Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 526
- 748
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema mfumo wa usaili kwa njia ya kidigitali utapunguza gharama kwa kiasi kikubwa kwa wasailiwa wa ajira tofauti na hapo awali ambapo watu walilazimika kusafiri hadi Jijini Dodoma kwa ajili wa usaili wa ajira.
Kikwete ameyasema hayo leo katika uzinduzi wa usaili kidigitali baada ya kutembelea kituo cha usaili kidigitali Jijini Dar es Salaam na kufafanua kuwa serikali itaendelea kuboresha mfumo huo ikiwemo kuongeza vituo vya usaili nchini ili kila mtu mwenye sifa aweze kupata ajira
Nao baadhi ya wasailiwa waliojitokeza katika kituo hicho wameishukuru serikali kwa kuanzisha mfumo huo na kuongeza kuwa sasa wamepunguziwa gharama ikiwemo chakula, nauli na malazi pindi wanapotakiwa kwenda kwenye usaili wa ajira Jijini Dodoma.
#KaziInaendelea
Pia soma: Usaili kada za Serikali kufanyika Dodoma ni kipengele. Mfumo ubadilishwe