatilie Khalid.Sitaki
lifanyike kosa hata moja”
akasema Ruby
“Sawa madam Annabel
jambo hilo linakwenda
kutekelezwa kwa ufanisi wa
aina yake.Tunayo timu ya
vijana mahiri wenye uwezo
mkubwa ambao watafanya
zoezi hilo.Hizi ni kazi zetu na
tuna uzoefu mkubwa wa
kuzitekeleza”
“Nitashukuru sana kama
zoezi likienda vizuri” akasema
Ruby
“Madam ninataka
kufahamu kama taarifa hii ya
ujio wa huyo mtu imetoka
katika chanzo cha kuaminika”
akasema Edwin.Ruby
akamtazama na kusema
“Taarifa imetoka katika
chanzo kisichokuwa na shaka
hata kidogo”
“Unaweza kunishirikisha
nikajua chanzo cha taarifa
hiyo? Akauliza Edwin
“Huniamini
Edwin?akauliza Ruby huku
akitabasamu
“Ninakuamini
madamAnnabel lakini
ninataka tu kuchukua
tahadhari kwani tumewahi
kupata taarifa kama hizo na
tukatumia nguvu kubwa
kujiandaa lakini baadae
tukagundua kwamba si taarifa
za kweli ndiyo maana
tumekuwa tunataka
kujiridhisha kila pale
tunapopata taarifa kama hiyo
kujua chanzo chake kama
kinaaminika ii tusije jikuta
tunatumia muda na rasilimali
kwa taarifa ambayo haina
ukweli wowote” akasema
Edwin
“Ni jambo zuri Edwin
kujiridhisha kila pale
mnapopata taarifa kama hizi
lakini kwangu mimi nakuomba
usiwe na wasiwasi
wowote.Nina uhakika na kile
ninachokisema.Naomba
ukaanze kufanya maandalizi”
akasema Ruby na Edwin
akatoka akaelekea sehemu
Fulani iliyojificha akachukua
simu na kumpigia simu
Melanie katika namba ambayo
huitumia kwa ajili ya
kuwasiliana na watu muhimu
tu.
“Edwin” akasema Melanie
“Melanie kuna jambo
limetokea nimeona nikujulishe
mapema”
“Jambo gani?akauliza
Melanie
“Tumetoka katika kikao
muda mfupi uliopita.Huwezi
amini mkurugenzi wetu tayari
anafahamu kuhusu ujio wa
Khalid” akasema Edwin
“That’s not true ! akasema
Melanie
“Nakwambia ukweli.Hata
mimi hapa nilipo mwili
unanitetemeka siamini
nilichokisikia kutoka kwa
mkurugenzi.Sifahamu
amepata wapi taarifa hizo”
akasema Edwin na Melanie
akashusha pumzi
“Hizi ni taarifa za kustusha
sana Edwin.Ujio wa Khalid
ulikuwa ni kitu cha siri kubwa”
akasema Melanie
“Inashangaza namna
mkurugenzi alivyofahamu “
“What are we going to do
Edwin?akauliza Melanie
“Nadhani njia nzuri ni
kutafuta namna ya kumjulisha
Khalid abadili uelekeo na asije
tena Tanzania”
“That’s impossible.Tayari
Khalid yuko angani anakuja
Tanzania.Hatuwezi kuahirisha
safari yake.Kwa nana yoyote
ile lazima Khalid aingie
nchini.Jukumu zima liko juu
yako hivyo fanya kila
linalowezekana kuhakikisha
Khalid anaingia nchini bila
matatizo yoyote” akasema
Melanie na Edwin akawa
kimya akitafakari
“Edwin ! akaita Melanie
“Nakusikia Melanie”
“Kama nilivyokueleza
kwamba fanya kila
linalowezekana kuhakikisha
Khalid anaingia nchini hata
kama tayari taarifa za ujio
wake zimekwisha ifikia idara
yako.Nini mnakusudia
kukifanya kuhusu
Khalid?akauliza Melanie
“Nimeelekezwa kuweka
timu itakayomfuatilia kutoka
uwanja wa ndege hadi mahala
atakapofikia”akasema Khalid
“Imekuwa vizuri umepewa
jukumu hilo wewe mwenyewe
hivyo basi hakikisha
unaivuruga timu hiyo
inayomfuatilia
Khalid.Umenielewa
Edwin?akauliza Melanie
“Nimekuelewa
Melanie.Niachie jambo hili
nitalishughulikia”
“Good.Nijulishe tafadhali
kila kinachoendelea
huko.Edwin kwa namna
yoyote hakuna kushindwa
katika hili.Ukishindwa
tutakuwa tumeshindwa wote
kwani mategemeo yetu yote
yako kwako” akasema Melanie
na kukata simu.
“Dah ! Huyu mkurugenzi
amenistua sana.Amejuaje
kuhusu Khalid?Amekuja jana
tu lakini tayari ameanza na
nguvu kubwa namna
hii.Natakiwa kujitahidi sana
katika jambo hili kwani kama
wakiwafinikiwa kumfuatilia
Khalid wanaweza wakagundua
kuhusu James Kasai na
wakifika hatua hiyo sote
ambao tuko kwenye mtandao
tunakwenda
kuangamia.Natakiwa
kujitahidi mno kuhakikisha
kwamba zoezi zima la
kumfuatilia Khalid
linavurugika” akawaza Edwin
na kurejea ndani akaenda
moja kwa moja katika meza ya
mwanadada mmoja mfupi
mwembamba akamtaka
amfuate wakaenda katika
chumba kimoja kilichokuwa na
kompyuta kadhaa na
hakukuwa na mtu.
“Dina unakumbuka
uliwahi kuniomba mkopo wa
fedha wiki iliyopita.Bado
unahitaji zile fedha?akauliza
Edwin
“Ndiyo bado ninahitaji
sana”akajibu Dina
“Ni kwa ajili ya nini?
Akauliza Edwin
“Ni ada kwa mdogo wangu
ambaye amekosa mkopo wa
serikali kwenda chuo
kikuu.Mimi ndiye
ninayemsomesha”
“Kiasi gani
unahitaji?akauliza
“Milioni tano”
“Nitakupa hizo fedha.Mara
mbili ya hizo
unazohitaji.Nitakupa milioni
kumi” akasema Edwin na Dina
akaruka ruka kwa furaha
“Uko tayari sasa hivi
nikakupatie hizo
fedha?akauliza Edwin
“Niko tayari Edwin.Mungu
akubariki sana” akasema Dina
kwa furaha kubwa.Haraka
haraka wakaingia garini na
kuondoka kuelekea nyumbani
kwa Edwin
“Edwin pamoja na furaha
nliyonayo kwa kukubali
kunikopesha fedha tena kiasi
kikubwa kama hicho nina wasi
wasi kwamba yawezekana
nikashindwa kurejesha kwa
wakati”akasema Dina wakiwa
garini
“Usiwe na wasi wasi
Dina.Fedha hizo ninakupa na
si mkopo”akasema Edwin na
Dina akastuka
“Unanipa siyo mkopo?!
“Ndiyo”
“Ni fedha nyingi sana hizo
mtu kupewa bila kutakiwa
kurejesha”
“Sitaki unirejeshee hata
shilingi moja lakini kuna kitu
nitahitaji kutoka kwako”
“Kitu gani Edwin?akauliza
Dina
“Si kitu kikubwa ni
msaada mdogo tu”
“Nieleze tafadhali”
“Nitakueleza usijali”
akasema Edwin
Walifika nyumbani kwake
akamkaribisha Dina sebuleni
na baada ya dakika chache
akarejea akiwa na mfuko wa
karatasi uliojaa mabunda ya
noti.
“Hizi ni milioni kumi”
akasema na kumkabidh Dina
ambaye alitokwa na machozi
ya furaha.
“Edwin ninashukuru
sana.Naona ni kama muujiza
mkubwa.Sikutegemea
kabisa”akasema Dina
“Dina baada ya kupata
kiasi hicho naamini mdogo
wako atakwenda shule bila
matatizo.Kuna kitu kidogo
ninakihitaji kutoka kwako”
“Sema Edwin unahitaji
kitu gani?akauliza Dina
“Jioni ya leo tutakuwa na
zoezi la kumfuatilia Khalid
Sultan kama alivyosema
mkurugenzi.Ninataka
unisaidie kuvuruga mfumo
wetu kwa dakika mbili tu kisha
uurejeshe tena katika hali yake
ya kawaida” akasema Edwin
“Sijakuelewa Edwin”
akasema Dina
“Ni hivi.Tutakuwa na zoezi
la kumfuatilia Khalid Sultan
jioni ya leo.Wakati zoezi hilo
linaendelea mimi nitakupa
ishara na utavuruga mfumo
wetu wote kwa dakika mbili
halafu utaurejesha tena kama
kawaida.” Akasema Edwin na
Dina akaonekana kushangaa
“Are you serious
Edwin?Yaani kwa kazi hiyo ya
dakika mbili unanipa kiasi
chote hiki cha fedha?akauliza
Dina
“Ndiyo Dina.Nataka
unisaidie kwa kazi hiyo pekee”
“Usijali nitakufanyia vile
utakavyo”
“Thank you” akasema
Edwin
“Lakini ni vipi kama
nikigundulika nimevuruga
mfumo wetu wakati wa zoezi
muhimu?
“Mimi ndiye kiongozi wa
operesheni hiyo.Hivyo hakuna
yeyote atakayekuletea tatizo
endapo itagundulika.Lakini
wewe ni mtaalamu sana wa
mambo haya ya mtandao hivyo
ufanye katika namna ambayo
hakuna atakayeweza
kugundua.Fanya ionekane ni
hitilafu za kiufundi au hali ya
hewa au chochote unachoweza
ili mradi isigundulike ni kitu
kimefanyika makusudi”
akasema Edwin
“Sawa Edwin nitafanya
hivyo”
“Kumbuka utafanya pale
tu nitakapokupa ishara”
akasema Edwin kisha
wakaondoka kurejea kazini.
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 9 : EPISODE 9
Mathew aliwasili
nyumbani kwake
“Mungu naomba
unisaidie” akawaza na kushuka
garini akaelekea ndani
akakutana na Lucy mlangoni
“Karibu kaka”
“Ahsante Lucy.Yuko wapi
Peniela?
“Yuko katika chumba cha
mapumziko anakusubiri huko”
akasema Lucy
“Nashukuru sana Lucy”
akasema Mathew na kupanda
ngazi kuelekea katika chumba
cha mapumziko kilichopo
ghorofani.Kupitia mlango
mkubwa wa kioo akamuona
Peniela akiwa amesimama
dirishani akitazama
nje.Akaufungua mlango
taratibu na kuingia
ndani.Peniela aliposikia
mlango ukifunguliwa akageuka
wakagonganisha macho.Kila
mmoja alisimama mahala pale
akimtazama mwenzake kwa
dakika mbili na taratibu
michirizi ya machozi
ikaonekana mashavuni mwa
Peniela
“Hallo Penny” akasema
Mathew
“Hallow Mathew” akasema
na kuchukua kitambaa akafuta
machozi
“Karibu sana.Pole na
safari” akasema Mathew na
kumtaka Peniela aketi.
“Ahsante sana kwa kuja
Peniela.Nimefurahi kukuona
tena” akasema Mathew
“Mathew I’m sorry
nimeshindwa nifanye nini
baada ya kuiona sura
yako.Nimeshindwa
nikukumbatie niangue kilio au
nifanye nini” akasema Peniela
“Nafahamu Peniela uko
katika mstuko bado na
itachukua muda kuamini kama
kweli ni mimi lakini naomba
nikuthibitishie kwamba ni
mimi Yule Yule
unayenifahamu” akasema
Mathew
“Kwa nini Mathew
umetutesa kiasi hiki?Unajua ni
mateso gani mimi na watoto
tumeyapitia ? akauliza Peniela
“Ninafahamu Peniela na
sipati neno zuri la kuwaomba
samahani kwa wakati mgumu
mliopitia lakini hata wewe
mwenyewe unafahamu
nising…..”
“Hapana hufahamu kitu
chochote Mathew ! akasema
Peniela kwa ukali na
kumkatisha Mathew
“Hufahamu chochote
kuhusu mateso ambayo mimi
na watoto
tumeyapitia.Ungejua kama
tutateseka usingetengeneza
kifo chako!
“Penny sikufanya hivyo na
siwezi kufanya hivyo hata siku
moja.Unajua ni namna gani
ninakupenda wewe na watoto
hivyo nisingeweza kufanya kitu
ambacho kingewaumiza”
“Mathew ninajuta
kukupenda mtu kama
wewe.Ningejua kama nitaishi
maisha kama haya nikiwa
nawe katu nisingekubali
kuolewa nawe!
“Usiseme hivyo Peniela”
“Ni lazima niseme ili
ufahamu.Ninajuta kuishi na
mtu kama wewe.Unadiriki
hata kutunga kifo chako na
hufikirii familia yako itateseka
kiasi gani.Kitu gani umekikosa
Mathew.Nimekupa utajiri
mkubwa maisha ya kifahari
lakini bado unarudia kazi zako
hizi zisizo na maana
yoyote.Unapata nini kutoka
katika kazi hizi zinazokufanya
uipe familia yako mateso
makubwa?Maneno yale ya
Peniela yakaonekana
kumchoma sana Mathew
“Peniela una haki ya
kunitukana mimi matusi ya
kila namna unayoyafahamu
lakini katu usithubutu
kuitukana na kuidharau kazi
yangu.Ni kazi hii hii ambayo
leo unaidharau ndiyo kazi
ambayo imekufanya leo hii
ukajulikana dunia
nzima.Isingekuwa kwa kazi hii
usingekuwa Peniela huyu wa
leo hivyo nakuonya usithubutu
kudharau kazi yangu !
“Lazima niseme ! Kazi hiyo
imekuingizia nini hadi sasa?
Toka umeanza kuifanya kazi
hii hakuna manufaa yoyote
uliyowahi kuyapata zaidi ya
hasara.Umeipoteza hadi
familia yako ya kwanza kwa
sababu ya kazi hii lakini bado
hujajifunza na sas…………..”
“Peniela stop !! akasema
Mathew kwa hasira
“You want to hit me?Go
ahead hit me I’m not scared of
you ! akatamba Peniela
“Sifahamu nani kakuloga
Mathew hadi unaacha hivi
vyote nilivyokupa na kurejea
katika kazi kama hizo zisizo na
mshahara wowote.I didn’t
know you are such a stupid…..”
Peniela hakumaliza kile
alichotaka kuisema akajikuta
ameanguka sakafuni baada ya
kulambwa kofi zito.Akagala
gala pale chini na kuinuka
akavua kiatu chake akaipiga
meza ya kioo ikavunjika
akachukua kipande cha kioo
akakirusha lakini Mathew
akawa hodari akakikwepa
halafu akamfuata tena na
kumnasa kofi lingine zito
Peniela akajikuta amekaa
sofani.Damu zilianza kumtoka
mdomoni.
“Nimekuonya dhidi ya
dharau na kejeli zako kwa kazi
yangu.Nitukane utakavyo
lakini si kutukana na kudharau
hiki ninachokifaya.Do you
know what I’m going through
right now?Nina majukumu
mazito ya kuisadia nchi hivyo
sintavumilia kejeli za mtu
kama wewe.Sintajali wewe ni
mke wangu au nani lakini
utakaponikosea heshima
katika kazi yangu lazima
nikufunze adabu ! Hii ni mara
ya kwanza ninakupiga toka
nimekuoa na nimekupiga
kutokana na dharau
ulizozionyesha.Ulipaswa
kunionea huruma badala ya
kuanza kunikejeli.Unadai
umenipa utajiri ?Mimi ndiye
niliyekupa huo utajiri ambao
leo hii unakupa kiburi!
Akafoka Mathew
“Everything came from
blood.You have nothing you
stupid ! akafoka Peniela huku
akilia
“Fine.Kwangu mimi utajiri
wa mali si kitu na sihangaiki
nao.Ninahangaika kwa ajili ya
nchi yangu na watu wake
wakae kwa amani na wala
sihitaji mtu anilipe kwa kazi
hiyo bali ni Mungu mwenyewe
ndiye atakayenilipa kwa njia
anazojua yeye mwenyewe
hivyo tafadhali usinitusi
kuhusu mali hizi ambazo
ninaweza kuzitafuta na kupata
kushinda hata hizo
ulizonazo.Nimekuta umeuza
mali zote na sijakulaumu kwa
sababu sihangaiki na mali”
“Kama uhangaiki na mali
kwa nini ukanipigia simu?
“Nilitaka kupata uhakika
kama ni wewe uliyeuza”
“Ni mimi nimeuza jasho
langu.Siwezi kuacha mali
zangu kwa mtu asiye na
shukrani hata chembe!
“Ni wewe ambaye
umekosa shukrani kwangu
kwani kama nisingesimama
imara mimi haya yote
usingekuwa nayo”
“Huna uimara wowote
Mathew.Ungekuwa imara
usingetengeneza kifo chako na
kuiacha familia yako katika
mateso makubwa”
“I didn’t fake my death but
…..” akasema Mathew na
kunyamaza kidogo
“Hukuonekana kuumizwa
na kifo changu hata kidogo
ndiyo maana hukusumbuka
kutafuta ukweli hukusumbuka
hata kutafuta kaburi langu
liliko”
“Ninajutia hata machozi
niliyoyamwaga kwa ajili
yako.Hustahili machozi
yanguMathew ! Wewe ni mtu
mnyama sana !
“Ninalifahamu
hilo.Sikustahili machozi yako
kwa sababu tayari ulikwisha
nitoa ndani ya moyo
wako.Nafahamu mapenzi kati
yetu yalikwisha zamani ni
mimi ambaye niliendelea
kubembeleza na ulipopata
taarifa za kifo changu
ulishukuru” akasema Mathew
na kuvuta pumzi ndefu
“Ninafahamu kuhusu
mapenzi yako na Nahum
kijana wa kutoka Israel.I saw
you and I was hurt”akasema
Mathew na Peniela akabaki
kimya akimtazama Mathew
“Ulifanya haraka sana
kuamua kuwa na mwanaume
mwingine wakati hujaupata
ukweli halisi kuhusu kifo
changu”
“Ouh kumbe ulikuwa
unanifuatilia ! Stupid. !
akasema Peniela na kufuta
damu kwa kitambaa
“Imekuwa vizuri kama
ulikuwa unanifuatilia na
umegundua kwamba nilikuwa
na mwanaume mwingine
anayejitambua kuliko wewe !
“Nahum alikuwa
anakuchezea tu
Peniela.Alikuwa ni jasusi wa
Israel na alikuwa kazini!
akasema Mathew na Peniela
akawa kimya.Baada ya muda
akasema
“Sijali kama alikuwa
ananichezea ama vipi lakini
alikuwa anajielewa kuliko
wewe.Sitaki mjadala mrefu na
wewe.Nimesafiri usiku kucha
kuja hapa Tanzania kwa ajili ya
kitu kimoja tu” akasema
Peniela na kunyamaza
akamtazama Mathew
“Nimekuja kulimaliza hili”
akasema tena na kufuta
machozi
“Mathew nilitegemea kuwa
mwanamke mwenye furaha
kubwa katika maisha yangu
lakini imekuwa kinyume chake
nimekuwa ni mwanamke
mwenye mateso makubwa
kuliko furaha.Nyakati
nilizowahi kuwa na furaha
toka nimekuwa nawe ni chache
sana.Nimejitahidi kuvumilia
nikitegemea labda siku moja
mambo yatabadilika lakini
hakuna dalili zozote za
mabadiliko na ninaendelea
kuumia na wewe mwenzangu
huonekani kujali furaha yangu
na wanangu.Umesema
nisidharau kazi yako na siwezi
kufanya hivyo lakini kwa kauli
hiyo umedhihirisha wazi
kwamba umechagua kazi
kuliko mimi na watoto.Hauoni
tena thamani yetu ndiyo
maana umekuwa ukiendelea
na maisha yako huku sisi
tukimwaga machozi kila siku
kukulilia na kukuombea.Sitaki
kuendelea na maisha haya
Mathew na Mungu
atanisamehe kwa maamuzi
haya niliyoyachukua” akasema
Peniela na kuinuka akaenda
kuchukua mkoba wake
akaufungua na kutopa bahasha
ya khaki akampatia Mathew
akaifungua na kukuta ni
nyaraka za mahakama za
kutengua ndoa.Mathew
akaziweka karatasi zile na
kumtazama Peniela kwa hasira
“Utanisamehe Mathew
hayo ndiyo maamuzi
niliyoyachukua na sintabadili
tena maamuzi yangu.Nataka
niwe na furaha katika maisha
yangu na furaha hiyo siwezi
kuipata nikiwa nawe hivyo
nimeamua kuachana nawe ili
kila mmoja aendelee na
maisha yake kwa amani.Wewe
utaendelea na kazi yako
ambayo ni ya muhimu kuliko
sisi na mimi nitaendelea na
maisha yangu na kama Mungu
akinijalia basi nitampata Yule
ambaye atanipa furaha ya
maisha ninayoihitaji” akasema
Peniela na Mathew
akazichukua tena zile karatasi
akazisoma kisha akamtazama
Peniela
“Are you sure you want to
do this?akauliza Mathew
“I’m sure 100%” akajibu
Peniela
“Please sign the papers
Mathew.Hakuna namna
unayoweza ukanishawishi
nikabadili maamuzi yangu.It’s
over please accept it.Kuhusu
mali usiwe na wasiwasi
nitakugawia robo ya mali
zangu zote” akasema
Peniela.Mathew akatafakari
akavuta pumzi ndefu na
kusema
“Arlight let’s end
this.Lakini…” akasema
Mathew na kumtazama
Peniela
“Naomba ufahamu
kwamba ninapo weka saini
makaratasi haya ninaufunga
mlango ambao hautafunguliwa
tena.Lifahamu hilo na
ninaomba uwe na uhakika na
hiki unachotaka kukifanya”
“Saini karatasi Mathew.I
don’t care if there is a door or
window between
us.Ninachokihitaji ni kuachana
nawe rasmi.Siwezi kuishi na
mtu ambaye anakufa na
kufufuka.Hujui lini atakufa
kifo cha kweli.Siwezi
kuendelea kuteseka kiasi
hiki.Labda Mungu atakujalia
utampata Yule ambaye
atakuelewa na atakuwa tayari
kuishi nawe lakini mimi
nimeshindwa kukuelewa na
siko tayari kuendelea kuishi
nawe” akasema
Peniela.Mathew akazitazama
tena zile karatasi kwa makini
“Kama alivyotamka yeye
mwenyewe kwamba it’s
over.Hakuna namna
ninavyoweza kumshawishi
akabadili maamuzi yake na
mimi siwezi nikaacha kazi hii
muhimu kwa nchi nikamfuata
mwanamke.Kwangu nchi
kwanza na mengine baadae
kwa hiyo niko tayari kuitoa
sadaka ndoa yangu.Ngoja
nimuache aende kwani
sintaweza kumpa furaha
anayoihitaji katika maisha
yake.Nitakuwa mchoyo kama
nitaendelea kung’ang’ania
kuwa naye” akawaza Mathew
“Peniela naomba
unisikilize” akasema Mathew
“Nimekuelewa kile
unachokitaka na
nitakutimizia.Sitaki kuwa
mchoyo nataka ukaitafute
furaha ya maisha unayoihitaji
lakini kabla ya kuweka saini
karatasi hizi kuna mambo
ambayo nataka tukubaliane”
akasema Mathew na
kunyamaza kidogo halafu
akasema
“Kwanza kabisa ni kuhusu
watoto.Ninaomba sana jambo
hili liwe ni letu peke yetu na
watoto wasifahamu
chochote.Wataendelea
kufahamu kuwa nimefariki
dunia hadi hapo baadae
mambo yangu yatakapotulia
nitawatafuta na kuwaeleza
ukweli.Jambo la pili ni kuhusu
mali” akanyamaza tena kidogo
“Sihitaji chochote kutoka
katika mali zako Peniela.Kama
uliamua kunitengea fungu
langu ligawanye mafungu
manne na kila mtoto wangu
apate fungu lake.Jambo la tatu
kuna msaada ninauhitaji
kutoka kwako”
“Kama umekataa mali
nilizokupa unataka nikusaidie
nini tena? akauliza Peniela.
“Ninahitaji taarifa”
“Taarifa zipi
unahitaji?akauliza Peniela
“Nataka kumfahamu Yule
mtu uliyemuuzia mali za hapa
Dar es salaam Melanie Davis”
akasema Mathew na uso wa
Peniela ukaonyesha mshangao
“Melanie Davis?! Kwa nini
unataka kumfahamu?
“Ninahitaji kupata taarifa
zake.Wewe ndiye
unayemfahamu vyema hivyo
basi nakuomba unipe taarifa
zake” akasema Mathew
“Unataka kumfanya nini
Melanie? Tafadhali naomba
usimguse mimi ndiye
niliyemuuzia mali zangu na
zilizobaki nikampa Gosu
Gosu.Sikujua kama utafufuka
tena” akasema Peniela
“Peniela narudia tena
kukukumbusha kwamba
sihitaji mali.Ninao uwezo wa
kuishi maisha ya aina yoyote
ile hivyo mali si kipaumbele
kwangu.Huyu Melanie sihitaji
kumsumbua kwa chochote
kuhusu mali alizonunua kwani
amenunua kihalali kabisa”
“Kwa nini sasa unataka
taarifa zake?
“Utanipa taarifa zake au
haunipi?Mathew akauliza
“Utanifanya nini kama
nisipokupa taarifa zake?
“Sintasaini karatasi hizi na
wewe utaendelea kuwa mke
wangu hadi kifo
kitutenganishe” akasema
Mathew na kuweka kalamu
chini.
“Simfahamu Melanie
Davis vizuri.Niliwatangazia
watu wangu wa karibu hasa
wafanya bishara kuhusu
mpango wangu wa kuuza mali
zilizoko Tanzania na kuwataka
wanisaide kutafuta
mnunuzi.Walikuja wanunuzi
wengi lakini akajitokeza
Melanie ambaye alikuja na bei
nzuri na kuwazidi wale wote
waliokuja mwanzo hivyo basi
nikamuuzia kila kitu”
“Melanie anatajwa kuwa
mmoja wa mabilionea
wakubwa nchini Ufaransa
utajiri ambao alirithi kutoka
kwa wazazi wake.Wewe
umekuwa miongoni mwa
mabilionea wa Ufaransa je
umewahi kumsikia Melanie
Davis hapo kabla?akauliza
Mathew.Melanie akafikiri na
kusema
“Hapana sikufahamu
Melanie kabla”
“Umewahi kuwasikia
wazazi wake?akauliza Mathew
“Hata wazazi wake sina
kumbu kumbu kama nimewahi
kuwasikia.Taarifa hizi zote
umezipata wapi?akauliza
Peniela
“Ukiacha haya makampuni
uliyomuuzia hapa Tanzania
unazifahamu biashara zake
nyingine? Akauliza Mathew
“Hapana sizifahamu”
“Ikawaje ukamuuzia
kampuni zako mtu ambaye
humfahamu vyema?akauliza
Mathew
“Nilihitaji mnunuzi na
alipojitokeza sikutaka
kumchunguza mara mbili
nikamuuzia” akajibu Peniela
“Unafahamu yalipo makazi
yake jijini Paris? Mathew
akauliza
“Mathew sihitaji maswali
yako tena.Kama unahitaji
kumfahamu mtafute wewe
mwenyewe ukamuhoji !
akasema Peniela kwa ukali
“Peniela I real need your
help.Muda mfupi ujao
nitakapoweka saini yangu
katika hizi karatasi utakuwa ni
mwisho wetu na mlango
utafungwa.Only God knows
when we’ll meet again hivyo
basi huu ni msaada wangu wa
mwisho ninakuomba
unisaidie.Ni muhimu sana
kwangu na ….” Akasema
Mathew na Peniela
akamkatisha
“Melanie ana umuhimu
gani kwako? Kwa nini
unatafuta taarifa zake
unamchunguza? Akauliza
Peniela
“Peniela nisingependa
kukueleza chochote kwa sa…”
“Kama hutanieleza sababu
za kutafuta taarifa za Melanie
sintakueleza chochote
ninachokifahamu” akasema
Peniela.
“Arlight unataka
kufahamu? Ni kwamba mtu
uliyemuuzia makampuni yako
hapa Tanzania Melanie Davis
ana mahusiano na kikundi cha
kigaidi cha IS na vile vile ana
mashirikiano na James Kasai
kiongozi wa kundi la waasi
ambaye hivi karibuni alifanya
shambulio hapa nchini ambalo
liliua wake za marais wa
Tanzania,Congo na Rwanda.IS
wamekuwa wakimtumia
Melanie kupitishia fedha
kwenda kwa James
Kasai.Umemuuzia mali mtu
hatari kabisa kwa usalama wa
nchi yetu” akasema Mathew na
Peniela akabaki mdomo wazi
na mara simu ya Mathew
ikaita alikuwa ni Dr Masawe.
“Samahani nataka
kuipokea hii simu” akasema
Mathew na kuipokea ile simu
“Dr Masawe” akasema
Mathew
“Mathew nimekupigia
kukupa taarifa kwamba
tumepokea taarifa muda mfupi
uliopita kutoka polisi kwamba
mwili wa Dr Sebastian
umeokotwa ufukweni akiwa
amekufa.Polisi wanasema
alipigwa risasi ya kichwa”
“Sebastian ameuawa!
Mathew akashangaa
“Ndiyo Mathew ameuawa”
“Dr Masawe suala hili ni
kubwa.Nitafika hapo hospitali
tutazugumza kwa kirefu
zaidi.Nashukuru sana kwa
taarifa” akasema Mathew na
kukata simu akamtazama
Peniela.
“Unafahamu kama
Melanie na Gosu Gosu wana
mahusiano ya
kimapenzi?akauliza Mathew
“Ndiyo ninafahamu.Ni
mimi ndiye
niliyewaunganisha.Nilimuita
Gosu Gosu Ufaransa kwa ajili
ya kufanya mauziano na
Melanie na walipokutana
wakapendana wakawa
wapenzi” akasema Peniela
“Tunahisi kwamba Gosu
Gosu kuna kitu alikigundua
kuhusu Melanie ndiyo maana
wakataka kumuua.Alipigwa
risasi nyingi ili afariki lakini
siku yake haikuwa imefika
akanusurika na jana
likafanyika tena jaribio lingine
la kutaka kumuua.Daktari
mmoja alitumika kumchoma
sindano ya sumu Gosu Gosu
kwa bahati mbaya jaribio hilo
la kumuua halikufanikiwa
lakini imelazimu Gosu Gosu
kufanyiwa upasuaji wa
kupandikizwa ini jana usiku
kwani ini lake liliharibiwa
kabisa na sumu.Melanie ni
mwanamke hatari kabisa hata
wewe ujihadhari naye sana
kwani mtandao wake ni
mkubwa” akasema Mathew
“Kwa hiyo hivi sasa
unaendesha zoezi la kumsaka
Melanie Davis?akauliza
Peniela
“Ndiyo.Ninamsaka
Melanie Davis na ndiyo maana
ninahitaji sana msaada wako”
“Mathew unamtafuta
Melanie kwa sababu
anashirikiana na magaidi wa
IS au kwa sababu amenunua
mali zako? Peniela akauliza
“Kwa mara nyingine tena
Peniela nakukumbusha
kwamba mimi sihitaji
mali.Hizi zote ni mali zako na
mimi nilikuwa msimamizi
wake tu hivyo sina kinyongo
chochote na Melanie kununua
mali zangu.Nilikuwa
naendelea na operesheni
yangu ya kuwasaka magaidi na
ndipo Melanie Davis
alipojitokeza na nikaanza
kumfuatilia na kugundua
ndiye aliyenunua mali zangu.
Sikuwa na sehemu nyingine ya
kuweza kupata taarifa zake ila
kwako ndiyo maana
nikakupigia” akasema Mathew
“Nilichokueleza ndicho
kitu niachokifahamu kuhusu
Melanie labda nitakusaidia
kufanya uchunguzi na nikipata
taarifa zozote za kumuhusu
yeye nitakujulisha” akasema
Peniela
“Nitashukuru sana”
akasema Mathew
“Maswali yamekwisha can
you sign now?akauliza Peniela
Mathew akaishika kalamu
na kumtazama Peniela kisha
akaanza kusaini zile
karatasi.Alipomaliza
akazirudisha ndani ya bahasha
na kumkabidhi Peniela
“Ahsante Mathew na
samahani sana kwa maamuzi
haya ” akasema Peniela.
“Usijali
Peniela.Ninakupongeza kwa
maamuzi haya magumu
ambayo umeyafanya.Unahitaji
furaha katika maisha yako na
mimi si mtu sahihi ninayeweza
kukupa hiyo furaha.Maisha
yangu hayataweza kubadilika
kamwe kwani nililetwa duniani
kwa ajili ya kazi hii na
nitandelea nayo hadi siku ya
kufa kwangu.Ninakushukuru
sana kwa kunivumilia kwa
muda mrefu na samahani vile
vile kwa kuwasababishia
maumivu makubwa lakini
halikuwa kusudi langu
kuwaumiza.Ninachokuomba
wakuze watoto katika maadili
mazuri wawe na bidii katika
masomo,wamjue Mungu
wafundishe kusaidia watu
wenye uhitaji kwa kuwa wao
wamezaliwa katika utajiri
mkubwa.Wasaidie kuhakikisha
wanatimiza ndoto zao lakini
kamwe,narudia tena kamwe
usiruhusu mtoto wangu yeyote
akafanya kazi kama
ninayoifanya mimi.Sitaki waje
kuishi maisha kama ninayoishi
mimi.Sitaki wayapitie yale
ninayoyapitia.Waweke mbali
kabisa na dunia hii ninayoishi
mimi.Nadhani umenielewa
Peniela” akasema Mathew na
Peniela akafuta machozi
“Nimekuelewa Mathew na
mimi pia ninakuomba
samahani sana kila pale
nilipokukosea.Najua sikuwa
mkamilifu nimekukwaza mara
nyingi,tuliwahi kutengana na
mimi nilikuwa
chanzo,nimewahi kuwa na
mahusiano na wanaume
kadhaa ulifahamu lakini
ulinivumilia.Nisamehe sana
kwa yote” akasema Peniela
“Hakuna mwanadamu
mkamilifu.Sote tuna
mapungufu yetu na mimi
niliyafahamu mapungufu yako
nikayakubali na
kuyabeba.Nategemea Yule
atakayekuja baada yangu naye
atakuwa mvumilivu kama
mimi.Ninakutakia kila la heri
Peniela”akasema Mathew na
kusimama
“Mathew kabla
hatujapeana kwa heri ya
kuonana kuna kitu nataka
kukifahamu.Ulizungumza
kuhusu
Nahum.Umemfahamuje?Ulifa
hamuje kama mimi na yeye
tulikuwa na
mahusiano?akauliza Peniela
na Mathew akaketi
“Haitakuwa na umuhimu
wowote tena kwako kwa sasa
lakini kwa umeuliza
nitakueleza ukweli wa kile
kilichotokea” akasema Mathew
na kumsimulia kuanzia Olivia
Themba alivyotekwa na
SNSA,sakata la Edger Kaka na
hadi operesheni ile ya
kuwakomboa mateka
waliotekwa na IS na hadi
alivyopigwa risasi na
kutekwa.Mashavu ya Peniela
yaliloa machozi
“Nilipofumbua macho
nilijikuta katika chumba
chenye kiza na baadae
nikagundua nilikuwa nchini
Israel. Nilianza kupatiwa
mateso makali na nimeteswa
kwa muda wa miaka mitatu”
akasema Mathew na kuvua
fulana akamuonyesha Peniela
makovu ya vidonda
vilivyotokana na mateso
aliyoyapata.Peniela akafumba
macho hakutaka
kutazama.Mwili wa Mathew
ulijaa makovu ya vidonda.
“Haya ndiyo niliyoyapitia
huko Israel kwa miaka
mitatu.Sikumbuki ni mara
ngapi nilipoteza fahamu
wakati nikiteswa lakini ni
mara nyingi.Pamoja na mateso
hayo makali lakini sikuwahi
kufungua mdomo wangu
kusema chochote na ndipo
walipoamua kuitumia familia
yangu kunilazimisha
niongee.Wakamtuma Nahum
Yatom aje Ufaransa aanzishe
mahusiano nawe na lengo lake
likafanikiwa.Nahum alikuwa
ni jasusi kutoka shirika la
ujasusi la Israel
Mossad.Hakuwa na malengo
yoyote nawe bali alikuwa
kazini.Zilifungwa kamera
chumbani kwako na Mossad
walikuwa wanafuatilia kila
mlichokuwa mnakifanya na
Nahum.Nilionyeshwa mkiwa
chumbani mkifanya mapenzi
na Nahum nikaumia sana na
Mossad walikuwa wakihitaji
niumie ili niweze kuzungumza
na kwa maumivu niliyokuwa
nayo nikajikuta nikianza
kuzungumza” akasema
Mathew
“It was true then ….”
Akasema Peniela akifuta
machozi
“Nini Peniela?
“Kabla ya kuuawa Nahum
aliniambia uko hai nikutafute
lakini nikapuuza maneno
yake”
“Alikwambia
hivyo?akauliza Mathew
“Ndiyo aliniambia hivyo”
akajibu Peniela
“Nani alimuua
Nahum?Mathew akauiza
“Hadi leo hii haijulikani
nani waliomuua”
“Lazima atakuwa
ameuawa na Mossad” akasema
Mathew
“Mathew I’m sorry
sikuyafahamu hayo yote
uliyoyapitia” akasema Peniela
“Usijali Penny yamekwisha
pita ila nakuomba usimueleze
mtu yeyote haya niliyokueleza”
“Sintamueleza mtu yeyote
Yule” akasema Peniela
“Naamini sasa utakuwa
huru Peniela jitahidi uwe na
furaha katika maisha
yako.Usiwaze chochote kuhusu
mimi.Maamuzi haya
uliyoyafanya ni maamuzi
sahihi kwa wakati sahihi”
akasema Mathew na Peniela
akaendelea kulia.
“Mathew please I need a
hug” akasema Peniela na
Mathew akainuka akaenda
kumkumbatia.
“Mathew I’m very sorry !
akasema Peniela akilia na
kumwaga machozi katika bega
la Mathew
“Peniela unahitaji kuwa
jasiri wala usisikitike kwa
maamuzi haya uliyoyachukua”
akasema Mathew na
kumuachia Peniela.
“Unarejea leo
Paris?Mathew akauliza
“Nimekuja na ndege yangu
ninaondoka leo hii kurejea
Paris.Kabla sijaondoka
naomba unipeleke nikamuone
Gosu Gosu” akasema Peniela
na Mathew akamuogoza hadi
katika gari lake wakaondoka
kuelekea hospitali kumtazama
Gosu Gosu.
“Watoto
wanaendeleaje?akauliza
Mathew
“Kwa sasa wametulia
wanaendelea vizuri na
masomo na maisha yao kwa
ujumla lakini kwa miaka
miwili hapo nyuma walikuwa
wameathiriwa sana na kifo
chako”
“Ndiyo maana sitaki
wafahamu chochote kuhusu
mimi kuwa hai kwa sasa hadi
hapo baadae.Nakuomba tena
usiwaeleze chochote kuhusu
mimi” akasema Mathew
“Sintawaeleza chochote
kwani watachanganyikiwa
zaidi”
“Peniela …” akaita Mathew
“Unasemaje Mathew?
“Naomba ufahamu
hayakuwa mategemeo yangu
maisha yetu yawe namna
hii.Sikutegemea kama siku
moja tungemaliza mahusiano
yetu namna h……” akasema
Mathew na Peniela
akamkatisha
“Mathew tumekwisha
yamaliza hayo kitu cha msingi
ni kutazama yale ya mbele
yetu.Muda wowote ukihitaji
kitu chochote tafadhali usisite
kuniambia.Namba yangu ya
simu ni ile ile”akasema Peniela
“Am I doing the right
thing?akajiuliza Peniela na
kumtazama Mathew kwa jicho
la wizi
“Namuonea huruma sana
Mathew kwa mambo
anayoyapitia.Mwili wake
umeumizwa vibaya sana hadi
nilisisimkwa mwili nilipoyaona
makovu yale katika mwili
wake.Sikuufahamu ukweli na
nikadhani alitengeneza kifo
chake kumbe alikuwa katika
mateso.Nimechanganyikiwa.N
ifanyaje wakati tayari
amekwisha saini hizi
karatasi?Nilimtamkia maneno
mabaya sana yaliyomuudhi
hadi akaamua kunipiga kitu
ambacho hajawahi kukifanya
toka tumekuwa wapenzi.I was
so stupid.Nilikurupuka sana
kufanya maamuzi kama haya
kwa mtu kama huyu ambaye
amekwisha fanya mambo
mengi sana kwa ajili
yangu.Amesimama nami
katika nyakati ngumu ambazo
hakuna
aliyewezaa,amenivumilia kwa
mengi,huyu ni mwanaume wa
kipekee kabisa na ninaumia
kwa hiki nilichokifanya lakini
maamuzi haya ni kwa faida
yetu sote.Mathew amechagua
kuendelea na kazi yake ya
ujasusi” akaendelea kuwaza
Peniela.
Walifika katika hospitali
kuu ya Mtodora alikolazwa
Gosu Gosu.Mathew akafanya
mpango na Peniela
akaruhusiwa kuingia kwenda
kumuona Gosu Gosu
akamwaga machozi
alipomuona akiwa amelala
kitandani hana fahamu.Baada
ya kutoka kumuona Gous Gosu
Mathew akampeleka katika
chumba alimolazwa Austin
akamtambulisha kwa Peniela.
“Huyu ndiye aliyejitolea
sehemu ya ini alilopandikizwa
GosuGosu” akasema Austin na
Peniela akamshukuru kwa kile
alichokifanya.Baada ya zoezi
hilo kukamilika Peniela
hakuwa na kitu cha ziada
ulikuwa ni wakati wake wa
kuondoka kurejea
Paris.Mathew akamsindikiza
uwanja wa ndege
“Nimeumizwa sana na hali
ya Gosu Gosu.Nakuahidi
nitakwenda kutafuta taarifa za
kuhusu Melanie Davis na
nitakujulisha” akasema
Peniela wakiwa garini
“Ahsante sana” akasema
Mathew
Hakukuwa na
mazungumzo mengi garini
hadi walipofika uwanja wa
ndege wa Julius
Nyerere.Mathew akashuka na
kumfungulia Peniela mlango
“Penny this is it.” Akasema
Mathew
“Mathew thank you for
everything” akasema Peniela
wakakumbatiana na kwa mara
ya mwisho Mathew akambusu
Peniela
“Please go and don’t look
back” akasema Mathew na
Peniela akaelekea ndani ya
jengo la uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere huku machozi
yakimdondoka.
Mathew hakuondoka pale
uwanjani hadi alipoiona ndege
ya Peniela yenye maandishi
makubwa Penny air ubavuni,
ikipaa na kuondoka.
“Kwa heri
Peniela”akasema Mathew na
kuingia katika gari lake
akaondoka.
“Naona kama ndoto lakini
ni kweli nimeachana na
Peniela.Nimetoka naye
mbali,tumepitia mengi na
hatimaye safari yetu
imehitimishwa rasmi
leo.Inaniumiza kuacha na mtu
ambaye niliahidi kuishi naye
hadi kifo lakini ahadi hiyo
imeshindwa kutimia” akawaza
Mathew
Kutoka uwanja wa ndege
wa Julius Nyerere akarejea
nyumbani kwake akaenda
moja kwa moja chumbani
kwake na kuchukua albamu
lenye picha mbali mbali
alizowahi kupiga na Peniela na
familia yake.
“Tumewahi kuwa na
nyakati nyingi nzuri lakini kwa
sasa sina hakika kama
ninaweza tena kumfanya
Peniela awe na furaha.Siwezi
kumlaumu kwa maamuzi
aliyoyachukua.Natakiwa
kusonga mbele na maisha
yangu” akawaza Mathew na
kumpigia simu Ruby
akamjulisha kilichotokea kati
yake na Peniela na Ruby
akamuahidi kwamba
atamfuata nyumbani kwake.
Ndege ya Peniela ilipokaa
sawa angani akachukua simu
yake ya intaneti akampigia
mtu Fulani na simu
ikapokelewa
“Peterson ni mimi
Peniela.Ninapozungumza
nawe hivi sasa niko
Afrika.Niliondoka jana jioni
lakini kwa sasa niko angani
narejea Paris”akasema Peniela
“Peniela pole kwa safari
ndefu” akasema Yule jamaa
aliyekuwa akizungumza na
Peniela simuni
“Nashukuru
Peterson.Nimekupigia simu
kuna kazi muhimu nataka
unisaidie kuifanya.Kuna mtu
mmoja anaitwa Melanie
Davis.Huyu anatajwa kuwa
mmoja wa mabilionea wa jiji la
Paris.Nataka umfanyie
uchunguzi wa kina na kesho
asubuhi uniletee ripoti
nyumbani” akasema Peniela
“Peniela nini hasa
unachotaka tukichunguze kwa
huyo Melanie Davis? Akauliza
Peterson
“Kila kitu kuhusu maisha
yake.Ametokea wapi,wazazi
wake,anakoishi hapa
Paris,anafanya biashara gani
na ziko wapi,akaunti zake za
benki,marafiki zake ni akina
nani wanafanya nini
n.k.Nataka kujua kila kitu
mnachoweza kukipata kuhusu
Melanie”akasema Peniela
“Sawa mama Peniela.Hiyo
ni kazi ndogo sana
kwetu.Kesho saa kumi na mbili
za asubuhi nitakugongea
mlango kukupa ripoti”
akasema Peterson na kuagana
na Peniela
“Ngoja niwatumie hawa
wapelelezi wa kujitegemea
kumchunguza
Melanie.Mathew amenistua
sana kuniambia kwamba
anashirikiana na magaidi wa
IS.Lakini Melanie ni
mwanamke mwenye uzuri wa
kipekee kabisa kwa nini
anashirikiana na magaidi wa
IS?Kinachoniumiza zaidi ni
kwamba anajificha nyuma ya
biashara nilizomuuzia
kutekeleza mambo
yake.Mathew aliniambia
kwamba amekuwa akipokea
kiasi kikubwa cha fedha
kutoka IS.Yawezekana ni fedha
hizo hizo ndizo ambazo
alizitumia kununulia kampuni
nilizomuuzia.Imeniuma sana
na ninajiona mjinga.Niliona
aibu kubwa mbele ya Mathew
aliponiuliza sababu ya kuuza
mali zetu kwa mtu
anayeshirikiana na magaidi.”
akawaza Peniela na sura ya
Mathew ikamjia akaanza
kutiririkwa machozi
“Mathew amepitia mateso
makubwa sana kwani mwili
wake wote umejaa makovu ya
vidonda vilivyotokana na
mateso makali aliyokuwa
akiteswa.Kwa nini lakini
Mathew ameamua kuchagua
kuendelea kufanya kazi hii na
kuacha maisha mazuri
aliyokuwa akiishi?akajiuliza
Peniela
“Mathew amenifanya
niwachukie magaidi na watu
wanaowasaidia kama akina
Melanie kwani ndio
waliomfanya Mathew
ashindwe kutulia na kutumia
muda wake mwingi
akihangaika kupambana nao
hadi kufikia hatua hii ya
kutengana” akawaza Peniela
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom