Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,594
- 13,274
Ziara ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Mwanza imeanza siku ya leo Jumamosi Oktoba 12, 2024 ambapo atatembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya barabara, Sekta za afya, elimu, na uwekezaji, sambamba na kutoa maelekezo mahsusi ya kuharakisha utekelezaji wa miradi hiyo.
Aidha, imeelezwa ziara hii itakuwa jukwaa kwa Rais Samia kuzungumza na Wananchi, kuhamasisha ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na Jamii katika kukuza uchumi wa viwanda, pamoja na kuboresha huduma za kijamii.
Hali kadhalika, imeelezwa kuwa hotuba zake zinatarajiwa kugusia masuala ya kisera, akisisitiza umuhimu wa utulivu na amani kama nguzo za msingi katika safari ya maendeleo ya Taifa.
ALICHOSEMA RAIS SAMIA
Ndugu wana-Mwanza, mabibi na mabwana.
Nitakuwa Mwanza kuanzia leo mpaka tarehe 15. Nitafanya shughuli kadhaa nikiwa ndani ya mkoa wa Mwanza, Leo baada ya kusalimiana nanyi nitakuwa na mazungumzo na viongozi wa dini, na baadaye nitakuwa nao usiku viongozi wa dini wa mkoa mzima wa Mwanza.
Sasa, kabla ya kuendelea na shughuli nyingine zitakazofuatia, nitumie fursa hii kuwashukuru sana wana-Mwanza kwa makaribisho makubwa hivi…
Kesho nitawatoroka kidogo wana-Mwanza kuelekea Geita kwenye shughuli ya kufunga maonesho ya teknolojia na uwezeshaji katika sekta ya madini. Lakini pia nitasalimia nikiwa njiani kuelekea au kurudi Geita.
Keshokutwa ni ile siku ambayo Mkuu wa Mkoa ameisema hapa. Ni siku ya kilele cha Mbio za Mwenge.
Nilikuwa naangalia jana kwenye ufunguzi wa Wiki ya Vijana nikaona mambo yamefana kweikweli. Wiki ya Vijana imekuja kwa kishindo.
Mwanza mmebahatika sana, mwenge unatimiza miaka 60 tangu kuasisiwa kwake. Lakini pia Mwenge unasindikizwa na miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, yametimiza miaka 60 mwaka huu. Lakini [pia], Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umetimiza miaka 60 mwaka huu.
Jeshi letu la wananchi wa Tanzania, limetimiza miaka 60 mwaka huu, na vivyo hivyo, jeshi letu la polishi limetimiza miaka 60 mwaka huu.
Kwahiyo, wana-Mwanza mmeingia kwenye historia nzuri.
Tukimaliza kilele cha Mwenge tarehe 14, mwenge utapelekwa Kilimanjaro kule ulipoanzia.