RC Makonda atengua uamuzi wa DC wa Ilala

Kuna watu wanajua kuwatia watu ubaya, si dhani Kama Bi Mjema aliishia hapo au alisema hivyo from no where.

Hivi karibuni makanisa yakilokole yameanzisha tabia ya kufanya ibada zao katikati ya wiki mpaka saa sita usiku wakifungulia mziki mkubwa na ukichunguza ndani utakuta wapo waumini wawili au watatu.

Mfano mzuri wale wakazi wa Salasala A Kuna Nabii mmoja anajiita Flora.

Hebu mleta uzi tupe taarifa kamili kabla hatujamchamba mtu kwa uonevu

Katafute video ya DC utajua kama alikosea ama alikua sahihi ila kiufupi alimaanisha watu waache kusali katikati ya wiki wafanye kazi.
 
UMCHE BWANA MUNGU WAKO
Na sasa, Israeli, Bwana, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche Bwana, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote; Kumbukumbu la torati19:12
Umewahi tafakari ili kujua Mungu anachotaka kwako? Ama shida gani na wewe? Alikuumba ili iweje? Mwanzo wako ni. Kuzaliwa mwisho wako ni kifo.
Mungu aliyekuumba ndiye mwanzo na mwisho wa uhai wako, maana Yeye ndiye Alpha na omega. Huyu alpha na Omega lipo jambo analitaka kwako. Anataka kuabudiwa, anataka umwabudu, anataka ushuke miguuni pake, anataka uimimine roho yako kwa imani, umche Bwana, uliinue 'na kulibariki jina lake.
Anataka uende katika njia zake, wala usikengeuke, hataki upotee, 'na mapito yako yatabarikiwa, Bwana atakuonyesha njia utakayoiendea, 'na jicho lake litakutaazama(Zab 32:8) kamwe hatakuacha. Inuka sasa umtumikie Mungu wako, kwa moyo wako wote, 'na kwa roho yako yote. Mungu akubariki katika jina Yesu Amen.
Mtumishi wa Mungu Clemence Mwandambo 0755068357/0653068357


Katika hili Makonda yuko sahihi
 
haka ka mkuu wa wilaya kamekuja juzi na kacheo ka kupewa ndio anajifanya kudharau katiba ya nchi,huna adabu.
 
Halafu hakuna pahali kwenye biblia pameandikwa siku ya kusali ni ipi mimi siku yangu ikifika kama ni j3 naenda kusali so sioni tatizo.

Makonda yupo sahihi kwa ili uhuru wa kuabudu uzingatiwe.

Naona sasa ivi akili zimeanza kumkaa vizuri hakuna haja ya kuwekeana vizuizi vya kufanya tutakacho.

Hapana mm nakataa hili la RC, naunga mkono alichosema DC Sophia Mjema
 
Mleta mada ,mada yako ingepata wachangiaji wengi ungeweka heading nzuri mfano Mkuu wa mkoa atengua kauli ya mkuu wa wilaya kuhusu siku za kuabudu.Au omba moderators wabadilishe au post upya .Kichwa ulichoweka hakina mvuto kwa wachangiaji
Kwa hisani ya Kigogo 2014
 
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Bi. Sophia Mjema amepiga marufuku shughuli zote za ibada ambazo zinafanyika katikati ya juma. Hivyo shughuli za ibada zitakuwa Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. Kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa atakayesali katikati ya wiki.

Hata hivyo
RC Paul Makonda ametengua agizo la DC wa Ilala, Sofia Mjema aliyepiga marufuku ibada kufanyika katikati ya wiki, akisema ibada ni Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. RC amesema wananchi waendelee na ibada bila kuvunja sheria, huku akiwasihi viongozi kuwa makini kwenye masuala ya dini.

Tena kwa kuwa mimi ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, ibada nazitaka sana kuliko sehemu yeyote ile, kwa sababu huko ndiyo uzima ulipo.
Asante Makonda huyu mama aliona atoke vipi jamani manake yule wa Mbeya ndio kashika usukani tumsamehe bure wapendwa
 
UMCHE BWANA MUNGU WAKO
Na sasa, Israeli, Bwana, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche Bwana, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote; Kumbukumbu la torati19:12
Umewahi tafakari ili kujua Mungu anachotaka kwako? Ama shida gani na wewe? Alikuumba ili iweje? Mwanzo wako ni. Kuzaliwa mwisho wako ni kifo.
Mungu aliyekuumba ndiye mwanzo na mwisho wa uhai wako, maana Yeye ndiye Alpha na omega. Huyu alpha na Omega lipo jambo analitaka kwako. Anataka kuabudiwa, anataka umwabudu, anataka ushuke miguuni pake, anataka uimimine roho yako kwa imani, umche Bwana, uliinue 'na kulibariki jina lake.
Anataka uende katika njia zake, wala usikengeuke, hataki upotee, 'na mapito yako yatabarikiwa, Bwana atakuonyesha njia utakayoiendea, 'na jicho lake litakutaazama(Zab 32:8) kamwe hatakuacha. Inuka sasa umtumikie Mungu wako, kwa moyo wako wote, 'na kwa roho yako yote. Mungu akubariki katika jina Yesu Amen.
Mtumishi wa Mungu Clemence Mwandambo 0755068357/0653068357


Katika hili Makonda yuko sahihi
Amen mtumishi..
Naunga mkono hoja..Katika hili baba Keegan yuko vizuri
 
Mleta mada ,mada yako ingepata wachangiaji wengi ungeweka heading nzuri mfano Mkuu wa mkoa atengua kauli ya mkuu wa wilaya kuhusu siku za kuabudu.Au omba moderators wabadilishe au post upya .Kichwa ulichoweka hakina mvuto kwa wachangiaji
Kwn ni kipi hujaelewa mpka a post upya??humfaham RC makonda??
 
Mungu aliagiza watu wafanye kazi ili wale sasa wakishinda Makanisani ni Misikitini muda wote watafanyakazi saa ngapi?
Mbona wanashinda kusali na unawaona hawafi. Walishakuja kwako au kuiomba serikali au huyo Sofia Mjema pesa ya kula? Wewe mtu unamwona kila siku anasali kaoga,katakata na kashiba sadaka na sadaka anatoa hushangai? Angekuwa Hana kipato SI angeshakufa siku nyingi kwa utapiamlo au kukosa chakula

Wewe pambana na Hali yako maisha ya wengine waachie wenyewe hasa yanayohusu Imani.Usijifanye unayajua kuliko wenyewe
 
Mungu aliagiza watu wafanye kazi ili wale sasa wakishinda Makanisani ni Misikitini muda wote watafanyakazi saa ngapi?
Wewe utakuwa maskini lofa.Si kila mtu anashinda kazini Kuna matajiri Wana majumba ya kupangisha,wengine Wana bodaboda kibao ,daladala kibao Kazi yao kusubiri tu hesabu jioni au pesa za Kodi za mwaka kwenye akaunti zao .Unataka wafanye Kazi gani zaidi ya kusali kutwa huku wakisubiria hesabu za pesa zao jioni ziingie.Si kila mtu ni kibarua serikalini au kwa muhindi Kama wewe
 
DC ningemuunga mkono angegusia pia misikiti inayopigia watu kelele asubuhi, mchana na jioni eti kuwakumbusha watu kuswali, hapo ningemuunga mkono
Ila tangazo lae lilionekana kama kuwalenga Wakristo walokole, sipendagi Walokole ila wana afadhali kuliko Waislam,
Waislam wakiwa wengi watataka kila mtu awe Muislam na mfumo wetu wote wa maisha kuanzia kwenye siasa hadi maisha binafsi iwe kama mtume wao alivyoagiza, ndio maana naona walokole wana afadhali mara 10,
 
Sawa, lakini kama kwa sababu ya ibada hawafanyi kazi na hivyo kufanya maisha yao kuwa magumu ni vema wakaelimishwa kuwa mahitaji ya msingi hayatakuja kwa maombi kwa sababi maombi hayajawahi kuwa mbadala wa wajibu.
Watu waombe kila siku bila kukoma lakini pia wafanye kazi kwa bidii kila siku. Kufanya kazi kwa siku sita na kupumzika siku ya Sabato ni amri ya Mungu. Haina mjadala!
RC Makonda yuko sahihi...... Ibada ni wakati na siku yoyote.
 
Back
Top Bottom