Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 1,012
- 2,480
Nimesoma kitabu cha "Will Propaganda Work in Modern World?" Mwandishi pamoja na mambo yote anasema, "moja ya sifa chanya na bora kwa kiongozi makini ni kujua watu wake wanahitaji nini kwa wakati gani na kwa sababu gani naye huenda na matakwa yao ili kukidhi na kukata kiu yao. Anasema kiongozi asiye na maono ya mbali hukinzana na matakwa ya umma na hata kusuguana nao kwa hila jambo ambalo hufanya mwisho wa kiongozi huyo kuwa mbaya au nzuri lakini uzuri wa mashaka.
Ukisoma nyuso za Watanzania, ukisikia kauli zao rasmi na zisizo rasmi kwa ujumla wao utagundua kuwa ni kikundi kidogo mno tena wa kuhesabu hata na mtoto wa darasa la pili ndio wanafurahia na kushangilia ufisadi maana wananufaika na ufisadi huo.
Kundi kubwa na hasa wenye maisha dhalili nyoyo zao zimevimba kwa hasira wanapoona hawasikilizwi wanataka nini kwa SASA sio kesho. Ukweli ni kwamba Ripoti ya CAG imeamsha hasira za wananchi walio wengi na hasa baada ya Spika kudai ripoti hiyo itajadiliwa Novemba.
Wananchi wanahoji kwa nini kama ni sheria inataka hivyo ni matukio mangapi mabadiliko ya sheria yalifanywa kwa hati ya Dharura? Wananchi hawana shida na mambo mengine yooooote. Sijui SGR, ndege Mpya, Busisi Bridge, maji asilimia 78 mijini, sijui akaunti za wasambaza ushoga kufungiwa nk. Hilo hawalijadili huku "site". Wao wanataka mjadala huru wa Ripoti hii na hatua kuchukuliwa kwa wezi wote na waziridishe pesa zao. Basi! Hayo mengine mnajifurahisha tu.
Na mimi naungana nao, wananchi wenzangu tuwaache wao wajadili ya kwao sisi tu-deal na wezi wetu na ikiwezekana tuwahukumu wenyewe.
Narudia, Samia achana na wapambe, sikiliza sauti za waajiri wako wanahitaji nini kwa sasa si November? Uchaguzi ni wako, uamuzi ni wetu. Ahsante.