Wakuu Ogah na Kuhani.
Naamini wote mko sahihi. Hakuna sheria inayomlazimisha mshitiri kumtumia msanifu wake original kwa ajili ya mabadiliko yoyote atakayotaka kufanya kwenye jengo lake. Anachotakiwa kufanya ni kutafuta msanifu aliyekuwa qualified ambayo kwa Tanzania ni aliyekuwa registered na AQRB na mwenye leseni hai. Huyu msanifu mpya kama kweli ni competent ataweza kuwasiliana na msanifu original kupata maoni yake hasa kama mabadiliko yanayotarajiwa ni makubwa. Hii hawajibiki kufanya maana kama Ogah alivyoeleza, msanifu original alitakiwa kukabidhi kumbukumbu zote zinazohusiana na jengo (working drawings, michoro na hesabu za wahandisi wote, michoro ya mabadiliko yote wakati wa ujenzi, minutes za vikao vyote vya usimamizi wa jengo n.k.) kwa mshitiri mara mradi unapoisha. Hizi zinatosha kutoa mwongozo kwa msanifu majengo yeyote anayeijua kazi yake. Kama tena alivyosema, Ogah, kuna design liability kwa msanifu original kwa hiyo katika kukwepa kumpa loop-hole hapo yatakapotokea matatizo baadae ( kwa kudai yamesababishwa na msanifu mpya), mshitiri anaweza kuamua kumpa tena kazi za mabadiliko katika jengo. Hawajibiki lakini ni kuwa prudent hasa kama aliridhika na kazi ya msanifu original.
Kuhani yuko sahihi kuwa kwa kuingiza kipengele hiki cha kudai msanifu original ilibidi ashirikishwe kunaingiza dosari katika ripoti ya tume. Bila shaka msanifu original alikuwemo kwenye tume na angependa kujitengenezea mazingira ya kuendelea kupata ulaji kutokana na miradi yake yote ya awali. Hapa aliteleza na tume ilionyesha udhaifu wake kwa ku-entertain hilo. Ni mapungufu lakini si lazima yafanye ripoti nzima iwe batili.
Haya ni mawazo yangu Fundi Mchundo. Nawaachia waliopasua vitabu zaidi yangu, yaani, wahandisi na wasanifu majengo, walete michango yao.
Amandla..........