Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,114
- 121,723
Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani, amekimbilia Tajikistan, kwa mujibu wa Al Jazeera!
Taliban wameshinda!
Taliban wamechukua nchi!
Mwezi mmoja uliopita, Rais wa Marekani alisema bila kumung’unya maneno kuwa Taliban kuchukua nchi hakuwezekani kwa sababu jeshi la Afghanistan liko imara.
Hahahaa. Well, tayari Taliban wameshachukua nchi na Rais wa Afghanistan kala kona.
===
Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani ameikimbia nchi yake leo jioni baada ya wanamgambo wa Taliban kuuzingira mji mkuu wa Kabul.
Maafisa wawili wa serikali ambao hawakutaka majina yao kutajwa wameliambia shirika la habari la Associated Press kuwa Ghani ameondoka Afghanistan na inaarifiwa amekimbilia taifa jirani la Tajikistan.
Mkuu wa Baraza la Maridhiano ya Taifa nchini Afghanistan Abdullah Abdullah pia amethibitisha habari hizo kupitia mkanda wa video.
Kuondoka kwa Ghani kunatoa taswira halisi ya uwezekano wa kundi la Taliban kuchukua madaraka nchini Afghanistan wakati wowote kuanzia sasa.
Wapiganaji wa kundi hilo waliingia kwenye viunga vya pembezoni mwa mji mkuu wa Kabul leo Alfajiri baada ya kupata mafanikio makubwa katika siku za karibuni kwa kuikamata miji mingi nchini humo.