Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,103
2,633
"Tutalala mpaka chini kumuomba Mungu"

Waumini wa dini mbalimbali wa dini ya kikisto wameendelea kuomba dua kwaajili ya kuifungua Tanzania katika nyanja mbalimbali.

Waumini hao kila mmoja alikuwa ananena kwa lugha yake.

 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amefanya tukio kubwa na la aina yake mkoani humo la kuwakutanisha viongozi mbalimbali wa dini na kufanya maombi ya pamoja kwaajili ya kuuombea mkoa huo pamoja na Taifa.

Maombi hayo yalianza kwa matembezi ya amani kutoka Round About ya Impala hadi mnara wa saa.
 
Na ukimuona mtu anajifanya katili na asiyekuwa na hofu ya Mungu ujue huyo ni mwema?

Acha wivu na kukariri.

Mwovu atabaki kuwa mwovu na mtu mwema atabaki kuwa mwema bila kujali maigizo au mwonekano wa nje
Mtu mwema hana haja ya kujibaraguza.
 
Sijui nani ametufunza au katika somo la Uchumi sijaona chapter au hata statement yoyote inayosema ili Uchumi ukue lazima muombe Mungu, sio kwamba napuuza uwepo wa Mungu wetu, la harsha, ni kwamba kama tunafanya mambo ambayo sio sawa, Uchumi kukua haihusiani na kukesha na kupiga makelele eti kumuomba Mungu, ni vitu viwili tofauti, nadhani hata Mungu wetu anatushangaa, maana watu wake wamekosa maarifa na Mwenyezi Mungu anasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, usikute ndio kuangamia huku.

Uchumi haukui kwa kukesha kwa maombi au kunena kwa lugha za uongo uongo, naona kama tunakwenda njia tofauti..!!
 
Anaangaika sana ili aonekane ni mtu mwema,mnyenyekevu na mwenye huruma lakini moyoni mwake lazima atakuwa anateseka kwa maovu aliyoyafanya dhidi ya wengine,anajuta.
Sina uhakika kama una ushahidi wa hayo maovu unayo yaongelea hapa,

Ila kitendo cha kusema Anajuta ni dalili ya mtu kutambua makosa yake na kua mwema,mtu muovu hua hajuti bali huendeleza uovu wake.
 
Back
Top Bottom