Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 4,011
- 6,753
Ripoti ya Prof Mruma kuhusu Makinikia na kampuni ya Accacia, ilikuja na jibu kuwa "Accacia ni kampuni feki".
NANUKUU ( It is confirmed that Accacia Mining is Non-Existing entity in Tanzania)
SOMA PIA:
Pamoja na mambo mengine, katika matokeo ya uchunguzi wake, kamati ilibaini kuwa Kampuni ya Migodi ya Acacia si halali na inafanya kazi nchini kinyume cha sheria kutokana na kutosajiliwa na Msajili wa Kampuni (Brela).
Profesa Osoro alisema licha ya kutosajiliwa, kampuni hiyo pia haina hati ya utambuzi (certificate of compliance) kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni, Sura ya 212.
“Kamati pia imebaini kuwa Kampuni ya Acacia Mining Plc, ambayo inajinasibisha kuwa mmiliki wa makampuni ya Bulyanhulu Gold Mines Ltd, North Mara Gold Mine Ltd na Pangea Minerals Ltd, haikuwahi kuwasilisha nyaraka wala taarifa yoyote kuonesha kuwa kampuni hiyo ni mmiliki wa makampuni hayo wala kuwa na hisa katika makampuni hayo.
“Kwa kuwa Acacia Mining Plc haina usajili wala utambuzi wa kisheria nchini Tanzania, haina sifa ya kupata leseni, kuchimba wala kufanya biashara ya madini nchini Tanzania,” alisema Profesa Osoro.
Inachekesha na kufikirisha, NA HAIINGII AKILINI PIA, Ndiyo haiingii akilini kwani NSSF/GEPF, Benki, Halmashauri, TRA na maeneo mengine walipataje huduma bila ya kuwa na nyaraka muhimu?
na hakukuwa na mtu wa kuhoji, hata Prof alionekana akipigiwa simu na maswahiba zake anamwambia Mkuu.
Mama yetu KIPENZI alikuwepo pale na ripoti alikabidhiwa pia.
Since then baada ya JPM kufariki kumekuwa na maelezo mengi kuhusu hilo Saga la makinikia to the extent hata wengine kusema kuwa ripoti ni ya mchongo.
Where is Prof Mruma, Ni wakati nadhani wa hii ngoma kurudishwa mezani, kuona kama Prof alifanya kwa usahihi na kwa nini hatua za kuwachukulia waliofanya Kanjanja kama alivyoagiza JIWE hazijafanyiwa kazi mpaka ssa, au Professa alifanya kwa MAELEKEZO??
UDANGANYIFU USAFIRISHAJI WA MAKINIKIA
Aidha, kamati ilibainisha udanganyifu katika uuzaji na usafirishaji wa makinikia nje ya nchi ambako husafirishwa kwa madai ya kwenda kuchenjuliwa, lakini ukweli ni kwamba husafirishwa ikiwa tayari imeshauzwa.
Kamati pia ilibainisha kuwa kampuni za Bulyanhulu na Pangea ndizo wazalishaji na wauzaji wa makinikia nje ya nchi.
“Kwa mujibu wa mikataba ya mauzo ya makinikia baina ya makampuni hayo na wafanyabiashara kutoka nje ya nchi, makinikia husafirishwa kutoka Tanzania yakiwa yameshauzwa na hupelekwa nje ya nchi kwa madai ya kwenda kuchenjuliwa kupitia bandari za Dar es Salaam na Tanga.
“Makinikia hayo hupelekwa nchi za China, Japan na Ujerumani, yakiwa kwenye makontena yenye urefu wa futi 20 na wastani wa tani 20 kila moja. Wafanyabiashara wa makinikia ni makampuni yaitwayo Aurubis AG na Aurubis Bulgaria ADM, Mark Rich Co. Investment AG na Pan Pacific Copper Co. Limited kutoka nchi za Ujerumani, Uswisi na Australia,” alisema Profesa Osoro.
Alisema mauzo hayo ya makininkia hufanywa kwa mujibu wa mikataba ya uchimbaji wa madini kati ya Serikali na makampuni ya uchimbaji madini ambapo kutokana na taarifa za kiuchunguzi kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mauzo ya makininkia hufanyika kupitia Ofisi ya Uhasibu ya makampuni hayo iliyopo Afrika Kusini.
“Kamati imebaini kwamba kifungu cha 51 cha Sheria ya Madini kinaruhusu mwenye leseni ya uchimbaji wa madini kufanya biashara ya madini, ikiwa ni pamoja na kuuza nje ya nchi.
“Kifungu hicho kinamtaka mwenye leseni ya uchimbaji kupata kibali cha kusafirisha madini kutoka kwa ofisa mwenye mamlaka atayethibitisha kwamba mrabaha stahiki umelipwa kwa Serikali.
“Mbali ya kupata kibali kinachoonesha malipo ya mrabaha, hakuna utaratibu mwingine maalumu katika biashara ya uuzaji na usafirishaji wa makinikia nje ya nchi. Aidha, kisheria makampuni ya madini yanapaswa kutoa taarifa sahihi kwa Serikali kuhusu aina, kiasi na thamani ya madini yaliyomo ili kuiwezesha Serikali kukokotoa na kutoza mrabaha stahiki,” alisema.
UDANGANYIFU WA WATUMISHI SERIKALINI
Akizungumzia ushiriki wa watumishi katika udanganyifu wa kutoa taarifa za uongo na kusaidia kampuni za madini kukwepa kodi, Profesa Osoro alisema wamelisababishi taifa hasara.
“Kwa kuzingatia nyaraka na taarifa mbalimbali za kiuchunguzi, kamati imeridhika kuwa baadhi ya watumishi wa Serikali, watumishi na wamiliki wa kampuni za madini, kampuni za usafirishaji na upimaji wa madini na kampuni zenyewe, zimetenda makosa mbalimbali ya kijinai, yakiwamo ukwepaji wa kodi, kutoa taarifa za uongo, kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu, uhujumu uchumi,” alisema.
Alisema kutokana na hatua hiyo, imelisababishia taifa hasara kinyume cha vifungu vya 18, 114 na 115 vya Sheria ya Madini ya 2010, vifungu vya 101 na 106 vya sheria ya kodi ya mapato, 2004 vifungu vya 79 na 82 vya Sheria ya Usimamizi wa Kodi, 2015 na kifungu cha 24 cha Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika sekta ya Madini Tanzania, 2015 kifungu cha 27 cha Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumi sura ya 200 na kifungu cha 203 cha Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, 2004.
UKWEPAJI WA KODI YA MAPATO
Akizungumzia ukwepaji kodi, Profesa Osoro alisema kamati pia ilibaini mauzo ya makinikia kwa wafanyabiashara na wachenjuaji nje ya nchi hayakufanyika kwa ushindani kutokana na kuonyesha vipindi virefu vya uhusiano wa kibiashara kwa kuzingatia nyaraka za mikataba baina yao.
Alisema masharti ya usafirishaji wa makinikia yalionyesha yanatakiwa kusafirishwa bure badala ya gharama za usafirishaji na mzigo au gharama ya bima na mzigo ambapo makinikia hayo yaliuzwa kwa wafanyabiashara wale wale na wachenjuaji wale wale wenye mahusiano ya kibiashara kama ilivyoonyeshwa katika mikataba ya mauzo ya makinikia baina yao.
“Madini yaliyouzwa nje ya nchi hayakuwa makinikia hasa, badala yake yalikuwa ni madini ya aina mbalimbali mahususi yaliyopatikana kutokana na uchenjuaji,” alisema.
Aidha, katika upandishaji wa gharama za uendeshaji migodi uchunguzi wa kisayansi wa mifumo ya kompyuta kupitia TRA, ulibaini kuwa gharama za utafutaji na upembuzi wa miamba yenye madini imejumuishwa kwenye gharama za mauzo na kwa sababu hiyo, kuathiri faida halisi ambayo ilipaswa
kutozwa kodi.
THAMANI YA MADINI KATIKA MAKONTENA
Pamoja na mambo mengine, Profesa Osoro alisema uchunguzi wa kamati ulibaini kuwapo takwimu mbalimbali za idadi ya makontena yaliyosafirishwa nje ya nchi kuanzia mwaka 1998 hadi Machi mwaka huu.
Alisema kamati iliamua kutumia takwimu kutoka Idara ya Forodha na Ushuru wa Bidhaa (TRA) kwa kuwa moja ya majukumu ya idara hiyo ni kukusanya takwimu za bidhaa zote zinazosafirishwa nje ya nchi kupitia bandari, viwanja vya ndege na mipaka ya nchi.
“Kutokana na chanzo hicho, idadi ya makontena yaliyosafirishwa yalikuwa 44,277 kwa kiwango cha chini na makontena 61,320 kwa kiwango cha juu kutoka kwenye vyanzo vyetu vya uchunguzi,” alisema.
VIWANGO VYA DHAHABU KATIKA MAKINIKIA
Aidha, viwango vya dhahabu vilivyobainishwa kwenye kamati ni wastani wa kilo 28 za dhahabu katika kila kontena.
“Kwa kutumia kiasi hiki cha dhahabu kwenye kila kontena katika makontena 44,277 yatakuwa na dhahabu kiasi cha tani 1,240, kiasi hiki kina thamani ya Sh trilioni 108.06 sawa na Dola bilioni 49.12.
Kwa kutumia kiwango cha juu cha dhahabu kwa kontena moja, kiasi cha dhahabu katika makontena 44,277 kitakuwa tani 2,103 ambazo thamani yake ni Sh trilioni 183.32 sawa na Dola bilioni 83.32,” alisema.
Hata hivyo, alibainisha thamani ya madini yote katika makontena 61,320 yaliyosafirishwa nje ya nchi katika kipindi kati ya 1998 na 2017 kwa kutumia kiwango cha wastani ni Sh trilioni 183.597 sawa na Dola bilioni 83.45.
“Jumla ya thamani ya madini katika makontena 61,320 yaliyosafirishwa nje ya nchi kati ya 1998 na 2017, kwa kutumia kiwango cha juu ni Sh trilioni 380.499 sawa na Dola bilioni 144.77,” alibainisha.
MAPATO YALIYOPOTEA
Kamati pia katika uchunguzi wake ilibainisha upotevu wa kodi kati ya mwaka 1998 hadi mwaka huu ambayo Serikali ilipoteza ni Sh trilioni 108.46, ambazo ni sawa na bajeti inayokaribia miaka mitatu.
“Kiasi hicho ni kwa kiwango cha chini ambapo robo ya fedha hizo zingetosha kujenga reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza,” alisema.