Rais Wangu Magufuli: Makonda Ulimtengeneza Alengwe - Wape Ushindi Wao...

Ngoja nikusome kwanza Mzee Mwanakijiji

Pia namba 0016 inakuwaga ya Female candidates, sasa wao wanadai ni ya Male. Na sitaacha kusema watu wanaojidai wamesoma na kusambaza uongo, hawajui hata kutunga uongo. Uongo hautungwi kukaa na kuropoka uongo ule uongo hadi kutetemesha na research inabidi ifanyike ya nguvu.

Makonda oyeeeee
Acha ujinga ww kama kulikua na wasichana wachache darasani bd itakua ya msichana?
 
Sisi kwa sasa tunasubiri ubuyu kwa Mange kuhusu makandokando na madudu mengine ya Rais!
 
Ukiangalia sakata la escrow mpaka kutumbuliwa kwa Tibaijuka JK akuwa amedhamiria kabisa. Lakini makelele yanapozidi kiongozi anafanya maamuzi ya kikundi ndio maana akatumbuliwa mkutanoni.

Kumwacha makonda au kumtumbua ni swala la raisi lakini kwa muda wote ambao atakuwa kazini ajue anabaki Kama ishara ya what is wrong na maamuzi ya serikari na hizo ni gharama anazobeba raisi na chama chake.

Sasa Kuna wenzake pia chamani je wapo kiroho safi kutembea na hayo madoa kipindi hiki cha ushindani na siasa za ushawishi kwa mambo ambayo Makonda anajitengenezea mwenyewe.
 
gwajima a.k.a N'GOLO KANTE ni mtu hatari nakumbuka pambano la kwanza bashite alilia kama mtoto pale KKKT,tunasubiri tena mzunguko wa pili tuone kante atakavyokichafua kwenye media
Wanajitakia kwani Gwajma alikuwa ameanza kuacha kujihami lakini makonda akaenda kumtafuta mwanamke ajidai kazaa na Gwajma ili amchafue ndipo Gwajma kaendelea kujihami cha ajabu wapo watu hawataki Gwajma ajihami ! Wanataka kuharalisha Udikteta wa makonda.
 
Mkuu kwa suala la vyeti la the so named Makonda halijakaa vizuri ila kwenye hoja yako unaonyesha kama is a none issue! Labda hujaelewa vizuri what transpired! Alifeli form four akachukua cheti cha aliyefaulu akaendelea kusomea! Kama wewe "pangu pakavu" unaamini is a none issue jaribu uone mamlaka zitakavyo kutolea macho.

Kuna current rulings nyingii as of recent watu wamehukumiwa kwa same issue jela including ya wiki iliyoisha ambapo mkunga aliyefanya kosa pacha na Bwana Bashite kahikumiwa miaka 35! au kuna watu wako above the law as per you mkuu? Nesi aliiba cheti cha mtu akasoma ukunga akafudhu na akafanya kazi kwa weledi na professionalism kama inavyotakiwa kosa ni kuiba cheti cha mtu cha form four tuu, these are absolutely twin issues! and kwa jinsi ya mahakama ni jinai! Why the double standards?

Kama hoja yako ni sahihi then tuangalie utendaji tuu wa watuhumiwa wa uizi wa vyeti na kama walikua wanafanya kazi vizuri warudishwe woote makazini na kesi zao za jinai zifutwe ili tuijenge nchi yetu.

Suala kwa wengi wetu hatuongei ili kukomoana kisiasa bali haki, kama kuna sheria ni vema kila mmoja wetu ahikumiwe kwa sheria hiyohiyo kusiwe na ndimi mbili!
Umeeleweka vyema sana Kiongozi; na mzizi wa hii issue ya Bashite ndio huo japo baadhi wanajifanya vipofu na viziwi hawataki kuelewa. Hakuna anayemwonea mtu wivu bali "haki iko wapi?"; kwanini wengine wanakuwa treated hivi na wengine vile? Why double standard? Wengine wako magerezani wanatumikia vifungo virefu huku wengine wanatanua mitaani tena kwa kodi za wananchi kwa kosa lile lile?
 
Huyu sio tu kupumzishwa ila anatakiwa awe jela kwa kutumia ofisi za umma kujinufaisha na kuleta taharuki kwenye jiji ambalo ni kitovu cha uchumi..

Lazima kuwe na double standards katika hili vinginevyo akina Masamaki waachwe waendelee na utumishi wao wa umma..

Tumeamua kudeal na kujinasibu serikali ya awamu ya tano ni hapa kazi tu sasa hii ndiyo hapa kazi tu?? Tuache unafiki sasa taifa liweze kuendelea...
 
Ukiangalia sakata la escrow mpaka kutumbuliwa kwa Tibaijuka JK akuwa amedhamiria kabisa. Lakini makelele yanapozidi kiongozi anafanya maamuzi ya kikundi ndio maana akatumbuliwa mkutanoni.

Kumwacha makonda au kumtumbua ni swala la raisi lakini kwa muda wote ambao atakuwa kazini ajue anabaki Kama ishara ya what is wrong na maamuzi ya serikari huo nao ni uamuzi wa raisi.
Uamzi gani huo wa kuziba masikio wakati makonda anafanya madudu? Maamuzi ya hivyo ni ya hovyo sana
 
Akina John Juma wote waliokuwepo serikalini wakifanya kazi wamefukuzwa wako mtaani, huyu John Juma wenu aliyevunja sheria kwa kuiba cheti cha mtu sheria inatengenezewa mazingira ya kuhalalishwa duh. Only in Tanzania
 
Naamini Magufuli ataziba masikio katika hili, whether Makonda is guilty or not, hatamtumbua. Sababu kubwa ni kuwa atawapa ushindi wale waliotajwa kujihusisha na ngada.

Kumbuka hii attack kwa Makonda ilianza mara tu baada ya kuanzisha vita dhidi ya wauzaji, wasambazaji na watumia ngada, na mkulu alimpa full support, leo imejulikana kuwa the guy is not clean. Yetu ni macho...

Acha uwongo suala la vyeti halikuanzia kwenye hii issue ya ngada, labda wewe ni mgeni humu..

Walitajwa Mwigulu, KINGWANGALA na Makonda humu, Magumu na Kingwangala wakaja humu kutoa ufafanuzi mpaka Mwigulu akashambuliwa humu na bwana vuta nikuvute akapiga kimya mpaka leo..
 
Uamzi gani huo wa kuziba masikio wakati makonda anafanya madudu? Maamuzi ya hivyo ni ya hovyo sana
Aindoi ukweli yapo chini ya mamlaka ya raisi. For how long he wants to be finger pointed uncessarily that is his decision too.

Hakuna anaekata asilimia kubwa ya wahusika wakuu ni wauza madawa kwenye kumchafua.

Lakini hawa awawezi mpagawisha kwenda kwenye private premise za watu na askari, kuchukua video airushe yeye. Shiwalandu ni brand Clouds media wanahaki ya kutaka ku manage brand reputation ya kipindi chao Na kutojiingiza kwenye ugomvi na Gwajima Kama kampuni. Mtu awezi lazimisha hayo Mimi ilo Tu ndio Makonda lazima achukuliwe hatua kisheria
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Ninalirudia hili mara nyingi siku hizi za hivi karibuni - tunatumia muda mwingi kujadili mambo ambayo yalitakiwa yawe ya kujadilika siku moja yakaisha. Inasikitisha, inaudhi, inakera na inakatisha tamaa kuona karibu taifa zima tunazungumzia suala ambalo kama kungekuwa na hekima, busara na weledi lingeisha mapema sana na wala lisingezaa mambo mengine.

Suala la cheti cha Makonda au kubadili jina lake wala halikuwa jambo ambalo halitatuliki kwa haraka. Naamini lingeweza kuzungumzwa, kutolewa uamuzi na watu wangesonga mbele; hata kama ni kuendelea na Makonda watu wangeendelea kama ingetolewa kauli ya kwanini watu wanaendelea. Ambao wangetaka kuendeleza ligi wangeendeleza tu.

Bahati mbaya sasa limefika mahali kwamba linahoji siyo tu hekima, bali uthubutu, busara, umakini, heshima na tunu nyingine mbalimbali za Rais na viongozi wenzake wa juu.

Niseme tu kuwa, Makonda angeweza kuendelea kuwa mkuu wa Wilaya au hata na utumishi ndani ya chama akiendelea kujengwa na hata kushughulikia mambo mengine. Niliandika wakati anateuliwa ukuu wa wilaya kuwa ilikuwa ni jambo la ajabu kidogo. Na sikutaka kuendelea kuandika muda wote baada ya hapo. Sababu kubwa ni kwamba, ni kiongozi kijana ambaye anahitaji muda wa kujifunza na kufunzwa. Sijui kama ameshajifunza lakini nina uhakika matukio ya hivi karibuni yatakuwa yamemfunza mambo mengi tu.

Hata hivyo, Makonda amejikuta kwenye hali ngumu ya mengi si kwa sababu ya yeye mwenyewe tu bali kwa sababu ya Rais wangu Magufuli mwenyewe. Alimteua kuwa Mkuu wa Mkoa na kumbakisha Dar-es-Salaam kama namna ya kuwakata ngebe watu waliokuwa wanamsemasema sana akiwa Mkuu wa wilaya. Alimpa Dar kama alama ya "wakome" waliokuwa wanamsema. Ni yeye alimfanya Makonda awe mlengwa wa kisiasa (political target). Katika siasa kama vile ilivyo katika mapenzi na vita - yote yanaruhusiwa (all is fair in politics just as they are fair in love and war). Kama alitaka kumtumia Makonda kama mjeledi wake wa kisiasa katika Jiji la Dar basi alipaswa kujua kuwa na wenzake wanaweza kumtumia huyo huyo Makonda kumfanya awe mjeledi wao.

Lakini pia pamoja na hayo kitabia, na weledi wa kiuongozi Makonda mwenyewe pia amejitengeneza kuwa mlengwa. Tangu sakata lake lianze na mashambulizi yaanze dhidi yake ni wachache wameonesha kujali kumuonea huruma. Hii imenishangaza kidogo lakini nimeelewa. Kama hawawezi kumgusa mfalme, kwanini wasimguse mtoto wa Mfalme? Tuliliona hili kwa Kikwete sana; pale ambapo watu waliona ni ngumu kumgusa Kikwete wakaamua kumgusa Ridhiwani - kwa ukweli au la. Bahati mbaya Makonda amechukuliwa na wengi na jinsi alivyojengwa kama vile ni mtoto wa Magufuli mwenyewe na hivyo kama watu hawawezi kumgusa Magufuli basi watamgusa "mwanaye mpendwa aliyependezwa naye".

Lakini, ukiondoa tuhuma za vyeti - ambazo kama nilivyoelezwa jana kwenye ZamaMpya - kwa kiasi kubwa zile zilikuwa ni siasa zaidi. Kulikuwepo na hoja lakini haikuwa hoja kubwa kivile bahati mbaya ni hoja inayomhusu mpendwa wake na hivyo imekuwa hoja kubwa. Kama ingewezakana kumuangusha Makonda kwa suala la cheti wangeweza lakini naamini lile lilikuwa linapita na nilitarajia lipite kwa maelezo machache tu. Ikulu ingeweza kulizima lile hata kwa hadaa za kisiasa (serikali inafuatilia tuhuma mbalimbali dhidi ya Makonda lakini hadi hivi sasa Rais ana imani naye - kauli ingesema). Watu wangekasirika na kulalamika lakini lingepita.

Nina uhakika lingepita kwa sababu hata waliotoa tuhuma zile za vyeti wanajua kabisa kuwa kipimo hicho kikiendelea kutumiwa kwamba hata mtu aliyesoma baada ya kubadilishwa jina lake na wazazi wake akiwa darasa la saba au kidato cha nne basi wengi watakwenda na maji. Wengi walikuwa na ukali zaidi kwa mtu aliyefoji cheti cha taaluma kuliko aliyetumia jina jingine kwenda kusoma na kupata taaluma ya ukweli. Kuna tofauti ya John Juma kusema ana shahada ya uhandishi na kuonesha cheti wakati hana elimu hiyo bali cheti kanunua mtaani na mtu ambaye anaitwa Juma John ambaye jina lake la asili ni Fredy Ramadhani. Juma John akaenda akasoma, akafaulu, akaenda chuo kikuu akapasi vizuri akiwa na jina hilo jingine na akawa na elimu ya uhandisi na kazi yake ikaonekana ana tofauti sana na John Juma mwenye cheti feki! Sidhani kama kuna mtu ambaye ama shule ya msingi au sekondari ambaye hakuwa kukutana au kusoma na kina Juma John na akawaheshimu.

Kuwafukuza kina Juma John kazi baada ya kuwekeza kote katika elimu yao ni dalili ya kutokuwa na hekima na kukosa ubunifu wa kusahihisha na kuadhibu makosa ya wa zazi wao lakini bila kuwapoteza hawa hasa kama ni watu wenye weledi na waadilifu. Bora unipe Juma John kuliko mtu ambaye ana jina lake la asili na amesome kote lakini hajaelimika, hana weledi na ni janga katika mahali pa kazi. Kuna faida gani ya kuwa mtu mwenye jina halisi lakini hana a wala be ya utendaji? Ndio maana nasema suala la cheti halikuwa kubwa isipokuwa limekuwa kubwa kwa sababu ni la mpendwa wa Rais.

NI kwa sababu hiyo basi naamini, tuhuma hizi mbili kubwa za wiki iliyopita ni kubwa mno kiasi kwamba wanaotaka Makonda aondolewe - hata kwa kuwa demoted - wanafanya hivyo kwa haki na ni ushindi ambao wameushinda.

Katika mapambano kuna kushindwa baadhi ya mapigano; si lazima ukubali umeshindwa vita. Magufuli raia wangu kwenye hili la Makonda umeshindwa pigano hili, na kwa vile wewe pia ni mwanasiasa unajua ni wakati gani wa kukubali kushindwa na kuamua kujipanga upya. Na njia mojawapo ya kujipanga ni kuhakikisha watendaji wako huwafanyi wawe walengwa wa kuangushwa na mojawapo ni kuhakikisha wanasimamiwa vizuri katika utumishi.

Kwa sababu sasa hivi ukiangalia kinachohojiwa siyo tena Makonda bali ni wewe mwenyewe. Kama ulimuondoa Kitwanga kwa kuhutubia Bunge akiwa amelewa na alikuwa ni Waziri na inadaiwa alikuwa ni rafiki yako wa karibu ni kitu gani kimefanya mtu mwenye tuhuma kama za Makonda kuendelea kuwepo hata kwa siku nyingine moja? Maana hata Mlevi anaweza kusema kweli akiwa amelewa na akawa sahihi!

Rais wangu Magufuli wape wapinzani wako ushindi huu kwani wamekushinda katika hili; halafu twende kwenhye mambo mengine ya kitaifa na ya kulijenga taifa, siyo ya kutafuta kujibu mashambulizi, kukomoa na visasi. Acha kazi yao na utendaji wako useme wenyewe. Waache Watanzania waangalie jinsi unavyotekeleza kazi zako na unavyowasimamia watendaji wako. Usiwape mianya isiyo ya lazima.

Lakini ukiwapa mianya hiyo, usishtuke, usikasirike wala kukwazika wao nao wakaaitumua kukugonga na wewe mumo kwa mumo.

Ndio siasa hiyo. Kuna magoli unaweza kuyapinga lakini mengine inabidi ukubali tu umefungwa. Huitaji kamera kukuonesha goli limeingia kweli kweli.

Wapinzani wa ndani na nje wamekushinda rais wangu. Hao wa ndani ni kikulacho.
 
Ngoja nikusome kwanza Mzee Mwanakijiji

Pia namba 0016 inakuwaga ya Female candidates, sasa wao wanadai ni ya Male. Na sitaacha kusema watu wanaojidai wamesoma na kusambaza uongo, hawajui hata kutunga uongo. Uongo hautungwi kukaa na kuropoka uongo ule uongo hadi kutetemesha na research inabidi ifanyike ya nguvu.

Makonda oyeeeee
Wewe ndio zezeta kabisa kumzidi hata Bashite mwenyewe, eti 0016 ni ya female candidates nawasiwasi na elimu yako.
 
Ok safii la vyeti tuliache lakini hili kutengeneza genge la kimafia kutumia kwa askari wetu kiasi rais hata wazir hawajathubutu kufanya hivyo alafu bado anaangalia tu,aah rais au mpaka ampe mimba jesca!
 
Mkuu kwa suala la vyeti la the so named Makonda halijakaa vizuri ila kwenye hoja yako unaonyesha kama is a none issue! Labda hujaelewa vizuri what transpired! Alifeli form four akachukua cheti cha aliyefaulu akaendelea kusomea! Kama wewe "pangu pakavu" unaamini is a none issue jaribu uone mamlaka zitakavyo kutolea macho.

Kuna current rulings nyingii as of recent watu wamehukumiwa kwa same issue jela including ya wiki iliyoisha ambapo mkunga aliyefanya kosa pacha na Bwana Bashite kahikumiwa miaka 35! au kuna watu wako above the law as per you mkuu? Nesi aliiba cheti cha mtu akasoma ukunga akafudhu na akafanya kazi kwa weledi na professionalism kama inavyotakiwa kosa ni kuiba cheti cha mtu cha form four tuu, these are absolutely twin issues! and kwa jinsi ya mahakama ni jinai! Why the double standards?

Kama hoja yako ni sahihi then tuangalie utendaji tuu wa watuhumiwa wa uizi wa vyeti na kama walikua wanafanya kazi vizuri warudishwe woote makazini na kesi zao za jinai zifutwe ili tuijenge nchi yetu.

Suala kwa wengi wetu hatuongei ili kukomoana kisiasa bali haki, kama kuna sheria ni vema kila mmoja wetu ahikumiwe kwa sheria hiyohiyo kusiwe na ndimi mbili!
Well said mkuu, kuna watu ama hawaelewi sawa sawa sakata hili la Bashite, au kwa makusudi wanafifisha makali yake-ukweli ni kwamba Bashite sio tu anapaswa kung'olewa ofisini, bali anastahili kuwa jela muda huu!
 
Ukisoma maandiko ya Mzee Mwanakijiji siku hizi utagundua the guy is in the middle of nowhere,yaani hana pa kushika.
Taratibu ameanza kupunguza matajio aliyokuwa nayo juu ya mtu yule anaetumia na kuhubiri unyonge na umasikini wa watanzania kama uchochohoro wa kuficha lililo moyoni mwake.
Makonda kuwepo madarakani hadi sasa inatufanya watanzania kuhoji huu uhusiano wa rais na mteule wake ni wa namna gani? Mbona wengine walitumbuliwa kwa tetesi tu za mitaani? kuna tofauti gani kwa Makonda na hao wengine?
Kuna hisia,tetesi kwamba rais anamtumia makonda kama msiri wake kwenye mambo binafsi.
 
Back
Top Bottom