Mwalimu Nyerere aliona mbali sana baada ya kujua kuwa nchi hii ya Tanzania ni ya Wakulima na Wafanya kazi.
Kati ya viwanda vingi alijenga ni kile cha Tanga Fertirlizer Company iliyokuwa inatengeneza mbolea ya NPK na nyingine kama sikosei.
Wajanja wakakiuza na hata ukigoogle leo hakipo kwenye uhai wowote.
Ni ajabu tunasheherekea siku ya wakulima Nanenane lakini kiwanda pekee cha mbolea ni kile cha Minjingu.
Mama Samia ukitaka kukukmbukwa na wakulima, tembea mwendo wa Mwalimu na kufufua kiwanda cha Mbolea Tanga.
Tatizo letu tunaita viwanda kumbe ni magofu. Mara nyingi ni viwanja tu vimebaki haya maeneo.