Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,732
- 13,485
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania ya Mwaka 2022 na Ugawaji wa Magari ya Kubebea Wagonjwa na Vifaa Tiba katika Ukumbi wa Mikutano wa JNICC leo tarehe 28 Oktoba, 2023.
Mwakilishi - Wizara ya Afya
Vifaa vya kuhudumia watoto njinti - wenye upungufu wa uzito, pamoja na watoto wagonjwa. Vina thamani ya Tsh. Bilioni 6.3 ambavyo tumevisambaza katika hospitali zetu Tanzania yote, katika hospitali 127.
(Rais anahoji wingi wa idadi ya vifaa vilivyonunuliwa)
"Jumla ni seti 120", mwakilishi kutoka Wizara ya Afya anajibu.
Mwakilishi mwingine anasema:
Lakini pia Mh. Rais, tuna vifaa vya kutibu dalili za saratani ya mlango wa kizazi ambavyo tumenunua 140 na ni vya kisasa kabisa na sasa haihitaji mama achukue umbali mrefu sana kwenda kupata huduma hii. Unaichaji inaweza kutibu wagonjwa kama 80.
Erasto Silvanus, Mkurugenzi wa Huduma za Dharura na Maafa - Wizara ya Afya
Mbele yako ni magari ambayo serikali yako tukufu imeyanunua. Magari ni 989 na katika hayo, magari ya wagonjwa ni 727 na magari mengine ya ufuatiliaji na huduma za afya katika halmashauri zote yapo 262.
Magari yaliyopo hapa yanayoenda kutumika na wagonjwa ni 216.
Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya
Kwenye suala la ambulance, kwasababu ya UVIKO-19, wanatuletea kidogo kidogo- 25, 30, kwahiyo mpaka sasa hivi, tumepokea ambulance 216 na magari ya usimamizi ni 153. Kwahiyo jumla leo utasaidia magari 369 kwa niaba ya magari 989.
Ambulance ni 727, lakini kwasababu ya COVID na vita ya Ukraine, demand ni kubwa hivyo yanakuja kidogokidogo.
Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha
Mh. Rais kazi unazozifanya zinaiheshimisha Tanzania, hata Mataifa mengine mbalimbali wanakuja Tanzania kupata huduma za afya, kazi unazofanya pia zinaiheshimisha CCM na kuitofautisha na Vyama vingine na pia zinaheshimisha utu wa Mwanamke na Watoto, umetoa magari yabwagonjwa na umetengeneza barabara zinazounganisha
Vijji vyote
Umejenga vituo vya afya Tarafa zote za Nchi hii na kila Kata za kimkakati, umeongeza fedha kwenye elimu, umehakikisha maji yanapatikana umeongeza bajeti ya maji kuliko kipindi kingine chochote
Sasa kwakuwa walisema aje Mtu wa maokoto hapa aweze kusema zaidi, niseme tu wale wanaofupisha kazi zako watasema ni kodi zetu lakini Mh. Rais kodi zilikuwepo tangu enzi za kodi ya kichwa, ikaja kodi ya mbwa, kodi ya baiskeli n.k, itoshe tu kusema maelekezo yako ya kutaka fedha ziende kutekeleza miradi ya maendeleo ndio matokeo yake haya tunayoyaona
Na wengine wanaosema fedha zinaibiwa Mimi swali langu limekuwa jepesi tu, kama fedha zinaweza zikaibiwa lakini bado ukapeleka MRI kote, ukatengeneza vituo vya afya Tarafa zote, ukanunua magari mengi kwa mpigo, Je, wakati haziibiwi?, Kwasababu wewe ni Rais wa sita, Je wakati haziibiwi zilikuwa zinaenda wapi? Kwasababu hivi ni vitu vinaonekana na vimenunuliwa
kwa fedha
Mchengerwa, Waziri, OR TAMISEMI
Kwa kipindi cha kuanzia 2017 hadi Septemba 13, idadi ya zahanati zinazotoa huduma za afya zimeongezeka kutoka 4,127 hadi kufikia zahanati 5,646. Vituo vya afya vilivyosajilia na kuanza kutoa huduma, navyo vimeongezeka kutoka vituo 535 hadi kufikia vituo 788.
Aidha vituo hinavyotoa huduma za upasuaji vimeongezeka kutoka 115 hadi 537hadi September 2023.
Jumla ya hospitali mpya zilizojengwa wakati wako ni 119. I8 zimekarabatiwa pamoja na kupanuliwa.
Katika kipindi cha miaka miwili, serikali ya awamu ya sita, OR TAMISEMI imetumia takriban bilioni 194.48 katika kuboresha huduma ya sfya ya msingi na upatikanaji wa vifaa ambapo yamejengwa majengo 83 ya dharura, majengo 28 ya wagonjwa mahututi na kituo cha matibabu.
Nyumba zilizojengwa ni 150, ununuzi wa vifaa tiba na mtambo ya kuzalisha hewa, mashine za mionzi 437, magari 316 kwa ajili ya kubebea wagonjwa ambayo Mh. Rais utayagawa siku ya leo, na pikipiki 517.
Katika kipindi cha miaka miwili, serikali imetoa bilioni 368.12 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kutolea huduma ya afya ya msingi na unajulikana wa vifaa tiba.