Kuelekea 2025 Rais Samia: Pikipiki zako za CCM zimeongeza ufanisi wa kiutendaji, zilizobaki naomba wapewe wenyeviti wa kata

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
1,686
1,590
Chama cha Mapinduzi kimejizatiti kwa kuongeza ufanisi ktk ngazi za chini kupitia program ya kugawa Pikipiki maarufu kwa Pikipiki za Samia Suluhu.

Hata hivyo baada ya kuzigawa kwa walengwa (Makatibu Kata, Makatibu wa Jumuiya Vijana, Wanawake, na Wazazi) nchi nzima kuna zilizobakizwa bila kugawiwa. Ni dhahili kuwa kutokana na uhitaji wa pikipiki haziwezi kuenea kila kiongozi wa CCM.

Pamoja na hayo katika ngazi ya kata kiongozi mwenye chama ni MWENYEKITI WA KATA husika. Sasa kitendo cha wasaidizi wake kupata Pikipiki halafu yeye akiwa kando inaweza kutafsiriwa kuwa wametengwa - lkn pia hili linakuwa kama linawashushia hadhi ya uongozi dhidi ya wanaowaongoza. HIVYO NASHAURI:

Soma Pia:

* Pikipiki zilizobakizwa baada ya Makatibu wa kata kugawiwa wapewe WENYEVITI;

* Uchaguzi wa Serikali za mitaa umefika - viongozi hawa wapewe semina ili wasijitenge na mchakato ulioko mbele yao;

* CCM ibaki kuwa kimbilio la wanyonge.
 
Pikipiki zaidi ya 18,000 zimeagizwa na SSH zenye hadi chapa SSH-2025 kwa ajili ya kampeni zake, huyu mama kweli anatutendea haki na fedha zetu?

Unajua ni kiasi gani cha fedha kimetumika hapo na kutakuwa na manufaa gani kwa nchi? Ni angalu 50bn zimetumika kwa ajili ya kuhonga watu kwa kutumia pikipiki na utaona kuana mtanzania anashabikia hilo wakati hana maji safi wala barabara kwenda kwao!
 
ktk Hali ya kushangaza chama tawala kimegawa PIKIPIKI NNE KILA KATA wakati ambazo ukienda ktk hospital za umma ukuti dawa na baadhi ya vituo vya afya asa vijijini havina wataalamu wa kitossha
 
Kelele za nini?Wakigawa 4 gaweni 10.Mnapinga kata zikigaiwa pikipiki. Kwani zimegaiwa na Serikali?
 
ktk Hali ya kushangaza chama tawala kimegawa PIKIPIKI NNE KILA KATA wakati ambazo ukienda ktk hospital za umma ukuti dawa na baadhi ya vituo vya afya asa vijijini havina wataalamu wa kitossha
Hiki chama kikishinda uchaguzi 2025 tumekwishaI
 
Takukuru wapo tu wanakenua meno.wengekuwa ni chama Cha chadema wangesema ni rushwa.
 
Kwahiyo kama serikali ianaongozwa na ccm ndio watumie fedha za walipa Kodi kwa MATUMIZI yasiyo na tija
 
CCM imepata wapi fedha zote hizi za kununua PIKIPIKI Kila KATA kama sio fedha kutoka serikalini
Shule za jumuia ya wazazi zimekufa Mbeya. Meta sekondari, Ivumwe walimu waligoma kudai mshahara. CCM pesa umetoa wapi? Itafahamika tu.
 
Karne ya 21 mtu kupewa usafiri wa pikipiki unafikia hadi hadhi ya kuuza utu wako!!
 
Pikipiki zaidi ya 18,000 zimeagizwa na SSH zenye hadi chapa SSH-2025 kwa ajili ya kampeni zake, huyu mama kweli anatutendea haki na fedha zetu?

Unajua ni kiasi gani cha fedha kimetumika hapo na kutakuwa na manufaa gani kwa nchi? Ni angalu 50bn zimetumika kwa ajili ya kuhonga watu kwa kutumia pikipiki na utaona kuana mtanzania anashabikia hilo wakati hana maji safi wala barabara kwenda kwao!

Huyu mtu ni janga kubwa sana sana sana kwa watanganyika .

Hata kauli zake na Tulia ndizo zinazoharibu uandikishwaji wa daftari la wapiga kura.
Kama JPM alikua dikteta ni bora mara mia maana alikua ni Mtanganyika Mzalendo na alijali sana Rasilimali za umma. Hakuuza mali za umma kindugu.
Uchaguzi utakua ni usanii na janga kubwa sana kwani Chawa wanaruhusiwa mpaka kuua bila kusemeshwa na yeyote.
 
Rushwa ya wasrabu hiyo
Ndio maana wanagawana ardhi kama vile wapo Kongo kusiko na serikali maalumu.

Tuna wanasiasa wa ajabu sana Tanzania . Ni basi tu hii nchi inaendeshwa kijeshi angalau waporaji wanaogopa kidogo Jeshi letu lakini watawala tulio nao wanatamani kuifanya hii nchi iwe kama Kongo alimradi wawe mabilionea . Hasa wale wa kutoka Zanzibar . Hawajali kabisa maslahi ya watanganyika zaidi ya rasilimali na madaraka.
 
Back
Top Bottom