JOHNGERVAS
JF-Expert Member
- Mar 22, 2016
- 952
- 1,583
Nimemsikiliza Waziri Mchengerwa na Rais Samia kuhusu wagonjwa kusafirishwa kwenye matenga Kata ya Mchoteka Wilayani Tunduru na kujiridhisha kuwa WAMEDANGANYWA, hawajapata picha halisi.
Kwenye maelezo yake, Mchengerwa anazungumzia uwepo wa ambulance Tunduru. Hili halikuwa na ubishani. Hata wale tulioibua taarifa ya wagonjwa kubebwa kwenye matenga tulilisema hilo. Hoja yetu ilikuwa na masuala mawili mbayo Waziri Mchengerwa hakuyagusa kabisa kwenye hotuba yake Tunduru;
1. Gari la Wagonjwa lililopaswa kuwa la Kituo cha afya Mchoteka limehamishwa na kupelekwa Nalasi ambako hakuna Kituo cha Afya Kilichokamilika.
2. Wagonjwa kutoka Mchoteka wanapohitaji huduma ya ambulance wanatozwa hadi Tsh. Elfu 50 ambayo wengi inawashinda hivyo wanasafirishwa kwa pikipiki kwenye matenga wale waliozidiwa.
Badala ya kueleza ukweli juu ya jambo hili, wahusika wameamua kumpotosha Waziri na Mh. Rais ili kuficha ukweli. Sisi ambao tumeamua kuitetea Tunduru HATUTAACHA kuusema ukweli kwa nguvu zote. Tutaedelea kuudema ukweli bila kujali gharama yake.
Rais ana njia zake za kuujua ukweli. Ni imani yangu ataujua ukweli wa mambo
C&P FROM MWANAHALISI ONLINE