Rais Samia awapongeza Simba kwa kuichapa CS Sfaxien, "Simba mnaendelea kutupa furaha"

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,419
3,631
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameipongeza klabu ya Simba kwa ushindi wake dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia katika Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Mechi hiyo imechezwa leo Jumapili Desemba 15, 2024 jijini Dar es Salaam ambapo Simba imeshinda kwa mabao 2-1.

Pia, Soma: Full Time: Simba SC 2-1 CS Sfaxien | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa National Stadium | Disemba 15,2024

Rais Samia kupitia mitandao yake ya kijamii ameandika: "Pongezi kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya CS Sfaxien.

"Mnaendelea kutupa Watanzania furaha na burudani kwa kuipeperusha vyema bendera ya nchi yetu kimataifa, huku tukiendelea kubaki wamoja katika kazi, amani, umoja, utulivu na mshikamano."

"Ninawatakia kila la kheri katika michezo yenu inayofuata."

Mabao ya Simba yamewekwa wavuni na mshambuliaji Kibu Denis.
IMG_1647.jpeg
 
Hizo pongezi zingekuwa ndiyo zimetolewa kwa Wananchi Yanga baada ya ushindi fulani, kuna watu wangenuna.
 
Goli la mama VS Viti 256 vilivyo ng'olewa na waarabu wa klabu ya simba, vile vile, uzalendo ni pamoja na kutunza vifaa vya jamii
 
Back
Top Bottom