Sijui nani ametufunza au katika somo la Uchumi sijaona chapter au hata statement yoyote inayosema ili Uchumi ukue lazima muombe Mungu, sio kwamba napuuza uwepo wa Mungu wetu, la harsha, ni kwamba kama tunafanya mambo ambayo sio sawa, Uchumi kukua haihusiani na kukesha na kupiga makelele eti kumuomba Mungu, ni vitu viwili tofauti, nadhani hata Mungu wetu anatushangaa, maana watu wake wamekosa maarifa na Mwenyezi Mungu anasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, usikute ndio kuangamia huku.

Uchumi haukui kwa kukesha kwa maombi au kunena kwa lugha za uongo uongo, naona kama tunakwenda njia tofauti..!!
IMEANDIKWA!
👇👇
Mathayo 6:5-8
5 Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.

6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.

8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.

وَاسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ
وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى الْخَاشِعِينَ

[ AL - BAQARA - 45 ]
Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kusali; na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu,
 
Sina uhakika kama una ushahidi wa hayo maovu unayo yaongelea hapa,

Ila kitendo cha kusema Anajuta ni dalili ya mtu kutambua makosa yake na kua mwema,mtu muovu hua hajuti bali huendeleza uovu wake.
Ila wewe ndiyo una ushahidi! Ushauri wangu kwako acha kudhulumu haki za kuishi za wenzako na kudhulumu mali zao,
Asikuongopee mtu, mtu muovu anaishi na majuto hadi siku ya kufa kwake na ataondoka nayo na hawezi kuacha ukatili wake licha ya kwamba ana majuto moyoni mwake kwa sababu huyo tayari anakuwa ni mtumwa na mfuasi mtiifu wa shetani.
 
Katika kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanzania, mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda pamoja na Viongozi wa dini wameitumia siku hii kufanya maombezi ya kuliombea taifa pamoja na mkoa wa Arusha, wananchi wamejitokeza kwa wingi.
View attachment 3172868
Soma, Pia: Paul Makonda: Tutakachofanya Tarehe 9 Disemba jijini Arusha hata wakisema ni uchawi poa tu

Masahihisho kwenye Andiko, Tanzania haijawahi kutawaliwa na wakoloni hivyo Tanzania haikupata uhuru Toka Kwa wakoloni.
Nchi iliyopata uhuru ni Tanganyika .
Leo tunakumbukizi ya uhuru wa Tanganyika Toka Kwa waingereza.
 
Ila wewe ndiyo una ushahidi! Ushauri wangu kwako acha kudhukumu haki za kuishi za wenzako na kudhulumu mali zao,
Asikuongopee mtu, mtu muovu anaishi na majuto hadi siku ya kufa kwake na ataondoka nayo na hawezi kuacha ukatili wake licha ya kwamba ana majuto moyoni mwake kwa sababu huyo tayari anakuwa ni mtumwa na mfuasi mtiifu wa shetani.
Jifunze kusoma na kuelewa kwanza kabla hujaamua kujibu jambo lolote lile,

Ni wapi mimi nimesema nina ushahidi? nimemdhulumu nani? nimemdhulumu nini?

Kumbe nilikua najadili na katoto ka elfu mbili.
 
Jifunze kusoma na kuelewa kwanza kabla hujaamua kujibu jambo lolote lile,

Ni wapi mimi nimesema nina ushahidi? nimemdhulumu nani? nimemdhulumu nini?

Kumbe nilikua najadili na katoto ka elfu mbili.
Wewe ni yule unayejifanya kumtetea,acha kutubabaisha hapa.
Huwezi kunifikia hata kidogo usijidanganye.
 
Tunaishi kiroho kwelikweli wabongo, ndio maana wasabato masalia walitaka kwenda kueneza injili kwa mataifa sugu yasiyoamini na yasiyo ya kiroho wakasahau dini hizo zilitokea hukohuko :D :D :D :D

Maisha yetu ni kuwaza miujiza tu, na zisipokuwepo hizi dini maana ya maisha inapotea kabisa, maana tunaishi ili tufe tukaishi tena mbinguni na firdaus :D:D:D:D

Na wapigaji wote wanacheza na beat hiyohiyo yani kama huyu mwanasanaa wa chuga
 
Back
Top Bottom