Raymond Mndolwa: Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeajiri Watumishi 320 kwa ajili ya kusimamia miradi ya umwagiliaji Nchini

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
347
551
IMG-20240430-WA0024(2).jpg

Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw, Raymond Mndolwa amesema miradi mingi ya Umwagiliaji inatekelezwa kwa kipindi cha miezi 18, hivyo kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wa skimu zinazoendelea kujengwa katika kipindi cha mwaka 2022/2023 – 2023/2024 kutaongeza eneo la Umwagiliaji kufikia Hekta 983,465.46 sawa na asilimia 81.9 na kufanya eneo la Umwagiliaji kufikia Hekta 1,200,000 ifikapo mwaka 2025 ambapo pia kutaongeza ajira 1,352,127.

Ameyasema hayo jijini Dodoma jana, wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba ya ujenzi na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa miradi ya umwagiliaji.
IMG-20240430-WA0035.jpg

Aidha Bw, Mndolwa amesema Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imefanikiwa kununua vitendea kazi kwa ajili ya watumishi wa Tume ikiwemo magari (48), mitambo 15 na magari makubwa (heavy trucks) 17 kwa ajili ya usimamizi, ufuatiliaji na ujenzi wa miradi ya umwagiliaji.
IMG-20240430-WA0036.jpg

Aidha, Tume imefungua ofisi 121 za Wilaya za Umwagiliaji na kuajiri Watumishi 320 kwa ajili ya kusimamia miradi ya umwagiliaji katika ngazi ya Mikoa na Wilaya.
 
Back
Top Bottom