Tetesi: Rais Samia, kama kuna upendeleo huu wa kielimu kwa Wasichana utaliangamiza Taifa

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
23,519
21,549
Wakuu naingia kwenye mada moja kwa moja pasipo kuwachosha. Baada ya kushuhudia upendeleo kwa watoto wa kike wanaochaguliwa kuingia kidato cha tano, imenilazimu kutoa angalizo. Kama nchi tunakoelekea sio kuzuri. Kuna baadhi ya watu watachukulia poa lakini upendeleo huu ikiwa utadumu, basi tutarajie kutokea majanga katika nchi yetu.

Kuna waraka nimeuona unatembea social media unaonyesha wanafunzi wa kike kupewa upendeleo maalumu kuingia kidato cha 5. Kwa mfano, kwa tahasusi ya PCB na PCM wasichana watakaochaguliwa kuingia kidato cha 5 ni wenye ufaulu kuanzia alama 7 mpaka 17 wakati kwa wavulana ni kuanzia alama 7 hadi 15! Mbali na tahasusi hizi pia kuna tahasusi nyingine ambazo wasichana wamepewa upendeleo maalumu ili kuwaboost waingie kidato cha 5 kwa ubwete. Waraka huo umetolewa na wizara ya elimu na utaanza kutumika rasmi kuanzia mwaka huu.

Tumekuwa tukishuhudia upendeleo kwa wanawake kwenye siasa kwa kugawiwa nafasi za ubwete kupitia viti maalumu. Sasa naona huu upendeleo umevuka mipaka hadi kwenye elimu. Tunaliangamiza taifa kwa mikono yetu wenyewe, ama kwa makusudi au kwa kutokujua madhara ya baadaye kwa hiki tunachokifanya. Nafikiri upendeleo huu hauwezi kufanyika pasipo Rais wa nchi kushirikishwa na huenda ndiye kaagiza ifanyike hivyo. Lakini amini nawaambia upendeleo wa aina hii una madhara makubwa kuliko unavyoweza kudhani.

Wewe fikiria watoto wa jinsia zote (ke & me) wanafundishwa na mwalimu mmoja kwenye madarasa na mazingira yale yale na mtaala ni mmoja lakini baada ya mitihani watoto wa kike wanapata upendeleo maalumu. Unafikiri watoto wa kiume watajisikiaje au unataka wafanye nini?

Kwa harakaharaka nimegundua madhara yafuatayo yatajitokeza:

1. CHUKI KWA WANAWAKE
Kwa kuwa upendeleo unafanyika waziwazi huku watoto wa kiume (wanaume) wanaona, itafika wakati itajengeka chuki kati ya wanawake na wanaume kuanzia mashuleni hadi makazini kwa wanaume kushindwa kuwapa ushirikiano wanawake. Hata wakati wa kuomba ajira, kwenye usaili wanawake watakuwa wanakaziwa zaidi kwa kuwa walipendelewa kufika hapo walipo. Hii itajenga chuki itakayosambaa na kusababisha mpasuko wa kitaifa.

2. KUSHUKA KWA UFAULU WA WASICHANA
Kwa kuwa watabakia kuwa na akili za kupendelewa, basi hata kwenye masomo watashindwa kufanya jitihada za makusudi na matokeo yake ufaulu wao utazidi kushuka mwaka hadi mwaka. Sasa huu upendeleo utakuwa umewasaidia nini zaidi ya kuwadidimiza?

3. KUONGEZEKA KWA VITENDO VYA KISHOGA
Watoto wa kiume watadhani kuzaliwa wanaume ni makosa au laana. Matokeo yake watatamani wangezaliwa kama wanawake, jambo ambalo lisingewezekana. So, kufuatia kuongezeka vitendo vya kishoga hapa nchini, itakuwa rahisi kurubuniwa kuingia kwenye ushoga, hata ikibidi kubadili jinsia kwa upasuaji ili wawe wanawake wapate upendeleo wa bwerere.

4. KUONGEZEKA UKENGEUFU MIONGONI MWA WANAWAKE
Kuanzia sasa tutarajie kuongezeka mimba za wanafunzi, school dropouts na ujinga mwingine mwingi tu kutoka kwa watoto wa kike kwa kuwa sasa wamepewa nafasi ya kurelax bila kusoma wakisubiri kupendelewa. Na pia tukumbuke tayari wanayo ofa nyingine ya kurejea shule baada ya kujifungua. Tutarajie idadi ya wanafunzi wazazi kuongezeka mara dufu.

5. UNAHARAKATI UCHWARA
Watoto hawa wanaobebwa sasa, wakiwa wakubwa lazima watajiingiza kwenye uanaharakati wa kukandamiza wanaume kwa kisingizio cha kutafuta "haki sawa kwa wote". Watakuwa siku zote, kutwa kucha, wanajikita kwenye uanaharakati na kusahau majukumu yao ya kuwahudumia waume zao na kulea familia. Wataenda mbali zaidi kutaka wanaume nao wafanyiwe upasuaji ili wawasaidie kubeba mimba. Kutakuwa na taifa hapo? Obviously, taifa litasambaratika na kuvunjika vipandevipande!

6. KUONGEZEKA DIGRII ZA CHUPI
Wanafunzi hawa wanaopendelewa kuingia kidato cha 5, kipindi wakifika vyuo vikuu watataka bado waendelee kupendelewa. Hapo ndipo idadi ya digrii za chupi itakapoongezeka. Na kuanzia hapo itakuwa ni mwendo wa kuvua chupi tu hadi kwenye kutafuta ajira na kupanda vyeo huko makazini. Tunajenga taifa la ovyo sana hapo baadaye.

MAONI YANGU
Huu upuuzi unafanyika nchini Tanzania tu. Kama kuna nchi yoyote hapa ulimwenguni inafanya ushirkina huu, niite umbwa mimekaa paleee! Haijawahi kutokea tukawa na upendeleo wa kielimu wa aina hii katika nchi hii. Upendeleo wa kipuuzi kama huu unapaswa kuishia kwenye siasa. Wewe fikiria binti kapendelewa hadi amekuwa daktari. Je, huko mtaani atakuwa anatibu wagonjwa wa upendeleo wenye magonjwa ya upendeleo? Hii ni hatari sana.

Nawasilisha.
 
Tofauti na hoja ya viti maaluma huna hoja nyingine yoyote ya msingi.

Kuhusu wanawake kupata nafasi za upendeleo katika masomo ni sahihi kwa sababu jamii nyingi hasa za vijijini hazikuthamini masomo kwa mtoto wa kike kwa muda mrefu hivyo serikali inachofanya ni kusahuhisha hiyo injustice ya muda mrefu. Kuna visa vya watoto wa kike wanaambiwa wafeli mitihani ya darasa la saba makusudi ili waolewe.
 
Kwasababu wasichana wapo more vulnerable kuliko wanaume.

Msichana akipata elimu jamii nzima inaendelea.

Nitaeleza kidogo.

Kwa mfano, ikiwa watoto wote wawili wa kike na kiume wakaishia form 4, unadhan yupi ataathirika kwa haraka zaid kuliko mwingine? Hasa linapokuja suala la uzazi? Na hivyo kuongezea serikal mzigo wa kulea watoto mapema.

Lakini pia, kazi na ajira nyingi semi skilled zinambeba zaid mtoto wa kiume kuliko wa kike.
Ufundi, Udereva, Umachinga, Ubaharia, uvuvi, kufuga, kulima, misitu nk

Nadhani uamuzi huo ni wa busara sana.
 
Hoja na ujumbe umefika.

Matokeo ya upendeleo wa jinsi ya ke uko wazi karne hii ambapo maadili yanamomonyoka kwa sababu mama wamekuwa wanaharakati zaidi kuliko mama walezi wa watoto. Tunachoshuhudia ni vijana wasiozingatia mila na desturi zetu za kiafrika kwa kukosa malezi sahihi wallipokuwa watoto.

Hivyo basi, kuendeleza upendeleo wa jinsi ya ke kutazidisha uhanarakati wao na wakati wa umama wao kupunguza muda wao wa kulea watoto katika mila na tamaduni zetu. Km kumetokea mtindo wasichana kuona fahari ya kuwa "single mother" ati kwa sababu "ndoa ni ndoano".

Tanzania ya kesho inafikirisha hivyo basi, tusilaumu mataifa ya nje kuhusu ndoa za jinsi moja. Naamini nao walipitia katika mifumo ya upendeleo wa jinsi ya kike.

Ikumbukwe kuwa mwanamke aliumbwa kuwa msaidizi wa mwanamme na si vinginevyo. Nanukuu Maandiko Matakatifu:

Mwanzo 2:7, 15, 16, 18, 21- 23 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza. Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula. Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.

Kwa maandiko hayo mwanamke wajibu wake mkuu ni kumsadia mwanamme kuitunza bustani iliyoumbwa na Mungu (kwa maana ya mazingira yatakayodumisha uhai wake, kijamii - utamaduni na mila; kisiasa; kiuchumi; kiteknolojia, nk) kama ilivyoandikwa: Mwanzo 2:15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.
 
Kuna kikundi cha local Andrew Tates na clout chasers kimeibuka hivi karibuni mtandaoni hapa bongo kinasumbua sana na harakati uchwara za kujifanya kumtetea "boy child" ila ukiangalia hoja zao karibia zote ni fallacies tu.
Kwasababu wasichana wapo more vulnerable kuliko wanaume.

Msichana akipata elimu jamii nzima inaendelea...
 
Feminism was about granting equal opportunities to both sexes. Now it's about advantaging women at the expense of men.

It's not even feminism anymore it's feminazism.

The ideology has infiltrated the education system. Boys are falling out. The family unit is indeed broken coz of this. Most filth in the society emerge from here.


 
Hii ya wasichana kuruhusiwa ufaulu wa chini kuliko wavulana si ipo toka zamani. Ni kwasababu msichana akirudi kutoka shule aanze kupika, kuchota maji, atunze wadogo zake, Lakini mvulana anarudi kucheza mpira na kupumzika!!

There are just too many variables in this problem kiasi kwamba I've just let Jesus take the wheel no joke. I see the debate futile.
 
Hii dunia inapoelekea mwanamme anenda kupata tabu sana. Cha ajabu hayo mambo yanafanyika huku baadhi ya mijanadume ikiwa ndani ya hizo projects.

Siku hizi hata ma bank company ikiwa na wanawake ina possibility kubwa ya kuwa na advantages nyingi tu kwenye suala zima la mikopo.

Hawa mashetani lengo lao ni kuwa hii dunia itawaliwe na wanawake. na kuna mipuuzi kibao bado inaendelea kusapoti hayo mambo utawaona wengi humu wakichangia.
 
Hii ya wasichana kuruhusiwa ufaulu wa chini kuliko wavulana si ipo toka zamani. Ni kwasababu msichana akirudi kutoka shule aanze kupika, kuchota maji, atunze wadogo zake, Lakini mvulana anarudi kucheza mpira na kupumzika!!

There are just too many variables to this problem kiasi kwamba I've just let Jesus take the wheel no joke. I see the debate futile.

kwa hiyo hiyondio hoja toshelezi?
 
Back
Top Bottom