ipyax
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 4,178
- 6,542
Investment ya nyumba return yake ni ya muda mrefu, usitarajie pesa yako uliowekeza itarudi mapema halafu uanze kula faida. Hata mashirika kama nsssf hayo maghorofa wanajenga ya bei mbaya huwa wanapiga hesabu za mbali sana kwenye return ya investment na kuanza kula profit.Kupangisha si inachukua muda mrefu kurudisha pea?
Nina rafiki yangu yupo mombasa bado kijana tu ila anamiliki nyumba saba ambazo zimekamilika na zote zimejaa wapangaji. Kwa mwezi anakusanya kama m5 ya tz Kwa sababu rent ipo Chini na pia viwanja na gharama za ujenzi zipo Chini sio kama Nairobi.
Nimejifunza kitu kimoja kwake kuwa sekta ya nyumba ni stress free business na pesa yake haina msimu, pia kila siku watu wana hamia mijini na watahitaji makazi. Kwa kile kidogo ulichonacho utaweza anza taratibu. Kama wewe ni mfanyabiashara biashara usimege pesa yako ya mtaji kujenga nyumba kwani utafilisika bali tumia pesa ambayo haita athiri biashara yako kabisa kujengea.