Naona umejibiwa - Hata hivyo niongeze tu.
Watanzania tuliheshimu sana bendera na tukasahau utaifa. Enzi hizo ilikuwa ndra kukuta bendera ndogo au kubwa kwenye ofisi yoyote isipokuwa ya serikali. Watu wanapojivunia utaifa, huvaa alama za bendera ya taifa lao kama skafu, kitambaa kichwani na kushonea kwenye mashati nk. na hii haimaanishi dharau kwa namna yoyote ile.
Tunahitaji tujivunie utaifa wetu na kuutangaza.
Wach masihara jomba, Inamaana hata underpants za bendera za USA or Brasil hujaziona Mkuu? Plz hebu "Chapa kazi" bana achana na hizi porojo!!!
Kwa wale wenye macho makali na upembuzi wa picha za TV na za mnato mtakuwa mmetupia macho maeneo maarufu mawili hapa nchini. La kwanza ni kwenye njia za ndani ya ukumbi wa Bunge toka milangoni kuja mpaka kwenye eneo la Spika. Hapa kuna zulia ambalo limetengenezwa makusudi kufuata rangi za bendera ya Tanzania kwenye fito zake.
Sehemu ya pili ni uwanja wa ndege wa JNIA (Dsm) wakati ambapo anakuja kiongozi wa nje kwenye ziara ya kitaifa. Hapo huwa linatandazwa zulia jekundu lenye fito za rangi za bendera ya taifa pembeni pia.
Ninavyoamini na kufahamu ni kwamba bendera ndiyo kitambulisho kikuu cha nchi yoyote duniani na kwa utaratibu wa kistaarabu haipaswi kugusa ardhi "deliberately, accidentally or permanently". Ndiyo maana hata wakati inashushwa huwa askari anayeishusha anahakikisha haivuki hata usawa wa magoti yake kuelekea ardhini.
Je, ni busara gani kama si dharau kuruhusu watu bila kujali wadhifa gani wanao kuikanyaga bendera ambayo ndiyo sura ya taifa aidha wanapoteremka kwenye ndege au wanapoingia na kutoka Bungeni?
Na hayo ni moja katika mabadiliko mema aliyoyafanya JMK.
Bendera si msahafu ni nembo tu. Watu wanaswaga na kuwarubuni watu waandamane wakakanyagwe kanyagwe itakuwa hizo rangi za bendera.
Hata kama sio bendera, je mnaona nchi nyingine zikifanya kitu kama hichi?
Mimi naiheshimu bendera ya Manchester United FC kuliko bendera ya taifa.