SHADOWANGEL
JF-Expert Member
- Sep 15, 2014
- 528
- 349
Ivi atujifunzi BBC redio ukisikiliza vipindi hadi raha... Ukija bongo mpaka unaisi waweke miziki tuu
KILA MTU ANAWEZA KUWA MTANGAZAJI,LAKINI SI KILA MTU ANAWEZA KUWA MTANGAZAJI MZURIUtAngazaji ni kipaji
Nimekuelewa sana. Gud point braza.Hao wamiliki wa hizo radio station wanaangalia cheap labour jamani . Wewe ukiajiriwa pale na PHD yako utakubali ulipwe laki 4 kwa mwezi au ndio utaleta sheria zako za kisomi.Hao wasiosoma hawana hata muda wa kujua haki zao kama wafanyakazi so ilimaradi wanapata salary end of the month kwao wameridhika.
h
Hata huku kwenye kazi zetu wapo sana watu wanaoajiriwa bila kufit qualifications za ajira husika ili mradi tu wamlipe mshahara mdogo ili wao wapate faida zaidi kuliko kuajiri professionals katika fani husika.
Na yawezekana pia kuwa hata Wasikilizaji wake nao ( akina sisi ) hatuna TAALUMA na ni wa " hovyo hovyo "
natune DW bon NA BBC alfajir,mchana na jion after that na off redio .maana redio nyngne ni majanga mfano redio standard fm pale singida ni pumba tupu jamani hata kusikiliza ni aibu mbele z watu maana unawez kuonekana na wew unayesikilza ni mwehu ...
Kina Misanya Bingi, Masoud Masoud mko wapi siku hizi?UtAngazaji ni kipaji
Na yawezekana pia kuwa hata Wasikilizaji wake nao ( akina sisi ) hatuna TAALUMA na ni wa " hovyo hovyo "
Na yawezekana pia kuwa hata Wasikilizaji wake nao ( akina sisi ) hatuna TAALUMA na ni wa " hovyo hovyo "
Kuna sababu nyingi, na zote zina mchango tofauti tofauti kwa hizi redio kuwa kama zilivyo leo. Zifuatazo ni baadhi
1. Redio ili iweze kujiendesha inahitaji matangazo, na ili ipate matangazo inabidi iwe inasikilizwa, na ili isikilizwe inabidi ivutie, na ili ivutie inahitaji kuwa na watangazaji ama vipindi vinavyovutia. Sasa, si kila wakati 'mvuto' wa mtangazaji utaambatana na elimu. Kuna watangazaji wanaovutia ila hawana elimu, kuna watangazaji wana elimu ila hawana mvuto kwa wasikilizaji. Ni mara chache sana utampata mtangazaji mwenye mvuto na akawa pia na elimu nzuri. Mfano mzuri ni RTD. Hawa wengi wao walikua na taaluma ila hawana mvuto ndio maana humu ndani wengi wetu tukiulizwa ni lini mara ya mwisho kusikiliza RTD tutajikuta tunajibu ni mwaka 1999! Pia, si lazima kila mtangazaji awe na elimu, ndio maana kuna vipindi vya aina mbali mbali. Mfano, huwezi kumpa mtangazaji mbumbumbu hata kama ana mvuto kiasi gani aende kuchukua ama kuripoti ama kufanya mahojiano katika mikutano muhimu ama ya kimataifa! Ila unaweza kumtuma mtangazaji mbumbumbu mtaani kwa masela akahoji, akaripoti etc.
2.Cheap labour: Radio ni biashara. Kama unaweza kupata usikilizwaji kwa mvuto wa mtanagazaji cheap, why employ the dearer na madigrii yake? Na uzoefu unaonesha kuwa wasio na elimu, hata malipo yao si makubwa ndio maana wanakua wengi katika radio za fm.
3. Market segment: Wakati mwingi, watu hupenda kuwa karibu ama kuwasikiliza wale wanaofanana nao, ama wenye viashiria vya kufanana nao. Ukiwa na masela, watapendelea mtangazaji msela n.k. Ukiwa na serious people, watapendelea serious people. So, majority ya wasikiliza radio ni vijana age ya '15 - 35' ambao pia wengi ya hao elimu na uelewa wao ni huo huo usio wa juu sana. Na katika jamii, hata leo, ingia barabarani ama katika mikutaniko mingi, angalia wenye 'ear phones' ni akina nani na fuatilia wanasikiliza nini! I can assure you, majority watakua vijana wa hiyo age bracket na watakua wanasikiliza miziki ama radio hizo hizo za fm! mara chache utakuta wanasikiliza taarifa za utafiti ama taarifa makini!
4. Kutokuiva kwa wasomi. Wasomi wenye digrii zao za habari hawana ile kuiamini ama mvuto unaotakikana katika soko la leo. Matokeo yake mtu anakuja ana elimu kubwa, anataka mshahara mkubwa ila soko la redio halitaki kumsikiliza. Na soko ni vijana hawa ama wasikilizaji hawa hawa wanaolalamika hapa.
Ndefu, ila ndio ukweli wenyewe!
Ni kweli kabisa mkuu.Baadhi ya studio utadhani ni vijiwe vya mipasho na kupiga domo.
Kiongozi! Kila kipindi kina maudhui yake. Kila maudhui yana wasikilizaji wake.Ni kweli kabisa mkuu.Baadhi ya studio utadhani ni vijiwe vya mipasho na kupiga domo.