Ripoti ya Benki ya Dunia: Tanzania ina uchumi unaokua kwa kasi kuliko nchi yoyote Afrika Mashariki

Watanzania tuchukue tahadhari kubwa dhidi ya PPPs

Miradi ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi - Public – Private Partnerships (PPPs) imeendelea kuchukua sehemu kubwa sana ya uwekezaji wa sekta ya miundo mbinu. Tunapozungumzia Miundo mbinu, ni pamoja na ile ya mawasiliano (telecommunications), nishati, bandari, barabara, reli, maji nk. PPPs zimeendelea kupata umaarufu mkubwa kwa sababu zinawezesha ‘debt repayments’ za nchi zisionekane kwa urahisi kwa wananchi na hata kwa wawakilishi wao bungeni. Miongoni mwa PPP schemes maarufu ni pamoja na “The Private Finance Initiative” ya Uingereza na nyinginezo.

Taasisi za aina hii zinasaidia sekta binafsi kutoka mataifa makubwa kuwekeza katika nchi maskini lakini kwa masharti kwamba serikali za nchi maskini zitoe ‘guarantee’ ya malipo kwa wawekezaji bila ya kujalisha hali ya uchumi itageuka vipi baade. Pia serikali za nchi maskini hutakiwa kujifunga (commit) ‘to bail out the private operator’ kama biashara itakwenda kombo. Kwa namna hii, PPPs zinakuwa na athari ile ile kwenye fiscal system ya nchi kama ilivyo kwa mikopo kwa sababu kimsingi serikali bado inakopa moja kwa moja, lakini tofauti na mikopo mingine, ‘payment obligations’ za serikali under PPP projects huwa hazionyeshwi kwenye takwimu za deni la nje la taifa.

Miradi ya PPP kwa kawaida hugharimu zaidi serikali kuliko ambavyo serikali ingeamua kukopesha yenyewe kutoka vyanzo vingine na kuwekeza katika miradi hiyo hiyo kwa mfano ujenzi wa miundo mbinu nk. Hii ni kwa sababu mikopo hii inatoka kwenye sekta binafsi, na vyanzo vya aina hii vya mikopo huwa na gharama kubwa; ukiachilia gharama zinazohusiana na viwango vya riba, pia private contractors huwa wanahitaji faida kubwa sana na vile vile ‘negotiations’ mara nyingi huwa zinapendelea sekta binafsi kuliko serikali husika.

Kwa mujibu wa utafiti wa Griffiths et al (2014), [“Financing for development post 2015: Improving the contribution of Private Finance”]:

“PPPs are the most expensive way for governments to finance infrastructure, ultimately costing more than double the amount than if the investment had been financed with bank loans or bond issuance”.

Katika hili, Mchumi Maximilien QueyRanne kutoka dawati la “Fiscal Affairs” la Mfuko wa kimataifa wa fedha (IMF), anaongeza kwamba:

“the fiscal risks of PPPs are potentially large because they can be used to move spending off budget and bypass spending controls and move debt off balance sheet and create contingent and future liabilities. They also reduce budget flexibility in the long term.”

World Bank pia kupitia utafiti wake huru hivi karibuni (World Bank’s independent evaluation Group) ilibaini kwamba kati ya miradi 442 ya PPP iliyo chini ya uangalizi wake, tathmini ya athari za miradi hii katika kutokomeza umaskini ilifanyika kwenye miradi tisa tu (sawa na 2%). Vile vile, tathmini juu ya ‘fiscal impact’ ya miradi hii ya PPP ilifanyika kwenye miradi 12 tu (sawa na 13%). Pamoja na haya yote, cha ajabu ni kwamba ‘debt payment obligations’ zinazotokana na miradi ya PPP bado huwa haipo covered katika ‘Debt Sustainability assessments’ zinazofanywa na World Bank/IMF. Maana yake ni kwamba, uhalisia juu ya obligations za malipo ya mbeleni ni kiasi kikubwa zaidi cha fedha za walipa kodi kuliko kile kinachowasilishwa kwenye ‘Debt Sustainability assessments.’

Tanzania, Deni la Nje na Public - Private Partnerships (PPPs)

Mikopo ya nje kwa mwaka 2013 (ilikuwa ni takribani TZS trilioni 3.5) na ilihusisha miradi miwili ya PPP. Leo hii, Serikali ya Tanzania ina ‘three hidden obligations’ zilizotokana na mikataba ya nyuma ya PPP. Miradi hii ni ya Umeme ambayo ilikua implemented kwa ajili ya kuiuzia serikali (Tanesco) umeme ‘at a pre-determined price’, ambayo ni guaranteed na serikali ya Tanzania (Kodi za wananchi). Mradi wa kwanza ulikuwa ni IPTL, na mradi wa Pili uliofuatia ukawa ni ule wa Songas.

Kwa mujibu wa mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG) mwaka 2007/2008, miradi hii miwili ilikuwa inaigharimu Tanesco 90% ya mapato yake na kufanya Tanesco kulemewa na mzigo mkubwa wa purchase agreements ambazo hazikuzingatia Public Procurement ACT pamoja na regulations zake. Lakini kama vile hiyo haitoshi, bado serikali ya ikaingia mkataba na Kampuni nyingine ya Richmond/Symbion/Dowans mwaka (2007/2007).

Kutokana na kulemewa na miradi hii ya kinyonyaji, mwaka 2009 Tanesco ililazimika kuongeza ‘tarrifs’ kwa 40%, lakini bado shirika hili likaendelea kujiendesha kwa hasara. Kwa mujibu wa ripoti ya IMF (2013), ruzuku ya serikali kwa tanesco iligharimu serikali 10% ya fedha za walipa kodi, na sehemu kubwa ya fedha hizi zilienda kulipia ‘inflated costs’ za miradi hii ya PPP ya uzalishaji wa umeme. Kwa maana hii, ruzuku ya serikali (10% ya kodi za wananchi kila mwezi) ilikuwa ni ruzuku kwa makampuni binafsi yaliyowekeza kupitia PPPs, na sio ruzuku kwa walipa kodi, ambao ndio wanaostahili kufaidika na ruzuku husika. Kwa mfano, inasemekana kwamba malipo ya fedha za walipa kodi kwenda IPTL ni TZS bilioni nane kwa mwezi.

Juzi mtakuwa mlimsikia waziri Muhongo akieleza bungeni jinsi gani miradi ya IPTL, SONGAS na SYMBION isivyokuwa na tija kwa taifa. Tufahamu kwamba World Bank kupitia IFC ina hisa katika mradi wa Songas.

City Water ni moja ya miradi ya PPP ambayo kama isingekuwa kwa Lowassa wakati ule akiwa waziri wa maji kuvunja mkataba ule, walipa kodi nchini wangebebeshwa mzigo mkubwa sana na usio wa lazima. Uamuzi wa Lowassa uliudhi wengi serikalini, lakini uliokoa fedha nyingi kwa maslahi ya wengi zaidi.

Serikali ya JPM imenuia kuhamasisha miradi ya aina hii katika miundo mbinu, ujenzi wa uchumi wa viwanda, nk. Ni mapema kujua kwa uhakika ni jinsi gani Serikali ya JPM itatetea maslahi ya wananchi katika miradi ya aina hii.

Siku nyingine tutaangalia athari za PPPs sekta kwa sekta.

cc Nguruvi3, Kobello
 
Nishauri tu kwamba tupokee ripoti hizi critically rather than passively. Ni dhahiri kwamba hapa tunaandaliwa kuuziwa mkopo. The World Bank core business is to sell loans. Kama huniamini, tizama kitakachofuata baada ya ripoti hii kuzinduliwa.

Walipotoa ripoti kuhusu tourism (The Elephant in the Room: Unlocking the Potential of the Tourism Industry for Tanzanians), kilichofuata tulichukua mkopo. Walipotoa ripoti kuhusu bandari (Opening the Gates: How the port of Dar es Salaam Can Transform Tanzania ), kilichofuata tulichukua mkopo kuboresha bandari ya Dar es Salaam. Sasa wamekuja na ripoti hii (The Road Less Travelled - Unleashing Public Private Partnerships in Tanzania). Kitakachofuata tutachukua mkopo.

Uandishi wa hizi ripoti unafanana: Unlocking the potential of tourism industry, Opening the gates, The Road Less Travelled. Ripoti hizi huandikwa kimkakati ili kutega wakopaji wachukue mkopo. Ripoti zinalenga kuonesha wakopaji kwa nini wachukue mkopo kwa jina la utafiti. Ukiwa mfanyakazi wa the Bank, hiyo ndiyo kazi yako ya kila siku - produce 'knowledge' that will enable selling of loans. Kimsingi, hizi ripoti si tafiti bali ni tools za kuuzia mikopo.

Kama unataka kujifunza zaidi jinsi the Bank inavyozalisha "knowledge", look for this book. Imperial Nature: The World Bank and Struggles for Social Justice in the Age of Globalization by Michael Goldman. See particularly Chapter III: Producing Green Science inside Headquarters.

swadakta kiongozi na kubaliana na wewe.
 
Alafu watu muwe mnatumia ubongo mlopewa vyema heko JPM zinatoka wapi hapo? Alafu hakuna cha kupongeza zaidi ya hasara,title iko wazi "The road less travelled" hapa cha kupongezana ni kipi? Inatakiwa kutumia report hiyo kujitathmini ili tufanye vyema.Kama Ivory Coast wameweza kukuza uchumi kwa kutegemea kilimo kwa nini tushindwe? Kama tumeshindwa tukaige na kujifunza mbinu zao
Mkuu tatizo siasa mbele utendakazi nyuma tu ....
Hivi ikifika kipindi cha uchaguzi, tukahamasishana kila mwenye umri wa kufanya kazi akatafuta shamba na kupanda miti 10 ya mbao, after ten years akavuna hiyo miti - mbona tutaanza kupeleka mbao nje ya nchi?
Huu ni mfano mdogo tu, yapo mambo mengi ya kufanya mwananchi kama mwananchi badala ya kuendelea kulalama mitandaoni. Wanasiasa kama ambavyo tumeona kwa miaka mingi hawana nia ya dhati kumkomboa mwenye kipato cha chini. Wao kama wao daima wanataka kutengeneza economic and social gapes kati yatu na wao.
 
Nishauri tu kwamba tupokee ripoti hizi critically rather than passively. Ni dhahiri kwamba hapa tunaandaliwa kuuziwa mkopo. The World Bank core business is to sell loans. Kama huniamini, tizama kitakachofuata baada ya ripoti hii kuzinduliwa.

Walipotoa ripoti kuhusu tourism (The Elephant in the Room: Unlocking the Potential of the Tourism Industry for Tanzanians), kilichofuata tulichukua mkopo. Walipotoa ripoti kuhusu bandari (Opening the Gates: How the port of Dar es Salaam Can Transform Tanzania ), kilichofuata tulichukua mkopo kuboresha bandari ya Dar es Salaam. Sasa wamekuja na ripoti hii (The Road Less Travelled - Unleashing Public Private Partnerships in Tanzania). Kitakachofuata tutachukua mkopo.

Uandishi wa hizi ripoti unafanana: Unlocking the potential of tourism industry, Opening the gates, The Road Less Travelled. Ripoti hizi huandikwa kimkakati ili kutega wakopaji wachukue mkopo. Ripoti zinalenga kuonesha wakopaji kwa nini wachukue mkopo kwa jina la utafiti. Ukiwa mfanyakazi wa the Bank, hiyo ndiyo kazi yako ya kila siku - produce 'knowledge' that will enable selling of loans. Kimsingi, hizi ripoti si tafiti bali ni tools za kuuzia mikopo.

Kama unataka kujifunza zaidi jinsi the Bank inavyozalisha "knowledge", look for this book. Imperial Nature: The World Bank and Struggles for Social Justice in the Age of Globalization by Michael Goldman. See particularly Chapter III: Producing Green Science inside Headquarters.
Vema sana. Umefanya vizuri kutuelimisha wanajamii, nchi nyingi duniani zinaishi kimkakati ikiwa ni pamoja na kupitia mashirika/taasisi za kimataifa. Ni vema sasa nasi kama Tanzania tukawa makini au wajanja zaidi siyo kila hongera au pendekezo ni jema. We must think and judge critically!
 
Ila ushiriki wa serikali usiwe wa kisiasa bali wa kitaalamu na kiutawala. Serikali inapoingiza siasa katika sekta binafsi inaongeza mianya ya rushwa
 
Alafu watu muwe mnatumia ubongo mlopewa vyema heko JPM zinatoka wapi hapo? Alafu hakuna cha kupongeza zaidi ya hasara,title iko wazi "The road less travelled" hapa cha kupongezana ni kipi? Inatakiwa kutumia report hiyo kujitathmini ili tufanye vyema.Kama Ivory Coast wameweza kukuza uchumi kwa kutegemea kilimo kwa nini tushindwe? Kama tumeshindwa tukaige na kujifunza mbinu zao
Nafikiria tu; hivi tungefunga macho tusitengeneze mabarabara angalau kwa mwaka mmoja tu na hizo trilioni 4 zikaenda kwenye kilimo tungekuwa wapi? mimi naona kama bado hatuna upeo au hatujapata wapangaji wa vipaumbele ambao ni wazalendo wa kweli. Hizo foleni si wahamishie mawizara Dodoma au wapangishe maofisi nje ya mji? kwani ni lazima kila asubuhi misururu ielekee down town na jioni ielekee viungani?
 
Back
Top Bottom