Rais wangu, pamoja na mengi uliyofanya mazuri, kwa hili la mikopo ya wanafunzi elimu ya juu litafanya hata mazuri uliyofanya yasionekane. Watoto wa maskini waliokupigia kura kwa ahadi zako nzuri wapo wanahaha, wameenda vyuoni kwa imani kuwa watapata mikopo, kufika kule mikopo hawapati. Katika ahadi zako ulisema tukuchangue na utahakikisha watoto wote wenye sifa ya kupata mikopo hawatahangaishwa (na kweli mwaka wa kwanza ulifanya hivyo). Mara hii baada ya mwaka mmoja umeishasahau uliyoahidi. Watoto wanapoandamana bodi ya mikopo, uoni au watoa taarifa wako hawakwambii?
Bodi ya mikopo wakawaomba wanachuo watarajiwa kulipa hela ya maombi bila kuwaeleza nani wanastahili kupata mikopo. baada ya kula hela yao ndio wanawambia kuwa waliosoma shule za binafsi baba zao wana hela hivyo hawastahili kupewa mikopo. Mbona hawakusema tangu mwanzo. Hivi kusoma shule za private ni dhambi? kwa hiyo zifungwe? serikali peke yake itaweza? Kwa kusoma private siyo kwamba watu wanahela, la hasha bali wanatafuta elimu bora na mara nyingi ndiyo unawakuta wana division 1 na 2.
Siyo hiyo tu, tunaona watoto wa walemavu na mayatima, tena wanasema wana na uthibitisho bado wamenyimwa mikopo. Hii ni sawa kweli, ndiyo kuwajali maskini na wasiojiweza.
Sisi tunaokaa uraiani tunasikia mengi, watu wanauliza, tunaambiwa TRA wanakusanya na kuvuka lengo, hela nyingi imeokolewa kwa matumizi yasiyokuwa ya lazima ya serikali, hela nyingi imeokolewa kwa watumishi hewa. hela yote hiyo iko wapi? kwa nini wasipewe wanavyuo? Wakati mnanunua ndege kwa taslimu ( badala ya kununua kwa - hire purchase) ilidaiwa kuna hela ya kutosha na bado mnataka kununua nyingine, tena kwa kupiku wale walioweka order kabla ya kwetu. Je ni sawa kununua ndege kwa taslimu badala ya kuwapa mikopo watoto wakaenda shule. kweli kupanga ni kuchagua na katika kuchagua lazima uangalie vipaumbele.
Kuwasomesha wanachuo pia nako ni kuwekeza tena kuliko vyote (utapata wasomi wa kulikomboa taifa, utakusanya kodi mara tu wapatapo ajira). kigugumizi cha kuwapa hela kiko wapi? tena ni mkopo wala siyo bure.