MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,002
- 64,641
Pentagon wamepeleka ripoti yao ya mwaka 2020 kwenye bunge la Marekani kuhusu nguvu ya kijeshi ya taifa la Uchina.
Uchambuzi huo umezungumzia ukuaji wa kasi wa nguvu ya kijeshi ya taifa la Uchina tokea mwaka 2000 hadi 2020: Kuna mambo ambayo yameshangaza wataalamu wengi wa Marekani kwasababu wengi hawakutegemea kama yangetokea hivi karibuni tena kwa taifa ambalo miaka 70 nyuma lilikuwa ni masikini sana.
Ukisoma kurasa za mwanzo kabisa imethibitika kwamba taifa la Uchina ndiyo taifa lenye jeshi kubwa la majini kuliko Marekani, ambapo Uchina ana meli zisizopungua 350 (Ukijumlisha manowari za vita na nyambizi) huku Marekani akiwa ana meli zisizopungua 293 (Ukijumlisha manowari za vita na nyambizi).
Ikumbukwe tangu vita ya dunia iishe Marekani ndiyo taifa lilikokuwa na jeshi kubwa sana la majini ambapo hadi kufika mwaka 1985 alikuwa ana meli zisizopungua 600 kule bahari ya Pasifiki, hasahasa ukanda wa Mashariki ya mbali.
Upande mwingine ripoti inasema Uchina ana makombora aina ya (Ground Launched Ballistic Missiles) na (Ground Launched Conventional Missiles) zaidi ya 1,250 yenye kufika umbali wa kilomita 500 hadi 5,500.
Huku Marekani akiwa ana makombora aina ya (Ground Launched Ballistic Missiles) pekee yenye kufika umbali wa kilomita 70 hadi 300. Sambamba na hili Uchina ndiyo taifa lenye mfumo mkubwa na ulio bora wa makombora ya kujihami dhidi ya mashambulio ya angani (Surface to Air Missiles) ambapo wanasema mfumo huo umejumuisha mifumo ya kisasa ya Urusi aina ya S-300 na S-400.
Miaka sita nyuma niliwahi kusoma jarida moja likisema kwamba hadi kufika mwaka 2020 Uchina atakuwa na meli nyingi kuliko Marekani wengi walipinga na kusema kwamba hata kama Uchina atakuwa na meli nyingi basi haziwezi kuwa za kisasa kama za Marekani.
Hata kwenye hii ripoti naona bado wanasema kwamba Uchina ana manowari za kubebea ndege (Air-Craft Carrier) moja tu huku Marekani akiwa nazo kumi. Lakini nadhani hili halitasaidia kwasababu tofauti kabisa na Marekani, mkakati wa ulinzi wa Uchina uko tofauti kabisa.
Mpaka sasa sehemu nyeti kwa Uchina ni eneo la Bahari ya Uchina Kusini (South China Sea) ambako kuna visiwa anavyogombania na nchi kama Ufilipino, Vietnam, Malaysia na Brunei.
Na eneo la Bahari ya Uchina Mashariki (East China Sea) ambako kuna Taiwan ambayo Uchina anasema ni sehemu yake, pia na visiwa vya Diaoyu/Senkaku ambavyo wanagombania na Japani.
Kwasasa haya ndiyo maeneo nyeti sana kwa ulinzi wa Uchina, tofauti na Marekani ambaye maeneo yake nyeti kiulinzi ni kama Bara lote la Marekani (Western Hemisphere), Ulaya (Europe), Ghuba ya Uajemi (Persian Gulf) na Mashariki ya mbali/Ukanda wa Pasifiki (South-East Asia).
KWANINI UCHINA ANAWEKEZA SANA KWENYE JESHI LA MAJINI ???
Kwa hii nguvu aliyonayo Uchina sasa, kama siku ataamua kutanua misuli kwenye lile eneo au hata kuvamia Taiwan kijeshi sidhani kama Marekani na NATO watakuwa na uwezo wa kufanya lolote kumzuia Uchina.
Mwaka 1996 (Third aiwan Strait Crisis) Uchina chini ya JIANG ZEMIN walipewa somo gumu sana na Marekani pale alipotaka kuwafanyia fujo Taiwani kwa kuanza kulipua bandari zao.
Uchina alifyatua makombora na kupeleka manowari zake za kivita, lakini bahati mbaya uongozi wa Bill Clinton ulijibu mapigo kwa kupeleka manowari mbili kubwa za kubebea ndege (Aircraft Carriers) pamoja na meli kubwa za vita kule eneo la Pasifiki ili kumtishia Uchina kwamba hawezi kuvamia Taiwan kijeshi.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani wa wakati huo William Perry alimuita moja ya maafisa wa Ulinzi wa Uchina (Liu Huaqui) kumwambia kama wakiendelea hivyo basi watapata madhara makubwa sana kwamba "there would be grave consequences".
Uchina alidhalilika na alijifunza somo gumu sana kwamba kama akiendelea kuwa kwenye hali ile basi kile alichofanyiwa na Muingereza mwaka 1839 (The Opium Wars) au alichofanyiwa na Japan mwaka 1931 (The Invasion) of Manchuria kinaweza kujirudia.
Ukimsikiliza Raisi wa Uchina XI JINPING aliwahi kusema dhahiri kwamba Uchina lilikuwa taifa kubwa sana ambalo lilidhalilishwa na mataifa ya Magharibi hivyo hawatakubali tena.
Chama Cha Kikomunisti kimewekeza rasilimali nyingi sana kwenye mambo ya Ulinzi na wakiwa wazi kabisa kwamba adui yao mkubwa ni Marekani.
KUHUSU UHUSIANO BAINA YA TANZANIA NA UCHINA:
Ukisoma hii ripoti kuna sehemu wanasema Uchina anataka kutumia maeneo kama Tanzania, Pakistan, Sri-Lanka na Kenya kuwekeza kambi kubwa za kijeshi ili kupambana na Marekani.
Ina maana ile bandari ya Bagamoyo mbali na kuwa na faida za kiraia na kiuchumi ingekuwa na manufaa kiulinzi pia: Huu mkakati Chama Cha Kikomunisti kimeuita THE MILITARY-CIVIL FUSION STRATEGY, ambapo miundombinu ya kijeshi inaweza kutumika kwenye shughuli za kiraia za kiuchumi, pia vivyo hivyo kwa miundombinu ya kiraia (Dual Use).
Lakini ukisoma mwishoni kabisa mwa Ripoti utagundua kwamba jeshi la Uchina limekuwa likifanya mazoezi na mataifa mbalimbali dunia, ili kutekeleza mkakati wa Chama Cha Kikomunisti unaotaka hadi kufika mwaka 2049 Uchina liwe taifa lenye nguvu kuweza kupambana popote duniani huku likiwa na nguvu kubwa ya ushawishi kwenye siasa za dunia.
Katika mazoezi hayo ni nchi mbili tu za Afrika zilihusika mwaka 2019, Afrika Kusini na Tanzania. Huku jina la Mazoezi na Tanzania yakiitwa SINCERE PARTNERS-2019. Sasa kama hili ni jambo zuri au baya kwa Tanzania mimi binafsi sifahamu.
Ripoti: https://media.defense.gov/2020/Sep/...020-DOD-CHINA-MILITARY-POWER-REPORT-FINAL.PDF