Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 29,880
- 21,083
Ndugu zangu Watanzania,
Kwa Hakika ninamshukuru Sana Mwenyezi Mungu kwa Kupata Bahati ya kipekee na adimu ya kuongozwa na Rais Samia Akiwa ni Rais Wa Nchi ,Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama.
Ni historia kwangu ambayo najivunia na ambayo nitaisimulia kwa wengi wajao panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu kama ataendelea kunipatia uhai na uzima na miaka Mingi hapa Duniani.
Huyu Mama Yangu ,Mama yetu na Rais wetu Mpendwa kipenzi cha watanzania namuona na kumtazama Kama Taa juu ya kilele cha Mlima. Ni Taa ya matumaini, Ni Taa ambayo kila mmoja akiitazama analiona pambazuko la tumaini la Maisha yake, anaona pambazuko la ndoto yake ,anaona pambazuko la uchumi wake ,anaona pambazuko la biashara na kuinuka kwake kiuchumi.
Namuona Rais Samia Kama Pumzi mpya kwa waliokata tamaa,pumzi mpya kwa walio ishiwa matumaini,pumzi mpya kwa walio ishiwa nguvu. Ni pumzi mpya kwa vijana waliomaliza vyuo vikuu, ni pumzi mpya kwa wakulima, wafanyakazi wa umma, vijana wa bodaboda, wafanyabiashara, mama ntilie, vijana wanaojiunga na Elimu ya sekondari.
Ni pumzi mpya kwa sababu wakulima wakilima wanapatiwa soko la uhakika kwa mazao yao baada ya kuwa wamepewa Ruzuku kwa wakati, ni pumzi kwa vijana wanaomaliza vyuo vikuu ambapo sasa wana Matumaini ya kupata ajira hata kama siyo wote wanaopata lakini vijana wanakuwa na imani mioyoni mwao kuwa ipo siku ndoto itatimia ya kuingia kwenye utumishi wa umma.
Ni pumzi mpya kwa watumishi wa umma ambao wanao namna ambavyo Mama anaendelea kuboresha maslahi yao na pamoja na kuongeza nyongeza ya mishahara yao kwa kadri hali ya uchumi inavyoruhusu na hata sasa wanasubiri Mei mosi ifike ili wasikie Sauti ya Mama kuwahusu Watoto wake ambao kwa hakika wanampenda sana na wao pia wanatambua upendo mkubwa alionao Mama kwao.
Kwa hakika tuna kila sababu ya kuendelea kumuombea huyu Mama,kumuunga mkono na kumpatia ushirikiano. Tusimvunje moyo na tusikubali wenye chuki binafsi wakamshambulia Mama na kumkwamisha . Tusimame na mama na tuwe upande wa Mama kama ambavyo naye amekuwa nasi wakati wote.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.