Kinuju
JF-Expert Member
- Mar 20, 2021
- 2,390
- 5,320
Rais Samia leo akiwa anaweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa barabara za pete(ring road) jijini Dodoma amesema bado sauti ya mtangulizi wake hayati Magufuli anaisikia ikimtaka akamilishe miradi yote aliyoiacha, ikiwemo huo wa ujenzi wa barabara za ring roads zitakazowezesha kuipanga na kuipendezesha jiji la Dodoma.
Rais Samia amesema ameachiwa urithi mzito wa kukamilisha miradi yote na atafanya kama alivyowaahidi watanzania kuwa hakuna hata mradi mmoja utakaoshindwa kukamilika na wananchi wasiwe na wasiwasi.
Rais Samia amesema ameachiwa urithi mzito wa kukamilisha miradi yote na atafanya kama alivyowaahidi watanzania kuwa hakuna hata mradi mmoja utakaoshindwa kukamilika na wananchi wasiwe na wasiwasi.