Wakuu,
Katika Mkutano leo Rais Samia amejitapa kuwa nchi ipo salama, lakini pia utalii na uwekezaji unaongezeka. Kwa matukio yanayoendelea ni kweli kuna usalama? Wewe jibu unalo lakini pia watanzania majibu wanayo.
Mnapoingia chaka ni kudhani matukio haya yanaathiri tu wananchi wa wachache, mnashindwa kuangalia kwenye picha kubwa kuwa matukio haya ya kutisha hayaishii tu Tanzania, Dunia inaangalia na kujua kinachoendelea, hii siyo nzuri kwenye uwekezaji na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Pia soma: Rais Samia Kwa Mabalozi: Hatupo hapa kuelekezwa nini cha kufanya kwenye nchi yetu
Hakuna mtu atajihisi salama kwenda kuwekeza kwenye nchi ambayo muda wowote anaweza kutekwa na kuuliwa, wala kwenda kutalii kwenye mazingira kama haya.
Hizo nchi unazotoa mifano watoto kwenda bastola shuleni, sijui wapi mtu kaua kundi la watu, wote wahusika wanakamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki ama wanauliwa on the spot. Huwezi kulinganisha na hapa ambako watu wanatekwa back to back na hakuna yoyote anayewajibishwa kwenye haya. Si kwa viongozi kujiuzulu wala kwa wahusika wa vitendo hivi kukamatwa.
Kwa mazingira kama haya unategemea wananchi watakaa kimya?
Badala ya kutoa vijembe na kuchamba wanaohamaki na wanaokosoa hatua za konono kutoka kwenye vyombo vya usalama kushughulikia matukio haya na hata wewe kama Mkuu wa Nchi kukemea haya, hatua stahiki zichukuliwe. CHUKUA HATUA