Random acts of kindness

Dah hilo tukio limeni-inspire sana. Wapo binadamu wachache sana ambao wanatamani dunia hii iwe sehemu nzuri ya kuishi na wewe Nyani Ngabu ni mmoja wapo japokuwa sikufahamu kwa kina.
Shukran katheeran mkuu.

Yaani kwa mfano ningekuwa na uwezo, ningewachukua watoto wote walio yatima na kuwatunza.

Basi tu sina huo uwezo.

Matendo ya wema hunigusa sana, na haijalishi ni tendo kubwa kiasi gani.

Kile kitendo cha mtu tu kuamua kutenda wema kwa mtu asiyemjua kwangu linasema mengi sana.

Wema bado upo hapa duniani.
 
Moja kati ya vitu vinavyonipa raha na faraja moyoni ni kutenda jambo la kustukiza kwa mtu nisiyemjua na jambo hilo likaleta tabasamu kwenye sura iliyochoka na kukuta tamaa. Inaweza kuwa keep change ya msimbazi kwa kununua karanga ya 100. Giving lift kwa mtu aliyekata tamaa ya kupata usafiri nk
 
Sawa kabisa.
 
Hivi jirani we ishawahi kukutokea hiyo?

Jirani kuna anonymous alinipa envelope yenye $$ iliyotosha bills za mwezi mzima plus house payment. Xmas present. Nilitoa macho mpaka leo sijamjua aisee! Mbaya zaidi na alienipa akagoma kumtaja.
Hadi keshooo I want to know that somebody maana alifunga kurasa ya surprises zangu!

Ktk restaurants stores mmmh, not a dime!
 
Pay it forward mkuu

Yes, indeed.

It's a very simple concept.

Someone does something nice to you and instead of paying them back by doing something nice to them you 'pay it forward' by doing something nice to someone else preferably someone who needs some sort of help on something.

Just a way of inspiring one another to be kind and help each other.

When I first brought it up, per usual, some folks thought I was 'stunting'. They missed the whole point.

Stunting about Bojangles? Imagine that hahahahahaaa......
 
You've got to do it now
 
Nyani ngabu unahakika zile Tabia za Mombasa hakuna huko?? Inalipiwa unafurahia..Hahaaa nawaza tu bhana..maana we unajua huko wanaruhusu hayo mambo..:D:D:p
 
Yes, indeed.

It's a very simple concept.

Someone does something nice to you and instead of paying them back by doing something nice to them you 'pay it forward' by doing something nice to someone else preferably someone who needs some sort of help on something.

Just a way of inspiring one another to be kind and help each other.

When I first brought it up, per usual, some folks thought I was 'stunting'. They missed the whole point.

Stunting about Bojangles? Imagine that hahahahahaaa......

Bojangles!!!
 
Mara nyingi nimekuwa ni admaya kiingereza chako kwa uzi huu nimejua kumbe mwenzetu ni dayaspora hongera sana
 
Heri ya 2017 JF massive.

Dakika chache tu zilizopita kuna jambo jema/ zuri limenitokea.

Nimeamka na njaa ikabidi niwashe gari niende Bojangles kununua staftahi.

Kufika hapo nikaamua kutokushuka kwenye gari hivyo nikatumia drive-thru window.

Nika place order yangu kwenye ubao wa menu. Sasa mbele yangu alikuwepo mtu mwingine kwenye gari lake aliyekuwa anachukua na kulipia order yake hapo dirishani.

Alipomaliza na kuondoka nami nikasogea hapo dirishani ili kulipia na kuchukua nilichoagiza.

Ile natoa debit card yangu kulipia yule mhudumu wa hapo dirishani akanambia kuwa yule mtu aliyekuwepo mbele yangu keshalipia hiyo order yangu. Hivyo akanikabidhi tu hicho nilichoagiza.

Nikapigwa na butwaa la furaha. Furaha si kwa sababu ya kusevu hela ambayo ningetumia bali furaha ya kile kitendo cha yule mtu ambaye simjui na yeye hanijui.

Mtu mwenyewe hata sikumwona anafananaje maana nilikuwa busy na simu yangu nikibishana na limtu huku JF.

Hicho kitendo chake kimenigusa sana. Na kusema ukweli si mara ya kwanza hilo jambo kunitokea. Limeshanitokea mara kadhaa huko siku za nyuma.

Ukarimu wa huyo mtu ambaye hata simjui umenipa hamasa nami nitende jambo kama hilo kwa mtu nisiyemjua. Sijui nitafanya lini na wapi lakini nami nitamlipia mtu order yake hivi karibuni bila hata ya yeye kujua.

Nitafanya hivyo kimya kimya na kusepa ili nami nimjaze mtu furaha hata kama ni kwa muda mfupi maana huwezi kujua hiyo furaha inaweza kuwa na athari gani kwa mtu.

Mtu anaweza akawa anapitia mengi na kitendo kama hicho chaweza kabisa kurudisha matumaini endapo mtu huyo atakuwa amekata tamaa kwenye jambo lolote lile linalomsibu.

Kwa kweli watu wema wapo hapa duniani. Na kilichonitokea mimi leo hii ni ithibati tosha kabisa.

Natamani sana walau ningepata hata sekunde moja ya kumshukuru huyo mtu lakini naamini mwenyewe wala hakutaka hayo. Katenda jambo la wema na akasepa zake.

Wooooow!!

Nothing is more touching than the kindness of total strangers!

Now I'm on my way to do that mannequin challenge but I'm also definitely going to do a random act of kindness to someone.

Hicho ndo nilichoagiza! Nothing major. Just a simple steak biscuit.

View attachment 452571

View attachment 452572

View attachment 452573
Hongera yako
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom