Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,685
- 1,235
RC SINGIDA AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI MILIONI MOJA NA NUSU WILAYA YA IKUNGI
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Peter Serukamba amezindua kampeni ya upandaji miti Milioni moja na nusu (1,500,000) katika Wilaya ya Ikungi.
Katika uzinduzi wa kupanda miti Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu ameshiriki kampeni ya upandaji miti kiwilaya iliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu (Mb) alipopata nafasi ya kusalimia wananchi waliojitokeza kwenye Kata ya Issuna aliwaambia wapande miti na kuitunza kwani miti ni kivutio cha Mvua na tukipata Mvua ya kutosha tutapata mavuno mengi hivyo kuwa ma usalama wa Chakula kwenye Wilaya, Mkoa hadi Taifa.
Aidha, Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu (Mb) alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Peter Serukamba kwa kuja kutuzindulia kampeni kwenye Wilaya yenye lengo la kupanda miti 4500 na siku hiyo walipanda miti 1500.
Wengine walishiriki uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry Cornel Muro.