Ray Kigosi ashangaa kusikia kuwa alikuwa anabebwa na Kanumba

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
18,469
28,315
Imeibuka sintofahamu baada ya Ray kuongea kwamba anashangaa sana watu kusema kuwa alikuwa anabebwa na Kanumba wakati ukweli ni kwamba yeye ndio alimtoa Kanumba, kiufupi Kanumba amepitia kwenye mikono yake.

Watu wengi wamebisha kauli hizo ila kwa upande wangu Ray yupo sahihi sana, tatizo ni kwamba Vijana wa Instagram wengi ni watoto wa 2005 ni Wabishi hatari, halafu hawajui Historia.

Kwa umri, Ray ni mkubwa kuliko Kanumba, hata ukiangalia Filamu zao utagundua hili. Ray ndio mtu wa kwanza kuingia Kaole na Alikuwa wa Kwanza pia kuonekana kwenye TV.

Kanumba ameenda Kaole akamkuta Ray Tayari ni Fundi. Hivyo Ray akawa mmoja wa Walimu wake. Kanumba amefuzu akawekwa kwenye series ambayo Ray Tayari alikuwa anaigiza na ni Maarufu.

Kilichokuja kutokea ni kwamba Kanumba akawa Na Upepo wake, Kiufupi Kanumba Hakuwahi kumzidi Ray kwa kukubalika, bali kila mmoja alikuwa na Watu wake, kulikuwa na Watu wanamkubali Ray huku wengine wakimkubali Kanumba.

Je Nini maoni Yako???

1688153129686.jpg
 
Ila Kanumba Alivyofariki Ndipo akapata Umaarufu na Sifa zaidi, ingetokea hata Ray amefariki kabla ya Kanumba basi sifa zote za Kanumba angesifiwa yeye.

Kiufupi watu hawa walikuwa Wanajua na haitakuja kutokea Ushindani Mkubwa kama wa Ray na Kanumba, Kidogo Seba na J Plus walileta Ushindani lakini bado sana.

Ray amepotea BAADA YA KIFO CHA KANUMBA MAANA HANA TENA MSHINDANI. HATA LEO HII ALIKIBA NA HARMONIZE WAKIFA DIAMOND HATASIKIKA KAMA ZAMANI MAANA WASHINDANI WAKE HAWAPO.
(CC: Hopetyga)

Toa maoni yako
 
Back
Top Bottom