Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ili kupunguza gharama hatuwez pta shortcut
Katika ujenzi, ni vyema ukafuata hatua zote bila kuruka hatua yoyote maana kuja kurekebisha madhara yatakayojitokeza baadae unaweza ukajikuta unatumia gharama kubwa kuliko gharama za ile hatua uliyoiruka

Zipo hatua ambazo unaweza ukaziskip na zisikuletee shida kubwa lakini kwa ishu ya plaster kwenye kuta ni muhimu sana hasa ukizingatia tofali za sasa ni tofauti na tofali za miaka ya nyuma kiuimara. Ukiangalia tofali za majengo yaliyojengwa zamani utaona kuna vikokoto ndani yake, kiujumla tofali za zamani zilikuwa ni ngumu na imara mithili ya zege tofauti na hizi tofali za miaka hii.
 
Wapo wanaokwepa hatua ya skimming wakidhani kwamba wanapunguza gharama, mtu amemaliza kupiga ripu (plaster) halafu anapiga rangi. Ukuta ambao haujafanyiwa skimming, ukipaka rangi juu yake rangi nyingi inafyozwa na ukuta na hautakuwa na muonekano mzuri ukilinganisha na ukuta uliofanyiwa skimming kisha ukapakwa rangi
Mkuu ni material gani nzuri kwa skimming kati wall putt, gipsum powder na White cement
 
10mm hapana mkuu, sikushauri. Yote hayo watu wanayafanya ili kukwepa ama kupunguza gharama ambazo baadae inaweza ikakuingiza hasara zaidi.

Katika nyumba za kawaida, minimum size ya nondo kwa structure yoyote iwe ni nguzo, mkanda ama slab ni milimita 12.
sawa sawa na kufunga tatu tatu badala ya nne kweny slab na mkanda
 
sawa sawa na kufunga tatu tatu badala ya nne kweny slab na mkanda
Kufunga nondo tatu tatu kwa nyumba za kawaida haina shida kama unapandisha kozi tatu juu ya mkanda japo ukiweka nondo nne nne inakuwa vizuri zaidi

Kuna muda unakuta ukuta wa gable unapanda juu hata kwa kozi 6 na zaidi, sasa kwa kesi kama hii inabidi mkanda (hasa sehemu za madirisha na milango) uwe imara zaidi kuweza kubeba huo uzito uliopo juu yake
 
Katika ujenzi wa ghorofa unaweza ukawa umetumia nondo nyingi lakini kama ulikosea mpangilio wa nondo katika usukaji bado jengo lako litakuwa katika risk ya kudondoka

Katika usukaji nondo, kuna maeneo yanahitaji nondo chache, kuna maeneo mengine yanahitaji nondo nyingi na kuna maeneo mengine hayahitaji nondo kabisa mfano kama ulishawahi kutembelea site za ghorofa utaona katika slab nondo za juu huwa zinakatwa kati kati hivyo ni muhimu kushirikisha wataalam katika hatua muhimu kama hizi ili usije ukaingia hasara baadae

Ramani, makadirio au ushauri kuhusu ujenzi tuwasiliane
 
Katika ujenzi wa ghorofa unaweza ukawa umetumia nondo nyingi lakini kama ulikosea mpangilio wa nondo katika usukaji bado jengo lako litakuwa katika risk ya kudondoka

Katika usukaji nondo, kuna maeneo yanahitaji nondo chache, kuna maeneo mengine yanahitaji nondo nyingi na kuna maeneo mengine hayahitaji nondo kabisa mfano kama ulishawahi kutembelea site za ghorofa utaona katika slab nondo za juu huwa zinakatwa kati kati hivyo ni muhimu kushirikisha wataalam katika hatua muhimu kama hizi ili usije ukaingia hasara baadae

Ramani, makadirio au ushauri kuhusu ujenzi tuwasiliane
kwa nini zinakatwa kati kati?
 
kwa nini zinakatwa kati kati?
Katika slab huwa kuna force mbili, tension force na compression force. Zege ni nzuri zaidi katika kuzuia compression forces, huku nondo yenyewe ikiwa nzuri zaidi katika kuzuia tension forces (japo kuna muda zege ikishindwa kuzuia compression forces, huwa tunaiwekea/kuiongezea nondo pia)

Tension force inaact zaidi chini ya slab, na compression force inaact zaidi juu ya slab

Upande wa juu wa slab, kipande cha 1/3L cha kati tensile stress huwa ni ndogo kiasi kwamba huwa tunaweza tukaachana nayo (ndio maana nondo za juu katika hili eneo huwa tunazikata), lakini compression force ni kubwa ambapo yenyewe itakuwa inabebwa na zege

Upande wa chini wa slab, kipande cha 1/3L cha kati tensile stress huwa ni kubwa (ambapo maximum tensile stress hutokea kati kati ya slab) hivyo lazima nondo ziwekwe na ikibidi spacing ya nondo iwe ndogo kuliko spacing ya vipande vya 1/3L vya pembeni (kushoto na kulia)

NB. "L" ni urefu/upana wa slab kutokea katika nyuso za mkanda (beam)
 
Nimekuwa nikipokea ramani kutoka kwa watu mbali mbali kwa lengo la kuzifanyia makadirio, kitu ambacho huwa kinanishangaza ni kuona kitchen inakuwa na uwazi unaoangaliana na dining room mbali na milango inayotumika kuingia ama kutoka jikoni (mpaka hapo privacy kwa mpishi jikoni inakuwa hamna, watu wakiwa wamekaa dining wanamuona mtu akiwa yupo jikoni)

Hebu tuangalie kiusalama madhara ya hii design ni nini. Tukuchukulie kwamba una familia yenye watoto (watoto wa primary/secondary etc) na wewe huwa unatoka kwenda zako kazini. Watoto wamerudi kutoka shuleni, na wana access ya kuingia jikoni sehemu ambayo hatari ya moto inaweza kutokea muda wowote pindi uzembe utakapofanyika.

Kama mnavyojua akili za watoto, mtoto anaweza akawasha jiko baada ya muda akajisahau akapitiwa na usingizi au akaenda kucheza na wenzake nje, usalama wa nyumba yako mpaka hapo tayari unakuwa ni wa mashaka, ni Mungu tu ndio anakuwa anatulinda lakini siku yoyote linaweza likatokea la kutokea ukajikuta unapoteza nyumba hivi hivi japo hatuombei iwe hivyo. Kama mtu mzima tu na akili yake timamu anaweza akafanya uzembe kama huu kwa kupitiwa, vipi kwa watoto ambao akili zao bado hazijakomaa?

Jiko kama jiko linatakiwa liwe na milango ambayo ikifungwa hiyo milango kusiwe na access nyingine yoyote ya kuweza kuingia jikoni mpaka ufunguliwe mlango mmoja wapo, chakula kikiiva weka hotpot Dining mezani watoto wakirudi shule watakula bila kuingia jikoni. Fuatilia matukio mengi ya nyumba kuungua moto, utagundua matukio mengi yamesababishwa na uzembe jikoni hasa kwa watu wanaotumia majiko ya gesi na majiko ya umeme.

Mimi mtazamo wangu katika designing ni huo (safety first) na huwa namshauri mtu anapokuja na idea yake jinsi inavyotakiwa iwe (akitaka nidesign kama anavyotaka yeye, mimi huwa nadesign hivyo hivyo lakini najua tayari nimeshamshauri)
 
Ukienda hardware kununua tiles, hakikisha unachukua na box zako za akiba uziweke store, zitakusaidia kufanya matengenezo miaka ya mbele.

Kumbuka hiyo design ya tiles unayonunua sasa, pengine usiione tena baada ya miaka kadhaa mbele.

Sasa ikitokea labda unataka kufanya repair ya vipande vilivyopasuka na huku ndani kwako ukiwa huna akiba itabidi uchanganye design ya tiles tofauti kitu ambacho kinaharibu muonekano mzima wa nyumba

Kama umetumia tiles za size ndogo mfano 30x30 au 40x40, weka box chache tu kwa sababu zenyewe zinakaa pc nyingi ktk box..weka store hata box 3 zinatosha

Kama umetumia tiles za size kubwa mfano 50×50 au 60x60, weka box nyingi kwa sababu zenyewe zinakaa pc chache ktk box..weka store hata box 5 mpaka 7 maana tiles za size kubwa ni rahisi zaidi kukatika tofauti na tiles za size ndogo

Kama ulisahau kuweka tiles za akiba na huko hardware zilishatoweka sokoni, tafuta tiles za rangi nyingine zenye size sawa na tiles za mwanzo kisha chagua chumba kimoja ubandue baadhi ya vipande vya tiles kisha ubandike hizi tiles zingine ulizonunua (iwe kama lile draft wanalochezaga watu na kete).

Tiles utakazokuwa umebandua katika hicho chumba, zitumie kama spare katika sehemu zingine zinazohitaji marekebisho


Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu ujenzi tuwasiliane
 
Katika ujenzi, kuna nondo mbichi na nondo kavu, nondo zinazotakiwa kutumika ni nondo mbichi.

Nondo kavu utaijuaje?
Nondo kavu ukiikunja huwa inakatika kabla hata haijatengeneza nyuzi 90 kama inavyokatika fimbo ambayo imekauka.
Ni hatari kutumia nondo kavu katika ujenzi kwa sababu ikitokea mfano kuna shida aidha mzigo umezidi kiwango n.k, haitakuonesha sign yoyote kabla ya jengo kudondoka tofauti na nondo mbichi.

Jitahidi unapoenda hardware kununua nondo, nondo zako zote ziwe ni nondo mbichi. Nondo kavu zinaingia sokoni kimakosa, na utakuta zimechanganywa na nondo mbichi hivyo unatakiwa uzitest nondo zako zote, usije ukaridhika na kutest nondo moja tu na kupakia mzigo wako


Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kawaida bati zinazouzwaga hardware huwa zinakuwaga na urefu wa mita 3, hivyo kama urefu wa sehemu unayotaka kupaua unazidi mita 3 inabidi uunge na bati lingine.

Kwa upande wa nyumba za bati la kuficha, kama urefu unazidi mita 3 ni vyema ukatumia bati za kupima kutoka kiwandani, usiunge bati na bati.

Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane
 
Inachukua muda gani kumchorea mteja ramani yake...na wamkoani anapataje ramani yake iliyokamilika...na malipo yako unalipwaje..je ni baada ya kazi kukamilika au nusu kwa nusu..??
 
Inachukua muda gani kumchorea mteja ramani yake...na wamkoani anapataje ramani yake iliyokamilika...na malipo yako unalipwaje..je ni baada ya kazi kukamilika au nusu kwa nusu..??
Muda inategemea na ukubwa wa project, lakini pia kuna changamoto zingine kama kukatika kwa umeme n.k zinaweza pia kuchangia kuongezeka kwa muda.

Kama una ndg au jamaa yako huku dsm, namkabidhi anakutumia kwa basi. Malipo unaanza na advance
Tuwasiliane +255(0)624068809
 
Hii mvua kubwa iliyonyesha siku mbili tatu imeathiri makazi yako kwa kiasi gani? Na umechukua hatua gani kuhakikisha athari hazijirudii tena pindi mvua itakaporudi tena siku za usoni?

Kiujumla maji huwa hatushindani nayo kama wengi wanavyofanya, utayazuia kwa muda lakini baada ya muda yatakushinda nguvu

Maji huwa tunayatengenezea njia yake ya kupita na tunayacontrol kwa kuyatengenezea mteremko (slope) ili kuyaelekezea mahali/njia tunapotaka yapite
 
Fundi mahiri wa kupaua utamjua tu katika upigiliaji wake wa bati. Kwanza atapiga bati na nyundo (kwenye mfereji wa bati, valleys) ili kujua kama kuna mbao chini ya bati kabla ya kupigilia msumari lakini fundi mwingine atapigilia tu msumari kwa kukisia na akiona msumari umepitiliza, anautoa na kupigilia sehemu nyingine (wakati huo anakuwa ameshaacha tundu kwenye bati, mpaka aje amalize kupigilia bati zote tayari ameshakuachia matundu kama 100 na kidogo ambapo hasara yake inakuja tena kuharibu na gympsum board zako baada ya kuvujiwa na maji ya mvua)

Kama huna utaalam na masuala ya ujenzi, ni vyema ukatafuta msimamizi hasa katika hatua ambazo zikikosewa hasara yake inakuwa kubwa zaidi.

Utakwepa kumlipa mtu sh 30,000 lakini utakuja kuingia hasara ya laki 5 na ushehe. Kama huna ujuzi na kitu kinachofanyika, hata ukisimamia bado inakuwa usimamizi haujakamilika maana hata mafundi wakikosea huwezi jua kama wamekosea

Ramani, Makadiirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika ujenzi wa karo la choo/kisima, hakikisha kuta zake zinajengwa kwa kulaza tofali hata kama utatumia tofali za nchi 6. Wapo mafundi wanaojenga kuta kwa kuzisimamisha tofali ili wawahi kumaliza waondoke
 
Kawaida bati zinazouzwaga hardware huwa zinakuwaga na urefu wa mita 3, hivyo kama urefu wa sehemu unayotaka kupaua unazidi mita 3 inabidi uunge na bati lingine.

Kwa upande wa nyumba za bati la kuficha, kama urefu unazidi mita 3 ni vyema ukatumia bati za kupima kutoka kiwandani, usiunge bati na bati.

Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane
hivi fundi akikuambia nyumba hii inataka bati 70 hizi bati 70 hua kwa mita moja moja au mita tatu tatu?
 
hivi fundi akikuambia nyumba hii inataka bati 70 hizi bati 70 hua kwa mita moja moja au mita tatu tatu?
Hapo ni mita tatu tatu, kama atatumia kipimo cha mita atakuambia bati mita 210 (sawa na 70pcsx3m kwa bati za mita tatu tatu).

Lakini pia fundi mwingine anaweza akapima nyumba nzima then akakupa idadi ya bati kulingana na urefu wa sehemu tofauti tofauti mfano bati za mita 5 pc 20, bati za mita 4.5 pc 15, bati za mita 3.6 pc 35 n.k ili kupunguza wastage ya bati kwenye kukata kata ambapo ukitaka kununua utaenda kiwandani moja kwa moja (kule wanachaji kwa running meter, mfano labda Tsh.15,000/m so bati moja la mita 5 inakuwa tsh 75,000/=)
 
Back
Top Bottom