Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,733
- 5,749
Kama CCM wenyewe wamekubali kuwa sasa hivi katiba ni hitaji la kitaifa na huu ndio wakati muafaka basi sasa ndio wakati wa kuweka mambo sawa.
Tuna bunge kibogoyo linalotafuna pesa za walipa kodi na huku wananchi wakiwa na maisha magumu.
Hatusikii bunge likifanya kazi yake kama bunge ya kuisimamia serikali na kutetea wananchi.
Tozo za ajabu zinapitishwa. Sheria za ajabu zinapitishwa huku wao wakilipana pesa lukuki na kuchangia hoja za hovyo.
Rasimu ya warioba ilipendekeza kuwa tutakuwa na mamlaka ya wananchi majimboni kuweka kikao na kupiga kura kukataa wabunge tuliowachagua na kuonyesha wanachezea kodi zetu wakiwa bungeni. Sasa ndio wakati wa rasimu hii kupita na kuwa katiba ili wananchi tuwe na sauti.