Hute
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,537
- 6,471
mbona kipindi cha kikwete mambo yalikuwa yanaenda safi tu, si waombe ushauri jaamaa alikuwa anaendeshaje nchi? kwanini tumewapa hawa watu nchi?Akihojiwa na mwandishi wa Gazeti la Mwananchi,toleo la tarehe 18/2/2017.
Ridhiwani anakiri kwamba kilio kikubwa cha wabunge ni kucheleweshwa (sema kutopelekwa) kwa fedha za maendeleo.
Anasema miradi mingi imekwama,na kwamba akiuliza serikali ni anaambiwa "MAKUSANYO HAYAJAKAA VIZURi"
Nadhani sasa ni wakati muafaka kwa serikali kutuambia hali ya makusanyo ya TRA na uwezo wa nchi kuhimili bills zake.
Hawa watu wamekuwa wakijigamba kwamba serikali ni tajiri na ina mahela mengi,huku pembeni wanawaambia wabunge kuwa hali ya makusanyo si nzuri.
Bora tuqmbiane mapema tujua kwamba mwaka huu hakuna kupanda madaraja,hakuna uhamisho,kodi zitaongezeka,na miradi ya maendeleo haitafanyika.
Zile barabara za maghorofa hakuna,badala yake inajengwa ya lusekelo,
Ni wakati wa kuambiana ukweli sasa