Rais Samia aweka historia nyingine ndani ya miezi mitatu ya kuvutia uwekezaji

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
Na Mwl Udadis, DSM-CBD

Kipimo cha mafanikio ni matokeo ya kile unachokusudia kifanyike. Kuna wakati baadhi yetu tulihoji ni wakati gani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan anapumzika? na hii ilitokana na ziara zake za kitaifa na kimataifa hasa zile zinazolenga kuvutia wawekezaji nchini. Nachelea kusema kuwa ni rasmi sasa ile kazi iliyomfanya na inayoendelea kumfanya kuwa 'busy' imeanza kuzaa matunda kwa kasi ya 5G.

Kwa mujibu wa taarifa ya rasmi kutoka kituo cha uwekezaji Tanzania, katika kipindi cha siku 90, yaani kuanzia Mwezi July hadi Septemba, miradi ipatayo 137 yenye thamani ya takribani Dola Milioni 2069.49 iliweza kusajiliwa kwaajili ya utekelezaji hapa nchini. Hili ni ongezeko la asilimia 67 ambapo kama kasi hii itaendelea tunaweza kufikia ongezeko la zaidi 70% hapo mwakani.

Ukuaji huu unaenda sambamba na kuwekwa Tanzania katika nafasi ya tatu barani Afrika kama nchi inayovutia zaidi wawekezaji wa ndani na wa nje na ya nchi ya kwanza kwa Afrika Mashariki. Miradi 137 katika utekelezaji wake kamili inatarajiwa kuzalisha ajira zipatazo 86,986. Juhudi za kuzalisha ajira kupitia sekta binafsi ni sehemu ya muarobaini wa suala la ajira.

Baadhi ya mambo yaliyofanywa kwa weledi na Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu kuwezesha haya ni pamoja na ;

Kuanzishwa kwa dirisha la kielektronic la huduma (TeIW), utolewaji wa muongozo wa watoa huduma(ISPs), uanzishwaji wa wizara, idara na mamlaka zilizo mahususi kwaajili ya uwekezaji(MDAs), kuweka mazingira wezeshi kwa sekta ya bidhaa(FMCG), kuendelea kuboresha mazingira ya kidijiti kwa wawekezaji, sera rafiki kwa wawekezaji wa ndani na wa nje na kutekeleza sera ya mambo ya nje inayochagiza Diplomasia ya uchumi.
 
Back
Top Bottom