The Sunk Cost Fallacy 2
JF-Expert Member
- Nov 8, 2022
- 9,426
- 10,927
My Take
Mlisema Samia ameuza Bandari Kuna bango lenu hili hapa, ni spana tuu Kwa kwenda mbele.
=======
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imevunja rekodi kwa kutoa jumla ya Shilingi za Kitanzania 153.9 Bln kama gawio kwa Serikali kuu kwa mwaka wa fedha Mwaka 2023/2024.
Gawio hilo limeifanya TPA, kuongoza kwa kutoa gawio kubwa zaidi kuliko taasisi zote za Serikali hapa nchini, “....na haya ni matunda ya uwekezaji uliofanywa katika Bandari ya Dar es Salaam”, amasema Mkurugenzi Mkuu, Bw. Prasduce Mbossa.
======
“TPA (Mamlaka ya Bandari Tanzania) mwaka jana (2023) nina hakika kiwango chenu hakikuwa hiki, lakini kwa mageuzi yaliyotokea bandarini mmeweza kufikia kiwango hiki na mwakani tunatarajia kiwango kikubwa zaidi pengine mara mbili yake ya hiki mlicholeta leo, hakuna sababu kama mtaendesha bandari na sekta iliyopo pale na pale kuna watu wawili ambao tumeshawaruhusu.
Mmeomba maombi zaidi lakini hata wale wawili mwakani mnaweza kuleta mara mbili ya hiki kiwango na huko ndiko tulikuwa tunaelekea ndugu zangu . Wale waliopiga kelele mama kauza bahari sijui mama kauza bandari mama kauza nini mama kauza..mauzo yale faida yake ni hii hapa leo, na huu ni mwanzo tutatarajia kutapata faida kubwa zaidi kwa bandari zetu zote kubwa ambazo zipo ndani ya nchi”- Dkt. Samia.
Pia soma:
- Rais Samia unadanganywa, DP World hajaleta tija yoyote kwenye Bandari ya Dar es Salaam
- TPA imesifiwa sana kwa kutoa Gawio la Bilioni 153.9 wakati 2018/19 Gawio lilikuwa Bilioni 480. Je, Rais Samia kasahau?
- Ufafanuzi kuhusu Gawio la Tsh. Bilioni 153.9 lililotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA kwa Serikali