Ridhiwani Kikwete: Ndani ya kipindi cha miaka miwili, Serikali imeshawaajiri Maafisa Maendeleo ya Jamii zaidi ya 2140

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
539
756
SERIKALI YAONGEZA AJIRA KWA WATUMISHI WA USTAWI WA JAMII

WANANCHI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KULINDA MAADILI

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Ridhiwani Kikwete ameliambia Bunge kuwa ndani ya kipindi cha miaka miwili serikali imeshawaajiri Maafisa Maendeleo ya Jamii zaidi ya 2140, ikiwa ni kundi la kwanza la watumishi linalokwenda kuwezesha jamii kuwa pamoja kama jumuiya ya pamoja huku upande wa Maafisa wa Ustawi ya Jamii wakiwa ni 403 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 na kwa mwaka wa fedha 2024/2025 tayari kibali cha kuajiri Maafisa Ustawi wa jamii 472 kimetolewa ambao wanakwenda kusimamia na kupambana na janga la mmomonyoko wa maadili katika jamii ya watanzania.

Mhe.Kikwete ameyabainisha hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Sophia Mwakagenda aliyetaka kujua serikali inampango gani wakuongeza kuajiri watumishi wa Ustawi wa Jamii.

#KaziInaendelea
 
Back
Top Bottom